Usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika semi: mifano kutoka ...
Transcript of Usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika semi: mifano kutoka ...
The University of Dodoma
University of Dodoma Institutional Repository http://repository.udom.ac.tz
Humanities Master Dissertations
2020
Usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika
semi: mifano kutoka vitendawili vya Kiswahili
Ngatungwa, Felista J.
The University of Dodoma
Ngatungwa, F. J. (2020). Usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika semi: mifano kutoka vitendawili
vya Kiswahili (Tasnifu ya Umahiri). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.
http://hdl.handle.net/20.500.12661/2919
Downloaded from UDOM Institutional Repository at The University of Dodoma, an open access institutional repository.
USAWIRI WA FALSAFA YA KIAFRIKA KATIKA SEMI:
MIFANO KUTOKA VITENDAWILI VYA KISWAHILI
FELISTA J. NGATUNGWA
SHAHADA YA UMAHIRI KATIKA FASIHI YA
KISWAHILI CHUO KIKUU CHA DODOMA
DISEMBA, 2020
USAWIRI WA FALSAFA YA KIAFRIKA KATIKA SEMI:
MIFANO KUTOKA VITENDAWILI VYA KISWAHILI
NA
FELISTA J. NGATUNGWA
TASNIFU KWA AJILI YA KUKAMILISHA MAHITAJI YA
SHAHADA YA UMAHIRI KATIKA FASIHI YA KISWAHILI
CHUO KIKUU CHA DODOMA
DISEMBA, 2020
i
IKIRARI NA HAKIMILIKI
Mimi, Felista Juma Ngatungwa, ninathibitisha kuwa tasnifu hii ni kazi yangu halisi
na haijawahi kuwasilishwa katika Chuo Kikuu kingine chochote ndani na nje ya nchi
kwa minajili ya kutunukiwa shahada inayofanana na hii au nyingine yoyote.
Saini
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili, kupiga chapa au kusambaza
sehemu yoyote ya tasnifu hii bila idhini ya mwandishi au Chuo Kikuu cha Dodoma.
ii
ITHIBATI YA MSIMAMIZI
Aliyetia saini hapa chini anathibitisha kwamba, ameisoma tasnifu hii iitwayo
“Usawiri wa Falsafa ya Kiafrika katika Semi: Mifano kutoka Vitendawili vya
Kiswahili” na anapendekeza kuwa inafaa kukubaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma
kwa ajili ya kutunukiwa Shahada ya Umahiri katika fasihi ya Kiswahili ya Chuo
Kikuu cha Dodoma.
iii
TABARUKU
Naitabaruku kazi hii kwa wazazi wangu wapendwa, Bw. Juma Ngatungwa na Bi
Tulelia Madenge kwa malezi na jitihada zao katika kunisomesha na kuniombea siku
zote ili niweze kufanikiwa katika masomo yangu. Pia, naitabaruku kwa mume wangu
kipenzi, Bw Braison Paul Mkiwa na watoto wangu wapendwa, Ivan Braison na
Edrick Braison kwa uvumilivu wao katika kipindi chote nikiwa masomoni. Sina cha
kuwalipa zaidi ya upendo wangu wa dhati kwao. Nawaombea nyote Mwenyezi
Mungu awabariki na kuwajazia pale mlipopunguza kwa ajili yangu.
iv
SHUKURANI
Kwanza, ninamshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha
kufanya kazi hii na kuikamilisha nikiwa mzima wa afya njema. Bila yeye
nisingeweza kufanya chochote.
Pili, ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa msimamizi wangu wa utafiti na
mwalimu wangu Dkt. Stella Faustine. Licha ya kuwa na majukumu mengi hakusita
kuwa bega kwa bega nami katika kunielekeza, kuniongoza na kunishauri kwa kila
hatua mpaka ninakamilisha utafiti huu. Mungu ambariki na kumlipa kila lenye kheri.
Tatu, ninapenda kuwashukuru wahadhiri wangu wa Chuo Kikuu cha Dodoma kwa
kunifundisha na kunipa miongozo mbalimbali iliyosaidia wakati wa masomo yangu.
Nao ni Dkt. Athuman Ponera, Dkt Stella Faustine, Dkt. Zuhura Badru, Dkt.
Abdumalik Feruzi na Dkt. Aginiwe Sanga. Mwingine kwa umuhimu ni Bw. Adrian
Fuluge kwa ushauri na mchango wake wa kimawazo ambao kimsingi umeijenga kazi
hii.
Mwisho, ninawashukuru wanafunzi wenzangu wa umahiri katika fasihi ya Kiswahili
mwaka 2018-2020 kwa ushirikiano wao tangu tulipoanza masomo mpaka
tulipomaliza. Mwenyezi Mungu awabariki.
v
IKISIRI
Tasnifu hii inayoitwa “Usawiri wa Falsafa ya Kiafrika katika Semi: Mifano kutoka
Vitendawili vya Kiswahili” iliongozwa na malengo mahsusi matatu. Nayo ni, mosi,
kubainisha vijenzi vya falsafa ya Kiafrika katika muktadha wa kitamaduni. Pili,
kujadili falsafa ya Kiafrika kama inavyojitokeza katika vitendawili vya Kiswahili na
tatu, kutathmini athari ya falsafa ya Kiafrika kwa jamii kama inavyosawiriwa katika
vitendawili vya Kiswahili. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Kisosholojia
kupitia misingi yake kama ilivyofafanuliwa katika utafiti huu. Nadharia hii ilitumika
katika michakato ya ukusanyaji wa data, uchambuzi na uwasilishaji wa matokeo ya
utafiti.
Utafiti huu ni wa kitaamuli, umetumia usanifu wa kifenomenolojia katika ukusanyaji
na uchanganuzi wa data. Utafiti huu ulifanywa uwandani na maktabani. Data
zilikusanywa kwa kutumia mbinu za mahojiano, mijadala ya vikundi lengwa na
udurusu wa nyaraka. Eneo la utafiti lilihusisha mikoa ya Kagera na Dodoma.
