foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

26
FOREWORD BY KENYA EVALUATION ASSOCIATION_KEA The translation of key terms used in aid evaluations and results based management into Kiswahili is motivated by the fact that Kiswahili is used widely across the vast region of East, Central and parts of Southern African countries, where virtually all the countries in this region are beneficiaries of development aid. Development evaluation and the politics of aids have aroused interest among a variety of stakeholders: aid agencies, civil society, community based organisations, government agencies and departments, academic institutions, the media and the private sector. Although European languages have been dominant in aid administration and evaluation until now there is evidence that Kiswahili is claiming it's rightful place as the lingua franca, national and official language in many countries in Africa. It is widely used as a language of the communication by community groups, NGOs and local government officials in active development planning, implementation and evaluation. It is important therefore, to avail at the earliest opportunity this standardised terminology that is currently used by international development partners and evaluators. Kenya Evaluation Association founded in 1999, is proud to spearhead this KISWAHILI version of the GLOSSARY. The process has benefited from inputs of a wide range stakeholders. Amongst these was Dr. Omboga Zaja who translated the terms from English into Kiswahili and a select panel of experts compromising KEA members, evaluation practitioners and development scholars from regional universities who ratified the translations at the workshop held in Nairobi_Kenya on 17th to 19th November 2005. KEA would like to thank the OECD/ DAC Network on Development Evaluation for funding the translation and the publication of this glossary. Karen T. Odhiambo(Ph.d) _ Chair Lecturer _ University of Nairobi, Kenya www.kenyaevaluation.org 1

Transcript of foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

Page 1: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

FOREWORD BY KENYA EVALUATION ASSOCIATION_KEA

The translation of key terms used in aid evaluations and results based management into Kiswahili is motivated by the fact that Kiswahili is used widely across the vast region of East, Central and parts of Southern African countries, where virtually all the countries in this region are beneficiaries of development aid. Development evaluation and the politics of aids have aroused interest among a variety of stakeholders: aid agencies, civil society, community based organisations, government agencies and departments, academic institutions, the media and the private sector. Although European languages have been dominant in aid administration and evaluation until now there is evidence that Kiswahili is claiming it's rightful place as the lingua franca, national and official language in many countries in Africa. It is widely used as a language of the communication by community groups, NGOs and local government officials in active development planning, implementation and evaluation. It is important therefore, to avail at the earliest opportunity this standardised terminology that is currently used by international development partners and evaluators.

Kenya Evaluation Association founded in 1999, is proud to spearhead this KISWAHILI version of the GLOSSARY. The process has benefited from inputs of a wide range stakeholders. Amongst these was Dr. Omboga Zaja who translated the terms from English into Kiswahili and a select panel of experts compromising KEA members, evaluation practitioners and development scholars from regional universities who ratified the translations at the workshop held in Nairobi_Kenya on 17th to 19th November 2005.

KEA would like to thank the OECD/ DAC Network on Development Evaluation for funding the translation and the publication of this glossary.

Karen T. Odhiambo(Ph.d) _ Chair Lecturer _ University of Nairobi, Kenya

www.kenyaevaluation.org

1

Page 2: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

UTANGULIZI WA KENYA EVALUATION ASSOCIATION

Tafsiri ya istilahi zinazotumika katika tathmini za misaada na usimamizi wa kimatokeo kwa Kiswahili imemotishwa na ukweli kwanba Kiswahili ni lugha inayotumika katika eneo pana la mashariki, kati ya kusini mwa Afrika, ambamo karibu nchi zote zilizoko katika eneo hili zimefaidika na misaada ya ufadhili wa kimaendeleao. Tathmini za maendeleo pamoja na siasa zinazohusiana na misaada ya ufadhili wa maendeleo ni mambo ambayo yamewashughulisha wadau wa aina nyingi wakiwemo: mashirika ya misaada, mashirika tetezi ya umma, mashirika ya nyanjani, mashirika na idara za serikali, taasisi za kielimu, mashirika ya uandishi wa habari na sekta za kibinafsi. Hata kama lugha za Ulaya zimekuwa katika mstari wa mbele katika usimamizi na tathmini za misaada, kuna ushahidi kwamba lugha ya Kiswahili imeanza kujitokeza kwa nguvu kama lugha ya mawasiliano inayotumiwa kwa upana na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, maofisa wa serikali, maofisa wa serikali katika sehemu za nyanjani wanaohusika na usanifu , utekelezwaji na tathmini za maendeleo. Ni muhimu, kwa hivyo, kuwasilisha mapema iwezekanavyo, istilahi zilizosanifiwa, zinazokubalika na zinazotumiwa na Washirika wa Kimaendeleo wa kimataifa pamoja wa watathmni wa misaada ya maendeleo.

