ANNUUR 1054.1.pdf

download ANNUUR 1054.1.pdf

of 7

Transcript of ANNUUR 1054.1.pdf

  • 7/29/2019 ANNUUR 1054.1.pdf

    1/7

    ISSN 0856 - 3861 Na. 1054 RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs

    Sauti ya Waislamu

    www.annuurpapers.co.tz

    Natafuta Mbia wa Biashara ya GAREJawe Jijini Dar es salaam au Mikoani au

    Kuuza vifaa vya Gereji.Nina Vifaa vya Kunyooshea magari, Vifa

    vya Makanika.Pia nina Spana aina zote za Ujerumani

    na Italia.

    Kwa mawasiliano zaidi pigasimu no 0784 939445, 0655

    919445.

    TANGAZO

    MAKAMO wa kwanzawa Rais wa Zanzibar,Ma a l im Se i f Sha r i f Hamad amesema kotila Muungano kwa sasalinawabana Wazanzibarina kudai kuwa haoni

    ILIKUWA almanusra,

    Maalim Ally Bassalehna Masheikh wenzakewangekosa swala yaAljumaa kutokana namfumokristo ulioifanyaT u m e y a W a r i o b aisijali kwamba wao niWaislamu na Masheikhwa Misikiti.

    Kwa kutokujali huko,anasema Bassaleh kuwaTume iliwapangia kufikakutoa maoni muda ambaowalitakiwa kuandaa hutubaza Ijumaa na kuchukuaudhu kwa ajili ya swala.

    Koti la Muungano

    linatubana-MaalimTanganyika ilifanya usanii, ikatowekaIkaibuka na joho la Tanzania inafaidiKwa miaka 49 usanii huo unaiumiza Zanzibar

    Mfumokristo nusurauwakosesheswala MasheikhNa Bakari Mwakangwale Hicho ni kielezo tosha

    k w a m b a U i s l a m u n aWaislamu hawathaminiwi nainachukuliwa kana kwamba

    hawapo kwa sababu hakukuwana sababu yoyote ya msingikuchagua siku ya Ijumaabadala ya siku nyingine sitaza wiki.

    Akiongea na Waandishiwa habari, mara baada yakuwasilisha maoni yao katikaTume ya maoni, Ijumaaya wiki iliyopita, MaalimAlly Bassaleh, al isema,wamekutana na Tume hiyokama wawakilishi wa makundimaalum ya kijamii.

    Mara kwa mara viongoziwa Tume ya kukusanya maoni,

    Na Mwandishi Wetu kuwepo kwa nia njemabaada ya kipindi chamiaka 49 ya Muunganohuo.

    Maalim Seif ambaye nikiongozi wa kwanza wa

    juu wa Serikali kukutanana Tume Katiba (Tumeya Warioba) katika

    Inaendelea Uk. 3

    Inaendelea Uk. 3

    SHEIKH Ponda Issa Ponda (kulia) akiteta na wakili wake Juma Nassor katika Mahakama yaKisutu, Jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni washitakiwa wenzake katika kesi hiyo. Uk. 4

    Kesi ya Ponda mashahidiwajichanganya mahakamani

  • 7/29/2019 ANNUUR 1054.1.pdf

    2/7

    2AN-NUU

    RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 20

    AN-NUURS.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

    Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 , DSM.www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

    Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

    MAONI YETU

    Tahariri/Habari/Tangazo

    Tanganyika, Zanzibarwaulizwe wanautaka?

    JUMUIYA ya Wanawakewa Kiislamu Zanzibari m e s e m a k u w autayarishaji wa katibampya hauwezi kuletamafanikio iwapo suala lamuungano halikujadiliwakwanza.

    W a m e s e m a ,kinachofanyika hivi sasani kama kulazimisha nakufanya udikiteta watuwakubali muungano uliopojambo ambalo haliwezikuleta amani ya kudumuinayotakiwa.

    Wanawake hao waJUWAKIZA wameyasemahayo mapema wiki hiikatika ukumbi wa ofisiya tume ya mabadiliko yakatiba Kikwajuni GofuZanzibar wakati wa kutoamaoni yao juu ya katibampya.

    Na Mwandishi Maalum,Zanzibar

    Mmoja wa wazungumzajiUkht . Hal ima Kasimalionyesha kushangaa watukujadili katiba ya muunganohuku kukiwa hakuna katibaya Tanganyika inayounganana Zanzibar.

    Akitoa dukuduku lakemjumbe huyo alisema kuwaWazanzibari wamechoshwana muungano uliokuwepona kwamba wanataka

    muungano wa mkataba,

    serikali tatu, la sivyo ujifilie

    kwa mbali.

    A m e s e m a h a l i y avurugu na kudhalilishwa

    kwa viongozi wa kijamii,kisiasa na kidini inayotokeaZanzibar, chanzo chake niaina ya muungano uliopoambao hauwapi uhuruWazanzibari wa kujiamliamambo yao wenyewe.

    Wachangiaji wenginewalionyesha udanganyifuunaofany ika ambapo

    hudaiwa kuwa nchi haindini wakati Jumapili sikya Wakristo ya kufanyibada imefanywa ndio sik

    ya mapumziko.Serikali inasem

    haina dini lakini siku zibada za Wakristo hakunkazi, siku ya Ijumaa watwanakwenda kazini kamkawaida. Amesema BAisha.

    Ni katika kuhoji hahiyo ikadaiwa kuwk a m a T a n z a n y i kwameona kuwa namnya kuuenzi Ukristo nkuifanya Jumapili kuwsiku ya mapumziko, baWazanzibari nao wanIjumaa.

    Kwa upande mwinginwakasema kuwa ni hitajla kidini kwa Waislamkuwa na Mahkama zaili kuhukumu mambo yaKiislamu.

    RAIS Jakaya Kikweteameeleza hivi karibunik u w a s e r i k a l i y a k ehaitavumilia vurugu zakidini, ukabila na ukandaambazo zilitaka kuliingizataifa katika matatizo.

    Rais Kikwete alitoa kauli

    hiyo wakati alipojumuikana Mabalozi mbalimbaliwanaoziwakilisha nchi zaohapa nchini, katika hafla yakuukaribisha mwaka mpyaIkulu jijini Dar.

    Hata hivyo hatuaminikwamba matatizo ya kidiniambayo yanayo i fanyaserikali ikose uvumilivu,yalishughulikiwa ipasavyokatika kuyatatua na watuwakaendelea kuishi kwaamani na kuamin ianakiimani.