Sampuli ya utafiti iligawiwa katika makundi matatu. Nayo ni wanafunzi wa shule ya
msingi na sekondari, wanajamii wenye umri kuanzia miaka hamsini na tano na
kuendelea na maandiko kuhusu vitendawili vya Kiswahili na falsafa ya Kiafrika.
Sampuli ilipatikana kwa kutumia mbinu ya sampuli lengwa ya mpokezo na wa
kutegemea fursa.
Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa falsafa ya Kiafrika hudhihirika kupitia mambo
mbalimbali yanayojitokeza katika maisha ya mwanadamu. Mambo hayo ni suala la
umoja na ushirikiano, ndoa na uzazi, “uchawi na ushirikina”, uhai na kifo, uduara,
maadili na suala la imani katika Mungu na mizimu. Aidha, kupitia mifano
mbalimbali ya vitendawili vya Kiswahili, utafiti umebaini kuwa, utanzu wa
vitendawili una hazina kubwa katika kuhifadhi na kutunza maarifa ya falsafa ya
Kiafrika na pia falsafa hiyo ina athari kubwa katika maisha ya jamii ya Kiafrika.
Utafiti umependekeza kuwa bado kuna haja ya tafiti nyingi zaidi kufanyika katika
uga wa fasihi simulizi, ili kubaini ni kwa namna gani tanzu za fasihi hiyo zinaweza
kutumika kama darasa la kufunza na kuhifadhi maarifa ya kifalsafa ya jamii za
Waafrika.
vi
YALIYOMO
IKIRARI NA HAKIMILIKI......................................................................................... i
ITHIBATI YA MSIMAMIZI.......................................................................................ii
TABARUKU............................................................................................................... iii
SHUKURANI..............................................................................................................iv
IKISIRI......................................................................................................................... v
YALIYOMO............................................................................................................... vi
ORODHA YA VIFUPISHO VILIVYOTUMIKA.......................................................x
SURA YA KWANZA................................................................................................. 1
UTANGULIZI.............................................................................................................1
1.1 Utangulizi kwa Jumla............................................................................................. 1
1.2 Ufafanuzi wa Istilahi Muhimu................................................................................1
1.2.1 Falsafa..................................................................................................................1
1.2.2 Falsafa ya Kiafrika...............................................................................................2
1.2.3 Utamaduni............................................................................................................2
1.2.4 Vitendawili.......................................................................................................... 2
1.3 Usuli wa Tatizo la Utafiti....................................................................................... 3
1.4 Tamko la Tatizo la Utafiti.......................................................................................5
1.5 Malengo ya Utafiti..................................................................................................5
1.5.1 Lengo Kuu........................................................................................................... 5
1.5.2 Malengo Mahsusi.................................................................................................5
1.6 Maswali ya Utafiti.................................................................................................. 6
1.7 Manufaa ya Utafiti..................................................................................................6
1.8 Mawanda ya Utafiti................................................................................................ 6
1.9 Muhtasari wa Sura ya Kwanza............................................................................... 7
SURA YA PILI........................................................................................................... 8
KIUNZI CHA NADHARIA NA MAPITIO YA MAANDIKO.............................. 8
2.1 Utangulizi............................................................................................................... 8
2.2 Kiunzi cha Nadharia............................................................................................... 8
2.3 Mapitio ya Maandiko..............................................................................................9
2.3.1 Mapitio Kuhusu Falsafa ya Kiafrika....................................................................9
vii
2.3.2 Mapitio ya Maandiko Kuhusu Falsafa ya Kiafrika na Fasihi............................ 14
2.3.3 Mapitio ya Maandiko kuhusu Vitendawili vya Kiswahili.................................19
2.4 Mapengo Yanayojitokeza..................................................................................... 22
2.5 Muhtasari wa Sura ya Pili.....................................................................................23
SURA YA TATU.......................................................................................................24
METHODOLOJIA YA UTAFITI.......................................................................... 24
3.1 Utangulizi............................................................................................................. 24
3.2 Usanifu wa Utafiti.................................................................................................24
3.3 Mkabala wa Utafiti............................................................................................... 24
3.4 Eneo la Utafiti.......................................................................................................25
3.5 Walengwa wa Utafiti............................................................................................ 25
3.5.1 Jamii Tafitiwa.................................................................................................... 26
3.5.2 Sampuli na Usampulishaji Wake.......................................................................26
3.5.2.1 Sampuli ya Utafiti...........................................................................................27
3.6 Ukusanyaji wa Data..............................................................................................28
3.6.1 Njia na Zana za Ukusanyaji wa Data.................................................................28
3.6.1.1 Mahojiano....................................................................................................... 28
3.6.1.2 Mjadala wa Vikundi Lengwa..........................................................................29
3.6.1.3 Udurusu wa Nyaraka...................................................................................... 29
3.6.2 Mchakato wa Ukusanyaji Data na Udhibiti wake............................................. 29
3.7 Uchanganuzi wa Data........................................................................................... 30
3.8 Itikeli za Utafiti.....................................................................................................30