Shirika la Kenya Evaluation Association, lililoanzishwa mwaka 1999, lina fahari kuongoza FAHARASA hii ya istahili zilizotafsiriwa kwa Kiswahili. Mchakato wote wa shughuli hii umefaidika kutokana na michango ya wadau wengi. Miongoni mwao ni Dkt. Omboga Zaja aliyetafsiri istilahi hizi kutoka Kiingereza hadi Kiswahili pamoja na jopo la wataalamu wakiwemo wanachama wa KEA, wataalamu wa tathmini, wasomi wa taaluma ya maendeleo na wahadhiri kutoka vyuo vikuu vya eneo hili walioshiriki katika warsha iliyoidhinisha tafsiri za istilahi hizi mnamo tarehe 17 hadi 19 Novemba 2005, Nairobi_Kenya.

Shirika la KEA lingependa kutoa shukrani kwa OECD/DAC juu ya mtandao wa tathmini za maendeleo kwa kufadhili tafsiri na uchapishali wa faharasa hii.

Karen T. Odhiambo(Ph.d) _ Mwenyekiti Mhadhiri_Chuo Kikuu Nairobi, Kenya

www.kenyaevaluation.org

2

Page 3: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

FOREWORD BY DAC NETWORK ON DEVELOPMENT EVALUATION

The publication of the Kiswahili version of the Glossary of Key Terms in the Evaluation and Results Based Management is an important development which will contribute to strengthening the use and quality of evaluation and will facilitate communication among evaluation experts and with non evaluation practitioners.

We would like to express our thanks to the Kenya Evaluation Association, and it's chair Dr. Karen T Odhiambo for taking this initiative and producing a Kiswahili version of the glossary. This compliments the other existing language versions of the glossary which are available on the network of the DAC Evaluation Network.

Eva Litman _ Chair Hans E. Lundgren _ Co-ordinator

www.oecd.org / dac / evaluationnetwork

3

Page 4: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

UTANGULIZI WA DAC MTANDAO WA TATHMINI ZA MAENDELEO

Uchapishaji wa Faharasa ya Kiswahili ya Istilahi zinazotumika katika Tathmini na Usimamizi wa Kimatokeo ni tukio muhimu litakalochangia kuimarisha matumizi na ubora wa tathmini pamoja na kuwezesha kuwepo kwa mawasiliano miongoni wa wataalam wa tathmini na baina ya wataalam wengineo wasiokuwa katika taaluma ya tathmini.

Tungependa kutoa asante zetu kwa shirika la Kenya Evaluation Association, Mwenyekiti wake, Dkt. Karen T. Odhiambo, kwa kuchukua hatua hii inaongeza mchhango wa maana kwa faharasa zilizoko katika lugha nyinginezo na ambazo zinapatikana katika tovuti ya DAC.

Eva Litman _ Mwenyekiti Hans E Lundgren _ Mshirikishi

www. oecd. org / e valuationnetwork

4

Page 5: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

Jopo Kazi la Kamati ya Misaada ya Maendeleo juu ya Tathmini za Misaada ni baraza la Kimataifa ambapo wataalam wa tathmini kutoka Mashirika ya Wafadhili hukutana mara kwa mara kubadilishana mawazo na tajriba na kutafuta njia za kuboresha na kuimarisha shughuli ya utathmini kama chombo katika sera za ushirikiano wa kimaendeleo.

Baraza hili linafanya kazi chini ya usimamizi wa Kamati ya Misaada ya Maendeleo ambayo kwa wakati huu ina wawakilishi 30 kutoka kwa wanachama wa Shirika la Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo (OECD—Organization for Economic Co-operation and Development) pamoja na mashirika ya wafadhili [Australia, Austria, Ubeligiji, Canada, Denmark, Umoja wa Nchi za Ulaya, Ujerumani, Greece, Ireland, Italy, Japan, Luxemburg, Netherlands, New Zealand, Norway, Portugal, Spain, Sweden, Switzerland, Uingereza, Merikani, Benki Kuu y Dunia, Benki ya Maendeleo ya Asia, Benki ya Maendeleo ya Africa, Benki ya Maendeleo ya Nchi za Amerika, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Shirika la Fedha Duniani].

Habari zaidi inaweza kupatika kutoka kwa Hans Lundgren, mshauri juu ya Ufaafu wa Misaada, Shirika la OECD, Halmashauri ya Ushirikiano wa Kimaendeleo, 2 rue Andre—Pascal, 75775 Paris Cedex 16, France. Tovuti: www.org/dac/evaluation.