    Hatuoni kama serikaliilikuwa na nia ya dhati katikakutatua hitilafu hizo zakidini, ambazo zimeachwaau kupuuzwa kwa mudamrefu b i la ku fany ikajitihada za dhati za kuzipatiasuluhu.

    T a n g u k a d h i a y aMwembechai, malalamikojuu ya ku jiunga OIC,kurejeshwa Mahakamaya Kadhi, mkataba waMoU, kashfa ya NECTA,malalamiko ya kuwepoMfumo Kristo serikalinink. Hakuna hata sualamoja lililopatiwa utatuzi namambo yakatulia, zaidi yakubainika dharau, ghiliba na

    kupuuzwa.Katika mazingira haya,tunaona kwamba ni vyemaserikali ikaeleza kwanzani kwa kiasi gani imefaulukutatua matatizo ya kidiniyal iyowahi kuji tokezanchini, kabla ya kuja nakauli za kukosa uvumilivuwa kile inachokiita vuruguza kidini.

    Tuelezwe ni kwa kiasigani serikali imefanikiwakutatua suala la kurejeshwamahakama ya kadhi nchini,ili ipatikane sababu yakukosa uvumilivu.

    Serikali ionyesheimetatuaje kero za kidini

    kabla ya kuja na vitishoTufahamishwe kwanza

    ni jitihada gani zimefanyikakufuatilia ukweli na uthabitiwa malalamiko ya Waislamukudai kuwa wanadhulumiwak u t o k a n a n a s e r i k a l ikuendeshwa na mfumokris to , unaolipendeleaKanisa. Serikalini imechukuahatua gani kuondoa kasorohiyo.

    Labda ungepat ikanaufafanuzi wa serikal i ,ilikuwaje iingie mkatabawa kutumia fedha za ummakulinufaisha kanisa (MoU),huku ikidai haina dini.

    Sote tunafahamu kuwatangu yawepo malalamikoy a W a i s l a m u j u u y amakataba huu wanaouita niowakibaguzi kiimani, serikalihadi leo imeshindwa kutoaufafanuzi juu ya hatua yake

    hiyo, na wala haipo tayarikufanya hivyo.Sisi tunaona kwamba

    serikali haitakuwa imetendahaki katika msimamo wakehuo wa kukosa uvumilivu,kwakuwa kiini cha matatizona hitilafu za kidini badovingalipo na vimeachwa bilakuguswa.

    Dawa ya jipu ni kuondoakiini chake. Hatudhanikwamba hata ukikosekanauvumilivu, basi kuendeleakupuuzia mata t izo aukutumia nguvu za dolakwa wanaodai haki au

    wanaodhulumiwa ndioitakuwa suluhu ya kudumuya matatizo ya kiimani kwawatanzania.

    Kuna haja ya serikali naviongozi wake kusikilizashida za wananchi wakena kuzifanyika kazi bilakumuonea mtu.

    Wenye haki wapewe hakiyao, wanaodhulumu walipewale waliodhulumiwa.Serikali ni ya watu wotekwa iman i zao . Hapoitapatikana suluhu ya kwelina si vinginevyo.

    Kama ilivyotangazwa na vyombo vya habari, Shule za Serikali zilizoshika nafas10 za mwisho katika matokeo ya mtihani wa kidato cha pili uliofanyika mwaka2012, zote zinatoka mikoa ya Mtwara na Lindi. Zaidi ya hayo, Mkoa wa Dodomaumeendelea kushika mkia katika matokeo ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2012huku wilaya ya Kondoa ikiongoza kwa asilimia 43 kwa kuwa na idadi ya shule 37ambazo hazikupata mwanafunzi hata mmoja aliyechaguliwa kuendelea na elimuya sekondari.

    Kama hatua ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuikabili changamoto ya hapojuu, Jumuiya ya Wataalamu wa Kiislamu Tanzania (TAMPRO) kwa kushirikiana naChuo cha Ualimu Safina, Dar es Salaam, inawaalika wamiliki wa shule na vyuo vyaualimu, wakuu wa shule na vyuo vya ualimu, walimu wa shule na vyuo vya ualimuna wadau wengine wa elimu katika kongamano la kujadili changamoto ya shule zamsingi na kata hasa katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Dodoma.

    Kongamano hilo litafanyika siku ya Jumamosi, Januari 26, 2013, kuanzia saa3.00 asubuhi mpaka 9.00 alaasiri katika ukumbi wa Basihaya Camp, Boko, Dar esSalaam. Wadau wanaotaka kuhudhuria kongamano hilo wanaombwa wathibitishekupitia simu japo kwa sms namba 0778 776226, 0653 326145, 0713 208585, 0655654900. Baadhi ya waheshimiwa wabunge na madiwani wa mikoa iliyotajwa hapojuu pia, watahudhuria.

    SHARIFU MUHAMMED(MRATIBU WA KONGAMANO)

    TANZANIA MUSLIM PROFESSIONALS ASSOCIATION

    P.O. BOX 72045, Dar es Salaam, TANZANIA. TEL+255 0655 654900,+255 713 731300, +255 754261600. Email: [email protected],

    Web: www.tampro.org

    KONGAMANO LA WADAU WA ELIMU

  • 7/29/2019 ANNUUR 1054.1.pdf

    3/7

    3AN-NUU

    RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 201Habari

    Koti la Muungano linatubana-MaalimInatoka Uk. 1

    utaratibu wa kukusanyamaoni, alisema hakunania njema katika kutatua

    kero za Muungano, haliinayopelekea usumbufukwa wa na nchi ha saupande wa Zanzibar.

    Maalim Seif alikutanana Tume hiyo hivi karibuninyumbani kwake Mbweni,Unguja ambapo alisemaMuungano wa Ser ika l imbili uliopo sasa hauwezikutatua kero zinazowakabiliwananchi:

    K o t i l a M u u n g a n olinatubana sana na tunahitajikushona koti jipya kulinganana hali zetu za sasa, alisemaMaal im Sei f mbele yaMwenyekiti wa Tume hiyo,

    Jaji Joseph Warioba.Alishauri kutokana na halihiyo ni vyema muundo waMuungano ukaangaliwa upyana kusisitiza msimamo wakewa kuwepo Muungano wamkataba ambapo kila nchiitakuwa na mamlaka yakekamili:

    T u n a m i a k a 4 9 y aMuungano bila kuonyeshamafanikio ya kuridhisha yakutatua kero za wananchisasa tunahitaji kushona koti,ili kila nchi iwe na mamlakayake ya ndani na nje, alisemaMaalim Seif.