3.9 Uhalali na Uthabiti wa Matokeo ya Utafiti...........................................................31
3.10 Changamoto Zilizojitokeza Wakati wa Utafiti na Utatuzi wake........................ 31
3.11 Muhtasari wa Sura ya Tatu................................................................................. 32
SURA YA NNE......................................................................................................... 33
UWASILISHAJI NA MJADALAWAMATOKEO YA UTAFITI.................... 33
4.1 Utangulizi............................................................................................................. 33
4.2 Vijenzi vya Falsafa ya Kiafrika katika Muktadha wa Kitamaduni.......................33
4.2.1 Suala la Umoja na Ushirikiano.......................................................................... 33
4.2.2 Suala la Maadili katika Jamii.............................................................................35
viii
4.2.3 Suala la Uhai na Kifo.........................................................................................37
4.2.4 Dhana ya Uduara............................................................................................... 38
4.2.5 Suala la Imani katika Mungu na Mizimu.......................................................... 41
4.2.6 Suala la Uchawi na Ushirikina.......................................................................... 43
4.2.7 Dhana ya Ndoa na Uzazi................................................................................... 45
4.3 Falsafa ya Kiafrika katika Vitendawili vya Kiswahili..........................................47
4.3.1 Falsafa ya Umoja na Ushirikiano...................................................................... 48
4.3.2 Falsafa ya Umuhimu wa Maadili Katika Jamii................................................. 52
4.3.3 Falsafa ya Uhai na Kifo..................................................................................... 55
4.3.4 Falsafa ya Uduara.............................................................................................. 58
4.3.5 Falsafa ya Imani katika Mungu na Mizimu.......................................................62
4.3.6 Falsafa ya Uchawi na Ushirikina.......................................................................65
4.3.7 Falsafa ya Uzazi na Malezi................................................................................68
4.4 Athari za Falsafa ya Kiafrika kwa Jamii Kama Inavyosawiriwa katika
vitendawili vya Kiswahili....................................................................................71
4.4.1 Athari Chanya za Falsafa ya Kiafrika kwa Jamii.............................................. 72
4.4.1.1 Inasaidia Kudumisha Umoja na Mshikamano................................................72
4.4.1.2 Inasaidia Kulinda Maadili ya Jamii................................................................ 74
4.4.1.3 Inasaidia Kutambulisha Jamii ya Waafrika Ndani na Nje ya Afrika..............76
4.4.1.4 Inasaidia Kuhifadhi na Kurithisha Amali za Kitamaduni za jamii.................77
4.4.1.5 Inasaidia wanajamii kushika imani ya dini.....................................................78
4.4.2 Athari Hasi za Falsafa ya Kiafrika kwa Jamii................................................... 78
4.4.2.1 Kuchochea Vitendo vya Uvunjifu wa Amani katika Jamii............................ 79
4.4.2.2 Kukwamisha Maendeleo ya Jamii.................................................................. 80
4.4.2.3 Inasababisha Hofu na Mashaka kwa Wanajamii............................................ 80
4.5 Muhtasari wa Sura ya Nne....................................................................................81
SURA YA TANO...................................................................................................... 83
MUHTASARI, HITIMISHO NAMAPENDEKEZO........................................... 83
5.1 Utangulizi............................................................................................................. 83
5.2 Muhtasari wa Tasinifu.......................................................................................... 83
5.3 Hitimisho.............................................................................................................. 85
5.3.1 Mchango Mpya wa Utafiti.................................................................................85
ix
5.3.2 Utoshelevu wa Nadharia....................................................................................86
5.4 Maoni na Mapendekezo kwa Tafiti Zijazo...........................................................86
5.5 Muhtasari wa Sura ya Tano.................................................................................. 87
MAREJELEO........................................................................................................... 88
VIAMBATANISHO................................................................................................. 94
x
ORODHA YA VIFUPISHO VILIVYOTUMIKA
BAKITA Baraza la Kiswahili Tanzania
Bi. Bibi
Bw. Bwana
Dkt. Daktari
Hm Hakuna mwaka
K.h.j Keshatajwa hapo juu
Ltd Limited
Prof. Profesa
TUKI Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili
Uk. Ukurasa
Wah. Wahariri
WWW World Wide Web
1
SURA YA KWANZA
UTANGULIZI
1.1 Utangulizi kwa Jumla
Sura hii inabeba utangulizi wa tasnifu yetu. Katika sura hii, istilahi muhimu
zilizotumika katika tasnifu hii zimefafanuliwa. Mambo mengine yaliyojitokeza ni
pamoja na; usuli wa tatizo la utafiti, tamko la tatizo la utafiti, malengo ya utafiti,
maswali ya utafiti, manufaa ya utafiti na mawanda ya utafiti.
1.2 Ufafanuzi wa Istilahi Muhimu
Istilahi muhimu zinazohusiana na utafiti huu ni falsafa, falsafa ya Kiafrika,
utamaduni na vitendawili. Katika kufafanua istilahi hizi, mtafiti amefafanua kwa
mujibu wa wataalamu mbalimbali na kisha kutoa maana ya jumla kama ilivyotumika
katika utafiti huu.
1.2.1 Falsafa
Kwa mujibu wa Wizara ya Elimu na Utamaduni (1992) falsafa ni taaluma
inayojishughulisha na kutafuta ukweli wa jambo kwa njia ya kutafakari. Maelezo
haya yanathibitisha kuwa, falsafa ni mtazamo alio nao mwanadamu katika kufikiria
mambo yanayotokea. Mawanda ya fasili hii yanabainisha kuwa, falsafa ni taaluma
inayoweza kusomwa au kufundishwa kama taaluma nyingine. Fasili inayofanana na
hiyo imetolewa na Chuachua (2010). Yeye anafafanua kuwa, falsafa ni taaluma ya
kutafuta ukweli kwa njia ya kutafakari kwa kina. Kwa hiyo, kutafakari kwa kina
kuhusu ukweli wa jambo fulani kunasaidia kubaini maarifa ya jamii kupitia mambo
mbalimbali yanayojenga maarifa hayo. Aidha, Wamitila (2010) anakwenda mbali
zaidi ya hapo kwa kufafanua kuwa, falsafa ni istilahi inayotumiwa kuelezea wazo au
mawazo anayoyaamini mtu, mwandishi au mtunzi kuwa yale anayoyaandika yana
ukweli unaotawala misingi ya maisha. Kwa mtazamo wa mtaalamu huyu, falsafa ni
jumla ya imani na mawazo aliyo nayo mtu juu ya jambo fulani kuwa ni kweli
kulingana na maisha halisi ya jamii. Hivyo basi, falsafa inaweza kufafanuliwa kuwa
ni taaluma au elimu ya kutafuta uhakika wa mambo fulani katika maisha kwa njia ya
kuutafakari ulimwengu. Falsafa hujishughulisha na kudadisi hali halisi ya maisha ya
binadamu katika jamii yake kwa kuzingatia imani, mila, desturi pamoja na mienendo
aliyo nayo binadamu.
