MIFANO YA KRISTOkatika Agano la Kale
par W. A. Deans
EVERYDAY PUBLICATIONS INC.
310 Killaly Street West
Port Colborne, ON
Canada L3K 6A6Copyright © 1973 Everyday Publications Inc.
ISBN 978-88873-139-5
Publié originalement parEditions Evangéliques,
Nyankunde, Bunia, D.R. Congo
Imprimé au Canada
Copyright © 1973 Everyday Publications Inc.
MAMBO YALIYO KITABUNI
UkurasaTangazo 5
Adamu, Mfano wa Kristo 7
Adamu (Sehemu ya pili) 9
Damu iliyovuja kwa Edeni 11
Kondoo ya Abeli 13
Safina ya Noa 15
Melkisedeki 18
Isaka (na Kondoo) 21
Yosefu 24
Kondoo ya Pasaka 26
Mana, Mkate toka Mbingu 29
Mwamba uliopasuka 32
Nyoka ya Shaba 35
Hema Takatifu 38
Mlango Mmoja 39
Mazabahu ya Shaba 40
Birika la Shaba 42
Kinara cha Zahabu 45
Meza ya Mkate wa Onyesho 47
Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49
Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51
Kuhani Mkubwa na Mavazi Matakatifu 54
Daudi na Kristo 57
Jumlisho 60
Copyright © 1973 Everyday Publications Inc.
4 MIFANO YA KRISTO
Mazabahu ya shaba, ona ukurasa 41.
Mazabahu ya kuchomauvumba, ona ukurasa 51.
Kinara cha zahabu, ona ukurasa 47.Copyright © 1973 Everyday Publications Inc.
TANGAZO
Biblia ni maandiko ambayo Mungu aliletea watu. Ina vitabu 66
ndani yake, vilivyo katika sehemu kubwa mbili. Sehemu hizi, ndizo
Agano la Kale na Agano Jipya, zinafungana kuwa moja. Sehemu moja
ya Biblia inatusaidia kufahamu sehemu ya pili.
Agano la Kale liliandikwa zamani sana, mbele ya kuzaliwa kwa
Bwana Yesu Kristo. Watu watakatifu waliongozwa na Roho Mtakatifu
kuandika maneno Mungu aliyotaka kujulisha watu.
Hata Agano la Kale liliandikwa mbele sana ya kuzaliwa kwa
Bwana Yesu, lina mifano mingi juu yake inayofanana naye katika
maisha yake, mauti yake, ufufuko wake, utumishi wake wa sasa na
utakatifu wake wa nyuma.
Kuna unabii kupasha habari za mambo yatakayotukia nyuma,
kutabiri vitu visivyotukia bado. Agano la Kale lina unabii juu ya Kristo
na vilevile mifano mingi ya ajabu juu yake. Mifano hii inaonekana
ndani ya maisha ya watu wa zamani, na katika mambo yaliyotukia juu
ya Waisraeli. Vilevile katika mambo ya hema ya kusanyiko jangwani
kuna maana nyingi za faida sana kueleza uzuri wa Kristo na utumishi
wake.
Mara nyingine matukio haya ya nyakati za zamani yanaonyesha
mifano ya Kristo waziwazi. Mara nyingine yanaonekana kama vivuli
kuonekana nusu nusu. Ni kama kivuli cha mtu kinachoonekana mbele
ya kufika kwake mwenyewe, kueleza namna yake kwa sehemu tu, si
wazi sana.
Kwa kuyafahamu kabisa tunahitaji kusoma Agano Jipya. Pale
mara nyingi maelezo ya mifano yanaonekana wazi kutufunulia maana
zao kabisa. Hivi tutatafuta mfano wa Kristo katika Agano la Kale, ha-
lafu tutapeleleza katika Agano Jipya kupata mashairi kueleza maana
yake.
5Copyright © 1973 Everyday Publications Inc.
Tutatumika na Biblia nzima pamoja na kitabu hiki kwa kufahamu
haki ya Mwokozi Yesu. Tuombe Mungu atuonyeshe Kristo katika mi-
fano hii. Tutashangaa na raha kwa kuona namna Agano la Kale linavy-
ofungana pamoja na Agano Jipya kutufunulia uzuri wa Kristo na
damani ya matendo yake.
Kama ukipenda Bwana Yesu na moyo wako, na ukiamini Neno
lake kabisa, utapata furaha kwa kusoma maelezo ya kitabu hiki.
Utajifunza maneno mengine mengi juu ya Mwokozi wako ambaye
unapenda.
Soma mashairi haya katika Biblia yako. Pale utafahamu Maandiko
Matakatifu yalitolewa na Mungu kwa njia ya mitume yake. Hata ma-
nabii ya zamani walitabiri juu ya Yesu. Soma mashairi haya :
2 Timoteo 3:16; 2 Petro 1:20-21; Yoane 8:56; Yoane 5:39,46; Zaburi
40:7; Waebrania 10:7; Matayo 22:45
6 MIFANO YA KRISTO
ADAMU, MFANO WA KRISTO
(Mwanzo 1:26-28 ; 2:7,8,15)
Mbele ya kusoma juu ya Adamu kwa kitabu cha Mwanzo kwa Agano
la Kale, tutakumbuka kwamba hata kwa Agano Jipya tunasoma ya
kuwa Adamu alikuwa mfano wa Kristo atakayekuja (Waroma 5:14).
Kufanana kwake kuna tofauti vilevile.
Pale kwa kitabu cha Mwanzo (1:26-28; 2:7,8,15), tunaona Adamu
alikuwa umbo wa kwanza katikati ya watu. Mungu alimwumba na
mavumbi ya udongo, akafulisha pumuzi ya uzima puani mwake.
Adamu alikuwa nafsi ya uhai.
Kwa Agano Jipya tazama kwa 1 Wakorinto 15. Shairi 45 linasema
Adamu alikuwa umbo wa kwanza wa watu, mtu wa kwanza. Yeye
ndiye kichwa cha umbo wa kwanza.
Shairi 47 linaita Kristo “mtu wa pili.” Yeye ndiye kichwa cha
umbo mpya.
Mtu wa kwanza (Adamu) ni yule wa asili. Mtu wa pili ni yule wa
roho. Mtu wa kwanza (Adamu) alitoka katika dunia, mwenye udongo.
Mtu wa pili ni Bwana aliyetoka mbinguni (1 Wakorinto 15:47-48).
Hivi Adamu anafanana na Yesu kwa mfano, lakini kuna tofauti
vilevile.
Adamu alifanywa katika sura ya Mungu (Mwanzo 1:26). Kristo ni
sura ya Mungu asiyeonekana (2 Wakorinto 4:4; Wakolosayi 1:15)
kwani yeye ni Mungu mwenyewe katika mwili (1 Timoteo 3:16).
Adamu aliitwa Adamu wa kwanza. Kristo ni Adamu wa mwisho.
Kwa kuzaliwa kwa mwili sisi tulichukua sura (na tabia) ya Adamu wa
kwanza. Lakini kama tukizaliwa mara ya pili kwa Roho, kwa imani
katika Kristo, tutachukua sura ya Adamu wa mwisho. Tulivaa sura ya
mtu wa udongo, lakini katika Kristo tutavaa sura ya Mtu wa mbingu
7
(1 Wakorinto 15:45-49). Soma vilevile 1 Yoane 3:2; Wafilipi 3:20-21.
Bwana Yesu alisema na Nikodemo, “Ila mtu azaliwe mara ya pili
hawezi kuona ufalme wa Mungu.” Na tena, “Kilichozaliwa kwa mwili
ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. Usishangae kwa sababu
nilikuambia, Sharti muzaliwe mara ya pill” (Yoane 3:3,6,7).
Katika Adamu tunariti hukumu ya mauti. Sisi tunaoamini Kristo
tunapata uriti wa uzima wa milele.
Angalia sasa katika Waroma. Tusome kwa Sura 5. Anza na shairi
15 mpaka 19. Katika mashairi haya tunaona maneno matano. Tunap-
ata katika:
1. Mtu mmoja (Adamu) KOSA na KUFA sh. 15
Mtu mmoja (Kristo) NEEMA na ZAWADI
2. Mtu mmoja (Adamu) HUKUMU na AZABU sh. 16
Mtu mmoja (Kristo) ZAWADI ya neema
(kuhesabiwa haki)
3. Mtu mmoja (Adamu) MAUTI sh. 17
Mtu mmoja (Kristo) UZIMA
4. Kwa kosa la mtu mmoja (Adamu) sh. 18
— watu wote walihukumiwa
Kwa tendo (msalaba) moja la haki (la Kristo)
— watu wote walipewa haki yenye uzima
5. Kwa kuasi kwa mtu mmoja (Adamu) sh. 19
— hali ya wenye zambi
Kwa kutii kwa mtu mmoja (Kristo)
— haki ya Mungu inapatikana
8 MIFANO YA KRISTO
ADAMU
(Sehemu ya pili)
KUPATA MKE
Tunaendelea sasa kuonyesha namna Adamu alifanana na Kristo.
Mungu alimpa mke wake. Vivyo hivyo, Mungu alimpa Kristo Kanisa
kuwa mke wake.
Adamu alikuwa pekee katika shamba la Edeni. Nyama walikuwa,
na ndege, lakini msaidizi kwaye hakuwa. Mungu alisema, “Si vema
mtu awe peke yake; nitamfanyia msaidia anayefaa kwake” (Mwanzo
2:18).
Mungu akalalisha Adamu na usingizi, akaondosha mfupa mmoja
toka mbavu, akafunga mwili wake tena. Kwa ule mfupa Mungu aka-
jengea Adamu mke wake. Akampa kwa Adamu. Tazama Mwanzo 2:20-
22.
Adamu akasema, “Huyu sasa mfupa wa mifupa yangu, na nyama
ya nyama yangu; akaitwa Mwanamke kwa maana aliondoshwa katika
mume” (Mwanzo 2:23).
Vile kwa Kanisa, mke wa Kristo. Kwa njia ya usingizi mzito
(ndiyo mauti) Kristo alipata mke. Yeye alitobolewa, akakufia wenye
zambi. Juu ya kuumia kwake na mauti yake, Mungu amempa Kanisa.
Kanisa ni mwili wa Kristo — mifupa yake, mikono yake. Kristo
ni kichwa chetu, sisi tuko viungo vya mwili wake (Waefeso 1:22-23;
1 Wakorinto 12:27).
Kwa sura ya mbegu tunasoma kwa Yoane 12:24 juu ya kufa kwa
Kristo. Namna mbegu, ikibaki na uzima, inabaki pekee. Lakini ikain-
gia udongoni, ikakufa, inatoa mavuno ya mbegu nyingi. Kanisa lina-
toka ndani ya mauti ya Kristo na ufufuko wake.
9
Kristo alipenda Kanisa na alijitoa kwa ajili yake (Waefeso 5:23-27).
Hivi Kanisa ni bibi ya Kristo, ndio watu walioletwa kwake na Baba
yake (Yoane 17:24).
KUTAWALA
Mungu aliwapa Adamu na mke wake ruhusa kutawala juu ya
kila kiumbe kilichokuwa hai. Adamu alifuga nyama zote (Mwanzo
1:26-28).
Kristo anatolewa enzi. Atasimama Mfalme wa wafalme. Adui zake
watakuwa kiti cha miguu yake (Ufunuo 11:15; Zaburi 72:8; Zekaria
9:10) .
Enzi yake itaenea duniani pote. Atatawala na fimbo ya chuma.
Mke wake, ndilo Kanisa, atatawala pamoja naye (Ufunuo 2:26-27;
3:21; 20:6). Kila kiumbe kitawekwa chini ya enzi ya Kristo (Zaburi
8:3-9). Kila ulimi utakiri ya kuwa Yesu ni Bwana kwa utukufu wa
Mungu Baba (Wafilipi 2:9-11).
Utawala wa Adamu shambani la Edeni unafanana na utawala wa
Kristo duniani pote.
10 MIFANO YA KRISTO
DAMU ILIYOVUJA KWA EDENI
Mungu alimpa Adamu ruhusa kula matunda yote ya shamba la Edeni
ila tunda la mti mmoja. Mti ule uliitwa “mti wa kujua uzuri na ubaya.”
Mungu alisema kama wakiasi wakikula tunda la mti ule, watakufa
(Mwanzo 2:9, 17).
Shetani alifika mbele ya Hawa, mke wa Adamu, kumjaribu. Ali-
fika na mwili wa nyoka, kusemezana na lugha ya watu. Alizarau
masemo ya Mungu na agizo lake. Alijaribu Hawa ale tunda hili.
Hawa alifahamu agizo la Mungu. Alisema na nyoka, “Mungu
amesema: Musile (matunda) yake wala musiyaguse, musife” (Mwanzo
3:3).
Lakini Shetani alidanganya Hawa. Mke yule akatazama matunda
ya ule mti, akayatamani, akachukua ya matunda yake, akampa mume
wake vilevile pamoja naye (Mwanzo 3:6). Wao wote wawili waka-
anguka kufanya zambi. Hawa alidanganywa, Adamu alikula na kusudi
(1 Timoteo 2:14).
Ahadi ya Mungu juu yao ilikuwa hivi: Mukikula, mutakufa. Sasa
Adamu na Hawa wanatambua ya kuwa walikuwa watupu. Wakatafuta
njia ya kujifunika kwani waliogopa Mungu. Wakashona majani kuvaa.
Wakajificha, Mungu asiwakute. Walikuwa wenye zambi.
Kisha Mungu aliwatafutatafuta. Akawakuta, wakifichama katikati
ya miti ya shamba. Kwa kukiri zambi yao mbele ya Mungu, Adamu
alichongea mke wake. Hawa alichongea nyoka. Sasa hukumu inawa-
ngojea.
Lakini kwa neema yake Mungu aliwapatia njia ya ukombozi.
Mauti waliyostahili kupata iliangukia nyama waliochinjwa na Mungu.
Damu ilivuja katika Edeni! Hivi Mungu aliwavalisha na mavazi ya
ngozi. Yeye mwenye huruma aliwapa njia ya ukombozi.
Pale tunapata mfano mwingine wa Kristo. Ngozi hizi zilipatikana
11
kwa njia ya mauti ya nyama. Damu ya ukombozi ilimwangika. Majani
waliyoshona kuwa mavazi hayakutosha. Kisha, Mungu aliwavalisha
na ngozi. Wakati Mungu alipotazama Adamu au Hawa, aliona alama ya
ukombozi, ukumbusho wa damu. Hivi, hata walihukumiwa kwa njia ya
kulima na jasho na mke kuzaa na taabu, hata walifukuzwa toka Edeni,
mauti iliwekwa kando kwa ajili ya damu. Walipata wakati wa kuishi
mbele ya kufariki, lakini Mungu aliwazuiza wasiingie tena shambani
kula tunda la uzima. Hawakustahili tena (Mwanzo 3:24).
Wenye zambi leo wanajaribu kubembeleza Mungu na majani ya
matendo yao, wakiwaza wataponea hukumu ya mauti. Lakini “Msha-
hara wa zambi ni mauti” (Waroma 6:23). Soma vilevile Ezekieli 18:20,
“Nafsi inayofanya zambi itakufa.”