5

Page 6: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

TERMS GROUPED BY CATEGORIES ISTILAHI KWA MUJIBU WA M A K U N D I

Quality assurance

Appraisal

Audit

Conclusions

Evaluability

Evaluation

Feedback

Finding

Monitoring

Lessons learned

Performance measurement

Quality Assurance

Recommendations

Results Based Management

Stakeholders

Beneficiaries

Partners

Reach

Stakeholders

Target Group

Logical Framework

Activity

Assumptions

Uhakika/Udhamini wa ubora

Tathmini

Ukaguzi

Mahitimisho

Utathrninikaji

Tathmini

Upokezi wa maoni

Matokeo

Usimamizi

Funzo

Upimaji wa utekelezwaji

Uthabiti wa Ubora

Mapendekezo

Usimamizi wa Kimatokeo

Wadau

Wafadhiliwa

Washirika wa Maendeleo Msambao wa Wafadhiliwa wa kimaendeleo

Wadau

Walengwa

Mf umo wa Kimantiki

Shughuli

Chukulizi

Devopment objective

Logical Framework

Results-Based Management

Benchmark

Inputs

Outcome

Outputs

Indicator

Performance

Performance Indicator

Performance Measurement

Project or program objective

Purpose

Results

Results chain

Results Framework

Results-based Management

Evaluation Tools, Measures,

Analyses and Criteria

Accountability

Analytical tools

Attribution

Base-line Study

Lengo la kimaendeleo

Mfumo wa kimantiki

Usimamizi wa Matokeo

Kigezo mahususi

Pembejeo za kimaendeleo

Matokeo

Mazao

Kiashirii

Utekelezwaji

Kiashirii cha Utekelezwaji

Upimaji wa Utekelezwaji

Lengo la Mradi au Mpango

Dhamira

Matokeo

Mfuatano wa Matokeo

Mfumo wa Kimatokeo

Usimamizi wa Kimatokeo

Zana, Vipimo, Uchanganuzi

na Vigezo vya Tathmini

Uwajibikaji

Zana za Uchanganuzi

Uhusishwaji

Uchunguzi wa Kimsingi

6

Page 7: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

Counterfactual

Data collection tools

Development Intervention

Economy

Effect

Effectiveness

Efficiency

Feedback

Goal

Impacts

Institutional Development

Impact

Lessons Learnt

Reach

Relevance

Terms of reference

Triangulation

Validity

Types of Evaluation

Cluster Evaluation

Country' Program

Evaluation

Country Assistance

Evaluation

Kinyume cha Uhalisi

Zana za ukusanyaji data

Ufadhili wa Kimaendeleo

Usarifu

Athari

Ufaafu wa Matokeo Tarajiwa

Ufaafu

Upokezi wa maoni

Shabaha

Taathira

Taathira katika Maendeleo

ya Kitaasisi

Mafunzo Yaliyopatikana

Msambao wa Walengwa

Umuhimu

Hadidu za Rejea

Uthibitishwaji

Uhalali

Aina za Tathmini

Tathmini Fungu

Tathmini ya Mpango katika

nchi maalum

Tathmini ya Misaada katika

nchi maalum

Ex-ante evaluation

Ex-post Evaluation

External Evaluation

Formative Evaluation

Independent Evaluation

Internal Evaluation

Joint Evaluation

Mid-term Evaluation

Participatory Evaluation

Process Evaluation

Program Evaluation

Project Evaluation

Review

Risk Analysis

Sector Program Evaluation

Self-evaluation

Summative Evaluation

Thematic Evaluation

Tathmini ya Awali

Tathmini Fuatilizi

Tathmini ya Nje

Tathmini Sarifu

Tathmini Huru

Tathmini ya Ndani.

Tathmini ya Pamoja

Tathmini ya muda katika

Utekelezwaji

Tathmini Shirikishi

Tathmini ya Mchakato

Tathmini ya Mpango

Tathmini ya Mradi

Ukaguzi wa Utekelezwaji

Uchanganuzi wa Vitisho na

Hatari

Tathmini ya Mpango katika

Sekta Maalum

Tathmini ya Kibinafsi

Tathmini ya Jumla

Tathmini ya Malengo

Maalum

7

Page 8: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

Uwajibikaji Ulazima wa kudhihirisha na kuhakikisha kwamba kazi imetekelezwa kwa mujibu wa kanuni na viwango vilivyowekwa au kuripoti kikweli na kwa usahihi juu ya matokeo ya utekelezwaji kwa kuhusiana na majukumu na /au mipango. Hii inaweza kuhitaji udhihirishaji wa makini na uwezao kutetewa kisheria kwamba kazi imetekelezwa kulingana na masharti ya mkataba. Kumbuka: Uwajibikaji katika masuala ya maendeleo unaweza kurejelea ulazima wa wabia kutenda kazi dhahiri kwa mujibu wa wajibu na majukumu yaliyowekwa pamoja na matarajio ya utekelezwaji; na mara nyingi kwa kuzingatia matumizi ya busara ya rasilimali. Kwa watathmini, uwajibikaji una maana ya wajibu wa kutoa ripoti za usimamizi na utekelezwaji zilizo sahihi, hakika na za kuaminika. Kwa wakurugenzi na wabunaji sera katika sekta za umma, uwajibikaji ni kwa walipaji kodi/umma.

Shughuli Maamuzi yanayofanywa au kazi iliyofanywa ambayo kupitia kwayo mambo kama pesa, misaada ya kitaalam na aina nyingine za rasilimali huhamasishwa ili kuzalisha mazao dhahiri. Istilahi Nasaba: Ufadhili wa Kimaendeleo.

Zana za Uchanganuzi Taratibu zinazotumiwa kuchanganua na kufasiri habari wakati wa utathmini.