2
1.2.2 Falsafa ya Kiafrika
Simchimba (2012) anafafanua kuwa, falsafa ya Kiafrika ni jumla ya mitazamo,
mielekeo na misimamo waliyo nayo Waafrika juu ya mambo yanayowazunguka na
yanayowatofautisha kati yao na jamii nyingine. Maana inayokaribiana na ya
Simchimba inatolewa na Faustine (2017) ambaye amefafanua zaidi kuwa falsafa ya
Waafrika ni fikra au mitazamo mbalimbali inayoeleza masuala mahususi ya kimaisha
yanayohusiana na jamii ya Waafrika (Wabantu). Fikra au mitazamo hiyo ndiyo
inayowawezesha kuutafakari ulimwengu wao kwa kuuhusisha na vitu vilivyomo na
hatimaye, kuutilia maana. Kwa jumla, falsafa ya Kiafrika inaweza kuelezwa kuwa ni
jumla ya fikra, mienendo, ukweli na matendo yanayohusu Waafrika (Wabantu)
ambayo wanayaamini na kuyazingatia katika nyanja mbalimbali za maisha yao.
1.2.3 Utamaduni
Stanley (2008) anafafanua kuwa, utamaduni ni jinsi binadamu wanavyoyakabili
maisha katika mazingira yao ikijumuisha ujuzi, imani, sanaa, maadili, sheria na
desturi. Hujumuisha namna wanavyovaa, mila zao za ndoa, lugha, maisha ya
kifamilia na sherehe zao za dini. Utamaduni wa Waswahili hautofautiani sana kati ya
jamii moja na nyingine zinazopatikana katika nchi ya Tanzania. Ufafanuzi huo
unaonesha kuwa utamaduni hujumuisha kanuni zote za maadili na hudhihirika katika
shughuli za kijamii, lugha na katika mlolongo mzima wa maisha. Aidha, fasili ya
mtaalamu huyu inakaribiana na ile iliyotolewa na Hoppenau na wenzake (2009).
Hawa wanafafanua kuwa, utamaduni ni mfumo wa pamoja wa kiimani, maadili,
desturi, tabia na kazi za sanaa ambao hutumiwa na wanajamii katika kukabiliana na
dunia. Mfumo huo hurithishwa kutoka kizazi hadi kizazi kwa njia ya kujifunza.
Fasili hii inafafanua kwamba, utamaduni humwezesha mwanadamu kuifahamu,
kutafsiri na kuielewa dunia inayomzunguka kwa namna mbalimbali. Hivyo, kwa
jumla tunaweza kusema kuwa utamaduni ni jumla ya mambo yote yanayofanywa
katika jamii kwa kuzingatia mila na desturi za jamii hiyo na huweza kurithishwa
kutoka kizazi kimoja kwenda kingine kwa njia ya mapokeo.
1.2.4 Vitendawili
Wamitila (2003) anafafanua kuwa, kitendawili ni aina ya semi ambayo huwa
imefumbwa na hutolewa kwa mwanahadhira ili aifumbue. Swali la fumbo hilo na
jawabu lake hufahamika katika jamii fulani inayohusika. Upekee wa fasili hii upo
3
katika matumizi ya sitiari katika utegaji wa vitendawili ambayo ndiyo sifa kuu ya
vitendawili. Maana inayofanana na hii inaelezwa na Mulokozi (2017) ambaye
anafafanua kuwa, kitendawili ni usemi wenye fumbo; ni swali ambalo huulizwa kwa
hadhira ili ilipatie ufumbuzi. Maelezo ya wataalamu hawa yanathibitisha kuwa,
vitendawili ni fumbo ambalo hutolewa kwa hadhira kama swali ili iweze kulifumbua.
Kwa jumla, vitendawili vinaelezwa kuwa ni semi zenye mafumbo ambazo hutolewa
kwa hadhira kwa kutumia sitiari ili kuifanya hadhira yake kufikiria kwa kina katika
kutoa majibu. Hata hivyo, vitendawili vinaweza kutofautiana kati ya jamii moja na
nyingine kutokana na tofauti za kimazingira na mabadiliko yanayotokea katika jamii
hizo kufuatia maendeleo ya sayansi na teknolojia.
1.3 Usuli wa Tatizo la Utafiti
Katika ulimwengu tunaoishi, kila jamii ina namna yake ya kuuelewa, kuuthamini na
kuutathmini utamaduni wake. Matendo na kila akifanyacho mwanadamu akiamini
kuwa ni kweli kulingana na matakwa ya jamii yake ndiyo falsafa ya jamii hiyo.
Aidha, kila jamii huishi kulingana na taratibu au miongozo inayokitwa ndani ya
falsafa yake ambayo huifanya jamii moja kutofautiana na jamii nyingine.
Mshiu na Wenzake (2007) kama wanavyonukuliwa na Makame (2016) wanaeleza
kuwa neno falsafa linatokana na maneno mawili yenye asili ya Ki- Giriki; “philos”
na “sophia” yakiwa na maana ya “love” au “kutafuta” busara na hekima. Maelezo
hayo yanabainisha kuwa, falsafa hujihusisha na kuchunguza na kutafakari kwa kina
juu ya asili ya vitu, sababu na maana ya vitu na kuyapatia ufumbuzi kwa kutumia
busara na hekima. Kwa hiyo, maelezo hayo yanafafanua kuwa, mwanafalsafa
afikiriapo kufanya jambo, fikra hizo lazima zitawaliwe na busara na hekima pamoja
na kuupata ufumbuzi wa jambo fulani lililojichomoza ndani ya jamii.