Mungu ametengeneza njia ya wokovu! Mwana wake, Yesu Kristo,
kama nyama katika Edeni, alikufa kwa ukombozi kwa wenye zambi.
Damu yake ilivuja kulipa deni ya zambi. Mtu anayetaka kuokolewa,
apokee Yesu kuwa Mkombozi wake. Hivi atapatana na Mungu kwa
salama.
12 MIFANO YA KRISTO
KONDOO YA ABELI
(Mwanzo 4:1-15)
Mzaliwa wa kwanza duniani alikuwa mwuaji. Kaina, mwana wa
kwanza wa Adamu na Hawa, aliua Abeli, mdogo wake.
Wakati Adamu na Hawa walipokosa katika Edeni, walijaribu ku-
ficha utupu wao na majani ambayo walishona. Lakini Mungu haku-
kubali matendo yao kufunika zambi. Alitaka damu kumwangika. Hivi
walifunikwa na ngozi za nyama za ukombozi.
Watoto wao, ndio Kaina na Abeli, walijua lazima damu ivuje kwa
kupata salama na Mungu. Tusiwaze ya kwamba Kaina alikuwa mwenye
zambi kuliko Abeli. Wao wote wawili walikuwa wenye zambi, walihitaji
usamehe.
Tofauti katikati yao ilikuwa namna ya matoleo yao. Kwa
kuwakubali au kuwakataa, Mungu alitazama matoleo yao.
Kaina alichagua matunda ya udongo kuwa sadaka mbele ya
Mungu. Lakini udongo ulilaaniwa (Mwanzo 3:17); toleo haliwezi ku-
toka pale. Lilifanana na majani Adamu aliyoshona kujaribu kufunika
utupu wake kwa Edeni. Hayakufaa. Ilikuwa sadaka pasipo damu.
Hata Kaina aliwaza ya kuwa mboga, matunda, maua ya umalidadi
yataweza kupendeza Mungu, hakukuwa vile. Hata alifikili Mungu ata-
furahia matunda ya kazi yake ya mlimaji, alianguka kwa mawazo. Njia
moja kufikia Mungu ilikuwa njia ya ukombozi, njia ya damu.
Abeli alikuwa mlinzi kondoo. Akachukua mwana-kondoo katika
kundi kuchinja sadaka mbele ya Mungu. Akamtoa pamoja na mafuta,
zabihu kwa Mungu.
Mungu hakutazama Kaina wala Abeli. Macho yake yalipita juu
ya sadaka. Mungu alikubali zabihu ya Abeli, yenye damu. Mungu
alikataa toleo la Kaina lisilo na damu (Mwanzo 4:4-5).
13
Kaina alikataliwa kwa ajili ya sadaka isiyofaa. Alikosa imani; ali-
jaribu kufikia Mungu kwa njia ambayo alitunga mwenyewe.
Abeli alikubaliwa kwa ajili ya sadaka ya kumpendeza Mungu.
Alitoa zabihu ya damu, kwa imani (Waebrania 11:4).
Mungu akahamakia Kaina, akamwonyesha njia ya kupokelewa. Ni
kutoa sadaka ya kufaa apate usamehe; kama sivyo, zambi itabaki
(Mwanzo 4:7).
Lakini Kaina hakutaka. Akaamukia ndugu yake, akamwua. Mungu
akamwekea chapa. Kaina akatoka kutangatanga duniani, kujulikana
kuwa mwenye zambi pahali po pote.
Kondoo ya Abeli ni mfano wa Kristo. Kristo ni kondoo safi ya
Mungu. Wakati Yoane Mbatizaji alipoona Yesu akikuja kwake,
akasema, “Tazama Mwana-kondoo wa Mungu anayechukua zambi ya
ulimwengu” (Yoane 1:29-30).
Kama mwana-kondoo anayepelekwa kuchinjwa, na kama kondoo
anavyonyamaza mbele yao wanaokata manyoya yake, Yesu hakufu-
ngua kinywa chake (Isaya 53:7).
Mwenye zambi leo anayetaka kupatana na Mungu, sharti awe na
imani juu ya sadaka ya Kristo msalabani. Damu ya Yesu, kama ya
mwana-kondoo, ni njia ya ukombozi, ndiyo njia ya usamehe kwa
zambi.
“Mumekombolewa, si kwa vitu vinavyoharibika ... lakini kwa
damu ya damani, kama ya kondoo asiye na kilema wala alama, damu
ya Kristo” (1 Petro 1:18-19).
Kama Mungu hakutazama Kaina au Abeli, lakini zaidi matoleo
yao, vivyo hivyo Mungu hatazami sisi, lakini sadaka ambayo tuna-
mtolea kwa kumkaribia.
Kaina akifika na matunda ya udongo, alikataliwa. Abeli akifika na
kondoo, akimwanga damu yake, alikubaliwa.
Sisi kujaribu kupendeza Mungu na matendo yetu ni bule. Lakini
kwa kuamini Yesu Kristo, Kondoo ya Mungu, aliyejitoa msalabani kwa
ajili yetu, tunapata usamehe wa zambi. Tutakubaliwa na Mungu kwa
milele.
14 MIFANO YA KRISTO
SAFINA YA NOA
(Mwanzo 6-9)
Ilikuwa watu hawajaona bado mvua duniani. Tangu mwanzo maji ya-
litoka katika chemchemi za udongo. Hivi watu walizihaki Noa wakati
alipowapasha juu ya hatari ya tufani. Walimchekelea wakati alipojenga
safina mbokani, mbali na mito ya maji.
Uovu ulizidi duniani. Mawazo ya watu yalikuwa mabaya tu siku
zote. Dunia iliharibika mbele ya Mungu (Mwanzo 6:5,11-13). Mungu
alisema, “Roho yangu haitashindana na mtu milele” (sh. 3). Alikusudi
kuharibu watu kwa garika ya maji. Alipasha ya kuwa watu na nyama
na ndege watazama, watakufa (Mwanzo 6:17).
Uovu wa dunia ya leo ni sawa. Watu hawataki kuogopa hukumu ya
Moto ambayo Mungu anayokusudi kuleta juu ya zambi.
Mungu aliwaza kuonyesha rehema kwa Noa, mtu wa haki. Noa
alitembea pamoja na Mungu, kama Enoka (Mwanzo 5:24; 6:8-9). Hivi
Mungu alitunga njia ya wokovu. Aliagiza Noa ajenge safina. Ali-
mwonyesha kipimo chake kwa urefu na upana na urefu juu. Alimwo-
ngoza kuweka dirisha moja juu, na mlango mmoja, kwa kuingia.
Alimwagiza kupakaa safina ndani na inje kwa lami (kama kasuku).
Noa alitii (Mwanzo 6:19-20).
Kwa wakati wa sasa, kama zamani, Mungu anatangaza njia ya
wokovu kwa neema, kwa watu walio katika hatari ya hukumu. Ana-
pasha habari ya Safina ya sasa, ndiye Kristo, pahali mwamini atakapo-
jificha na amani katika zoruba ya moto kwa kuja.
Noa alitangaza hatari ya hukumu kwa watu kwa wakati wake.
Alikuwa mhubiri wa haki (2 Petro 2:4-5). Alihubiri hukumu na
wokovu.
15
Noa na wana wake (Semu, Hamu na Yafeti) walidumu kujenga sa-
fina kubwa namna Mungu alivyowaagiza. Hata watu walizarau, Noa
alihubiri na alidumu kwa kujenga. Kazi ilitimia, ilikwisha.
Noa na jamaa yake, wote watu wanane, waliingia ndani ya safina,
kwa imani (Waebrania 11:7). Nyama namna zote na ndege wakaingia.
Mungu mwenyewe akawafunga ndani. Mlango ulifungwa (Mwanzo
7:16).
Kwa wakati wa sasa wahubiri wanatangaza hatari ya hukumu juu
ya zambi. Wanapasha habari ya kutokea kwa Mwana wa Mungu.
Lakini kama kwa wakati wa Noa, leo watu wanaendelea katika zambi.
Hawataki kupokea neema ya Mungu na kuingia ndani ya Kristo, Safina
yetu (2 Petro 2:5).
Basi, wakati Noa alipoingia ndani ya safina, mvua ikaanza kunye-
sha. Maji yalitokatoka katika udongo, chemchemi zilijaa. Udongo
ulianza kujaa na tufani kuwa garika kubwa ya kumeza dunia pia.
Watu waliokuwa wakizihaki, wale wasioamini, walibaki inje.
Walianza kukimbiakimbia juu ya vilima. Labda wengine waligonga
mlango wa safina, wakitaka kuingia. Lakini wakati wa wokovu uli-
kuwa umepita. Watu walikufa wote, na nyama zote, na ndege (Mwanzo
7:21-23). Wale waliokuwa ndani ya safina —watu na nyama na ndege
— walipona wote.
Tunaona safina ya Noa ni mfano wa Kristo. Watu walioingia ndani
ya safina waliishi kwa amani. Njia ya wokovu ilikuwa safina tu.
Haikuwa nyingine. Mlango ulikuwa mmoja tu kupata raha (Mwanzo
6:16; Yoane 10:9).
Safina ilipokea uzito wa tufani juu yake. Zoruba ilipiga na nguvu
lakini safina ilipata ukali wake; watu walioingia walipona pia. Kwa
hivyo Bwana Yesu amebeba hasira ya Mungu sisi tuliyostahilia kupata.
Gazabu ya hukumu ilimwangukia. Alitukomboa. Yeye ni Mkombozi
wetu. Kwa imani tunaishi kwa amani ndani yake, kwa milele.
Nyuma ya garika wakati maji ya tufani yalipoanza kupunguka, sa-
fina ilikwama juu ya Mlima Ararati. Wakatoka wote. Noa akajenga
mazabahu (Mwanzo 8:1-5). Akatoa sadaka za sifa mbele ya Mungu
(Mwanzo 8:20-22). Mungu akaweka upindi wa mvua winguni, alama
ya agano katikati ya Mungu na watu. Hataharibu tena dunia kwa maji
16 MIFANO YA KRISTO
(Mwanzo 9:8-17). Hukumu ya nyuma itakuwa kuharibu dunia kwa
moto (2 Petro 3:4-14).
“Kama lalo inavyoshuka upande mmoja wa mbingu na kungaa
hata upande mwingine wa mbingu, ndivyo Mwana wa watu
atakavyokuwa katika siku yake . . . Kama ilivyokuwa siku za Noa, ndi-
vyo itakavyokuwa siku za Mwana wa watu. Walikula, walikunywa,
walioa, waliolewa hata siku ile Noa alipoingia katika safina, na garika
ilifika ikawaangamiza wote” (Luka 17:24, 26, 27).
Safina ya Noa 17
MELKISEDEKI
(Mwanzo 14 :17-24)
Melkisedeki ni mfano wa Yesu Kristo, Mfalme na Kuhani Mkubwa.
Mtu yule aliishi zamani kwa wakati wa Abrahamu (Abramu). Alikuwa
mfalme wa Salemi (nyuma yake mji ule uliitwa Yerusalema). Alikuwa
vilevile kuhani la Mungu aliye juu (Mwanzo 14:18).
Melkisedeki alikuwa mtu, lakini Biblia haituonyeshi habari za
wazazi wake. Mambo ya kuzaliwa kwake na uzazi wake yalifichwa
kusudi awe mfano wa Kristo aliyezaliwa kwa ajabu, bila baba duniani
na mama bikira.
Soma maneno ya Melkisedeki katika Mwanzo 14:17-24. Wafalme
wane walipiga vita na wafalme watano (sh. 9), halafu wafalme wa
Sodomo na Gomora walikamatwa. Wafalme washindaji walichukua
mali zote za Sodomo na Gomora, na vyakula vyo vyote na watu. Wa-
likwenda vilevile na Loti, mwana wa ndugu ya Abrahamu, aliyekaa
katika Sodomo (mash. 10-12).
Abrahamu akasikia habari hizi, akakusanya watu wa nyumba yake,
na watumishi wake (wote watu 318), akafuata wale adui. Akawakuta,
akapigana nao, akawashinda. Kwa hivi Abrahamu alinyanganya mali
zote za nyara, na kurudisha Loti na mali zake na watu (mash. 13-16).
Kwa kurudi toka vita na nyara zake, Abrahamu alikutana na
Melkisedeki aliyetokea mbele yake. Yule mfalme wa Salemi, kuhani la
Mungu aliye juu, akatoa mkate na mvinyo. Melkisedeki akabariki
Abrahamu katika jina la Mungu aliye juu. Abrahamu akimpa zaka ya
moja ya kumi katika vyote alivyopata (sh. 20).
Vilevile mfalme wa Sodomo alitokea mbele ya Abrahamu. Ali-
mwambia arudishe tu watu, abaki na mali zote. Lakini Abrahamu
18
alikataa kupokea kitu kimoja mikononi mwa mfalme wa Sodomo, asi-
jisifu kusema alitajirisha Abrahamu (sh. 23).
Hivi Abrahamu alichagua katikati ya wafalme wale wawili:
Melkisedeki (mfalme wa Salemi, kuhani la Mungu aliye juu) na
mfalme wa Sodomo. Alichagua Melkisedeki. Alipokea zawadi yake na
baraka yake. Alitoa zaka yake kwake. Lakini alikataa zawadi za mfa-
lme wa Sodomo, mji mwovu.
Tunapata maelezo ya mfano wa Melkisedeki kwa Waebrania 6:20;
7:1-28. Angalia namna Kristo anavyofanana na Melkisedeki.
A. Kuzaliwa kwa Yesu ni ajabu. Maneno ya kuzaliwa kwa Melki-
sedeki yanafichwa. Baba na mama yake hawajulikani, wala mwanzo
wake au mwisho wake. Hivi alifanana na Yesu, Mwana wa Mungu,
aliyezaliwa kwa ajabu bila baba duniani, na mama yake bikira (Wa-
ebrania 7:3).
B. Kristo ni Mfalme. Melkisedeki alikuwa mfalme wa haki,
mfalme wa Salemi (maana mfalme wa Salama) (Waebrania 7:2). Kristo
ni Mfalme:
— Herode nyuma ya kuzaliwa kwa Yesu alimtaja “Mfalme wa
Wayuda” (Matayo 2:2).
— Manabii walitabiri (Matayo 21:4-5; Zaburi 2:8; Danieli 7:13-14)
— Pilato alimwuliza, “Wewe mfalme basi?” (Yoane 18:37; 19:14-
15)
— Mfalme wa wafalme (Ufunuo 17:14; 19:16; 1 Timoteo 6:15)
C. Kristo ni Kuhani Mkubwa kuliko (Waebrania 7:1-28). Kristo
alizaliwa katika kabila la Yuda, si katika kabila la Lawi lililotolewa
ukuhani (Waebrania 7:5,14). Haruni, kuhani mkubwa wa kwanza,
alikuwa Mlawi, na wote ambao walimfuata katika ukuhani walikuwa
Walawi.
Lakini Melkisedeki, kuhani la Mungu aliye juu, aliishi mbele ya
kuzaliwa kwa Lawi. Wakati Abrahamu alipojinyenyekeza mbele ya
Melkisedeki akitoa zaka kwake, ni kama Lawi atakayezaliwa kwa
uzazi wa Abrahamu. Alianguka mbele yake (ndani ya Abrahamu). Hivi
ni wazi, mkubwa alikuwa Melkisedeki, si Lawi. Soma Waebrania 7:2.