Tathmini Tathmini ya jumla kuhusu umuhimu, ufaafu na uwezekano wa kudumishwa kwa ufadhili wa kimaendeleo kabla ya kutolewa kwa maamuzi ya kutoa misaada.

8

Page 9: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

Kumbuka: Katika mashirika ya kimaendeleo, benki, n.k. umuhimu wa tathmini ni kwamba tathmini unawawezesha watoaji maamuzi kukadiria iwapo mradi unaonuiwa umebuniwa kwa njia zitakazotumia raslimali za shirika kwa njia ya busara. Istilahi Nasaba: Tathmini ya awali.

Chukulizi Chukulizi za mambo au hatari zinazoweza kuathiri maendeleo au kufanikiwa kwa ufadhili wa kimaendeleo. Kumbuka: Chukulizi zinaweza kueleweka kama hali zinazokisiwa kuwepo na ambazo zitachangia usahihi wa tathmini zenyewe kama vile, sifa za idadi ya watu au wakaazi wakati wa kutayarisha taratibu za uchanganuzi awali wa sampuli au ukaguzi wa awali. Chukulizi zinawekwa wazi katika tathmini za kinadharia ambapo tathmini hufuatilia matokeo yanayotarajiwa hatua kwa hatua.

Uhusishwaji Sifa ya uhusishwaji wa mahusiano yaliyoko kati ya mabadiliko yanayochunguzwa (au yanayotarajiwa kuchunguzwa) na mabadiliko yatakayoletwa na ufadhili maalum wa kimaendeleo. Kumbuka: Uhusishwaji unarejelea kile kiini ambacho kinahusika hasa katika mabadiliko ambayo yamedhihirika au katika matokeo ambayo yamepatikana. Unawakilisha kiasi ambacho matokeo fulani yatasemekana kuwa yamesababishwa na ufadhili fulani, au yametokana na kuhusika kwa mshirika fulani wa kimaendeleo au fadhila nyingine za kimaendeleo (zinazotarajiwa au zisizotarajiwa), sababu nyingine zisizotarajiwa na pengine miyumbisho kutoka nje.

9

Page 10: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

Ukaguzi Kitendo cha ukaguzi huru kinachobuniwa na kusanifiwa kuongeza thamani na kuboresha utenda kazi wa shirika. Ukaguzi huu husaidia shirika kufanikisha malengo yake kwa kuzingatia utekelezwaji wa mambo hatua kwa hatua, kufuata mielekeo yenye nidhamu katika kukadiria na kuimarisha taratibu zinazoleta matokeo yanayotarajiwa pamoja na kupunguza hatari katika taratibu za ukurugenzi, usimamizi na utawala. Kumbuka: Kuna tofauti ya kimsingi kati ya ukaguzi unaofanyika mara kwa mara (hasa wa kifedha) unaoshughulika na kufuatwa kwa kanuni na masharti yaliyowekwa katika matumizi ya fedha; na ukaguzi wa kiutendaji unaojishughulisha na ufaafu, usarifu, umathubuti na upatikanaji wa matokeo yanayotarajiwa. Ukaguzi wa ndani hutoa ukadiriaji wa taratibu za usimamizi zinazofuatwa na kitengo cha ukaguzi kilicho chini ya wakurugenzi. Nao ukaguzi wa nje hufanywa na shirika huru.

Kigezo Mahususi Kigezo au kienzo kinachotumiwa kupimia utekelezwaji au upatikanaji wa matokeo yaliyokusudiwa. Kumbuka: Kigezo mahususi kinarejelea utekelezwaji wa ufadhili wa kimaendeleo uliokwisha tekelezwa hivi karibuni na mashirika sawia au katika hali zinazoweza kuwa sawa na za hali ya sasa.

Uchunguzi wa Kimsingi Uchunguzi unaofanywa kueleza hali ilivyo kabla ya ufadhili wa kimaendeleo. Hali hii huwa kigezo cha kupima na kukadiria maendeleo yatakayopatikana au pia kufanya ulinganishaji.

10

Page 11: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

Wafadhiliwa Watu binafsi, makundi ya watu au mashirika, yanayolengwa au yasiyolengwa, yanayofaidi moja kwa moja au kwa njia zisizo za moja kwa moja kutokana na ufadhili wa kimaendeleo.

Tathmini Fungu Utathmini unaofanyiwa shughuli, miradi na / au mipango ya maendeleo inayohusiana.

Mahitimisho Mahitimisho huashiria mambo yanayohusiana na kufanikiwa au kutofanikiwa kwa ufadhili wa kimaendeleo unaofanyiwa tathmini, huku ikitilia maanani matokeo na athari za manufaa zilizokusudiwa na zile ambazo hazikukusudiwa, hali kadhalika inamulika kijumla manufaa mengine au udhaifu unaohusiana na ufadhili wa kimaendeleo. Mahitimisho hutegemea data iliyokusanywa pamoja na hoja za wazi zinazotokana na data hiyo.