Historia inaeleza kuwa, uchunguzi kuhusu kuwepo kwa falsafa ulibaini kwamba,
falsafa ilianza mnamo karne ya kumi na sita katika maeneo mbalimbali. Hii
inathibitishwa na Mshiu na wenzake (2007), kama wanavyonukuliwa na Makame
(2016). Wanasema kuwa;
4
By its origin philosophy started in the sixteenth 16th century in Asiaand Europe. This can be proved by many documents present inEurope and Asia and other parts of the world such as Africa (uk.14).
Kwa asili yake falsafa ilianza katika karne ya 16 katika Afrika naUlaya. Hii inathibitishwa kwa maandiko mengi yapatikanayo Ulayana Asia na katika sehemu nyingine duniani kama vile Afrika (tafsiriya mtafiti).
Maneno haya yanabainisha kuwepo kwa falsafa katika jamii mbalimbali
ulimwenguni. Hii ni kwa sababu, hakuna jamii inayoishi kiholela pasipo kuwa na
misingi au miongozo fulani inayojikita katika utamaduni wao. Kwa hiyo, falsafa ya
Kiafrika inajumuisha mambo yote ambayo Waafrika wanayaamini kuwa ni ya kweli
na wanayatenda katika nyanja zote za maisha yao.
Kwa vile falsafa ya jamii fulani hujifungamanisha na maisha ya jamii hiyo, fasihi
nayo kama sehemu ya jamii, hujinasibisha kwa namna ya moja kwa moja na falsafa
ya jamii hiyo. Hii inatokana na sababu kuwa, fasihi ni zao la jamii na hutumika kama
jukwaa la kuelezea uzoefu, kaida, mila na desturi za jamii husika. Pia, fasihi kama
tawi mojawapo la sanaa, hutumika kudhihirisha falsafa ya jamii husika. Kwa maana
hiyo, hatuwezi kuitenganisha au kuondoa fasihi ya jamii husika katika kuchunguza
falsafa ya jamii hiyo kwa sababu falsafa hubebwa na misingi ya vipera vya fasihi
inayotawala na kutumika katika jamii hiyo. Kwa kutambua hilo, tumeona ni vema
kuchunguza usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika vitendawili vya Kiswahili.
Baadhi ya watafiti na wataalamu wa fasihi wamefanya uchunguzi kuhusiana na
falsafa ya Kiafrika. Watafiti kama vile Simchimba (2012), Duwe (2016), Faustine
(2017) na Mlelwa (2017) wamefanya tafiti zao kuhusu Falsafa ya Kiafrika
inavyosawiriwa katika kazi za fasihi andishi na fasihi Simulizi (methali, sanaa za
maonyesho na hadithi). Hata hivyo, uchunguzi wa falsafa ya Kiafrika katika
vitendawili haujafanyika kwa kina. Baadhi ya wataalamu waliotafiti kuhusu
vitendawili kama vile Khumalo (1974), Stefanova (2003), Gwaravanda na Masaka
(2008), Badru (2012; 2015) hawakuhusisha uchunguzi wa vitendawili na falsafa ya
Kiafrika. Jambo hili linasababisha jamii kutokuwa na uelewa mkubwa kuhusu
vitendawili kama amali muhimu katika kuhifadhi na kufunza maarifa ya jamii.
Utafiti huu ulikusudiwa kuziba pengo hilo kwa kuangalia namna vitendawili vya
5
Kiafrika vinavyoweza kusawiri falsafa ya Kiafrika pamoja na athari za falsafa ya
Kiafrika kwa jamii.
1.4 Tamko la Tatizo la Utafiti
Wataalamu kadhaa wamefanya tafiti zao kuonesha namna falsafa ya Kiafrika
inavyosawiriwa katika tanzu mbalimbali za fasihi. Miongoni mwao ni Mbiti (1969),
Balisidya (1973), Hussein (1976), Mulokozi (1983), Senkoro (1996), Simchimba
(2012), Duwe (2016), Faustine (2017) na Mlelwa (2017). Hata hivyo, wengi wa
wataalamu hawa tafiti zao zimekitwa katika fasihi andishi. Kwa wale
walioshughulikia fasihi simulizi mahususi katika kipera cha vitendawili kama vile
Amana (2013), Badru (2015) na Mshana (2015) kwa kuwataja baadhi, hawajahusisha
tafiti zao na jinsi vitendawili vinavyoweza kubeba falsafa ya Kiafrika. Hali hii
inasababisha vitendawili kama kipera cha fasihi kutoeleweka na kupewa hadhi sawa
kama ilivyo kwa vipera vingine vya fasihi katika ufunzaji na utunzaji wa maarifa ya
falsafa ya Kiafrika. Utafiti huu umekusudia kuziba pengo hilo kwa kuchunguza
usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika vitendawili vya Kiswahili na kubainisha athari
zake kwa jamii.
1.5 Malengo ya Utafiti
Utafiti huu uliongozwa na malengo ya aina mbili, ambayo ni lengo kuu na malengo
mahsusi.
1.5.1 Lengo Kuu
Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika
vitendawili vya Kiswahili.
1.5.2 Malengo Mahsusi
Utafiti huu uliongozwa na malengo mahsusi matatu ambayo ni;
a) Kubainisha vijenzi vya falsafa ya Kiafrika katika muktadha wa kitamaduni,
b) Kujadili namna falsafa ya Kiafrika inavyojitokeza katika vitendawili vya
Kiswahili,
c) Kutathmini athari ya falsafa ya Kiafrika kwa jamii kama inavyosawiriwa
katika vitendawili vya Kiswahili.
6
1.6 Maswali ya Utafiti
a) Je, ni vijenzi vipi vinavyobainisha falsafa ya Kiafrika katika muktadha wa
kitamaduni kwa jamii ya Waafrika?
b) Ni kwa namna gani falsafa ya Kiafrika inavyojitokeza katika vitendawili vya
Kiswahili?
c) Je, falsafa ya Waafrika kama inavyosawiriwa katika vitendawili vya
Kiswahili ina athari gani kwa jamii ya Waafrika?