Melkisedeki 19
Mungu ametia Yesu Kristo kuhani kwa milele kwa daraja la
Melkisedeki (Waebrania 6:20; 7:17, 21). Makuhani wengine wanaku-
fakufa, lakini yeye anaishi milele kuombea watu wake (mash. 15-16).
D. Agano la Kuhani Mkubwa Kristo linapita agano la makuhani yaWalawi (Waebrania 7:22) :
— Kristo ni Mpatanishi wa agano linalosimamishwa juu ya ahadi
zinazozidi kwa uzuri (Waebrania 8:6)
— Ni Agano Jipya (Waebrania 8:7-8)
Makuhani wote wa daraja la Lawi walihitaji kutoa kwanza sada-
ka kwa zambi zao wenyewe. Lakini Kuhani Yesu Kristo hana
zambi. Alijitoa mara moja kwa ajili ya wenye zambi kutupatia
wokovu kwa milele (Waebrania 7:23-28).
— Hakuna ukumbusho tena wa zambi kamwe (Waebrania 8:12-
13; 10:17-18)
Soma vile Waebrania 10:9-18 kwa kupata shangwe juu ya kazi
kamilifu ya Mwokozi Yesu, ndiye Sadaka yetu, Kuhani Mkubwa wetu,
Mfalme wetu.
20 MIFANO YA KRISTO
ISAKA (NA KONDOO)
(Mwanzo 22:1-44)
Katika habari za Abrahamu na Isaka tunapata mfano wa Mungu
mwenyewe akikubali kutoa mwana wake wa pekee. Lakini vilevile tu-
napata mfano wa Kristo kwa kondoo ndume ambaye Mungu alimleta
kuwa mkombozi kukufilia Isaka.
Hivi tuseme tuna mifano miwili ya Kristo katika matukio ya ma-
neno ya sadaka ya Abrahamu wakati alipotii Mungu kwa kutoa mwana
wake kuwa zabihu ya kuteketezwa.
Tuanze kwanza juu ya Isaka, mwana mpendwa wa baba Abra-
hamu.
Katika Mwanzo 22, shairi 2, kitabu kinaita Isaka “mwana wako,
mwana wako wa pekee ambaye unampenda, hata Isaka.” Isimaeli,
mwana wa Hagari, Mungu hakuhesabu kwani ahadi yake kwa Abra-
hamu ilikuwa juu ya mwana wake wa utaratibu, ndiye Isaka. Alimwa-
giza kutoa mwana huyu wa ahadi kuwa sadaka ya kuteketezwa.
Abrahamu anafanana na Mungu Baba. Isaka anafanana na Yesu,
Mwana Mpendwa wake. (Tazama Marko 1:11). Abrahamu hakukataa
kuchinja mwana wake kuwa zabihu. Mungu Baba hakuachilia Mwana
wake, lakini alimtoa kabisa badala yetu sisi sote (Waroma 8:32).
Isaka, mtoto wa ahadi, anafanana na Kristo, mtoto wa ahadi. Soma
Mwanzo 17:16; Mwanzo 3:15; Isaya 7:14.
Kuzaliwa kwa Isaka kulikuwa ajabu, vile kuzaliwa kwa Kristo.
Abrahamu na Sarai walikuwa wazee. Wakati wa kuzaa ulipita
mbali (Mwanzo 18:13). Lakini yule mama mzee alichukua mimba,
akazaa mtoto wake wa kwanza.
Mastaajabu juu ya kuzaliwa kwa Kristo. Baba yake ni Mungu
mwenyewe. Roho ya Mungu alikuja juu ya Maria akiwa bikira, akazaa
Kristo bila kujua mwanamume.
21
Kuzaliwa kwa Isaka kulifuata utaratibu wa unabii. Vile Kristo
(Mwanzo 21:2; Wagalatia 4:4).
Jina la Isaka lilitajwa mbele ya kuzaliwa kwake (Mwanzo 17:19).
Vilevile, jina la Kristo (Matayo 1:21).
Isaka, mwana mpendwa wa baba yake, alimtii. Wakati Abrahamu
aliposhika njia kwenda kutoa Isaka juu ya kilima Moria, mwana ali-
kwenda pamoja naye akiwa na roho ya kutii (Mwanzo 22:3-6).
Ushirika katikati ya baba Abrahamu na mwana Isaka ulionekana wazi.
Bwana Yesu alisema, “Baba hakuniacha peke yangu, sababu ni-
nafanya saa zote maneno ambayo yanampendeza” (Yoane 8:29).
Abrahamu aliamini Mungu. Hata kama Isaka atakufa, sharti
Mungu atimize ahadi yake. Hivi Abrahamu aliwaambia watumishi,
“Mukae hapa pamoja na punda, nami na kijana tutakwenda kule; na
tutaabudu na kurudi tena kwenu” (sh.5).
Katika ushirika Abrahamu na Isaka walipanda kilima kutayarisha
toleo. Abrahamu akajenga mazabahu pale, akatandika kuni, akafunga
Isaka, mwana wake, akamweka juu ya mazabahu juu ya kuni. Abra-
hamu akanyosha mkono wake, akatwaa kisu achinje nacho mwana
wake.
Kweli, hapa tunapata sura ya msalaba. Baba Mungu alitoa Mwana
wake mpendwa wa pekee. Damu yake ilivuja. Yesu alikufa kuwa toleo
kwa zambi.
Sauti ya malaika ilizuiza Abrahamu asiue Isaka. Lakini kule kwa
Kalvari Mungu alinyamaza kimya. Hakuponyesha Mwana wake
mpendwa. Hakuachilia Mwana wake, lakini alimtoa kwa ajili yetu yote
(Waroma 8:32).
Kwa habari za Abrahamu, Isaka alinyakuliwa toka mauti kuwa sura
ya Yesu katika ufufuko wake. Kufika pale kweli Isaka ni mfano wa
Kristo.
Lakini sasa tunaangalia mfano wa pili katika habari hizi. Wakati
Isaka alipouliza baba yake mbele, “Tazama moto na kuni; lakini wapi
mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa?” (sh.7), Abrahamu aka-
jibu, “Mungu atajipatia mwenyewe mwana-kondoo kwa sadaka ya
kuteketezwa” (sh.8).
22 MIFANO YA KRISTO
Hivi sasa, kweli kondoo ndume ameonekana, akafungwa na pembe
zake katika kichaka (sh.13). Mungu alimpatia kondoo kuwa mko-
mbozi. Isaka alifunguliwa. Amepona!
Abrahamu akakwenda, akatwaa yule kondoo ndume, akamtoa kwa
sadaka ya kuteketezwa badala ya mwana wake (sh.13).
Kondoo huyu ni mfano wa Kristo vilevile. Damu ya Yesu ilivuja
kwa ukombozi wa wenye zambi.
“Mumekombolewa, si kwa vitu vinavyoharibika . . . lakini kwa
damu ya damani, kama ya kondoo asiye na kilema wala alama, damu
ya Kristo” (1 Petro 1:18-19).
Isaka 23
YOSEFU
(Mwanzo 36-50)
Habari za maisha ya Yosefu zinakula sura nyingi katika Biblia. Lakini
msomaji atakayedumu kupeleleza habari hizi atapata faida nyingi.
Mtafutaji atakuta mambo mengi ya damani na mifano juu ya Kristo.
Nafasi inatukosa kwa kutaja mifano yote. Tutaonyesha maneno
machache tu.
Yosefu alipendwa sana na baba yake (Mwanzo 37:3). Yesu ni
Mpendwa wa Mungu (Matayo 3:17; 17:5; Yoane 10:17).
Yosefu, mchungaji wa kondoo (37:2), anafanana na Yesu, Mchu-
ngaji Mwema aliyetoa uzima wake badala ya kondoo zake (Yoane
10:11).
Yosefu alichukia zambi za ndugu zake. Alifahamisha baba yao
mambo ya uzalimu wao (37:2). Bwana Yesu alichukia zambi lakini
alifika hapa duniani kuokoa wenye zambi (1 Timoteo 1:15).
Ndugu zake Yosefu walimchukia (Mwanzo 37:4, 5, 8). Ndugu zake
Yesu walimzarau (Luka 4:28-29; Yoane 8:40; 15:25; Yoane 7:5). Kwa
Yosefu na kwa Yesu ndugu zao walikuwa na uwivu juu yao (Mwanzo
37:11; Matayo 27:17-18; Marko 12:6-7).
Kama Bwana Yesu alivyotumwa na Baba toka mbinguni kwa watu
wake, vivyo hivyo Yosefu alitumwa na baba yake karibu na ndugu zake.
Lakini walimbeua, wakamkataa (Mwanzo 37:13-14,18; Yoane 1:11) .
Ndugu za Yosefu na taifa la Yesu walishauri kuwaua (Mwanzo
37:18; Matayo 12:14). Walizihaki Yosefu, wakimwondoshea mavazi
yake (Mwanzo 37:23). Kwa Yesu vivyo hivyo (Matayo 27:27-28;
Yoane 19:23).
Ndugu zake Yosefu wakamwuza kwa Waisimaeli kwa vipande 20
vya feza (Mwanzo 37:28) . Hesabu juu ya Yesu ilikuwa bei ya mtumwa
katika Israeli (Zekaria 11:12), ndiyo vipande 30 vya feza (Matayo
26:14-15; 27:3, 9).
24
Vazi la Yosefu lilichovya katika damu kuonyesha mfano wa mauti
(Mwanzo 37:31), wadanganye baba zao awaze nyama mkali wa poli
amemwua. Lakini Waisraeli waliua Yesu kabisa, damu yake kuvuja
kwa kukomboa wenye zambi na hukumu ya Mungu (Matendo 2:22-
23; Waebrania 9:14-15; Waroma 5:8-9).
Yosefu aliwekwa ndani ya shimo la birika bila maji. Nyuma
wakampandisha tena hai (Mwanzo 37:24,28). Pale tunafikili mfano wa
kuzikwa na ufufuko wa Yesu (1 Wakorinto 15:3-4).
Yosefu alikuwa mfano wa Yesu vilevile wakati alipotumikia Poti-
fari katika Misri. Alikuwa mtumwa wa heri, mwenye kutii, kujitenga
na zambi (Mwanzo 39:1-6; Wafilipi 2:5-8; Isaya 52:13). Wakati Yosefu
alipojaribiwa na mke wa Potifari, alikataa (Mwanzo 39:7-20). Bwana
Yesu alikuwa bila zambi kwa wazo wala tendo (1 Petro 2:22; 2 Wako-
rinto 5:21).
Unabii ulionyesha ya kuwa Yosefu atapata enzi kutawala juu ya
jamaa yake (Mwanzo 37:7, 9-10). Hivi, nyuma ya mateso (Mwanzo
39:20), Yosefu aliondoshwa pale katika gereza (mnyororo), ali-
heshimiwa, aliwekwa juu ya kiti cha enzi kutawala katika Misri
(Mwanzo 41:38-44).
Yesu atatimiza mfano huu kwani unabii juu yake umeandikwa,
“Utawala utakuwa juu ya bega lake” (Isaya 9:6-7). Jina lake linapita
kila jina (Wafilipi 2:9-11; 1 Wakorinto 15:25).
Yosefu alikuwa mwenye kusaidia ndugu zake wakati wa njaa. Kwa
neema, hata walimtesa, alisamehe zambi zao. Aliwakulisha katika
mahitaji yao. (Soma katika Mwanzo, Sura 41). Bwana Yesu alifikia
watu wake lakini walio wake hawakumpokea. “Lakini wote ambao
walimpokea aliwapa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu, ndio wale
walioamini jina lake” (Yoane 1:12).
Habari Yosefu alizowapa watu wa kumtambua kwa neema zi-
likuwa: “Yosefu anaishi hata leo, naye ni mtawala” (Mwanzo 45:26).
Habari zetu tunaoamini Yesu kutangaza ni: Yuko hai, jina lake
linatukuzwa, ni mwenye neema. Kuja kwake kuokolewa, watu wa
kufa. Uzima mutapata kwake. Yeye ni MFALME WA WAFALME NA
BWANA YA WABWANA (Ufunuo 19:16).
Yosefu 25
KONDOO YA PASAKA
(Kutoka 12)
Katika mifano ya Kristo kwa Agano la Kale hakuna mfano mwingine
unaopita kondoo ya pasaka kwa kuonyesha wazi maana ya Kalvari.
Kondoo ya pasaka alichinjwa kuwa mkombozi wakati Mungu
alipokusudi kuhukumu Misri na mauti. Lakini alisema, “wakati ni-
takapoona damu, nitapita juu yenu” (Kutoka 12:13). Elfu za watu
walipona na elfu za wengine waliuawa.
Neno hili lilitokea nyuma ya kufa kwa Yosefu. Kwa wakati wa
maisha yake Waisraeli waliishi vizuri. Farao alipenda Yosefu na jamaa
yake. Aliwapa sehemu ya inchi, ndiyo Goseni, kwa pahali pa kupanga.
Pale walilinda ngombe, walipata vyakula vya kutosha.
Lakini nyuma ya kufa kwa Yosefu Farao mwingine asiyejua Yosefu
alianza kutawala. Alipata hasira na hasidi juu ya Waisraeli, akawageuza
kuwa watumwa wa Wamisri. Walipiga matofali, walitumika kazi ya
nguvu bila mshahara, waliteswa zaidi. Farao aliwaogopa vile, hivi ali-
agiza waue watoto wanaume wote wakati wa kuzaliwa kwao. Wa-
sichana tu waache hai.
Kwa huruma Mungu aliamusha mwongozi kwa Israeli. Alikuwa
Musa aliyesikia sauti ya Mungu jangwani wakati aliposemezana naye
toka kijiti uliowaka moto bila kuteketea.
Hivi Musa alitokea mbele ya Farao kuomba uhuru kwa Waisraeli.
Farao alikataa. Kwa kulipa kisasi, Mungu alituma mapigo juu ya inchi
ya Misri na juu ya Farao mwenyewe. Lakini roho yake ilikuwa ngumu
kama jiwe.
Katika mapigo tisa Mungu aligeuza maji kuwa damu, alituma
vyula, chawa, mainzi, ugonjwa katikati ya nyama, majipu, mvua ya
mawe, nzige na giza. Farao alibaki na roho ngumu; hakukubali kuwapa
26
Waisraeli uhuru. Hivi Mungu alikusudi kupiga Misri na pigo la kumi,
ndilo mauti.
Mungu alitangaza kusudi lake la azabu (Kutoka 12:12,23).
Alisema, “Nitapita katika inchi ya Misri usiku ule, na nitapiga waza-
liwa wa kwanza wote, mtu na nyama vilevile.” Alipasha mbele juu ya
hukumu ya mauti.
Vilevile Mungu, kwa neema, alitangaza njia ya kuponea hukumu.
Ilikuwa hivi sababu ya kufa kwa mkombozi. Aliagiza kila mtu atwae
mwana-kondoo kwa jamaa yake. Ilimpasa kuwa ndume ya mwaka wa
kwanza, pasipo kilema. Sharti ndume awekwe muda wa majuma mawili
kuonyesha usafi wake, halafu wamchinje mangaribi (Kutoka 12:3-6).