Uhalisi wa Kinyutne Hali ya mambo ambayo inakisiwa kimawazo kuwepo miongoni mwa watu, mashirika au makundi ya watu lau kama hakungekuwa na ufadhili wa kimaendeleo

Ufadhili wa Kimaendeleo Chombo au ufadhili wa mshirika wa kimaendeleo (mfadhili au asiye mfadhili) kinachokusudiwa kufadhili au kuchangia maendeleo.

11

Page 12: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

Tathmini ya Mpango au Usaidizi katika Nchi Maalum

Tathmini ya mipango ya pesa ya mfadhili au shirika moja au mashirika mengi juu ya ufadhili wa kimaendeleo, pamoja na mikakati ya usaidizi inayohimili ufadhiliwa huo.

Zana za Ukusanyaji Data Taratibu zinazotumiwa kutambua na kubainisha vyanzo vya habari pamoja na ukusanyaji wa habari hiyo wakati wa utathmini.

Lengo la Maendeleo Taathira ya kimaendeleo inayokusudiwa kuchangia kuboresha na kunufaisha nchi, jamii au kundi la watu; kihali, kifedha, kitaasisi, kimazingira au kwa njia nyingine yoyote ile kupitia kwa ufadhili wa kimaendeleo.

Usarifu Ukosefu wa uharibifu au ufujaji wa rasilimali katika mpango wowote wa kimaendeleo. Kumbuka: Shughuli yoyote husemekana kwamba haina usarifu wakati ambapo hakuna uharibifu au ufujaji wa rasilimali wakati ambapo gharama za raslimali adimu zinazotumika kuitekeleza zinawiana na gharama za chini kabisa zinazohitajika kupata malengo yaliyopangwa.

12

Page 13: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

Ufaafu wa Matokeo Tarajiwa Kiasi cha upatikanaji wa malengo ya ufadhili wa kimaendeleo yaliyokusudiwa, au yanayotarajiwa kupatikana kwa mujibu wa umuhimu wa malengo hayo. Kumbuka: Upatikanaji wa malengo unatumiwa pia kama kipimo cha wastani (au mahitimisho juu ya) ustahili au thamani ya shughuli yoyote ya ufadhili, yaani kiwango cha malengo yaliyopatikana au yanayotarajiwa kupatikana kutokana na ufadhili wa kimaendeleo, malengo yake ya kimsingi, udumishwaji wake na taathira nzuri kwa maendeleo ya kitaasisi.

Ufaafu Kipimo cha jinsi rasimali, pembejeo za kimaendeleo au mitaji ya kimaendeleo (fedha, utaalam, wakati, n.k.) zinavyotumiwa kuzalisha matokeo.

Athari Athari au matokeo yanayotarajiwa au yasiyotarajiwa, ya moja kwa moja au yasiyo ya moja kwa moja yanayotokana na ufadhili wa kimaendeleo. Istilahi Nasaba: matokeo, mazao.

Utathminikaji Kiwango au upeo unaotumika kupima shughuli au mradi kwa njia ya kutegemewa na kuaminika. Kumbuka: Utathminikaji wa tathmini huhitaji uchunguzi wa mapema wa shughuli inayohitaji kutekelezwa ili iweze kukadiriwa kama malengo yake yamesanifiwa vizuri na kama matokeo yake yanaweza kuthibitishwa.

13

Page 14: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

Tathmini Uchunguzi halisi na wa hatua kwa hatua unaofanywa juu ya mradi, mpango wa kimaendeleo au sera ya kimaendeleo inayoendelea au iliyokwisha kutekelezwa, miundo yake, utekelezwaji wake na matokeo yake. Lengo lake ni kuukilia na kupima ufaafu wake, utimizwaji wa malengo ya kimaendeleo, ufanisi wa kimaendeleo, taathira na udumishwaji wao. Ni sharti tathmini itoe habari inayoaminika na iwezayo kutumika na iwezeshayo kuingizwa kwa mafunzo yaliyopatikana katika mifumo na taratibu za kutoa maamuzi kwa wafadhiliwa na wafadhili. Tathmini pia inarejelea taratibu za kupima umuhimu au maana ya shughuli za kimaendeleo, sera au mpango wa kimaendeleo unaotekelezwa kihalisi na hatua kwa hatua kwa kadiri iwezekanavyo juu ya ufadhili wa kimaendeleo unaopangwa, unaoendelea au uliokamilishwa. Kumbuka: Katika baadhi ya hali fulani fulani tathmini inahusu ufafanuzi wa viwango na kanuni mwafaka, ukadiriaji wa utekelezaji kwa mujibu wa viwango na kanuni hizo, ukadiriaji wa matokeo halisi na matokeo yanayotarajiwa pamoja na ubainishaji wa mafunzo. Istilahi Nasaba: Udurusu

Tathmini ya Awali Tathmini inayofanywa kabla ya kutekelezwa kwa ufadhili wa kimaendeleo.