1.7 Manufaa ya Utafiti
Matokeo ya utafiti huu yana manufaa yafuatayo; Mosi, kusaidia katika kupanua wigo
wa ufahamu juu ya uhusiano wa fasihi na falsafa ya jamii husika. Pili, kutoa
mwongozo kwa wasomi na watafiti wa baadae ambao watahitaji kufanya utafiti
katika uga wa falsafa ya Kiafrika. Tatu, kutoa nafasi kwa watafiti wengine kutumia
taaluma hii ya falsafa katika kuzichambua kazi nyingine za fasihi simulizi kama
hadithi, nyimbo na ngoma na kazi za fasihi andishi. Nne, utafiti huu utaiendeleza na
kuisheheneza fasihi simulizi ya Kiswahili kwa kuonesha umuhimu wake katika
kuhifadhi na kufunza maarifa ya kifalsafa ya jamii ya Waafrika.
1.8 Mawanda ya Utafiti
Utafiti huu umechunguza usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika semi: mifano kutoka
vitendawili vya Kiswahili. Malengo mahsusi ya utafiti huu yalikuwa ni matatu. Nayo
ni mosi, kubainisha vijenzi vya falsafa ya Kiafrika katika muktadha wa kitamaduni.
Pili, kujadili namna falsafa ya Kiafrika inavyojitokeza katika vitendawili vya
Kiswahili. Tatu, kutathmini athari ya falsafa ya Kiafrika kwa jamii kama
inavyosawiriwa katika vitendawili vya Kiswahili. Kwa jumla, utafiti huu umeitazama
falsafa ya Waafrika katika muktadha wa utamaduni tu na sio katika nyanja
nyinginezo. Aidha, utafiti huu unawaangalia Waafrika kwa kujiegemeza katika jamii
ya Wabantu. Hii inatokana na utambuzi kuwa, Waafrika wamegawanyika katika
makundi makubwa matatu, yaani Wabantu, Wakushi na Wanilo. Tumechagua
Wabantu kwa sababu, kwa mujibu wa Chuachua (2016:2) na Faustine (2017),
Wabantu ndiyo jamii kubwa zaidi Afrika yenye mfumo wa lugha unaofanana. Hivyo,
ni rahisi kuelewa mawazo na mitazamo ya kifalsafa ya Waafrika kupitia lugha zao
zaidi ya makundi mengine. Zaidi ya kuwa na kiungo cha lugha wanaunganishwa na
mila, desturi na falsafa ambazo zinashabihiana sana.
7
Aidha, vitendawili vilivyotumika vilikusanywa kutoka kwa wanafunzi wa shule za
msingi na sekondari wa wilaya ya Bukoba na vile vilivyopatikana katika matini
mbalimbali za kifasihi zinazohusu vitendawili vya Kiswahili. Data zilizokusanywa
na mtafiti zilichambuliwa na kuwasilishwa kwa kuzingatia malengo ya utafiti huu tu
na si vinginevyo.
1.9 Muhtasari wa Sura ya Kwanza
Sura hii imefafanua vipengele mbalimbali ikiwemo utangulizi, usuli wa tatizo la
utafiti, tamko la tatizo la utafiti, malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, manufaa ya
utafiti pamoja na mawanda ya utafiti. Vipengele hivyo vimefafanuliwa kwa
kuzingatia mada ya utafiti huu. Sura inayofuata imefafanua kuhusu nadharia
iliyotuongoza katika utafiti huu pamoja na mapitio ya maandiko mbalimbali kuhusu
falsafa ya Kiafrika kwa jumla, falsafa ya Kiafrika katika fasihi na maandiko kuhusu
vitendawili vya Kiswahili.
8
SURA YA PILI
KIUNZI CHA NADHARIA NA MAPITIO YA MAANDIKO
2.1 Utangulizi
Sura hii imefafanua kuhusu mambo makuu mawili. Mosi, kiunzi cha nadharia
iliyotumika katika utafiti huu. Pili, maandiko mbalimbali yaliyopitiwa
yanayohusiana na mada ya utafiti. Katika mapitio yanayohusiana na mada hii tuna
vipengele vitatu ambavyo ni; mapitio kuhusiana na falsafa ya Kiafrika kwa jumla,
mapitio kuhusu falsafa ya Kiafrika katika fasihi na mapitio kuhusu vitendawili vya
Kiswahili. Aidha, kutokana na mapitio hayo, mapengo ya utafiti yamebainishwa.
2.2 Kiunzi cha Nadharia
Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Kisosholojia. Nadharia hii iliasisiwa na
mtaalamu wa Kifaransa Hippolyte Taine (1828-1893). Taine aliangalia kazi ya fasihi
kama taswira ya kijiografia, kitamaduni na kimazingira iliyochimbuka kutoka katika
jamii husika. Akifafanua kuhusu nadharia hii anasema kuwa kazi ya kifasihi
inatakiwa kuchukuliwa kama taarifa ya kweli inayohusu maisha halisi ya watu. Kwa
hiyo, nadharia hii inajishughulisha na kazi yeyote ya sanaa kulingana na hali ya jamii
ambayo sanaa hiyo imechipuka na kukuzwa. Pia, hutumika katika kuchunguza
uhusiano uliopo baina ya kazi ya sanaa, jamii na namna jamii hiyo ilivyoundwa.
Wananadharia wa Kisosholojia wanazingatia mambo makuu mawili ambayo ni,
namna gani jamii inahusiana na fasihi na namna ambavyo fasihi inafanya kazi katika
jamii.
Burke (1941) anaona kuwa kazi ya sanaa ikiwa ni pamoja na fasihi inatumia mbinu
mbalimbali ambazo zinamsaidia mwanajamii kuelewa vizuri na kuongeza uwezo wa
kujiongoza juu ya jamii yake. Wahakiki wa Kisosholojia wanaweka mkazo zaidi
katika utendaji na msisitizo juu ya dhima ya fasihi katika jamii. Wanaona kuwa
fasihi ina dhima kubwa ambazo ni kuelimisha, kuburudisha na kuonya jamii.