Pale tunapata mfano safi wa Kristo. Leo wenye zambi duniani pote
wanastahili hukumu ya Mungu, ndiyo mauti. Lakini Mungu amete-
ngeneza njia ya wokovu. Ilipasa Kristo anayeitwa “Mwana-kondoo wa
Mungu” (Yoane 1:29) kufa kuwa Mkombozi wa watu. Kondoo aliye-
kufa katika Misri anafanana na Bwana Yesu aliyekufa msalabani kwa
ukombozi wetu.
Kondoo katika Misri alikuwa bila kipako, ndume safi. Vivyo
hivyo, Kristo alikuwa bila laumu au kipako (1 Petro 1:19; 2:22).
Hakustahili kufa, lakini alikufa “mwenye haki kwa ajili yao wasio haki,
ili atulete kwa Mungu” (1 Petro 3:18).
Hata kwa kila nyumba au jamaa na jirani yake kondoo alichinjwa
kwa wakati wa Musa, Mungu hakufikili juu ya kondoo wengi, lakini
aliona kondoo zote kama mmoja tu (Kutoka 12: 3-5). Kwaye kondoo
zote walifanana na kondoo mmoja wa pekee, ndiye Yesu Kristo.
Mungu aliagiza Waisraeli kukamata damu ya kondoo aliyechin-
jwa, ndani ya bakuli, na kuitia juu ya nguzo mbili za kando ya mlango
na juu ya kizingiti cha juu (Kutoka 12:7). Alisema, “Damu itakuwa
alama kwenu juu ya nyumba pahali mutakapokuwa; na wakati ni-
takapoona damu, nitapita juu yenu, wala pigo halitakuwa juu yenu
kuwaharibu ninyi; wakati nitakapopiga inchi ya Misri” (sh. 13).
Hivi Waisraeli walichinja kondoo, walipakaa damu yake mla-
ngoni, kwa imani. Walibaki nyumbani kula nyama ya kuchomwa ya
kondoo namna Mungu alivyowaagiza. Walikula kwa haraka, wakiwa
na fimbo mikononi, viatu miguluni, tayari kwa safari.
Kondoo ya Pasaka 27
Saa sita ya usiku Mungu alipiga wazaliwa wa kwanza wote katika
inchi ya Misri (Kutoka 12:29). Hata mzaliwa wa kwanza ya Farao
aliuawa na malaika ya kuharibu.
Lakini pahali pote Mungu alipoona alama ya damu mlangoni,
alipita juu bila kuharibu. Damu ya kondoo ilipokelewa na Mungu kuwa
malipo ya hukumu. Wale waliojificha na damu waliishi kwa imani.
Walipata uzima kwa njia ya ukombozi.
Kristo ni Mkombozi wetu. Wote ambao wanamwamini, wakipokea
damu yake kuwa ukombozi kwao, wamepata uzima. Wamekombolewa
toka hukumu ya Mungu daima (1 Petro 1:18-19).
28 MIFANO YA KRISTO
MANA, MKATE TOKA MBINGU
(Kutoka 16)
Kisha Mungu alipoondosha Waisraeli katika utumwa wa Misri, wali-
furahi kwanza. Aliwaongoza kuvuka Bahari Nyekundu akiwafanyizia
njia kavu katika maji. Kuonekana kwa Mungu kulikuwa kwa nguzo ya
wingu mchana na kwa nguzo ya moto usiku (Kutoka 13:21). Shekina
iliwaangazia njia ikisimama katikati yao na adui zao.
Jeshi la askari za Misri walijaribu kuwafuata kuwafunga tena kwa
utumwa. Wakaingia juu ya njia kavu baharini, lakini Mungu alirudisha
maji juu yao, wakazama wote (Kutoka 14:26-31). Hivi Mungu alipita
mbele yao kuwaongoza kwa njia ya Kanana.
Lakini jangwani walianza kunungunikia Musa na kumchambua.
Hawakufurahia uhuru wao tena kwa sababu ya majaribu ya safari. Wa-
likumbuka nyama na mkate waliokula kwa Misri, wakashitaki Musa,
wakisema, “Mumetutoa katika jangwa hili kuua kusanyiko hili lote
kwa njaa” (Kutoka 16:3).
Mungu aliwaambia Musa na Haruni jangwani ya kuwa atanyeshea
watoto wa Israeli mkate toka mbingu (Kutoka 16:4). Alitaka kuwapima
kama watashika sheria yake au sivyo na vile wajue ya kuwa Mungu ni
Bwana kweli (sh. 12).
Mungu aliahidi kuwapa mkate toka mbinguni asubui na nyama ya
kutosha mangaribi, washibe (mash. 6-8, 11). Iliwapasa kuokota mana
kila siku asubui, ila siku ya sita wakati watakapopaswa kuokota vipimo
viwili, kimoja kwa siku ile, kimoja kwa sabato (siku ya pumziko la
Waisraeli, ndiyo siku ya saba).
Hivi Mungu alitimiza ahadi yake. Mangaribi kanga wengi waka-
panda, wakafunika kambi. Waisraeli wakawaua wengi (sh. 13).
Asubui, nyuma ya kukauka kwa umande, juu ya udongo wa
jangwa, kulikuwa kitu kidogo cha mviringo, cheupe. Utamu wake
29
ulikuwa kama asali (sh. 31). Watu walitafuta kukitambua, wakasema
wao kwa wao, “Hiki ni nini?” (mash. 13-15).
Musa akawajibu akisema, “Ni mkate ambao Bwana aliwapa ninyi
kula” (sh.15). Waisraeli wakataja jina lake “mana” (sh.31). Mkate toka
mbingu uliwafikia kuwaponyesha katika njaa. Unaona namna mana
inafanana na Kristo?
Basi, kila mtu alipaswa kuokota kwa yeye mwenyewe kwa kadiri
ya njaa yake na kipimo cha kula kwake (sh.16). Hivi kila mtu alichukua
kipimo cha kufaa kumaliza hitaji lake.
Wengine waliasi, wakiokota siku moja vipimo viwili, wasirudi tena
kuitafuta kesho. Lakini kesho yake walikuta imeoza kabisa. Tena
wengine wakaasi, wakisema, “Faida gani kuokota mara mbili siku ya
sita. Itaoza!” Hivi hawakuokota vipimo viwili namna Mungu alivyo-
waagiza. Basi kesho yake, ndiyo siku ya sabato, mana haikuanguka.
Walibaki na njaa. Lakini wenye kutii waliokota mara mbili siku ya sita,
wakakuta mana yao safi, haikuoza kwa sabato.
Katikati ya safari nzima ya Waisraeli muda wa miaka 40 walikula
mkate kila siku. Mana iliacha kuanguka wakati walipovuka Yorodani,
wakaingia inchini mwa ahadi, wakikula muhindi mpya wa Kanana.
Sasa tufananishe mana ya zamani na Kristo, Mkate wa mbingu.
Zaidi tunapata maelezo haya katika Sura 6 ya Habari Njema ya Yoane.
Pale tunakuta wanafunzi wa Yesu wakati walipokamata mikate mitano
na samaki wadogo wawili kwa mkono wa kijana.
Kwa mwanzo wa Sura 6 ya Yoane Yesu alikulisha wanaume 5000
na zaidi (wanawake na watoto) (mash. 1-13). Lakini toka shairi 22
mpaka 59 tunapata mafundisho mengi juu ya Kristo, Mkate wa
mbingu.
Watu walisema (sh. 31), “Baba zetu walikula mana katika jangwa,
kama ilivyoandikwa: Aliwapa kula mkate toka mbinguni.”
Kwa shairi 32 Yesu aliwaambia, “Siye Musa ambaye aliwapa ninyi
mkate ule toka mbinguni, lakini Baba yangu anawapa ninyi mkate wa
kweli toka mbinguni.”
Tena aliendelea na msemo mwingine kwa shairi 33. “Mkate wa
Mungu ni ule unaoshuka toka mbinguni, na kupa dunia uzima.” Kwa
30 MIFANO YA KRISTO
shairi 35 aliongeza maneno akisema, “Mimi ni mkate wa uzima, yeye
anayekuja kwangu hatasikia njaa kabisa, naye mwenye kuniamini
hataona kiu kabisa.”
Kweli mana ni sura ya Kristo. Yeye alitoka mbinguni. Alitumwa na
Baba yake, Mungu. Alifika na usafi wote hapa duniani kuwapa watu
uzima.
Watu walinungunikia Yesu wakati aliposema, “Mimi ni mkate
ulioshuka toka mbinguni” (sh. 41). Waliuliza, “Huyu siye Yesu, mwana
wa Yosefu, ambao baba yake na mama yake tunajua? Basi, kwa sababu
gani anasema sasa: Ninashuka toka mbinguni?”
Hawakumtambua kuwa Mwana wa Mungu, si mwana wa Yosefu.
Hawakufahamu yeye ni Mwana wa Mungu tangu milele. Hawakujua
namna alivyoshuka toka mbinguni, “akitwaa namna ya mtumwa,
akakuwa na mfano wa mtu, na akionekana na sura ya mtu, ali-
jinyenyekeza mwenyewe, akakuwa mwenye kutii hata mauti, ndiyo
mauti ya msalaba” (Wafilipi 2:7-8).
Na saburi na mapendo Bwana Yesu aliwaelezea mambo ya siri ya
mkate toka mbinguni. Alisema, “Yeye mwenye kuniamini mimi ana
uzima wa milele. Mimi ni mkate wa uzima. Baba zenu walikula mana
katika jangwa, wakakufa. Huu ni mkate unaoshuka toka mbinguni, ili
mtu apate kuukula, asife. Mimi ni mkate wa uzima ulioshuka toka
mbinguni; kama mtu akikula mkate huu, atakaa milele; na mkate
ambao nitatoa ni mwili wangu, ambao nitatoa kwa ajili ya uzima wa
dunia” (Yoane 6:47-51).
Mana 31
MWAMBA ULIOPASUKA
(Kutoka 17:1-7)
Sawasawa Waisraeli walivyokuwa na kiu bila maji jangwani, vivyo
hivyo watu duniani leo wanakufa na kiu cha roho, bila tumaini. Mungu
alisaidia Waisraeli kupata maji kuwaponyesha. Sasa Mungu ni tayari
kuwapa maji ya uzima watu wote ambao wanayahitaji.
Waisraeli okoa watu yanapatikana kwa sababu walipata maji safi
toka mwamba uliopasuka. Leo maji ya uzima ni tayari kwa wenye
zambi, wenye kiu kwa roho. Maji ya uzima kuokoa watu yanapatikana
kwa sababu Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, alitobolewa wakati alipo-
fungwa juu ya mti wa msalaba. Kwa kupigwa kwake sisi tumepona
(Isaya 53:5).
Mwamba ulipigwa zamani jangwani kusudi maji yatoke, che-
mchemi kumaliza kiu, ni mfano wa Kristo aliyepigwa juu ya msalaba
kwa ajili ya zambi zetu. Alipigwa mara moja tu. Kwa njia ya mauti
yake tunaweza kupata maji ya uzima bila bei (Ufunuo 22:17).
Tuwaze kwanza juu ya mwamba jangwani. Kwa Sura 17 ya Ku-
toka tunapata habari za Waisraeli waliosafiri katika jangwa toka Sinai.
Wakasimama kwa Refidimu. Pale walipiga kambi, wakitandika hema
zao.
Maji ya kunywa yalikosa. Watu wakaanza kugombana na kion-
gozi chao, ndiye Musa, “Utupe maji tupate kunywa” (Kutoka 17:1-2).
Wakaona kiu kabisa, wakanungunikia Musa, wakisema, “Kwa nini
umetupandisha toka Misri, kutuua sisi na wana wetu na nyama zetu
kwa kiu?” (sh.3).
Musa akaomba Yehova Mungu, “Nitafanyia watu hawa nini? Wao
ni karibu kunitupia mawe” (17:4).
Wale watu walikosa tumaini. Walisikia taabu ya kiu, waliogopa
kifo. Watafanya nini? Hivi waligombana na Musa. Mungu alijibu
32
maombi ya Musa, “Tazama, nitasimama mbele yako pale juu ya
mwamba kwa Horebu; na utapiga mwamba, na maji yatatoka ndani
yake, watu wapate kunywa” (17:6).
Asante. Mungu alisikia kuugua kwa watu, hivi alitunga njia ya
kuwaponyesha. Alichagua mfano wa kufa kwa Kristo na maji ya
wokovu kusaidia Waisraeli.
Musa alipiga mwamba mbele ya wazee wa Israeli (17:6). Maji
yakatoka ndani yake, watu wanakunywa, wakapona. Kristo alipigwa
msalabani kwa gazabu sisi tuliyostahili kupata. Musa alipiga mwamba
mara moja tu.
Nyuma ya miaka mingi Waisraeli walifika tena karibu na mwamba
huu. Wakasikia kiu. Mara hii Mungu aliagiza Musa aseme tu na
mwamba (asiupige). Lakini kwa kasirani juu ya kutokuamini na ku-
tokutii kwa watu, alipiga mwamba na fimbo yake tena. Hivi aliasi
Mungu ambaye alimwagiza aseme tu.
Mfano wa Kristo kupigwa mara moja tu uliharibika. Hivi Mungu
aliazibu Musa, akasema hataingia katika Kanana, inchi ya ahadi. (Soma
Hesabu 20:7-12). Nyuma ya miaka mingi ya kutangatanga kwa Wais-
raeli jangwani, Mungu alipeleka Musa juu ya mlima Pisiga. Toka pale
aliona Kanana mbali, lakini hakupata ruhusa kuingia. Musa alifariki
jangwani. Mungu tu alimzika. (Soma Kumbukumbu la Torati 34:1-8).
Hivi mara ya kwanza mfano ulikuwa sawa. Mwamba ulipigwa
mara moja. Mara ya pili mwamba ulipigwa, lakini haukufaa kwani
ulikuwa sura ya Mwamba wetu Kristo (1 Wakorinto 10:4). Kupigwa
kwa Kristo mara moja kwa msalaba kulifaa kwa kumaliza hasira ya
Mungu juu ya wenye zambi. Waamini wanapata kuondolea kwa zambi
kwa milele. “Kwa kupigwa kwake muliponyeshwa” (1 Petro 2:24).
“Kristo ametolewa mara moja achukue zambi za watu” (Waebra-
nia 9:26,28). Alijitoa mwenyewe kuwa “zabihu moja kwa zambi hata
milele” (Waebrania 10:12). “Kwa toleo moja amekamilisha hata milele
wenye kutakaswa” (Waebrania 10:14). “Basi, pahali maneno haya
yanaposamehewa, hapana toleo tena kwa zambi” (10:18).
Maji yalitoka kwa sababu mwamba ulipigwa katika mapenzi ya
Mungu jangwani. Kristo alipigwa katika mapenzi ya Mungu msala-
bani. Maji ya uzima yanapatikana kama tunda la kufa kwa Kristo.
Mwamba uliopasuka 33
Maji haya ni sura ya Roho Mtakatifu wote wanaoamini Yesu wana-
pata, ndiyo faida ya ukombozi wake.