14

Page 15: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

Tathmini Fuatilizi Ni tathmini inayofanyiwa ufadhili wa kimaendeleo baada ya ufadhili huo kutekelezwa. Kumbuka: Tathmini hii inaweza kufanywa mara tu baada ya kutekelezwa kwa ufadhili huo au kitambo kirefu baada ya kutekelezwa kwa ufadhili wenyewe. Dhamira ya tathmini hii ni kubainisha mambo yanayochangia ufanisi au yanayozuia ufanisi huo, kukadiria udumishwaji wa matokeo au taathira za ufadhili wa kimaendeleo, pamoja na kutoa mahitimisho yanayoweza kutumiwa wakati wa usanifu wa fadhili nyingine za kimaendeleo.

Tathmini ya Nje Ni tathmini inayofanyiwa ufadhili wa kimaendeleo na mashirika na /au watu ambao hawatoki katika mashirika ya wafadhili au ya watekelezaji wa ufadhili wa maendeleo.

Tathmini Sarifu Tathmini inayokusudiwa kuboresha utekelezwaji wa kimaendeleo, ambayo kwa kiasi kikubwa hufanywa katika awamu ya utekelezwaji wa miradi au mipango. Kumbuka: Tathmini sarifu zinaweza pia kufanywa kwa sababu nyinginezo kama vile kwa sababu ya kuafikiana na mahitaji ya kisheria au kama sehemu ya tathmini kubwa. Istilahi Nasaba: Tathmini ya mchakato.

Upokezi wa Maoni Upokezi na uwasilishaji wa matokeo yaliyopatikana kutokana na taratibu za tathmini kwa wote wanaohusika na wanaonufaishwa na ufadhili wa kimaendeleo ili kuzindua mafunzo. Uwasilishwaji huu wa maoni unaweza kuhusisha ukusanyaji na usambazwaji wa matokeo, mahitimisho, mapendekezo na mafunzo yatokanayo na tajriba.

15

Page 16: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

Shabaha Kile kinachotarajiwa kupatikana kutokana na ufadhili wa kimaendeleo. Istilahi Nasaba: Malengo ya kimaendeleo.

Tathmini Hum Tathmini inayotekelezwa na mashirika au watu wasiokuwa chini ya usimamizi wa wale waliosanifu au wanaotekeleza ufadhili wa kimaendeleo. Kumbuka: Kuaminika kwa utathmini kunategemea kwa kiasi fulani uhuru uliokuwako wakati wa kufanywa kwa utathmini huo. Uhuru huu una maana ya kutokewepo kwa ushawishi wa kisiasa au shinikizo za mashirika husika. Una sifa ya uhuru kamili katika udadisi na uwasilishaji wa matokeo.

Taathira Matokeo chanya na hasi ya kimsingi au ya ziada ya muda mrefu, ya moja kwa moja au yasiyo ya moja kwa moja, yaliyokusudiwa au yasiyokusudiwa, yanayotokana na ufadhili wa kimaendeleo.

Kiashirii Kipengee au kiarifu cha idadi au ubora kinachotoa njia rahisi na ya kutegemewa katika kukadiria mafanikio, kuangaza mabadiliko yanayosababishwa na ufadhili wa kimaendeleo, au inayotumiwa kupima utekelezaji wa mshirika mmoja wa maendeleo.

Pembejeo za Kimaendeleo Rasilimali za kifedha, binadamu, na vifaa vinavyotumiwa katika ufadhili wa kimaendeleo.

16

Page 17: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

Taathira katika Maendeleo ya Kitaasisi Kiwango au kiasi ambacho kwacho ufadhili wa kimaendeleo huboresha au hudhalilisha uwezo wa nchi au eneo fulani kutumia kwa ufanisi, usawa na kwa njia ya kudumisha rasilimali ya binadamu, fedha na malighafi, kwa mfano, (a) ufafanuzi bora, uthabiti, uwazi, utumikizwaji na utabirikaji wa mipangilio ya taasisi, (b) usawazishaji bora wa malengo, uwezo na majukumu ya shirika yanayotokana na mipangilio ya taasisi. Taathira kama hizo zinaweza kujumuisha matokeo yasiyotarajiwa ya shughuli za kimaendeleo.

Tathmini wa Ndani Tathmini inayofanyiwa ufadhili wa kimaendeleo unaotekelezwa na kitengo n a / a u watu walioajiriwa na wanaowajibikia wafadhili, washirika wa maendeleo au mashirika ya utekelezaji. Istilahi Nasaba: tathmini ya kibinafsi

Tathmini ya Patnoja Tathmini inayoleta pamoja na kushirikisha mashirika mbalimbali ya wafadhili na washirika wa maendeleo. Kumbuka: Kuna daraja mbalimbali za ushirikishwaji kutegemea ni kwa kiasi gani wafadhili binafsi wanashiriki katika tathmini, wanavyoleta pamoja rasilimali zao na kuziunganisha ripoti zao za tathmini. Tathmini ya pamoja inaweza kusaidia kuepuka matatizo ya ukisiaji kuhusu ufanifu wa mipango na mikakati ya mipango hiyo, ushirikishwaji wa juhudi zinazoungwa mkono na wafadhili mbalimbali, pamoja na ubora wa kuratibu misaada.