Utafiti huu umetumia mihimili miwili ya nadharia hii kama ifuatavyo;
a) Fasihi haiwezi kujitenga na jamii ambayo fasihi hiyo imetengenezwa
kutoka kwenye jamii hiyo (Taine, 1873 na Narizvi, 1982). Mhimili huu
umetusaidia kujadili namna falsafa ya Kiafrika inavyojitokeza katika
vitendawili vya Kiswahili. Hii ni kwa sababu fasihi ya jamii fulani ina
9
mfungamano na maisha ya jamii husika. Kwa hiyo, vitendawili vya
Kiswahili vilivyotumika katika utafiti huu ambavyo vimesawiri falsafa ya
Kiafrika vimetokana na jamii na vinahusu maisha halisi ya jamii ya
Waafrika.
b) Kazi ya kifasihi ni taswira ya kijiografia, kimazingira na kiutamaduni
ambamo kazi hiyo imechimbuka kutoka katika jamii husika (Mungah,
1999). Mhimili huu umesaidia katika uchambuzi wa data ili kukamilisha
lengo la kwanza, la pili na la tatu. Malengo hayo yanahusu kubainisha
vijenzi vya falsafa ya Kiafrika katika muktadha wa kitamaduni, namna
falsafa ya Kiafrika inavyojitokeza katika vitendawili vya Kiswahili na
athari zake kwa jamii ya Waafrika. Hii ni kwa sababu, vitendawili hivyo
vinaakisi maisha halisi ya jamii ya Waafrika na hivyo, vimemwezesha
mtafiti kupata picha halisi ya maisha ya Waafrika wanavyoishi katika
mazingira yao. Kwa hiyo, kupitia hayo, athari za imani na mitazamo yao
imeweza kubainika.
Hivyo, nadharia hii inahusiana na utafiti huu ambao unachunguza usawiri wa falsafa
ya Kiafrika katika vitendawili vya Kiswahili. Hii ni kwa sababu nadharia
inachunguza jamii mahsusi na mihimili yake inaweka mkazo fasihi kuendana na
miktadha ya maisha ya jamii husika. Kwa hiyo, nadharia hii imesaidia kukamilisha
malengo ya utafiti huu ambayo yamejikita katika kuchunguza jamii mahsusi ya
Waafrika (Wabantu) katika vitendawili vya Kiswahili kama yalivyobainishwa katika
mihimili hapo juu.
2.3 Mapitio ya Maandiko
Sehemu hii inahusu mapitio mbalimbali yaliyotumika katika utafiti huu. Mapitio
hayo yamegawanyika katika vipengele vitatu. Navyo ni, mapitio kuhusu falsafa ya
Kiafrika, mapitio kuhusu falsafa ya Kiafrika na fasihi na mapitio kuhusu vitendawili
vya Kiswahili.
2.3.1 Mapitio Kuhusu Falsafa ya Kiafrika
Katika kuifafanua falsafa ya Kiafrika, kumekuwa na mzozo miongoni mwa
wataalamu juu ya kuwapo ama kutokuwapo kwa falsafa ya Kiafrika. Kutokana na
mzozo huo zimeibuliwa hoja mbili kinzani. Wapo wataalamu wanaosema kuwa
10
falsafa sharti iwe katika maandishi; na kwa kuwa falsafa ya Kiafrika haikuandikwa
basi hakuna falsafa hiyo (Kaponda, 2018). Naye Chuachua (2016) anamtaja
Bodunlin (1981) anayekubaliana na mtazamo huu kuwa, falsafa ya Kiafrika imekuwa
ikitawaliwa na mgogoro wa fikra kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa falsafa ya
Kiafrika. Anaeleza kuwa mgongano huo wa hoja unakwenda mbali zaidi na kutaka
kujua kama falsafa ya Kiafrika ipo, ni ipi hiyo? Kwa mtazamo huu, Waafrika kama
watu ambao hapo awali falsafa yao haikuwekwa katika maandishi, walitazamwa
kama watu wasio na falsafa yao. Hivyo, tunakubaliana na Duwe (2016) anayeona
kuwa, mtazamo huu umejikita katika fikra za wataalamu wa Kimagharibi wenye
lengo la kuwadhihaki na kuwadhalilisha Waafrika.
Duwe (2016) anataja baadhi ya wataalamu wanaodai kuwa Waafrika hawana falsafa
kuwa ni: Muller, 1873; Spencer, 1851 na Bruhi, 1978. Sababu ya madai yao ni
kwamba, hakuna maandishi au vielelezo vyovyote vinavyofafanua suala la kuwapo
kwa falsafa ya Kiafrika. Wataalamu wengine wanakwenda mbali zaidi na kusema
kuwa, falsafa ya Waafrika haijitoshelezi kwani wanafalsafa wa Kiafrika wamechota
mbinu za wanafalsafa wa Kimagharibi katika kufafanua na kuelezea falsafa yao. Pia,
uchunguzi uliofanywa na waandishi wa Kiafrika unachukuliwa kuwa chanzo chake
ni katika nchi za Magharibi, (Hontondji 2004). Andiko la mtaalamu huyu
limemsaidia mtafiti kupata mawazo ya jumla kuhusu mtazamo wa wataalamu wa
Kimagharibi wenye lengo la kuwadhalilisha Waafrika kuwa hawana falsafa. Utafiti
huu unapingana na mawazo ya wataalamu hao kwa kuthibitisha kuwa Waafrika wana
falsafa yao inayodhihirika katika vitendawili vya Kiswahili.