Bwana Yesu alisema na mwanamke yule wa Samaria, “Kama
ungalijua zawadi ya Mungu, naye ni naniambaye anakuambia, Unipe
maji ya kunywa, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo
hai” (Yoane 4:10). Tena Yesu akamwambia, “Kila mtu . . . anayeku-
nywa maji yale . . . hataona kiu hata milele; lakini maji ambayo ni-
nampa yatakuwa ndani yake kisima cha maji, yanayochemuka hata
uzima wa milele” (Yoane 4:13-14).
Kwa Sura 7 ya Yoane tunasoma maneno haya yaliyotoka kinywani
mwa Yesu: “Mtu akiona kiu aje kwangu, anywe. Yeye anayeamini
mimi, kama maandiko yalivyosema, mito ya maji ya uzima itatoka
tumbo lake. Neno hili alisema juu ya Roho ambaye wale wenye
kuamini watapokea” (7:37-39).
Kwa sisi kuweza kupata maji ya uzima bule kumaliza kiu yetu,
Yesu alipaswa kuteswa msalabani katika moto wa gazabu ya Mungu.
Yeye Mkombozi wetu alitukomboa katika kiu ya Hadeze na ziwa la
moto. Msalabani Yesu alisema, “Nina kiu” (Yoane 19:28).
“Haya, kila mtu anayeona kiu, muje kwa maji, naye asiye na feza;
muje, mununue na mule; ndiyo, muje, mununue mvinyo na maziwa,
pasipo feza na pasipo bei!” (Isaya 55:1).
“Kuja . . . Naye mwenye kiu aje, na yeye anayetaka atwae maji ya
uzima bule” (Ufunuo 22:17). Bwana Yesu anasema, “Mimi nitampa
yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bule” (Ufunuo
21:6).
34 MIFANO YA KRISTO
NYOKA YA SHABA
(Hesabu 21:4-9)
Tunashangaa kusoma mara kwa mara maneno ya manunguniko ya
Waisraeli. Mungu alitumika na ajabu kwa kuwaondosha katika utumwa
wa Misri. Musa alikuwa kiongozi chao kuwapeleka katika uhuru.
Lakini walitesa Musa tena na tena kwa kumnungunikia.
Kwa wakati wa njaa walisingizia Musa. Mungu alisikia maombi ya
Musa, akawasaidia na mana ya kula. Kwa wakati wa kiu walinungu-
nikia Musa tena. Mungu aliwapa maji kutoka ndani ya mwamba ya ku-
pasuka, wanywe. Kwa kuchambua Musa walinungunikia Mungu
mwenyewe!
Tutasoma sasa katika kitabu cha Hesabu, Sura 21. Tuanze kwa
shairi 4: “Wakasafiri toka mlima Hori kwa njia ya Bahari Nyekundu ili
kuzunguka inchi ya Edomu; na roho za watu zilitiwa mashaka sana
kwa sababu ya njia. Watu wakanungunikia Mungu na Musa: Kwa nini
mumetuleta sisi toka Misri ili tufe katika jangwa? Maana hapana mkate
na hapana maji; na nafsi yetu inachukia chakula hiki bule,” (ndicho
mana, mkate wa mbingu) (Hesabu 21:4-5).
Azabu ya Mungu ilitokea kwao. Mungu alituma nyoka wakali za
moto kuwauma. Watu wengi wakakufa kwa sababu ya sumu ya nyoka
hawa.
Hivi Waisraeli walikuwa pasipo na tumaini. Kwa sababu ya zambi
zao kunungunikia Mungu na Musa, na kubeua mana ambayo alituma
kwao, walikuwa na hatari ya mauti. Wale nyoka wakatambaa huko na
huko katika kambi, tayari kukata watu na sumu.
Watu wakafikia Musa kwa kutubu: “Tumekosa kwa sababu tume-
nungunikia BWANA na wewe; omba BWANA aondoshe nyoka hawa kati
yetu. Musa akaombea watu” (Hesabu 21:7).
35
Mungu aliwaonyesha neema kwa kuwapa njia ya kupona. Walifa-
hamu makosa yao, walikiri zambi mbele ya Mungu na Musa. Hivi
Mungu alitunga njia ya wokovu.
Aliagiza Musa kufanya nyoka ya shaba, aiweke juu ya mti pale
jangwani. Mungu aliahidi ya kuwa mtu ye yote atakayetazama nyoka
ile ya shaba juu ya mti, atapona! (Angalia Hesabu 21:8).
Musa akafanya vile. Akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya
mti. Alipasha watu habari njema. Mtu ye yote aliyeumishwa na nyoka
mkali na kuangalia ile nyoka ya shaba juu ya mti, ataishi. Watu wengi
wakafurahi, wakaangalia nyoka ya shaba kwa imani. Mungu aka-
chunga ahadi yake. Walipona! (Soma Hesabu 21:8-9).
Tunajua nyoka ile ya shaba juu ya mti jangwani ni mfano wa Kristo
juu ya msalaba. Bwana Yesu, yeye mwenyewe, aliifananisha vile.
Fungua Agano Jipya yako pahali Yesu alipozungumuza na Niko-
demo usiku. Utakuta maneno haya kwa Yoane 3:14-15: “Na kama
Musa alivyonyanua nyoka jangwani, vivyo hivyo sharti Mwana wa
watu anyanyuliwe, ili kila mtu akimwamini asipotee, lakini awe na
uzima wa milele.”
Sumu ya nyoka (Shetani) inatupata sisi sote watu wa sasa. Mauti
ni mbele yetu — si mauti ya mwili tu, lakini mauti ya pili, kutengana
na Mungu kwa milele katika ziwa la moto. Hatari ya mauti, mshahara
wa zambi, ni mbele yetu. (Soma Waroma 6:23). Lakini Mungu anataka
tupokee zawadi ya uzima!
Tazama Yesu juu ya msalaba. Yeye anafananishwa kama nyoka
kwa kutuokoa. Yeye ni Mkombozi wetu. “Yeye asiyejua zambi alim-
fanya kuwa zambi kwa ajili yetu ili sisi tuwe haki ya Mungu katika
yeye” (2 Wakorinto 5:21).
Bwana Yesu “hakutenda zambi wala hila haikuonekana kinywani
mwake . . . alichukua zambi zetu katika mwili wake juu ya mti, hata
sisi, tukiwa wafu kwa maneno ya zambi, tuwe hai kwa maneno ya haki;
na kwa kupigwa kwake muliponyeshwa” (1 Petro 2:22-24).
“Kristo alitukomboa kwa laana ya torati, akiwa alifanywa laana
kwa ajili yetu, kama ilivyoandikwa: Amelaaniwa kila mtu anayetu-
ndikwa juu ya mti” (Wagalatia 3:13).
Bwana Yesu alibeba ubaya wetu juu yake, akanyanyuliwa msala-
36 MIFANO YA KRISTO
bani kama nyoka, kitu kibaya. Laumu yetu na laana yetu zilimfanan-
isha hivi. Mungu alihukumu mwili wetu ndani yake (Waroma 8:3-4).
Mwokozi Yesu alionya watu, “Mutakufa katika zambi zenu; kwa
sababu hamwamini ya kama mimi ndiye, mutakufa katika zambi zenu”
(Yoane 8:24). Yesu aliwaambia: “Wakati mutakaponyanyua Mwana
wa watu, mutafahamu ya kuwa mimi ndiye” (sh.28).
Tena Bwana Yesu alisema katika Yoane 12:32-33: “Nami kama
nikinyanyuliwa juu ya dunia, nitakokota watu wote kwangu. Alisema
maneno haya, akionyesha ni mauti gani ambayo atakufa.”
Musa alihubiri habari njema kwa watu wa zamani walioumizwa
na sumu ya nyoka. “Angalia kwa imani nyoka ya shaba juu ya mti.”
Wakaangalia kwa imani. Wakaponyeshwa!
Leo sisi, watumishi wa Mungu, tunaonyesha Bwana Yesu akikufa
juu ya msalaba, kubeba zambi zetu. Hivi anafanana na nyoka ya shaba.
Tunahubiri Habari Njema: Tubu, tazama Yesu msalabani, kwa
imani. Sumu ya nyoka, hukumu ya zambi, itaondolewa. Uzima uta-
patikana badala ya mauti.
Nyoka ya Shaba 37
HEMA TAKATIFU
(Kutoka 25:1-9)
Mambo mengi juu ya Kristo yanaonyeshwa katika mifano ina-
yoonekana kwa Hema. Mungu alitaja na Musa, mlimani mwa Sinai,
namna ya kufanya Hema. Alitaja vipimo vyote, namna ya vyuma,
ngozi, vitambaa na vitu vingine vyote. Alituma Musa ashuke mlimani
apashe watu watunge Hema kufuata maagizo ambayo Mungu alimpa
(Kutoka 25:8, 9, 40; 27:8).
Kumbe Hema na vitu vyake vina maana nyingi kueleza juu ya
maisha ya Kristo, kufa kwake na ukuhani wake mbinguni.
Maneno magumu yanayoandikwa katika kitabu cha Waebrania
yanafumbulikana wazi wakati tunapofahamu mifano ya Hema. Hema
ina “mifano ya mambo yaliyo mbinguni” (Waebrania 9:23). Mungu
akusaidie kudumu kutafuta maana hizi za mifano katika Hema, ukue
katika neema na kujua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo (2 Petro
3:18).
Tufahamu ya kuwa Hema ilikuwa nyumba ya nguo na ngozi ili-
yozungukwa na luba kwa kuweka mpaka wa kiwanja. Waisraeli wa-
likaribia Mungu pale. Utakatifu wake ulionekana katika wingu lili-
losimama juu ya Hema.
Hema ilikuwa pahali watu wakosaji walipofikia Mungu na zabihu
kupata ondoleo la zambi. Makuhani waliotajwa na Mungu walimtu-
mikia Hemani siku kwa siku miaka yote waliposafiri jangwani.
Kila mara wakati waliposhika tena njia, Shekina ya Mungu ili-
waongoza. Walipobomoa Hema, Walawi wakabeba vipande vipande.
Waliitandika pahali pengine wakati waliposimama kupanga kwa muda
fulani.
Waisraeli hawakukusanyika ndani ya Hema kama watu wa
makanisa wanavyofanya sasa katika chapelles. Watu walitokea mmoja
mmoja, wakifikia mlangoni mwa Luba, wakitokea na matoleo kumpa
Mungu kama zabihu ya kuteketezwa.
38
MLANGO MMOJA
(Kutoka 27:9-18)
Waisraeli wasafiri jangwani walitoa vitu walivyokuwa navyo kwa ku-
tunga Hema. Zahabu, feza, shaba na nguo ya kitani, na ngozi ndiyo
vitu vyote vilivyohitajiwa. Watu walitoa na roho moja kufanya Hema
kama Mungu alivyowaagiza.
Mafundi wengine walipasua miti ya mshita, wengine walichonga
vyuma. Wanawake walisokota nyuzi kufanya nazo vitambaa, na
kushona mifano juu yao na nyuzi za rangi mbalimbali, kama maagizo
yalivyowaonyesha. Wakati vitu vyote vilipotayarishwa, wakasima-
misha Hema (Kutoka 40).
Kiwanja cha Hema kilikuwa kipimo cha mikono 100 kwa urefu, na
mikono 50 kwa upana. Mkono ni kipimo cha Waisraeli, kutoka kwa
ncha ya vidole kufika kwa kunjo la mkono (coude). Ulikuwa na cen-
timètres 50.
Kuzunguka kiwanja kulikuwa luba ya nguo ya kitani nzuri ya ku-
sokotwa. Urefu juu wa luba ulikuwa mikono mitano. Nguzo 60 zilibeba
nguo ya luba, zenye shaba kwa matako, na vitanzi vya feza.
Luba hii ilikuwa na mlango mmoja tu. Pahali pengine pote mtu
hakuweza kupita luba nyeupe, safi. Lakini kwa mlango wa pekee
atapita.
Nguo ya kitani nyeupe safi, yenye kuzuiza watu, ni sura ya haki
na utakatifu wa Mungu. Mtu hawezi kupita pale. Lakini kwa mlango
atapita na kuingia.
Unafikili mlango huu ni mfano wa nani? Bwana Yesu alisema,
“Mimi ni mlango; kama mtu ataingia kwa mimi, ataokolewa” (Yoane
10:9).
Mtu hawezi kufikia Mungu Mtakatifu leo kwa njia nyingine ila
kwa Yesu mwenyewe. Yeye alisema, “Mimi ndimi njia, na kweli, na
uzima: mtu hakuji kwa Baba, ila kwa mimi” (Yoane 14:6).
39
Mlango wa luba ya Hema ni mfano wa Yesu. Upana wa mlango
ulikuwa mikono 20. Tandiko la mlango lilikuwa nguo za rangi ya
samawi (bleu) na zambarau (pourpre) na nyekundu na kitani nzuri
yenye kusokotwa. Rangi hizi zinatukumbusha juu ya mbingu pahali
Yesu alipotoka, na ya kuwa yeye ni Mfalme kabisa. Nyekundu
inaonyesha damu yake, na kitani safi, utakatifu wake. (Tazama Kutoka
27:16-17 na Kutoka 38:9-20).
MAZABAHU YA SHABA
(Kutoka 27:1-8; 38:1-7)
Mara moja ndani ya mlango wa kiwanja cha Hema kulikuwa ma zabahu
ya sadaka. Ilisimama mlangoni kama zamu. Mtu hawezi kufika mbele
ya Mungu ila damu ya mkombozi imwangike.
Mazabahu hii ilikuwa mraba ndiyo kusema vipimo sawa pande
zote. Urefu mikono mitano, upana mikono mitano. Urefu wake juu
mikono mitatu. Ilifanywa na mbao za mti wa mshita, usiooza, kufu-
nikwa pande zote na chuma cha shaba kisichoweza kuyeyuka katika
moto.
Mazabahu ikiwa mraba inaonyesha ya kama mtu ye yote toka
pande zote duniani ataweza kufika namna moja bila tofauti kupata faida
ya mkombozi. Mti wa mshita unaonyesha mwili wa Yesu wa kimtu,
bila kosa, usioweza kuoza (1 Petro 2:22; Matendo 13:35) .
Shaba ina maana ya hukumu, katika Biblia. Vilevile hapa tunaona
umungu wa Yesu (shaba) na umtu wa Yesu (mti wa mshita). Mazabahu
ni sura ya Kristo aliyevumilia hukumu ya Mungu na moto wa gazabu
yake kwa ajili yetu. Yesu ni mazabahu (Waebrania 13:10), na vilevile
sadaka juu ya mazabahu ni Kristo. Hivi kwa pahali pamoja kuna mi-
fano miwili juu ya Mwokozi wetu. Kristo mwenyewe alitakasa zabihu
iliyotolewa juu ya mazabahu. Kwa Matayo 23:19 tunasoma, “Maza-
bahu inayotakasa sadaka.”
Mwenye zambi aliweza kufikisha nyama safi (kama ndume ya
ngombe au kondoo au mbuzi, hata hua). Aliweka mkono wake juu ya
40 MIFANO YA KRISTO
kichwa cha nyama kuonyesha ya kuwa nyama huyu amekuwa mko-
mbozi wake. Nyama alichinjwa pale, damu yake kuvuja kando ya ma-
zabahu. Vipande vya nyama kuhani alivyoweka juu ya mazabahu,
vikiteketezwa kwa moto. Hivi mtu yule alipokelewa na Mungu, zambi
zake zilifunikwa.