17

Page 18: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

Funzo Mahitimisho ya kijumla kutokana na uzoevu wa tathmini za miradi, mipango au sera zinazoangazia hali halisi na jinsi zinavyoweza kutumika katika miktadha maalum. Mara kwa mara mafunzo yanayopatikana yanaonyesha ubora na udhaifu katika maandalizi na usanifu wa kimaendeleo, na jinsi mambo hayo yanavyoathiri utekelezwaji wa ufadhili, matokeo na taathira zake.

Mfumo wa Kimantiki Chombo cha usimamizi kinachotumiwa kuboresha usanifu wa fadhili za kimaendeleo, mara nyingi katika kiwango cha mradi. Chombo hiki kinahusisha ubainishaji wa elementi za kimkakati (mitaji, matokeo, mazao, taathira) pamoja na mahusiano yao, viashirii, ukisiaji au hatari zinazoweza kuathiri mafanikio au kushindwa kwa ufadhili. Kwa hivyo kinawezesha upangaji na utekelezwaji wa ufadhili wa kimaendeleo. Istilahi Nasaba: usimamizi wa kimatokeo.

Tathmini ya Tathmini Istilahi hii inatumiwa kusanifu tathmini za kukadiria mahitimisho ya wastani ya tathmini mbalimbali. Istilahi hii inatumiwa pia kurejelea tathmini za tathmini zinazotumiwa hasa kukadiria ubora wa tathmini au kukadiria utekelezi wa watathmini.

Tathmini Shirikishi Utaratibu wa kutathmini ufadhili wa kimaendeleo ambapo wawakilishi wa mashirika yanayohusika na wadau (pamoja na wafadhiliwa) hufanya kazi pamoja katika kubuni, kusanifu, kutekeleza na kufasiri tathmini.

18

Page 19: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

Washirika Watu binafsi na / au mashirika yanayoshirikiana katika kupatikana kwa malengo maalum ya kimaendeleo yaliyoafikiwa miongoni mwao. Kumbuka: Dhana ya ushirikiano inaashiria malengo ya pamoja, uwajibikaji wa aina moja na matokeo ya aina moja, mahusiko yanayoridhiana.Washirika wanaweza kuwa ni pamoja na serikali, mashirika ya kutetea umma, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, vyuo vikuu, mashirika ya kutaaluma na kibiashara, mashirika ya nchi mbalimbali, makampuni ya kibinafsi, n.k

Tathmini ya Muda Tathmini inayofanywa kuelekea katika awamu ya katikati ya kipindi cha utekelezwaji wa ufadhili wa kimaendeleo.

Usimamizi Shughuli inayoendelea inayotumia taratibu za kukusanya data hatua kwa hatua kwa kuzingatia kanuni na viashirii vilivyowekwa ili kuwawezesha wakurugenzi na wadau wa kimsingi katika ufadhili wa kimaendeleo unaoendelea ili kupima kiasi cha maendeleo yaliyopatikana au malengo yaliyotekelezwa na jinsi fedha zilizotengwa zilivyotumiwa. Istilahi Nasaba: usimamizi wa utekelezwaji, kiashirii.

Matokeo Matokeo yanayotarajiwa au matokeo ya muda mfupi yaliyopatikana kutokana na ufadhili wa kimaendeleo. Istilahi Nasaba: matokeo, mazao, taathira, athari.

19

Page 20: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

Mazao Mazao, rasilimali au huduma zinazotokana na ufadhili wa kimaendeleo, yanaweza pia kujumuisha mabadiliko yanayotokana na ufadhili huo lakini ambayo ni muhimu katika upatikanaji wa mazao hayo.

Utekelezwaji Kiwango ambacho kwacho ufadhili wa kimaendeleo au washirika wa kimaendeleo hutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa kanuni, vigezo, viwango na miongozo ili kuyafikia matokeo yaliyokusudiwa na kwa kuzingatia malengo yaliyowekwa.

Kiashirii cha Utekelezwaji Kigezo kibadilikacho kwa mujibu wa hali kinachotumika kuthibitisha mabadliko katika ufadhili wa kimaendeleo au kinachotumika kuonyesha jinsi matokeo yanavyohusiana na malengo ya ufadhili. Istalahi Nasaba: usimamizi wa utekelezwaji, upimaji wa utekelezwaji

Upimaji wa Utekelezwaji Utaratibu wa kuchunguza utekelezwaji wa ufadhili wa kimaendeleo kwa mujibu wa malengo yaliyowekwa. Istilahi Nasaba: Usimamizi wa utekelezwaji, kiashirii.

Usimamizi wa Utekelezwaji Utaratibu endelevu wa kukusanya na kuchanganua data ili kupima ni kwa kiasi na kwa ubora gani mradi, mpango au sera ya ufadhili wa kimaendeleo inatekelezwa kwa mujibu wa matokeo yanayotarajiwa.

20

Page 21: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

Tathmini ya Mchakato Tathmini inayopima uwezo wa ndani wa mashirika, sera zao, taratibu zao za uwasilishaji matokeo, mbinu zao za usimamizi na jinsi mambo haya yote yanavyohusiana. Istilahi Nasaba: utathmini sarifu.