    Alisema katika kipindihicho Tume na Kamatikadhaa zimeundwa katikakushughu l ik ia kero zaMuungano, lakini mafanikioyake ni madogo, hali inayotiawa s i wa s i , k u o n g e z e k akwa kero hizo badala yakutatuliwa.

    Maalim Seif alifahamisha,Z a n z i b a r i m e k u w amuathirika mkubwa waMuungano uliyopo, hasakatika nyanja za uchumi nasiasa, baada mshirika wakeTANGANYIKA kutoweka,na kutumika jina la Tanzaniakwa maslahi ya upande mmojawa Muungano.

    Maalim Seif ambaye pia niKatibu Mkuu wa Chama cha

    wananchi (CUF), baada yakutoa maoni hayo, alikutanana waandishi wa habari katikahoteli ya Bwawani, ambapoalifafanua maoni yake hayo nakuweka bayana kwa wananchiwote maelezo yake aliyoyatoakwa Tume ya mabadiliko yaKatiba mpya.

    Akizungumzia mfumowa muungano wa mkataba,Maalim Seif amesema kuwakumekuwa na upotoshajiwa makusudi juu ya dhanahii wakidai kuwa huko nikuvunja muungano.

    W a s i o i t a k i a m e m aZanzibar au wanganganizi wa

    mfumo uliopo wa Muunganowaliouzoea (pengine kwasababu unawanufaisha wao)wanaweza kudai kwambahatua hizi zinazopendekezwahaziashirii nia njema yakuendeleza na kuimarishaMuungano. Mimi binafsina wenzangu tunaoaminikatika Muungano wa Mkatabahatuamini hivyo. Tunaaminikatika kuwa wakweli nawawazi , kwamba hivyondivyo mahitaji ya wakati huu

    na zama hizi yanavyodai.Hata hivyo akasema kuwa

    yote hayo hufanyika kwasababu kuna watu waliozoeyakufanya mambo kibabe nahawataki kubadilika.

    Ulimwengu unabadilikakwa kasi. Zama za kuendeshamambo kwa ubabe na ukichwangumu zimepitwa na wakati.Tuache ile tabia ya kuyaonamapendekezo ya kubadilim f u m o w a M u u n g a n okuwa yana nia ya kuuvunja

    Muungano huo. Muunganoili udumu unahitaji ridhaaya walioungana. Muasisi waMuungano huu, MwalimuNyerere mwenyewe, aliwahikueleza umuhimu wa ridhaakatika masuala haya nakuonyesha kwamba ridhaaya mshirika mmojawapoi k i o n d o k a , M u u n g a n ohauwezi kusimama.

    Maalim akasisitiza kuwaWazanzibari ni watu wenyehistoria ya maingiliano ya

    jamii za watu mbal i mbana hivyo hawawezi kukataumoja, alimradi tu umojhuo uwe na maslahi na faidkwao.

    Bali akasema kuwa Mfumuliopo sasa hauinufaishZanzibar na hivyo haukubalikwa Wazanzibari.

    Ndio pale akasema kuwKoti la Muungano kamlilivyo sasa linabana san(na kwamba) Wakati umefiktushone koti jipya kwa mujibwa mahitaji ya zama hizi.

    Mfumokristo nusura umkoseshe swala Maalim BassalehInatoka Uk. 1

    wamekuwa wakiripotiwawakidai kuwa wanaotoa maoni

    juu ya masuala yahusuyoWaislamu, wanashindwakutoa ufafanuzi kama kuwepokwa Mahakama ya Kadhi,Tanzania kujiunga na OIC,katiba kutokutoa fursa yaibada kwa Waislamu, kamailivyo kwa Wakristo.

    A k i e l e z a n i y e p iwaliyowasilisha katika Tumehiyo, Maalim Bassaleh,alisema wameeleza kwambak u w e p o k i s h e r i a k w aMahakama ya Kadhi, nisehemu ya Waislamu katikauhuru wao wa kuabudu.

    Alisema, waliieleza Tumekuwa pamoja na kat iba

    ya nchi ina sheria zake zakisekula, lakini hizo sheriaza kisekula zinakubali nakutambua katika masualaya ndoa, talaka, mirathi nawaqfu, kwa mujibu wa Shariaza Kiislamu.

    Alisema, walibainishiatume hiyo kwamba, tatizolililopo ni pale familia yaKiislamu mfano, ikiwa namgogoro wa mirathi huendaM a h a k a m a n i , n a h u k ohujitambulisha kwamba waoni Waislamu, na mgogorowao wanataka uhukumiweKiislamu.

    Alisema, hakimu hukubalikwamba sheria inawarahusukumaliza Kiislamu lakinihakimu mwenyewe haelewisheria ya mirathi ya Kiislamu,hivyo inamlazimu kutoa baruawaende katika taasisi fulani yadini, huko wakagawiane kishawarejee Mahakamani hapo ilihakim aidhinishe, ili iwe nanguvu.

    Anaidhinisha nini wakatisheria yenywewe huijui,anapiga muhuri kitu ambachohakijui, yule atakayegawaakikosea au akifanya makusudikupindisha haki. AlisemaMaalim Bassaleh.

    Nikawapa mfano wa

    m g o n j wa a l i y e k we n d ahospitali ya Rufaa Muhimbili,amefika pale amechunguzwaikaonekana kwamba ana

    sara tan i (Kansa) , pa leM u h i m b i l i , a t a a m b i waugonjwa huo una kitengochake maalum, ambapo nihospitali ya Ocean Road,mgonjwa huyo atapelekwahuko ili aweze kupata tibasahihi. Alisema.

    Alisema, huo ni mafanona pesa inatoka Serikalini,akatanabaisha kwamba, kwaWaislamu, kitengo chao chaKansa ni hiyo Mhakama yaKadhi, linapokuja shauri mbeleya Mahakama ya kawaidawakashindwa kulitafutia dawamgogoro ule wapelekwe kulekatika Mahakama ya Kadhi.

    A l i s e m a , W a i s l a m uwa n a p o s e m a wa n a t a k aMahakama ya kadhi wanatakahaki yao ya Uhuru wa kuabudu,katika utaratibu unaokubalikana mamlaka ya nchi, katikamasusla ya ndoa, mirathi,Talaka na waqfu kama ilivyoutatuzi wa masuala mengine,ya kitabibu au kisheria na sivinginevyo.