Kuzidi sana zabihu ya Kristo ni sadaka ya kupendeza Mungu. Kwa
toleo lake amepatia usamehe wa zambi mtu ye yote ambaye
anamwamini, na salama na Mungu.
Bwana Yesu alijitoa kukubali mapenzi ya Baba Mungu, kuwa mkom-
bozi wetu. Mara moja tu, katika mwisho wa dunia, ameonekana aondoe
zambi kwa kujitoa mwenyewe (Waebrania 9:26; Yoane 10:17-18).
Matoleo mbalimbali yalitolewa pale juu ya mazabahu. Yanaonye-
sha mifano ya Kristo. Katika kitabu cha Walawi tunapata maagizo juu
ya sadaka hizi namna namna. Kama ukisoma sura hizi, utashangaa juu
ya maana ya damani juu ya Kristo pale.
Tukamate sadaka mbili kwa kukuonyesha. Kwa Walawi 4 tunap-
ata “Sadaka kwa zambi.” Soma mashairi 1-12. Uisawanishe na Kristo
aliyebeba zambi zetu juu yake kwa ukombozi wa hukumu yetu. “Yeye
asiyejua zambi alimfanya kuwa zambi kwa ajili yetu ili sisi tuwe haki
ya Mungu katika yeye” (2 Wakorinto 5:21). Kristo alikuwa sadaka ya
zambi kwa sisi.
Tuangalie sasa Walawi, Sura 1. Soma juu ya sadaka ya kuteke-
tezwa. Anza kwa shairi 3, soma mpaka shairi 13. Toleo hili ni moja
katika matoleo yenye harufu ya kupendeza Mungu (mash. 9, 12). Kwa
zabihu hii ya kuteketezwa (ndiyo kuchomwa, kuungua pia) tumepata
mfano wa Yesu kwa usafi wake akijitoa mbele ya Mungu kuwa sadaka
ya kumpendeza, kufikia pua ya Mungu kama manukato matamu.
Kwa Kristo, kama katika nyama ya sadaka kwa zambi, tunapata
ukombozi toka hukumu ya Mungu kwa ajili ya zambi (Waefeso 1:7).
Kwa Kristo, kama katika nyama ya zabihu ya kuteketezwa, tuna-
pata kukubaliwa na Mungu kwa ajili ya uzuri wa Kristo na kutii kwake.
Nyama ya zabihu ya kuteketezwa ilitolewa “ikubaliwe kwa ajili yake
kwa kumfanyia upatanisho” (Walawi 1:4). Sisi tunakubaliwa kwa
upatanisho na Mungu kwa njia ya kufa kwake badala yetu.
Mazabahu ya shaba 41
BIRIKA LA SHABA
(Kutoka 30:17-21)
Mazabahu ya shaba ilikuwa ndani ya mlango wa luba ya kiwanja cha
Hema. Pale sadaka zilitolewa, damu ilimwangika, zabihu iliteketezwa
kwa moto.
Mbele kidogo, ndani, katikati ya mazabahu na Hema Takatifu
yenyewe, kulikuwa birika la shaba, kama sahani kubwa ya chuma pahali
makuhani walipopaswa kunawa mikono na miguu (Kutoka 30:17-21).
Hivi kulikuwa vitu viwili tu kiwanjani, vyote vya shaba. Mazabahu
ilichanganyisha shaba na mti wa mshita. Maana ya shaba ni umungu na
utakatifu wa Kristo, na mti wa mshita ni umtu wake (Kutoka 40:30-32).
Kisha kuhani alipoingia kwa mlango wa pekee wa luba, alipita kwa
mazabahu ya sadaka. Halafu aliendelea mbele kwendea Hema.
Lakini siku kwa siku ilimpasa kunawa mikono na miguu kwa
birika la shaba mbele ya kuingia ndani ya Hema kutumikia Mungu.
Alihitaji maji katika birika kujinawa kuondosha uchafu aliopata kwa
kutembea udongoni, na kukamatakamata vitu mikononi mwake.
Wakati Haruni na wana wake walipowekwa kuwa makuhani mara
ya kwanza, Musa aliwapeleka kwa mlango wa Hema, akawasafisha
mwilini mwote pia na maji safi. Hawakuhitaji kuoga kwa kutimiza she-
ria tena. (Ndiyo, hemani zao, pahali walipopanga, walioga maji kama
watu wote, lakini si kwa sheria ya utumishi wao wa ukuhani). Mara
moja ilitosha. Toka pale, iliwapasa kunawa kila siku kwa birika.
Vivyo hivyo kwa makuhani wa sasa. Waamini wote wanapata
ruhusa ya ukuhani (1 Petro 2:5,9). Tuna ruhusa kufikia Mungu.
Tukipata faida ya sadaka ya Kristo msalabani kwa ajili yetu, tume-
okolewa kwa milele. Tunatakaswa daima kwa zabihu moja. Soma Wa-
ebrania 10:14, “Kwa toleo moja amekamilisha hata milele wenye
kutakaswa.” Tumepata usamehe, hatuhitaji toleo tena (Waebrania 10:18).
42
Wakati Petro alipoona Yesu akinawa miguu ya wafuata wenzake,
na Yesu alitaka kunawa yake vilevile, Petro alikataa. Bwana Yesu
alimwambia, “Kama nisipokunawa wewe, huna shirika pamoja nami”
(Yoane 13:8). Hivi Petro aliomba Yesu amwogeshe mwili mzima.
Lakini Yesu alimwambia, “Yeye aliyeoga hahitaji ila kunawa miguu
yake tu, lakini yeye ni safi kabisa” (Yoane 13:10).
Mkristo ametakaswa mbele ya Mungu siku alipoamini Yesu. Damu
yake inamsafisha. Sasa yeye ni kuhani kutoa zabihu ya roho za kupe-
ndeza Mungu kwa njia ya Yesu Kristo (1 Petro 2:5). Lakini hawezi ku-
fika mbele ya Mungu na zambi za mwenendo. Sharti anawe mbele ya
kufika kwake.
Zamani kuhani aliyetumikia Mungu katika Hema jangwani ali-
kwenda kwa birika la shaba kunawa. Birika la shaba linafanana na
Yesu. Sisi makuhani tunahitaji kufika mbele yake kila siku, kukiri
zambi zetu na kuomba kusafishwa.
Yesu ni NENO (Yoane 1). Tunafika kwake atusafishe kwa Neno
lake la haki, ndilo Maandiko Matakatifu. Maji katika birika zamani
yanafanana na Neno la Mungu. Bwana Yesu aliomba Baba Mungu
(Yoane 17:17), “Uwatakase kwa kweli; neno lako ni kweli.”
Tunahitaji kusafishwa kila siku na maji ya Neno la Mungu. “Kristo
alivyopenda kanisa, na kujitoa mwenyewe kwa ajili yake; apate kuli-
takasa, akiwa amelisafisha kwa maji katika neno” (Waefeso 5:25-26).
Mtu anayeamini Bwana Yesu anasafishwa na zambi. Paulo
aliandikia Wakorinto, “Wengine kwenu mulikuwa hivi; lakini
mulioshwa, lakini mulitakaswa, lakini mulihesabiwa kuwa na haki
katika jina la Bwana Yesu, na katika Roho ya Mungu wetu” (1 Wako-
rinto 6:11). Hii ni kuoshwa kwa wokovu.
Nyuma Paulo aliwaandikia maneno mengine juu ya kusafishwa
kwa kila siku, “Tujisafishe kwa uchafu wote wa mwili na wa roho, tuk-
itimiza utakatifu katika woga wa Mungu (2 Wakorinto 7:1).
Mkristo anayechafuka na zambi ya dunia, sharti afike kwa Bwana
Yesu ndiye Birika letu, kukiri na kutubu. “Kama tukisema kwamba
hatuna zambi, tunajidanganya wenyewe, wala kweli si ndani yetu.
Tukikiri zambi zetu yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee
zambi zetu, na kutusafisha na uzalimu wote (1 Yoane 1:8-9).
Birika la shaba 43
Kuhani akiingia mbele ya Mungu kutoa sifa, asiyesafishwa na
zambi zake za mwenendo, ana hatari ya azabu ya Mungu.
Fikili maneno ya watoto wa Haruni, Nadabu na Abihu. Wao wa-
likuwa makuhani lakini walifika mbele ya Mungu kutoa uvumba na
kuuchoma na moto usiofaa. Moto ulitoka kwa Bwana, ukawakula,
wakakufa mbele ya Bwana (Walawi 10:1-2).
Hivi, “Mtu ajihukumu mwenyewe ... kwa sababu hii wengi kwenu
ni zaifu na wagonjwa, na wengi wamelala. Lakini kama tungejihukumu
sisi wenyewe, tusingehukumiwa” (1 Wakorinto 11:28, 30-32) .
Birika la shaba
44 MIFANO YA KRISTO
KINARA CHA ZAHABU
(Kutoka 25:31-40)
Hema ya kusanyiko ilikuwa na vyumba viwili: Pahali Patakatifu na
Pahali Patakatifu pa Patakatifu. Hivi chumba cha pill kilikuwa patakat-
ifu zaidi sana. Pale wingu wa utukufu wa Mungu ulikawa juu ya kiti
cha neema.
Katika chumba cha kwanza, ndicho Pahali Patakatifu, kulikuwa
vitu vitatu: kinara cha zahabu, meza ya mkate wa onyesho na maz-
abahu ya uvumba. Meza na mazabahu zilifanywa kwa mti wa mshita,
zikifunikwa na zahabu. Lakini kinara kilifanywa na zahabu safi tike.
Fundi hakuyeyusha zahabu wakati alipofanya kinara, lakini aliipi-
gapiga na nguvu iwe chuma kimoja.
Tuwaze kwanza juu ya kinara cha zahabu. Urefu wake haujulikani,
lakini kilikuwa kitu cha damani, kizuri sana. Nguzo ya kati pamoja na
matawi matatu ngambo moja na matatu ngambo nyingine yalifanya
matawi saba (hesabu kamilifu). Nguzo na matawi yake yalichongwa na
zahabu safi kwa fundi aliyefuatua maua ya mbegu ya lozi. Nguzo na
matawi yalibeba taa saba za zahabu.
Kuhani aliingia kila siku, nyuma ya kunawa inje katika birika,
kutengeneza taa hizi saba, kuondosha makaa juu ya vitambi na kujaza
mabakuli na mafuta ya zeituni kama Mungu alivyowaagiza. Hivi taa
ziliwaka daima (Walawi 24:2, 4). Maneno haya tunapata katika kitabu
cha Kutoka 25:31-40 na vilevile kwa Sura 37:17-24.
Nuru ya inje haikuingia ndani ya Pahali Patakatifu. Taa saba zili-
waka zikiangaza nuru juu ya kinara kuonyesha uzuri wake (Kutoka
25:37). Kinara kilimetameta katika usafi wake wa zahabu ya ku-
chongwa.
Sasa tutafute maana ya kinara na taa zake. Kinara ni mfano wa
Kristo. Zahabu inaonyesha umungu wake. Usafi wa zahabu unashuhu-
dia usafi wa moyo wa Kristo.
45
Kristo alipigwa, aliteswa kama chuma cha kinara kilivyopigwa na
kilivyokatwa wakati wa kukichonga (Soma Isaya 53:5).
Kristo ni nuru ya ulimwengu, akifika kuangazia watu katika giza
la dunia (Yoane 1:4-5; 8:12; 9:5; 12:46).
Taa saba ni sura ya makanisa katika umoja wa Kristo duniani pote.
Kuwaka kwa kuangaza na nuru sasa ni kazi ya makanisa (Ufunuo 1:20;
Waefeso 5:8). Kama taa zilivyowaka kuonyesha uzuri wa kinara, vivyo
hivyo makanisa yanashuhudia uzuri wa Kristo na neema yake. Petro al-
ituambia ya kuwa kazi yetu ni kutangaza uzuri wake aliyetuita toka
giza tuingie katika nuru yake ya ajabu (1 Petro 2:9).
Moto wa ushuhuda unawaka na mafuta ya Roho Mtakatifu. Mafuta
ndani ya mabakuli ya taa za kinara ni mfano wa Roho Mtakatifu. Roho
Mtakatifu anafurahi kuonyesha utukufu wa Kristo. (Soma Yoane
16:13-14).
Hesabu ya saba katika Biblia ni hesabu ya ukamilifu. Tunaona
hesabu hii kwa Ufunuo 4:5 juu ya Roho Mtakatifu na ukamilifu wa
ushuhuda wake. Kwa Ufunuo 1:10-13 tunaona Yesu katikati ya
makanisa saba, akipitisha mawazo yake kwao. Makanisa saba ni se-
hemu sehemu ya Kanisa la dunia pote.
Maua na mbegu ya lozi zilizochongwa juu ya kinara zinaonyesha
matunda toka katika mauti na maisha ya Kristo. Yeye ni mwenye kuzaa
tunda (Yoane 12:24).
Kama sisi tukitaka kuzaa tunda kwa Yesu, tujitoe kwake, uzima
wake utumike ndani yetu. Soma Yoane 15 juu ya mzabibu na matawi
yake. Tuko mwili mmoja na yeye. Kukaa kwake kunatupa uwezo kuzaa
tunda la Roho.
Roho Mtakatifu ndani ya Mkristo analeta mafuta kwa taa kuwaka.
Lakini kama makaa ya zambi yakifungana juu ya kitambi, inafaa
kuhani aondoshe makaa, mafuta ya Roho yatelemke na usafi hata moto
wa ushuhuda uwake vizuri bila zuizo.
46 MIFANO YA KRISTO
MEZA YA MKATE WA ONYESHO
(Kutoka 25:23-30; Walawi 24:5-9)
Meza hii inatuonyesha mfano wa Kristo na watu wake katika ushirika.
Urefu wake ulikuwa mikono miwili. Upana wake ulikuwa mkono
mmoja. Kusimama kwake juu ulikuwa mkono mmoja na nusu.
Mafundi walitumia mti wa mshita kufanya meza hii. Juu yake
pande zote walifunika mbao na zahabu. Taji ya zahabu iliizunguka pale
juu. Pete zilikuwa kwa pembe zake ine, pahali pa kuingiza magongo.
Magongo ya mshita yalifunikwa vilevile na zahabu. Wakati wa kusafiri
walibeba meza na magongo haya.
Meza ilikuwa pamoja na kinara cha zahabu ndani ya chumba cha
Hema kilichoitwa “Pahali Patakatifu.” Kila sabato kuhani ataweka
mikate kumi na miwili juu ya meza, kwa mistari miwili, sita, sita.
Wakati wa kuondosha mikate ya mbele, makuhani waliikula.
Juu ya mikate mezani kuhani alimimia marashi, ndiyo ubani safi,
kwa manukato. Hivi kwa juma moja zima mikate ilishinda pale kwa
meza kunuka na harufu tamu mbele ya Mungu.