Tathmini ya mpango Tathmini ya fadhili kadhaa za kimaendeleo, zilizosanifiwa kutekeleza majukumu maalum katika misingi ya kiulimwengu, kimaeneo, kitaifa au katika sekta maalum za kimaendeleo. Kumbuka: Mpango wa kimaendeleo ni ufadhili wa kimaendeleo uliofungika kiwakati na unaojumuisha shughuli mbalimbali za sekta mbalimbali, malengo mbalimbali na / au maeneo mbalimbali. Istilahi Nasaba: Mpango wa nchi maalum /Mkakati wa tathmini. Matokeo ya kihali, kifedha, kitaasisi, kijamii, kimazingira au mengine yoyote yale yanayotarajiwa kutokana na mradi au mpango wa maendeleo.

Tathmini ya Mradi Tathmini ya ufadhili maalum wa kimaendeleo uliosanifiwa kutekeleza malengo fulani maalum, kwa kutumia kiwango maalum cha rasilimali na kutekelezwa katika kipindi na wakati maalum, mara nyingi chini ya ufadhili mpana wa kimaendeleo. Kumbuka: Uchanganuzi wa gharama ni kigezo maalum katika tathmini za miradi iliyo na manufaa yanayoweza kupimika. Wakati ambapo manufaa hayawezi kupimika kitakwimu, uchunguzi wa gharama za ufanisi ni mwelekeo mwafaka wa kufanyia tathmini.

21

Page 22: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

Lengo la Mradi au Mpango Matokeo ya kihali, kifedha, kitaasisi, kijamii, kimazingira au kimaendeleo yanayotarajiwa kuchangiwa na mradi au mpango wa maendeleo.

Lengo Matarajio yaliyotangazwa wazi yanayotarajiwa kupatikana kutokana na mpango au mradi wa kimaendeleo.

Uthibiti wa ubora Uthibiti wa ubora unahusu shughuli yoyote inayohusu uchanganuzi na uimarishaji wa ustahili au thamani ya ufadhili wa kimaendeleo, au jinsi ufadhili huo unavyoafiki viwango vilivyowekwa. Kumbuka: mifano ya uthabiti wa ubora ni pamoja na tathmini, ukaguzi wakati wa utekelezwaji, pamoja na tathmini za aina mbalimbali. Uthabiti wa ubora unaweza pia kurejelea uchunguzi wa ubora pamoja na ufanisi wa ufadhili wa kimaendeleo.

Mapendekezo Mapendekezo yanayokusudiwa kuimarisha upatikanaji wa matokeo yanayotakiwa, ubora au ufanisi wa ufadhili wa kimaendeleo, yanaweza kuhusu pia usanifu na uandalizi mpya wa malengo; na / au ugavi na utengaji upya wa rasilimali. Mapendekezo ni sharti yahusishwe na mahitimisho.

Umuhimu Kiwango ambacho kwacho malengo ya ufadhili wa kimaendeleo yanaafikiana na matakwa au matarajio ya wafadhiliwa, matakwa ya nchi, vipaumbele vya ulimwengu pamoja na sera za washirika na wafadhili.

22

Page 23: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for

Kumbuka: Kwa usemi mwingine, suala la umuhimu mara nyingi hugeuka kuwa suala la kuangalia kama malengo ya ufadhili wa kimaendeleo au usanifu wake bado unafaa katika hali zilizogeuka.

Utegemekaji Kiasi cha uthabiti na utegemekaji wa data na mahitimisho ya tathmini, kwa mujibu wa ubora wa zana, taratibu na uchanganuzi uliotumiwa katika kukusanya, kufasiri na kutathmini data. Kumbuka: taarifa za tathmini zinaweza kutegemewa iwapo uchunguzi wa mara kwa mara, matumizi ya zana zile zile na katika hali zile zile zinafikia mahitimisho yale yale.

Msambao wa Wafadhiliwa Msambao wa wafadhiliwa na wadau wa ufadhili wa kimaendeleo. Istilahi Nasaba: wafadhiliwa

Matokeo Mazao, matokeo au taathira (zinazotarajiwa au zisizotarajiwa, zilizo na faida au zisizokuwa na faida) kutokana na ufadhili wa kimaendeleo. Istilahi Nasaba: Mazao, taathira, matokeo.

Mfuatano wa kimatokeo Mfuatano wa mahusiano katika ufadhili wa kimaendeleo unaoweka masharti na hatua za lazima ambazo zitahitaji kufuatwa ili kuyafikia matokeo yanayotarajiwa kuanzia kwa pembejeo za kimaendeleo, kupitia kwa utekelezwaji na matokeo hadi kufikia mazao, athari na upokezi wa maoni. Katika baadhi ya mashirika walengwa ni sehemu ya mkufu wa matokeo. Istilahi Nasaba: chukulizi, mfumo wa matokeo.

23

Page 24: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for
Page 25: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for
Page 26: foreword by kenya evaluation association_kea - Organisation for