    Alisema, suala lingineambalo wamelitolea maonini kuhusu katiba kutoa fursaya ibada kwa Waislamu,pamoja na kwamba Katibaya sasa inadai inatoa uhuru wakuabudu, lakini kwa Waislamu

    uhuru huo haupo. Ni k a wa m b i a m fa n ouliohai, ni hivi sasa kwambaleo Waislamu tunatakiwakujiandaa na Ibada ya swalaya Ijumaa, na nyinyi mmetuitaviongozi wa dini bila kujali leoni siku maalum ya kuabuduWaislamu na miongonimwetu ndio Mashekh katikaMisikiti yao na wanangojewakuongoza ibada.

    Hivyo hamkuona siku yakutuita ikawa ni Ijumaa, tenaasubuhi hii? Hali hii ndiyoinayo wasababisha Waislamuwalalamike, kuwa hawanauhuru wa kuabudu, wanaona

    kwamba hawatendewi haki,hawathaminiwi kama wenzaoWakristo. Alisema MaalimBassaleh.

    M a a l i m B a s s a l e h ,aliilalamikia hali hiyo akidaikwamba nusra yeye nawenzake waikosa ibada yaSwala ya Ijumaa, baada yakupangiwa siku ya Ijumaa,kuonana na wajumbe wa Tumeya Maoni kutoa maoni yaokupitia Baraza Kuu la Jumuiyana Taasisi za Kiislamu (T).

    Wametuita leo (Ijumaailiyopita), tena asubuhi mudawa kujiandaa na ibada, lakiniukiangalia jambo lenyewenalo ni zito, la kuangaliamustakabali wetu kamaWaislamu kama Watanzaniakwa miaka ijayo, hata hivyo

    tumeweza kwenda tumeonananao kwa kuwa muda ulikuwahautoshi maoni mengine naufafanuzi tumekubalianakuyapeleka kwa maandishi.Alisema Maalim Bassaleh.

    Alisema, katika kuwasilishamaon i yao wal iyagawakatika makundi mawil imakuu, kwanza ni yaleambayo yanawagusa waokama Waislamu, ambayondiyo hayo aliyoyaeleza nayale yanayowagusa kamaWatanzania.

    Alisema, kwa upande wapili wakiwa kama Watanzania,walipendekeza kuwepo namfumo wa Serikali tatu, ambapowalipendekeza kuwepo naSerikali ya Zanzibar, Serikaliya Tanganyika na Serikali yaMuungano.

    Alisema, mfumo huoutaodoa migogoro na kerozinazoitwa za Muungano,lakini pia wamependekezakuwepo kwa Mahakamaya Katiba ya nchi, ili sualalinalohusiana na mgogoro waMuungano, lipelekwe katikaMahakama ya Katiba.

    Wakati huo huo, MaalimAlly Bassaleh, amesisistizakwamba Mfumokristo katikanchi hii upo na kwambaWaislamu wanauleza kwaushahidi.

    Akiongea na Waislammara baada ya swala yIjumaa, ya wiki iliyopitkatika msikiti wa Idrisalisema Maaskofu wamekuwwakijaribu kukanusha hukwakidai mfumo huo unaletwna Waislamu.

    Alisema, Waislamu nMasheikh wanaozungumzkuwepo kwa Mfumokrisnch in i , wanazungumzkwa ushahidi, kupitia wawenyewe waliyoandika katikvitabu mbalimbali.

    S i s i t u n a w a e l e zk wa u s h a h i d i k wa m bMfumokristo katika nchhii upo, na waliotulielezkwamba kuna mfumo huo wkuwapendelea na kuwabaguWaislamu ni wao wenyewWakristo kupitia vitabu vyambalimbali sisi tulikuwhatujui. Alisema MaaliBassaleh.

    Maalim Bassaleh, aliwatakMaaskofu wasiishie kukanusht u , a u k u d a i k w a m bwanaoleta mfumo huo nWaislamu bali waje na hoja nushahidi au wakanushe yayaliyoandikwa katika vitabjuu ya ushahidi wa kuwepmfumokristo Serikalini.

    Tunawaambia MaaskofW a i s l a m u k a m whawatanyamazia hili, kwambwataendelea kuiambia Serikakwa mtindo huo huo wkuainisha yaliyomo ndanya vitabu, kisha wasem

    kipi walichozua Waislamkuhusiana na kuwepo kwMfumokris to . AlisemMaalim.

    M a a l i m B a s s a l e hal iwashangaa Maaskofhao kuwaingiza Waislamlawamani kwa kusoma nkunukuu vitabu ilihali vitabhivyo vipo na waandishi wakwangali hai huku wakishindwkuyatolea ufafanuzi yayal iyomo kat ika vi tabhivyo.

    Alitoa mfano wa kitabkingine kilichomnukuu MwJulius Nyerere, akisemkwamba atalipa Kanisa furya upendeleo ya kunawiri.

  • 7/29/2019 ANNUUR 1054.1.pdf

    4/7

    4AN-NUU

    RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 20Habari

    BAADHI ya wanafunzi wa Answaar Islamic Model School ya jijini Dar es Salaamwakiwa kwenye chumba cha kompyuta shuleni hapo.

    PICHA juu na chini baadhi ya wathumiwa Waislamu wakiwa pamoja na SheikhPonda (hayupo pichani) katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana.

    Kesi ya PondaILE kesi inayomkabiliK a t i b u w a S h u r aya Maimam, Sheikh

    Ponda Issa Ponda, janailiendelea kusikilizwakatika mahakama yaHakimu Mkazi Kisutu

    ji ji ni Da r es Sa la am,mbele ya hakimu Bi.Victoria Nongwa.

    Safari hii kesi ilikujakwa ajili ya kuendeleakusikiliza mashahidi waupande wa mlalamikaji,ambapo mashahidi wawiliMzee Masoud Kome,ambaye ni Mwenyekitiwa Baraza la wadhaminiBakwata na Bw. Hafidh SeifOthman, aliyejitambulisha

    kuwa ni mdau katikakampuni ya Agritanza namfanyabiashara wa vifaavya ujenzi.

    Akitoa ushahidi wakembele ya mahakama yahakimu mkazi Kisutu,M z e e K o m e k u t o k aDodoma, alipoulizwa nawakili wa utetezi Bw. JumaNassoro, iwapo anajuauwiano wa thamani kati yakiwanja cha ekari nne chaChangombe kilichouzwana Bakwata kwa Agritanzana lile eneo la ekari arobainililipo Kisarawe kupewa

    bakwata, alisema hajuiuwiano wa thamani yake.