Makabila 12 ya Israeli yalionyeshwa mbele ya Mungu ndani ya
mkate wa onyesho. Ni kama vilevile kuhani mkubwa alivyobeba ma-
jina yao mbele ya Mungu juu ya kifua chake (Kutoka 28:15, 21) na
kwa mabega yake kwa efodi (Kutoka 28:6,12). Wakati kuhani mkubwa
alipoingia, alipeleka majina ya makabila ya Israeli mbele ya Mungu.
Wakati mwingine taifa la Israeli lilitengana kuwa sehemu mbili
mbalimbali. Sehemu moja ilikuwa na makabila mawili. Sehemu
nyingine ilikuwa na makabila kumi. Lakini hata hivi, wakati wote kwa
meza mikate ilikuwa 12. Vilevile Mungu hakuita mikate 12 “mikate.”
Aliiita “mkate wa onyesho,” kutangaza umoja wao.
Mikate 12 ilikuwa alama ya watu wa Mungu pia. Sisi sasa tunap-
ata maana nzuri sana katika meza ya zahabu na mkate wa onyesho.
47
Kwa mfano, tunafahamu Yesu ni meza ya zahabu anayebeba watu
wake wote mbele ya Mungu daima. Kwa umoja anawaonyesha na
manukato matamu mbele ya Baba yake.
Vilevile analinda watu wake kwa uwezo wake, mkononi mwake.
Hawawezi kuponyoka kamwe. Ni kama meza ilivyochunga mkate kwa
taji ya zahabu iliyoizunguka pande zote.
Mti wa mshita meza iliyofanywa nao unafanana na umtu wa Kristo
ambaye alitukufilia msalabani. Zahabu inatangaza umungu wake na
utukufu wake. Taji ya zahabu iliyozunguka meza inaonyesha utawala
wake. Yeye ni Mfalme wa wafalme. Atatawala duniani pote.
Mkate ni watu wake. Meza na mkate juu yake zinafanana na
Bwana Yesu katika ushirika wake na watu wake. Anawaonyesha mbele
ya Mungu kama meza ilivyobeba mkate mbele yake zamani (Waroma
8:34).
Tunaweza kusawanisha mkate vilevile na Yesu mwenyewe. Yeye
ni mkate aliyetoka mbinguni, kuwapa watu uzima. Yeye alikufa kama
punza ya ngano (Yoane 12:24). Alisagwa kama mbegu ya ngano kuwa
unga wa kufanya mkate. Tena Bwana Yesu aliwekwa kwa moto katika
tanuru ya gazabu ya Mungu hata sisi tuwe mkate kutoka ndani ya
mateso yake, ndani yake mwenyewe. Anatuonyesha mbele ya Baba
yake kwa utamu, tunda la mateso na mauti yake.
48 MIFANO YA KRISTO
Meza yaMkate wa Onyesho
MAZABAHU YA KUCHOMA UVUMBA
(Kutoka 30:1-10)
Vyumba viwili vya Hema vilikuwa na kitambaa kubwa kuvigawa. Ki-
tambaa hiki kiliitwa “pazia.”
Vitu viwili vilikuwa chumbani cha kwanza. Vilikuwa kinara cha
zahabu na meza ya mkate wa onyesho iliyofunikwa po pote kwa za-
habu.
Kitu cha tatu kilichokuwa ndani ya chumba cha kwanza kiliitwa
“mazabahu ya kuchoma uvumba.” Mazabahu hii haikuwa pahali pa
kutoa nyama ya sadaka. Ilikuwa mazabahu pahali kuhani alipochoma
uvumba mbele ya Mungu ndio manukato ya kuteketezwa.
Mazabahu hii ilifanywa na mti wa mshita na kufunikwa pahali po
pote na zahabu. Soma Kutoka 30:1-10. Urefu wake ulikuwa mkono
mmoja, upana wake vivyo hivyo kwani ilikuwa mraba. Kusimama
kwake juu kulikuwa mikono miwili. Ilikuwa na pembe zake za zahabu
na taji ambayo iliizunguka. Taji vilevile ilifanywa na zahabu.
Mazabahu ya kuchoma uvumba iliwekwa mbele ya pazia iliyo-
gawa vyumba viwili vya Hema. Kila mangaribi wakati kuhani alipo-
tokea kuwasha taa za kinara, aliongeza makaa kwa mazabahu hii ya
zahabu. Makaa yalitoka kwa mazabahu ya shaba ya sadaka ya nyama
kiwanjani. Hivi moto uliwaka na uvumba mtamu juu mazabahu ya za-
habu daima.
Kila mwaka mara moja kuhani mkubwa alikamata damu ya zabihu
toka mazabahu ya shaba kiwanjani kuifikisha ndani ya Pahali Pataka-
tifu. Pale alinyunyiza pembe za mazabahu ya kuchoma uvumba na
damu, kufanya upatanisho na Mungu. Kama mwabudu ametakaswa na
damu aliweza kutoa sifa ya kufaa mbele ya Mungu. Shukrani isiyo-
takaswa haiwezi kupokelewa na Mungu.
Mazabahu ya kuchoma uvumba inatukumbusha kazi ya Kristo
49
sasa mbinguni kwa ajili ya watu wake. Yesu anatuombea mbele ya
Mungu (Waebrania 7:25; 9:24).
Kwa yeye tu tunaweza kutoa sifa zetu. Yeye ni mazabahu yetu ya
zahabu. Tulifahamu mbele namna mti wa mshita ulivyoonyesha utu
wa Kristo na zahabu ilivyoonyesha umungu wake. Yeye ni Mwana wa
mtu na Mwana wa Mungu. Ni Yesu, mtu, ambaye anatuombea mbi-
nguni (Waebrania 7:25).
Sisi Wakristo tunatoa shukrani na kuabudu mbele ya Mungu kwa
njia ya Yesu. Soma Waebrania 13:15, “Basi, kwa njia yake, tumpe
Mungu zabihu ya sifu siku zote, ndiyo tunda la midomo inayokiri jina
lake.”
Kwa Ufunuo 8:3-4 tunasoma juu ya malaika aliyesimama mbele ya
mazabahu ya kuchoma uvumba. Malaika huyu ni Yesu. Sikia neno hili
juu yake, “Malaika mwingine alikuja, akasimama mbele ya mazabahu,
mwenye chungu cha zahabu; akapewa uvumba mwingi, ili autie
pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya mazabahu ya zahabu
iliyo mbele ya kiti cha ufalme. Na moshi wa ule uvumba ukapanda
mbele ya Mungu pamoja na maombi ya watakatifu toka mkono wa
malaika.”
Asante kwa Mungu. Bwana Yesu sasa, kuhani letu mkubwa,
anaongeza uvumba wa marashi yake juu ya maombi na shukrani zetu.
Hivi zote zinapanda pamoja kuwa manukato matamu kwa moto ya
Roho Mtakatifu kufurahisha Mungu.
Wakristo wote wana ruhusa ya ukuhani mbele ya Mungu. Petro
aliandika, “Ninyi vilevile, kama mawe yaliyo hai, mumejengwa muwe
nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, kutoa zabihu za Roho, za kupe-
ndeza Mungu kwa njia ya Yesu Kristo” (1 Petro 2:5). Kwa yeye, kuhani
letu mkubwa, tunatoa zabihu za sifa mbele ya Mungu.
Lakini makaa ya kuchoma uvumba wa sifa yawe ya Roho Mtaka-
tifu, kwa moto wa msalaba na damu ya Sadaka yetu. Mtu asilete sifa toka
moto mgeni. Soma azabu juu ya wana wa Haruni (Walawi 10:1-2).
50 MIFANO YA KRISTO
PAZIA, SANDUKU YA AGANO NA
KITI CHA REHEMA
(Kutoka 26:31-32; 25:10-22; 37:1-9)
Pazia liligawa vyumba katika Hema. Lilifanywa kuwa kitambaa cha
kitani nzuri ya kusokotwa. Nyuzi za rangi ya samawi, zambarau na
nyekundu zilishonwa kuonyesha sura ya makerubi (Kutoka 26:31-32).
Makuhani wo wote hawakuwa na ruhusa kuingia kupita kwa
chumba cha ndani ndicho “Pahali Patakatifu pa patakatifu,” ila kuhani
mkubwa mara moja kila mwaka kwa siku ya malipizo. Yeye alipaswa
kubeba damu kunyunyiza juu ya kiti cha rehema kwa ajili yake
mwenyewe na kwa zambi za Israeli wote (Waebrania 9:6-7).
Miaka mingi nyuma, wakati Waisraeli walipoishi katika inchi ya
Kanana, walikomboa Hema na hekalu, kwani safari yao jangwani ili-
kwisha. Pazia liligawa vyumba vya hekalu namna lilivyogawa vyumba
vya Hema. Watu walizuizwa kufika ndani kabisa, ila kuhani mkubwa.
Lakini wakati Yesu alipokufa msalabani, pazia la hekalu lilipa-
suliwa toka juu fika chini. Njia ya kufikia Mungu kwa kila mwamini
imefunguliwa wazi sasa. Mazuizo yaliondoshwa wakati Mwokozi Yesu
alipotobolewa.
“Tuna uhodari wa kuingia Pahali Patakatifu kwa damu ya Yesu,
njia ile aliyoanza kwa ajili yetu, mpya, na hai, katika pazia, ndio mwili
wake; na tukiwa na kuhani mkubwa juu ya nyumba ya Mungu; tukari-
bie kwa moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, mioyo yetu ikikwisha
kunyunyiziwa kwa kuacha zamiri mbaya, na miili yetu kuoshwa kwa
maji safi (Waebrania 10:19-22).
Vivuli vya zamani vinatimizwa katika haki ya mbingu.
Turudi sasa kwa maneno ya Hema jangwani. Ndani ya chumba cha
pili (cha ndani, nyuma ya pazia) kulikuwa sanduku ya agano na juu
yake kiti cha rehema. Tunapata habari zao katika Kutoka 25:10-22.
51
Sanduku ilifanywa na mti wa mshita kufunikwa ndani na inje na
zahabu safi. Urefu wake juu ulikuwa mikono mmoja na nusu. Ilikuwa
na pete ine za zahabu kwa kuibeba wakati wa kuhama, na magongo ya
mshita yaliyofunikwa na zahabu.
Kifuniko cha sanduku kilikuwa ya zahabu tike waliyopigapiga ku-
tunga makerubi wawili wakitazamana. Katikati yao ni pahali kuhani
mkubwa alipoweka damu toka sadaka inje juu ya mazabahu ya shaba.
Kifuniko hiki kiliitwa “kiti cha rehema.”
Ndani ya sanduku kulikuwa vitu vitatu. Tusome kwa Waebrania
9:3-4, “Nyuma ya pazia la pili ilikuwa hema iliyoitwa Pahali Patakat-
ifu pa patakatifu, yenye chetezo cha zahabu na sanduku ya agano iliy-
ofunikwa na zahabu pande zote, na ndani yake kulikuwa kopo la
zahabu lenye mana, na fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vibao vya
agano; na juu yake makerubi ya utukufu, yakitia kivuli juu ya kiti cha
rehema.”
Kopo la zahabu (Kutoka 16:33-34) lilichunga kipimo cha mana
ambayo Waisraeli walikula jangwani. Haikuoza. Ilikuwa ushuhuda wa
uaminifu wa Mungu ambaye aliwakulisha jangwani. Kwa sisi mana
hii ni mfano wa Kristo, mkate wa mbingu (Yoane 6:31-35, 50-51).
Fimbo ya Haruni iliyochipuka (Hesabu 17:5-11) iliwekwa katika
sanduku kushuhudia zambi za watu (Hesabu, Sura 16 na 17). Mungu
aliazibu waasi. Fimbo 12 zisizo na uzima ziliwekwa zamani mangaribi
Mungu aonyeshe ni nani atakayemchagua kuwa kuhani lake. Asubui
fimbo ya Haruni ilionekana pekee kuwa na uzima, kuchipuka na kuzaa
maua na matunda ya lozi. Kwa sisi tunaona kwa fimbo ya kuchipuka
mfano wa Kristo katika mauti yake tena kuonekana na uzima, mwenye
kuzaa matunda katika ufufuko wake (Yoane 12:24).
Vibao vya sheria vilikuwa katika sanduku kwa Hema na kwa hekalu
(mana na fimbo hazikuwa kwa hekalu). Vibao vya sheria vilibaki kuonye-
sha ya kuwa sheria ya Mungu inadumu daima. Mwokozi Yesu hakufika
kuharibu sheria, lakini kuitimiza (Matayo 5:17).
Kiti cha rehema cha zahabu safi kinaonyesha namna mtu ataka-
vyoweza kukutana na Mungu. Damu ya sadaka inanyunyizwa juu ya
kiti cha rehema. Ushirika katikati ya Mungu na watu unawezekana kwa
ajili ya damu ya Yesu kumwangika kwa ajili yetu, kutuliza gazabu ya
52 MIFANO YA KRISTO
Mungu.
Makerubi ya zahabu juu ya kiti cha rehema kwa sanduku ya agano
hayakuwa na mapanga ya hukumu kama wale waliowekwa kulinda
njia ya shamba la Edeni wakati Adamu na Hawa walipokosa na ku-
fukuzwa.
Makerubi hapa yanakunja mabawa yao kimya, yakitazamana na
kuangalia damu juu ya kiti cha rehema. Sheria iliyovunjwa kwa
mikono ya watu sasa imewekwa chini ya damu ya ukombozi, ndiyo
damu ya zabihu. Hivi salama na amani zinapatikana kwa wenye zambi.
Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema
Pazia 53
KUHANI MKUBWA NA MAVAZI MATAKATIFU
(Kutoka 28:1-43; 39:1-31)
Kuhani mkubwa wa kwanza wa Israeli alikuwa Haruni, ndugu yake
Musa. Yeye alikuwa mtu wa kabila la Lawi. Watoto wake walitakaswa
kuwa makuhani.
Kuhani mkubwa wa zamani ni mfano wa Kristo na utumishi wake
wa sasa. Ukuhani wa makuhani ya zamani ulibadilika. Kuhani alikufa,
mwingine alimkomboa kwa kazi. Lakini ukuhani wa Kristo unapita
ule wa Walawi, namna ya Haruni, kwani Kristo anaishi kwa milele,
haubadiliki kamwe. Anadumu kuombea watu wake mbele ya Mungu
daima (Waebrania 7:21-27) .
Ukuhani wa Kristo ni mzuri kupita ule wa Haruni. Kristo alitoka
kabila la Yuda, ndilo la wafalme. Kweli yeye ni mfalme. Lakini namna
gani ataweza kuwa kuhani asiye wa kabila la Lawi? Yeye ni kuhani
namna ya Melkisedeki aliyekuwa kuhani la Mungu aliye juu na mfalme
wa Salemi (Mwanzo 14:18-20).
Melkisedeki alikuwa mtu wa ajabu. Namna ya kuzaliwa kwake
haijulikani. Anafanana na Kristo aliyezaliwa kwa ajabu: Baba yake
Mungu, mama yake bikira.