    Al ipoul izwa iwapoanawafahamu washatakiwana anayeshtaki, MzeeK o m b e a l i s e m ah a w a f a h a m u . A i d h aalipoulizwa iweje amekujakutoa ushahidi katika kesiasiyoifahamu, hakutoajibu.

    Waki l i wa u te t ez ialipouliza iwapo shahidihuyo aliwahi kuliona eneohilo la ekari arobaini hukoKisarawe zilizotoleewana agritanza kwa Bakwataakiwa Mwenyekiti waBaraza la wadhaminiBakwata, Mzee Komealisema mbele ya hakimukuwa hajawahi kufikakatika eneo hilo na walah a f a h a m u K i s a r a w ekwenyewe.

    Ilielezwa kuwa dhumunila Bakwata kupewa eneola Changombe, lilikuwani kujengwa Chuo Kikuucha Kiislamu kwa msaadawa serikali ya Misri.

    Hata hivyo, shahidi huyoalipoulizwa na wakili wa

    Na Mwanishi Wetu utetezi Bw. Juma Nassorojuu ya ukubwa wa eneohilo wakati wakikabidhiwaBakwata l i l ikuwa je,alisema lilikuwa kubwa

    ila liliuzwa kidogo kidogona viongozi wasiokuwawaaminifu, ambao kwasasa hawapo Bwakata.

    K w a u p a n d e w aShahidi mwingine Bw.Hafidh Othaman, yeyealipoulizwa na wakili huyojuu ya thamani ya vifaavilivyoibwa katika kiwanjahicho cha Chabgombe,alijibu kuwa vilikuwa nathamani ya shilingi milioni56 ukiondoa saruji.

    A l i u l i z w a i w a p owaliokuwa wamevamiakiwanja anawafahamu,

    alijibu kuwa hawafahamu.Lakini alipoulizwa iwapoa l i w a o n a w a v a m i z i ,alijibu kuwa hakuwaonaisipokuwa Sheikh Ponda.

    Awali wakili JumaNassoro alisema shahidiHafidh Othmani, wakatialipoulizwa juu ya umilikiwa eneo la Kisarawe,alisema ni la kwake.Lakini kwenye mkataba wakubadilishana na Bakwata,imeelezwa kuwa eneo hiloni mali ya Agritanza. Kwaupande mwingine, Shahidi

    Hafidh alipokwenda kwamara ya kwanza Polisikulalamika, alieleza kuwaeneo la Kisarawe ni mali yakampuni ya Al-Hilal.

    Awali ilielezwa kuwaBw. Hafidh alisema eneohilo aliuziwa na serikali yakijiji. Lakini alipoulizwana wakili wa uteteziYahya Njama, Hilal huyohuyo alisema kuwa eneohilo la Kisarawe aliuziwana familia ya Bw. JamesMabina.

    Kwa maana hiyo wakili

    Nassoro anaeleza kuwa,inaonyesha mkatabawalioingia Bakwata naAgritanza ulikuwa hewa,na ungeweza kuleta utatamkubwa hapo baadae.

    Yule shahidi mwinginewa upande wa mlalamikajia l i y e a m r i w a n amahakama kukamatwa,ba do ha jak ama tw a nakufikiwshwa mahakamanihapo kama ilivyoamriwa.

    Kesi hiyo imeahirishwahadi itakapotajwa tenaJanuari 31 mwaka huu.

  • 7/29/2019 ANNUUR 1054.1.pdf

    5/7

    5AN-NUU

    RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 201Habari za Kimataifa

    RAIS wa utawala Israel,Shimon Peres, kwa maraya kwanza amekiri kuwautawala huo ulihusika na

    mauaji ya Rais wa zamaniwa Mamlaka ya Ndani yaPalestina Yasir Arafat.

    Peres, amesema Arafathakupasa kuuliwa kwa sababuulikuwepo uwezekano wakufikia maelewano na yeye.

    A m e o n g e z a k u w akukosekana kwa Yasir Arafat,hali ya mambo imekuwangumu na tata zaidi.

    Oktoba 12 mwaka 2004,Yasir Arafat, alipelekwaUfaransa kwa matibabu nakulazwa katika hospitali mojaya kijeshi iliyoko kwenyeviunga vya mji mkuu wa nchihiyo Paris.

    Hata hivyo sio tu kwambahakupata nafuu, bali hali yakeilibadilika ghafla na kuwambaya zaidi na ilipofika

    Novemba 11 mwaka huo huo,alifariki dunia hospitalini hapokutokana na athari ya sumu.

    Kwa muda wa miaka miwilikabla ya kufariki kwake,kiongozi huyo wa kwanza waMamlaka ya Ndani ya Palestina,al ikuwa kwenye k izuizinyumbani, alichowekewa nautawala wa Kizayuni wa Israelhuko Ramallah katika Ukingowa Magharibi wa Mto Jordan,Palestina inayokaliwa kwamabavu.

    Tangu wakati ilipotangazwahabari ya kifo cha Arafat,

    Peres akiri Israel ilihusika

    na mauaji ya Arafat

    Rais wa utawala Israel, Shimon Peres (kushoto) akisalimiana na Rais wa zamani waMamlaka ya Ndani ya Palestina Yasir Arafat wakati huo.

    wachambuzi wengi wa mambona wanaharakati wa kisiasana hata vyombo vya habari,viliamini kuwa kifo chake

    kilikuwa cha kutatanisha.Ripoti za vyombo vyahabari zilieleza kwamba kifocha Yasir Arafat, hakikuwa chakawaida bali aliuawa kutokanana athari za mada za sumu yaPolonium, iliyotiwa kwenyenguo zake.

    T a n g u w a k a t i h u o ,mtuhumiwa mkuu wa mauajiya kiongozi huyo ulikuwa niutawala wa Kizayuni wa Israelambao kwa muda wote huohaukuwahi kukana tuhumahizo.

    Siku za hivi karibuni,viongozi wa Palestina pamojana mke wa hayati Arafat, Bi.Suha, walitaka maiti yakeifukuliwe na kufanywauchunguzi tena wa kujuasababu ya kifo chake.

    Hatimaye mwishoni mwamwezi Novemba mwaka janamaiti ya Yasir Arafat ilifukuliwana kufanyiwa uchunguzi nawataalamu kutoka nje.

    Ingawa hii ni mara yakwanza kwa kiongozi rasmiwa utawala wa Israel kukirikwamba utawala huo ulihusikana mauaji ya Arafat, lakini hatakabla ya kufukuliwa maiti yakiongozi huyo wa Palestinakwa ajili ya uchunguzi, mkeweyaani Suha Arafat, alikuwaamefichua hapo kabla kwambaIsrael ndiyo iliyohusika na

    mauaji ya mumewe.I n a e l e z w a k u w a

    k i l i c h o m f a n y a S h i m o nPeres, akiri kuhusika utawala

    wa Kizayuni na kifo chaYasir Arafat, si matamshiyaliyotolewa na mke wa Arafat

    bali ni hali mbaya zaidi ambayoimekuwa nayo Israel hivi sasa

    baada ya kifo cha kiongozihuyo wa zamani wa Mamlakaya Ndani ya Palestina.

    Kuungama kwa Perezkunazidi kudhihirisha surahalisi ya Israel mbele ya fikraza walio wengi duniani.

    Imeonekana kuwa hatuahiyo ya Rais Perez inadhihirishau k w e l i w a m a m b o w akiutambulisha Israel kuwa nauhusiano na mfungamano wamoja kwa moja na mauaji naugaidi.

    Inaelezwa kuwa kitu pekeekinachoitofautisha Israel namakundi ya kigaidi kama alQaeda, ni kwamba kundi hilohalina mfungamano wowotewa kiserikali wakati Israel nidhihirisho halisi la ugaidi wakiserikali duniani.

    Jambo jingine muhimu nikwamba, kukiri kwa ShimonPeres kwamba utawala waKizayuni wa Israel ulihusikana mauaji ya Yasir Arafat,kunaweza kuwapa haki yakisheria viongozi wa Palestinaya kuufungulia mashtakautawala huo haramu katikaMahakama ya Kimataifa yaJinai. (IRIB)

    TEHRANI r a n i m e z i n d u ahalikopta mpya ya kivitainayojulikana kamaToufan 2.

    H e l i k o p t a h i y oimezindul iwa kat ikahafla iliyohuduriwa naWaziri wa Ulinzi wa Iran,Brigedia Jenerali AhmadVahidi.

    Akizungumza wakati

    wa hafla hiyo, Bw. Vahidia m e s e m a h e l i k o p t ahiyo ni ya kizazi kipyacha helikopta za kivitana imetengenezwa kwakutumia teknolojia yakisasa kabisa, ikiwana uwezo mkubwa wakulenga shabaha.

    Amesema helikoptahiyo iliyotengenezwanchini humo ni ishara yaubunifu na kujitegemeaIran licha ya kuwepovikwazo vya maadui.

    W a k a t i h u o h u o ,Jeshi la Wanamaji la

    Jamhuri ya Kiislamu yaIran limesema mazoeziyake yamemalizika kwamafanikio.

    Mazoezi hayo ya sikusita yalianza 28 Desemba,na yamefanyika katikaeneo pana la fukweni,baharini na angani kwenyelango la Hormuz, Bahariya Oman, kaskazini mwaBahari ya Hindi, Ghubaya Aden na lango la BabulMandab.

    Msemaji wa mazoezih i y o , A d m e l i A m i r Ras tegar i , amesemamalengo ya mazoezi hayoyamefikiwa kikamilifukama ilivyopangwa.

    M a z o e z i h a y oyalijumuisha nyambizi,manowari, makombora,ndege zisizo na rubani,ndege za upelelezi na vitavya kielektroniki.

    W a k u u w a J e s h iW a n a m a j i l a I r a nw a m e s i s i t i z a k u w amazoezi hayo ya kijeshiyana ujumbe wa urafikina udugu kwa mataifarafiki na onyo kali kwamaadui.

    Iran yazinduahelikopta

    mpya ya kivita DEHLK I T A B U C H AQurani na vitabvya fasihi ya Kiislamvimekuwa ndivyvitabu vinavyouzwkwa wingi zaidi katiktamasha la vitabnchini India, amballimefanyika katikmji wa Vijaywadk a t i k a j i m b o l

    Andhra Pradesh.Tovuti ya The Hindu

    imeripoti kuwa kusomna kuelewa Qurani nvitabu vya fasihi vyKiislamu, ilikuwa kazngumu kwa wananchwa India kutokana nvitabu hivyo kuandikwkwa lugha za KiarabuKifarsi na Urdu.

    Hata hivyo tamashla vitabu la Vijaywadalimepunguza kwa kia

    kikubwa tatizo hilkwa kuuza nakala zQurani na vitabu vyfasihi ya Kiislamu kwlugha za Kiingereza nTelgu.

    Was imamiz i wtamasha hilo wanasemk u w a t a r j u m i yQurani Tukufu kwlugha za Kiingereza nTelgu zinauzwa kwwingi zaidi kulikvitabu vingine katikmatamasha hayo.

    Baada ya Quranv i t a b u v i n g i nvinavyouzwa zaidi nvile vinavyozungumzimaisha ya MtumMuhammad (saw)swala na MwenyezMungu SW, wanawakkatika Uislamu nQurani ya Sayansi.

    Tamasha la vitabu lVijaywada hufanyikkila mwaka kuanziJanuari Mosi hadi 1(IQNA)

    Qurani kitabukinachouzwa

    kwa zaidi India

  • 7/29/2019 ANNUUR 1054.1.pdf

    6/7

    6AN-NUU

    RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 20Makala

    JANUARI 12, mwaka2013 tumeadhimisha

    Sikukuu ya Mapinduziya Zanzibar. Historia yaMapinduzi ya Zanzibar,kama ilivyo historia yaharakati za kupiganiauhuru wa Tanganyika,i m e p o t o s h w a k w akiasi kikubwa na watuw a s i o i t a k i a m e m aZanzibar.

    Watanzan ia weng ihawafahamu ukweli kuhusuMapinduzi ya Zanzibar.Hawajui jinsi Mfumo- Kristo ulivyosimamiaM a p i n d u z i h a y o n a

    baadaye Muungano waTanganyika na Zanzibar.Fuatana na mchambuziwako Said Rajab.

    Ni mia ka ya h iv ikaribuni tu ndiyo utafitikuhusu Uislamu katikaeneo la Afrika Masharikiu m e a n z a k u w a v u t i awanazuoni na watafitiwa kisasa. Lakini wengiwao, walipuuza vita vyaMsalaba dhidi ya UislamuAfrika Mashariki, hususanZanzibar. Ilipuuzwa kwa

    sababu migogoro ya kidinikama hii ilionekana ni yaMashariki ya Kati, ingawaukweli ni kwamba vita vyamsalaba (crusade) dhidi yaUislamu inaweza kuwepokwenye nchi yoyote yaWais l amu, Zanz ibar ikiwemo.