Abrahamu, baba yake Isaka aliyezaa Yakobo baba ya Lawi, ali-
jinyenyekeza mbele ya kuhani Melkisedeki, akitoa zaka ya moja ndani
ya kumi ya nyara zote alizopata ndani ya vita. Hivi Abrahamu aliinama
mbele ya mkubwa. Lawi alitoka kwa uzazi wa Abrahamu. Hivi ni kama
Lawi alijinyenyekeza mbele ya Melkisedeki. Maana: ukuhani wa Lawi
(Haruni) haufiki kwa ukubwa wa ukuhani wa Melkisedeki. Kristo ana-
fuata Melkisedeki katika ukuhani wa juu kupita. (Soma Waebrania
6:20; 7:1-28).
Mara moja kila mwaka kuhani mkubwa aliingia kupita pazia ndani
ya chumba cha pili ndicho Pahali Patakatifu pa Patakatifu. Alipeleka
damu toka mazabahu ya sadaka kunyunyiza juu ya kiti cha rehema.
54
Yesu, Kuhani letu mkubwa anayeishi milele, aliingia mara moja
kwa Pahali Patakatifu na damu yake mwenyewe. (Soma Waebrania
9:11-15). Hahitaji kujitoa mara nyingi kama kuhani la zamani, lakini
kwa toleo lake mara moja ametakasa na kukamilisha watu wake (Wa-
ebrania 9:23-28; 10:14).
Itakuwa faida kusoma Waebrania 4:14-16 na Sura 5, 7, 8, 9, 10.
Pale utapata mambo ya kutimiza mifano ya Hema ya jangwa, na ma-
toleo na kazi ya kuhani mkubwa. Utafahamu maneno ya Kristo zaidi
kupita kama ukiwaza juu ya mifano katika Agano la Kale, na kusoma
maana katika Agano Jipya.
Makuhani ya zamani walitumikia Hema ya dunia lakini Kuhani
letu mkubwa anatumikia mbinguni kabisa. Kwa Hema ya zamani tu-
napata kivuli cha maneno ya kweli mbinguni. Sadaka za Israeli zamani
hazikuweza kukamilisha wenye kukaribia Mungu wala kumpendeza.
Lakini zabihu ya Kristo inafaa. (Soma Waebrania 10:14, 19-22).
Mavazi ya kuhani mkubwa wa zamani yana maana kwa kufana-
nishwa na utumishi wa Kristo katika ukuhani wake. Alivaa nini wakati
alipokaribia Mungu?
Kwanza, kanzu yenye mkono, nyeupe ya kitani nzuri na
mirabaraba (kazi ya mshonaji). Nyeupe kuonyesha usafi wa Yesu
katika utu wake (Kutoka 28:4). Juu ya kanzu alivaa joho (koti) mfupi
bila mikono ya rangi ya samawi (kama mbinguni). Hili vazi lilisokotwa
kwa umoja. Kristo ni mwenyeji wa mbingu. Pindo za joho chini
zilibeba mifano ya matunda ya makomanga, yenye rangi ya samawi,
zambarau na nyekundu. Katikati ya matunda kulikuwa kengele. Yesu
ni mwenye kuzaa tunda katika ufufuko wake. Kengele linatukumbusha
faida ya ushuhuda wake.
Juu ya joho kulikuwa efodi kuvaa juu ya mabega na kwa mbavu
yake. Ilikuwa vilevile na mkaba wake. Ilisokotwa vizuri na umalidadi
wa nyuzi za samawi, zambarau na nyekundu pamoja na uzi wa zahabu.
Juu ya mabega kulikuwa vito viwili vya shohamu. Walichora juu ya
vito hivi majina ya wana wa Israeli. Vito vilifungwa katika vijalizo vya
zahabu. Hivi kila mara Haruni alipotokea mbele ya Mungu, alibeba
majina ya watu wa Mungu. Vivyo hivyo, Kuhani letu Mkubwa
anapeleka majina yetu kwa uwezo wa mabega yake mbele ya Mungu
Mtakatifu. Tunakumbuka Mchungaji Mwema akibeba kondoo
Kuhani Mkubwa 55
mpotevu juu ya bega lake wakati alipomkuta, pahali pa amani na
salama.
Kwa kifua kuhani alibeba vito 12 katika mfuko wa umalidadi
wenye rangi. Kulikuwa kito kimoja kwa kila kabila la Israeli, kila kito
na jina lake. Tunawaza juu ya Yesu, Kuhani letu anayelinda majina
yetu, sisi watu wake, karibu na moyo wake wa mapendo.
Kulikuwa kilemba kama kofia na bamba la zahabu safi kuhani ali-
yobeba kwa paji la uso. Juu ya bamba hili, kwa kuchora, kulikuwa
mhuri, TAKATIFU KWA BWANA. Haruni alisimamia utakatifu wa
Israeli mbele ya Mungu. Kristo anasimamia utakatifu wa Kanisa lake
(2 Wakorinto 5:21).
Namna Mungu zamani alivyoona watoto wa Israeli katika mavazi
matakatifu na ya umalidadi wa Haruni, vivyo hivyo Mungu anatu-
tazama ndani ya Kristo, Kuhani letu mkubwa, katika mali ya neema
yake na uzuri wake wote.
Sisi waamini tunapata njia wazi kuingia Pahali Patakatifu kwa
damu ya Yesu. Mungu anatuita kumkaribia bila woga kama makuhani
yake waliosafishwa na damu ya sadaka iliyokubaliwa pia.
“Tuna uhodari wa kuingia Pahali Patakatifu kwa damu ya Yesu,
njia ile aliyoanza kwa ajili yetu, mpya, na hai, katika pazia, ndio mwili
wake; na tukiwa na kuhani mkubwa juu ya nyumba ya Mungu; tukari-
bie kwa moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, mioyo yetu ikikwisha
kunyunyiziwa kwa kuacha zamiri mbaya” (Waebrania 10:19-22).
“Basi, tukaribie kiti cha neema pasipo woga, ili tupewe rehema,
na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji” (Waebrania 4:16).
56 MIFANO YA KRISTO
DAUDI NA KRISTO
Mungu alituma nabii Samweli kutaja mtu atakayekuwa mfalme wa Is-
raeli. Kwa mji wa Betelehemu, Samweli aliita watoto wa Yese
kuonekana mbele yake mmoja mmoja.
Wote wakatokea ila Daudi, mtoto aliyekuwa akilinda kondoo.
Samweli alitaka kuchagua Eliabu, mwana wa kwanza, lakini Mungu
alimwambia, “Usiangalie use wake, wala urefu wa mwili wake; kwa
maana nimemkataa. Kwa maana Bwana haoni kama mtu anavyoona,
maana mtu anaangalia kuonekana kwa inje, lakini Bwana anatazama
moyo” (1 Samweli 16:1-13).
Wakamwita Daudi. Mungu alimwagiza nabii, “Simama umpakae;
kwa maana huyu ni yeye. Halafu Samweli akachukua pembe ya
mafuta, akampakaa kati ya ndugu zake; na roho ya Bwana alikuja na
uwezo juu ya Daudi tangu siku ile” (1 Samweli 16:12-13). Mungu
akachagua Daudi, mtumishi wake, akamwondoa katika mazizi ya ko-
ndoo (Zaburi 78:70).
Kristo alizaliwa kwa uzazi wa Daudi kwa njia ya mama yake (Luka
1:31-32). Yeye ni Mwana wa Mungu, Mchaguliwa mwenye heshima
(1 Petro 2:6).
Maana ya “Kristo” ni “Mpakaliwa.” Wakati Yesu alipobatizwa
katika Yorodani, kwa kutoka mtoni, Roho ya Mungu alimshukia kwa
sura ya hua. Mungu alimshuhudia akipaza sauti toka mbinguni
akisema, “Wewe ndiwe Mwana wangu, mpendwa wangu, ninape-
ndezwa nawe” (Marko 1:11).
Daudi alipakaliwa na mafuta (sura ya Roho Mtakatifu) kuonyesha
ya kuwa yeye ni mfalme wa watu wa Mungu duniani (Waisraeli).
Vivyo hivyo Mwana wa Mungu aliyezaliwa kwa mbegu ya Mfalme
Daudi alionyeshwa kuwa Kristo Mpakaliwa. Yeye ni Kichwa cha watu
wa Mungu, wenyeji wa mbingu.
57
Daudi alichaguliwa kutawala ufalme wa taifa la dunia. Ali-
pakaliwa ajulikane kuwa mfalme, akitumika kwa uwezo wa roho ya
Mungu (1 Samweli 16:13). Roho ya Mungu alishukia Kristo aliye-
chaguliwa na Mungu kuwa Mfalme wa wafalme na Bwana ya wa-
bwana (Matendo 4:26-28; Ufunuo 19:11-16). Yeye ana ufalme usio na
mwisho.
Ndugu zake Daudi walimbeua (1 Samweli 17:28). Vivyo hivyo
ndugu zake Yesu hawakumwamini (Yoane 7:5; Marko 6:26; Yoane
1:11; Luka 9:22).
Daudi, akitaja jina la Yehova, alishindana na adui Goliata. Ali-
mshinda na kitu cha uzaifu, ndilo jiwe (1 Samweli 17:49-50).
Bwana Yesu Kristo alishinda adui Shetani na kitu cha uzaifu ndiyo
mauti ya msalaba. Tunasoma, “Kwa njia ya kufa apate kuharibu yeye
aliyekuwa na nguvu za kufa, ndiye Shetani, na kuwafungua wale wote
waliokuwa maisha yao yote katika hali ya utumwa, kwa woga wa
mauti” (Waebrania 2:14-15).
Wakati Daudi alipokataliwa na kuzarauliwa, alijiondosha katika
mji, akijificha ndani ya pango la Adulamu. Watu wachache walitoka
mjini wakimfikia na kuambatana naye pangoni (1 Samweli 22:1-2).
Vivyo Kristo sasa ni inje ya kambi ya dunia. Hashikamani na hali
ya ulimwengu wa sasa. Kazi ya Roho Mtakatifu sasa ni kuita watu ku-
toka katika dunia ya uovu kujitenga, kuwa kundi kwa jina lake. Hii ni
“eklesia” ndilo Kanisa la watu wanaotoka kukuta Yesu inje ya kambi
(Matendo 15:14).
Soma Yoane 17:14-17 na Yoane 15:19. Watu wa dunia wali-
chukia Yesu; watatuchukia sisi. “Twende kwake inje ya kambi, tu-
kichukua laumu lake” (Waebrania 13:13).
Daudi amefanana na Kristo kwani alikuwa mlinzi wa kondoo
(1 Samweli 16:11; 17:15). Alipiga vita kuponyesha kondoo zake kwa
adui simba na dubu (1 Samweli 17:34-36).
Bwana Yesu alijiita mwenyewe Mchungaji Mwema. Alijitoa kwa
ajili ya kondoo zake, ndio watu wake (Yoane 10:11,14). Kwa kufa
kwake anapatia kondoo zake uzima wa milele.
Kwa Luka 15:4-7 tunasoma juu ya mchungaji anayetafuta kondoo
58 MIFANO YA KRISTO
yake mpotevu. Akimkuta akafurahi na shangwe. Mbingu inajaa furaha
wakati mwenye zambi anapotubu, akiponyeshwa na Kristo, Mchun-
gaji Mwema.
Tulikuwa tukipotea kama kondoo, lakini sasa tumerudi kwa
Mchungaji na Mwangalizi wa roho zetu. (Tazama 1 Petro 2:25).
Tupendane na Mwokozi Yesu sasa kwa wakati wa kukataliwa
kwake kama Yonatana alivyopendana na Daudi. Yonatana alikuwa na
mapatano na Daudi kwa kuwa alimpenda kama nafsi yake mwenyewe.
Yonatana aliondosha vazi alilovaa, akampa Daudi, na nguo zake, hata
upanga wake na upindi wake na mshipi wake (1 Samweli 18:3-4).
Yonatana akapendezwa sana na Daudi (1 Samweli 19:2), akasifu
Daudi (1 Samweli 19:4) , akamwambia Daudi, “Kitu gani nafsi yako
inachotaka nitakufanyia” (1 Samweli 20:4).
Mungu atupe roho namna ya Yonatana mbele ya Daudi hata sisi
tupendane na Kristo hivi. Tuwe tayari kutoa vitu vyetu vyote mbele
yake na kumwambia, “Nitafanya vitu vyote unavyovitaka nifanye.”
Hivi mapenzi yake yatatutawala na mapatano yetu na Kristo yatahaki-
kishwa katika matendo ya mapendo.
Daudi na Kristo 59
JUMLISHO
Tumefika kwa mwisho wa kitabu hiki. Tumepata mifano mingi katika
Agano la Kale juu ya Bwana Yesu. Wakati tunaposoma Agano Jipya,
tunafahamu namna mifano hii inafanana na Mwokozi wetu. Hivi tu-
napata masawanisho na maelezo juu ya hali ya Bwana na maisha yake
na mauti yake.
Tusikwame juu ya vivuli, tuendelee kwa maana ya kweli katika
Yesu mwenyewe. Waebrania 10:1 linasema, “Basi kwa kuwa torati ni
kivuli cha yale mema yatakayokuwa, wala si sura yao yenyewe.” Tu-
endelee mbele, kufahamu maana ya torati na vivuli vingine kupata
maana ya kweli ndani yao juu ya Bwana Yesu aliyefika duniani, si
kuharibu torati, lakini kuitimiza. (Soma Matayo 5:17).
Kuna mifano mingi mingine katika Agano la Kale inayofanana na
Yesu. Yona, kukaa ndani ya samaki siku tatu na usiku tatu, anafanana na
Yesu katika kaburi (Matayo 12:40). Boazi wa jamaa ya bwana yake Ruta
anafanana na Yesu aliyejifananisha kuwa mtu akomboe Kanisa, tuwe
bibi yake (Ruta 4:1,6,9,10). Kamba nyekundu Rahaba aliyofunga juu ya
ukuta wa Yeriko kwa kujiponyesha na jamaa yake inatuku-mbusha juu
ya damu ya Yesu kutupatia wokovu na amani (Yosua 2:21; 6:17, 25).
Hata mawe 12 yaliyowekwa ndani ya Yorodani wakati Waisraeli
walipovuka ngambo kwa inchi kavu ni sura ya Mwokozi Yesu akizama
chini ya gazabu ya Mungu msalabani. (Tazama Zaburi 42:7). Waisraeli
walipanga mawe mengine 12 kwa pwani kando ya Yorodani katika
Kanana. Mawe 12 ndani ya mto yalikomboa mawe 12 ya kupona kwa
pwani ya Yorodani. Sura ya ukombozi wa Kristo kwa watu wake!
Mbele ya mambo haya, wakati wa kusafiri kwa Waisraeli ja-
ngwani, walifika kwa maji machungu “Mara.” Walikuwa na kiu lakini
hawakuweza kunywa maji pale. Walinungunika juu ya Musa. Yeye
aliomba Mungu. Alimwonyesha mti. Wakati Musa alipotupa mti ule ndani
ya maji machungu yaligeuka matamu. Watu wakakunywa, wakapona. Pale
tunapata sura ya msalaba — kuleta uzima badala ya mauti.
Biblia inajaa na maneno mazuri mazuri — kama hazina ya damani.
Tutafutetafute ndani yake kupata mali kufurahisha roho zetu na roho za
wengine kwa utukufu wa Mwokozi wetu Yesu Kristo.
60
Top Related