    Ama kuhusu crusadeya Wakatoliki Zanzibar,Nyerere alifanyakazi kwakaribu sana na OscarKambona, mwandani wakena mwanafunzi mwenzakekatika Chuo Kikuu cha

    Edinburgh, Scotland,ambapo mwaka 1910,mkutano wa pili wa WCC(World Conference ofChurches) Kongamano laDunia la Makanisa, ulijadilitishio la Uislamu AfrikaMashariki. Ilikubaliwakwa kishindo kwambaMwafrika Mkristo ni mzurizaidi (kwa uongozi) kulikoMwafrika Muislamu. Kwahiyo Nyerere alipewakila aina ya msaada ili

    Mapinduzi ya Zanzibar, ilikuwa ni CrusadeNa Said Rajab

    aupige vi ta UislamuAfrika Mashariki, baadaya kuondoka kwa Ukoloniwa Uingereza.

    Wakati Tanganyikailipopata Uhuru wakem w a k a 1 9 6 1 , J o m oKenyatta wa Kenya, MiltonObote wa Uganda na Julius

    Nyerere wa Tanganyikawalifanya Mkutano mzitoji j in i Nair obi Juni 5,mwaka 1963. Katika njamahii ya viongozi Wakristo,Zanzibar haikuwakilishwawala kutajwa kwenyemkutano huu. Viongozihawa, kwa kauli moja,walitangaza kushirikianakikanda, chini ya msukumowa Umajumui wa Kiafrika(Pan Africanism):

    Sisi (Nyerere, Obotena Kenyatta), viongozi

    wa watu na Ser ikal iza Afr ika Mashar iki(i.e.Tanganyika, Ugandana Kenya)...tumejifungakuunda shi r ikisho lakisiasa la Afrika Masharikina tunasukumwa zaidina Uafrika na wala siyomaslahi ya Kikanda (p.1)

    W a k a t i Z a n z i b a r ilipopata uhuru wake,Desemba 10, mwaka1963 kutoka Serikaliya Uingereza, ikawa nimwanachama wa Jumuiya

    ya madola. Ikajiungana Umoja wa Mataifa,Desemba 16, mwaka 1963na iliwakilishwa na baloziHilal bin Muhammed binHilal.

    Lakini, wakati Serikalim p y a y a Z a n z i b a r i l ipotangaza muundo

    unaofanana na Dola yaKiislamu, Makrusedawa Kiafrika wa Kikristo,wakaanza kupiga kelelekwamba Ser ikal i i lei t apand ik iza Uarabuna Uislamu Zanzibar.Wakaivamia Zanzibarusiku wa manane waJanuary 11, mwaka 1964,chini ya Field Marshallaliyejipachika mwenyewecheo hicho, John Okello,ambaye ni mpiganajiw a K i k r i s t o k u t o k a

    Uganda. Malengo hasa yaMapinduzi ya Zanzibaryalikuwa ni Vita dhidiya Uislamu kama Okellomwenyewe alivyobainishandani ya kitabu chake,Revolution in Zanzibar (Mapinduzi Zanzibar),kwamba Mungu alimteuakufanya Mapinduzi yalekwa ajili ya Ukristo. Nakisha akanukuu kifungukifuatacho cha Bibliakuhalalisha alichofanya:

    Na sasa sikil izeni

    enyi matajiri! Lieni nakuomboleza kwa sababuya taabu zitakazowajieni.Mali zenu zimeoza, nanguo zenu zimeliwa nanondo. Dhahabu yenu nafedha vimeota kutu, nakutu hiyo itakuwa ushahididhidi yenu, nayo itakula

    miili yenu kama vile moto.Ninyi mmejilundikia malikatika siku hizi za mwisho!Hamkuwalipa mishaharawatumishi waliofanya kazikatika mashamba yenu.Sikilizeni malalamiko yao!Kilio cha hao wanaovunamashamba yenu kimefikamasikioni mwa Bwana,Mwenye Nguvu. Mmeishid u n i a n i m a i s h a y akujifurahisha na ya anasa.Mmejinenepesha tayarikwa siku ya kuchinjwa.

    Mmemhukumu na kumwuamtu asiye na hatia, nayehakuwapigeni (James5:1-6)

    Okello pia amebainishakwamba WapiganiaUhuru wake wametokaTangany ika , Kenya ,U g a n d a , R h o d e s i a(Zimbabwe), Nyasaland(Malawi) na Msumbiji.Waliua Waislamu 13,635n a w e n g i n e 2 1 , 4 6 2waliwekwa kizuizini.January 11, mwaka 1964,

    Okel lo al iwaamrishM a k r u s e d a k w a m bWaarabu wote (Waislamuwalio na umri kati ya miak

    18 na 55 lazima wauawSiku iliyofuata, mauaya Waislamu yakaanzn a O k e l l o a k a s e mhaya kwenye Redio yZanzibar:

    Mimi ni Field MarshalOkello! Enyi Mabeberuhakuna tena Serikali yMabeberu katika visiwhivi. Hii sasa ni Serikaya Wapigania UhuruAmkeni enyi watu weusKila mmoja wenu achukubunduki na risasi na kuanzkupigana na masalia yoya ubeberu katika visiwhivi (p.143).

    Asubuhi ile ile, Okelakatoa agizo kwa Jamshbin Abdullah bin Khalifa(1963-1964), Sultan wZanzibar: Umepewdakika ishirini tu za kuuwatoto wako na wake zakna kisha ujimalize wewmwenyewe. Revolutioin Zanzibar (p.145).

    Lakini hata hivyo, Sultawa Zanzibar alifanikiwkutoroka kupitia Mombas

    Kenya.W a a f r i k a w a l i o k

    Tanganyika walisaidsana kuipindua Serikaya Zanzibar ambapMakruseda walikuwa nsilaha bora za kisasa kutokKenya na TanganyikZaidi ya Makruseda 60waliivamia Zanzibar usikwa kuamkia January 12mwaka 1964. Keith KylMwandishi wa Habari wUingereza katika eneo Afrika Mashariki, aliandikmakala zake mbili kwenygaze t i l a Spec ta toGideons (Okello) Voicesiliyochapishwa February mwaka 1964 na How happened iliyochapishwFebruary 14, mwak1964 anasema baadhi yWakristo katika Serikaya Tanganyika walihusikkatika Mapinduzi (Vita vyMsalaba) ya Zanzibar

    Inafahamika vizukwamba mauaji yalikuw

    Inaendelea Uk.

    MWALIMU Julius Kambarage Nyerere (kushoto)

  • 7/29/2019 ANNUUR 1054.1.pdf

    7/7

    7AN-NUU

    RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 201Makala

    Mapinduzi ya Zanzibar, ilikuwa ni CrusadeInatoka Uk. 6

    ya kutisha mno kiasikwamba Waislamu 100waliuawa kwa kuokwa

    kwenye tanuri kama mikatekule Bambi. Abeid Karume(1905-1972, akawa Raiswa kwanza wa Jamhuri yaWatu wa Zanzibar. Karumealifanya mazungumzo yasiri na Rais wa Tanganyika,Julius Nyerere kuhusukuiunganisha Zanzibar naTanganyika.

    Hali kama hii iliyotokeaZanzibari, iliwahi kutokeavisiwa vya MindanaoU f i l i p i n o , D o l a y aKiislamu iliyoanzishwana Sultan Sayyid bin AbuBakr al - Hadhramy zaidiya miaka 400 kabla yaKanisa Katoliki halijaingiaUfilipino na Tanganyika.

    S i k u m o j a b a a d aya Crusade visiwaniZanzibar , Umoja waVijana wa KANU, chamakilichokuwa kinatawalaKenya wakati ule, ulifanyamkutano wa dharura jijiniNairobi. Katika Mkutanohuu, azimio la kupongezakuangushwa kwa utawalawa Zanzibar lilipitishwa

    bila kupingwa. Azimiohilo lilifuatiwa na kikaocha siku mbili cha Barazala Mawaziri wa Kenya,kilichoitishwa na Ofisiya Waziri Mkuu. Kikaohicho pia kilihudhuriwana Waziri wa Mambo yaNje wa Tanganyika, OscarKambona, ambaye piani mjumbe wa Baraza laMakanisa Duniani (WCC).Alikuwepo pia Waziri waNchi wa Uganda GeorgeMagezi, wakati JosephMarumbi, Waziri wa Nchina Mambo ya Nje wa Kenyaalikuwa akiwasiliana naZanzibar kwa simu wakatiwote. Alikuwa akiwasilianana Ed ing ton Kisas i ,Mkatoliki kutoka Moshinchini Tanganyika, ambayealikuwa Superintendentw a P o l i s i Z a n z i b a r aliyewekwa na Waingereza,ambaye baadaye akawaKamishna wa kwanza waPolisi Zanzibar baada yaCrusade ya Zanzibar

    VICTOR Okello

    kufanikiwa. Mkutano ulewa Baraza la Mawaziri,uliolenga kujadili matokeo(aftermath) ya Crusade piaulihudhuriwa na Balozi waUingereza nchini Kenya,vikosi vya Uingerezavilivyopo Kenya na Mkuuwa Jeshi la Polisi, R.CCating.

    Ndani ya siku mia moja zakwanza baada ya Crusadevisiwani Zanzibar, Nyererealikula njama na viongozimashuhuri wa KikristoAfr ika Mashar iki namabeberu wa Magharibikuhusu Muungano waTanganyika na Zanzibar.Njama hii ilikuwa muhimumno kiasi kwamba Serikaliya Marekani iliyokuwaik iongozwa na Ra i sLyndon Johnson (1963

    - 1969), ikaipa Zanzibarkipaumbele cha juu katikaSera ya Nje ya Marekani,ukiondoa Vietnam naCuba wakati ule. WilliamAttwood, aliyekuwa baloziwa Marekani nchini Kenyaalisema kwamba: TheWestern powers prepareda contingency plan in casethe Union would fail...and (after the union), thelaws of Tanganyika wouldbecome supreme to roundup (Muslim) radicals inZanzibar.

    T a f s i r i : M a t a i f amakubwa ya Magharibiyalishaandaa mpangokabambe iwapo Muunganohuo ungeshindikana...na(baada ya muungano)sheria za Tanganyika ndizozingetumika kuwadhibiti

    w a k o r o f i v i s i w a n iZanzibar

    Pia Waziri wa Mamboya Nje wa Marekani,Dean Rusk alitoa witokwa mataifa ya Magharibi:

    It is essential for Nyerereto be given the maximumsupport from the West(Ni muhimu sana kwaNyerere kupewa kilamsaada atakaohitaji kutokamataifa ya Magharibi).

    Kwa h iyo , waka t iN y e r e r e a l i p o e n d aZanzibar April 22, mwaka1 9 6 4 k u m s h i n i k i z aKarume kuhusu kuunganana Tanganyika, tayarialishapeleka askari wake

    Zanzibar, January 1mwaka 1964 wakiwna silaha nzito kwa kikilichoelezwa kama sababza kiusalama, baada ykushauriana na OkelloMwandishi Martin Baileamemnukuu Nyererwaka t i a l ipohu tub imkutano wa hadhara jijinDar es Salaam, Novemb15, mwaka 1964:

    Tulituma Polisi wetZanzibar. Baada ya kuvukmatat izo mbal imbatuliungana. Sisi wenyewkwa hiyari yetu tulikubakuungana. Karume nMimi tulikutana. Siwawili tu tulikutanaWakati nilipotaja suala Muungano, Karume hahakufikiria mara mbilAlinitaka palepale kuitishmkutano wa Waandishwa Habari na kutangaznia yetu. Nilimshaukusubir i k idogo kwsababu ilikuwa mapemmno kwa waandishi whabari kufahamishwa

    Ni ukweli usiofichikkwamba mapinduzi yZanzibar yalisimamiwn a h a y a t i M w a l i mNyere re kwa maslahya Mfumo Kristo zaidkuliko Wazanzibar. Kupit

    Mapinduzi hayo, Zanzibimepoteza haiba yake yKiislamu na mamlaka yakya Dola kwa Tanganyiktangu April 26, mwak1964.

    Wataendesha semina fupi elekezi juu ya utoaji na ugawaji wa

    Zaka.Aidha, semina hiyo itakwenda sambamba na zoezi la ugawaji wa

    Zaka kwa baadhi ya kinamama wajane wa Kiislamu na wanafunzi

    waliochaguliwa kupitia Misikiti yao.

    MUDA: SAA 2:30 ASUBUHI - SAA 6:45 MCHANA

    SIKU: ALHAMISI TAREHE 24/01/2013

    UKUMBI: Lamada Hotel

    Kwa mawasiliano piga namba: 0716 776226, 0754 654900

    Jumuiya ya Wanataaluma wa Kiislamu Tanzania

    (TAMPRO) kwa kushirikiana na Jumuiya ya

    Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania (HAIYA)