Kwa upande mwingine, wapo wataalamu ambao wametafiti juu ya falsafa ya
Kiafrika na kugundua kuwa Waafrika wana falsafa yao inayojidhihirisha kutokana na
namna wanavyoishi, uzoefu, mila na desturi zao. Baadhi ya wataalamu hao ni kama
Temples, 1959; na Mbiti, 1969. Kwa mujibu wa wataalamu hawa falsafa sio lazima
iandikwe na kila jamii ina miongozo yake inayoaminika na kufuatwa kwa lengo la
kuendesha maisha ya jamii. Wataalamu hawa wanakubaliana kuwa Waafrika wana
falsafa yao ila kuja kwa wageni kumeiathiri falsafa ya Kiafrika. Mawazo ya
wataalamu hawa kuhusu falsafa ya Kiafrika ni kama ifuatavyo:
11
Temples (1959) anaeleza kuwa mtu yeyote anayedai kuwa Waafrika hawana falsafa
anawaondoa katika kundi la wanadamu. Waafrika wana uwezo wa kufikiri na
kutenda kutokana na misingi ya jamii zao. Fikra za Waafrika zimetawaliwa na vitu
viwili ambavyo ni uhai na kifo. Waafrika wanaamini kuwa mtu akiumwa nguvu za
uhai zinapungua hivyo anaamini atakufa. Anataja vipengele mbalimbali
vinavyodhihirisha falsafa ya Waafrika kama dini, “uchawi na ushirikina”, uganga,
uduara, matambiko. Kuhusu uduara, anasema kuwa maisha ya Waafrika
yametawaliwa na wazo la duara, yaani maisha yana sifa ya uzuri. Mambo hayo
huonekana katika vitu kama vile viti (vigoda), vyungu, vinu, nyungo na hata baadhi
ya nyumba huonekana katika umbo la duara. Andiko hilo lina mchango katika utafiti
huu kwani limesaidia kubainisha vipengele mbalimbali ambavyo kwavyo, maarifa ya
kifalsafa huibuka ndani yake. Hata hivyo, andiko hilo halijajikita katika utanzu
wowote mahsusi ma kuonesha ni kwa namna gani falsafa ya Kiafrika inavyoweza
kusawiriwa katika fasihi simulizi. Ili kuziba pengo hilo, utafiti huu umechunguza
usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika vitendawili vya Kiswahili.
Mbiti (1969) amefanya kazi nyingi zinazohusiana na falsafa ya Kiafrika. Katika kazi
hizo amebainisha mambo yanayofanywa na Waafrika ambayo yanaipambanua
falsafa ya Waafrika. Baadhi ya mambo hayo ni kama suala la umoja na ushirikiano.
Anasema kuwa Waafrika wanaishi kwa kushirikiana katika mambo mbalimbali. Hii
inathibitika pale anaposema:
Whatever happens to the individual happens to the whole group,and whatever happens to the whole group happens to the individual.The individual can only say, “I am because we are: and since weare therefore, I am” (uk. 106)
Kila kinachomtokea mtu binafsi kinakuwa kimetokea kwa kundizima, na kila kinachotokea katika kundi zima kinakuwakimemtokea mtu binafsi. Mtu anaweza kusema” nipo kwa sababutupo na kwa kuwa tupo basi nipo” (Tafsiri ya mtafiti)
Maelezo hayo yanathibitisha wazi kuwa, Waafrika wanaishi kwa kutegemeana. Mtu
akipata tatizo jamii nzima huchukulia tatizo hilo kama ni lao wote. Jambo hili
linawafanya kuishi kwa ushirikiano mkubwa miongoni mwao. Masuala mengine
yanayojitokeza katika falsafa ya Kiafrika kama inavyofafanuliwa na Mbiti (1969) ni
suala la imani katika dini za asili, matambiko na suala la wakati. Kuhusu suala la
12
wakati anasema kuwa, Waafrika wanaishi katika sasa na hawana kesho. Andiko hilo
ni la msingi katika utafiti wetu kwani limedokeza kuwa, Waafrika walikuwa na dini
zao na utamaduni wao ambao ndio hubainisha falsafa yao na hivyo kutoa msukumo
kwa mtafiti kuchunguza namna falsafa hiyo inavyoweza kusawiriwa katika
vitendawili vya Kiswahili. Hata hivyo, pamoja na umuhimu huo, andiko hilo
limeacha mwanya wa kutafiti kwa kuwa halijabainisha vijenzi vya falsafa ya
Kiafrika katika muktadha wa kitamaduni. Utafiti huu umeziba pengo hilo kwa
kubainisha vijenzi vya falsafa ya Kiafrika katika muktadha wa kitamaduni.
Aidha, Mbiti (1975) anaeleza kuhusu dhana ya roho kama kipengele cha falsafa ya
Kiafrika. Mtaalamu huyu anaona kwamba, kuna aina mbili za roho ambazo ni roho
asilia na roho ya binadamu. Katika maeneo hayo inaaminiwa kuwa, kuna kani uhai
inayoongoza kuwepo kwa roho asilia ambayo huhusisha vitu kama anga, nyota na
maumbile ya asili kama maji na milima. Vile vile, kwa upande wa roho za binadamu,
huhusisha zile za watu waliokufa kipindi cha vizazi vinne au vitano vilivyopita. Hii
inathibitishwa pale anaposema:
They are considered to be part of their families. They are believed tolive close to their homes where hey lived when they were human being.They show interest in their surviving families, and inturn theirfamilies remember them by pouring out parts of their drinks andleaving beats of food for time to time. The living dead may also visittheir surviving relatives in dreams or vision or even openly and maketheir wishes known. (Uk 72-73)
Wanachukuliwa kama ni sehemu za familia zao. Wanaaminiwakuendelea kuishi jirani na makazi yao ambayo waliishi wakati wakiwahai. Wanaonesha kuvutiwa na ndugu zao wanafamilia wanaoishi, nafamilia zao pia zinaendelea kuwakumbuka kwa kumwaga sehemu zavinywaji vyao na kuacha chakula mara kwa mara. Pia wahengahuwatembelea ndugu zao walio hai katika ndoto au maono au hatakwa wazi na kutoa matarajio yao. (Tafsiri ya mtafiti)
Maelezo katika nukuu hiyo yanaonesha kuwa, kwa Waafrika roho za binadamu
zinahusisha pia zile za watu waliokwisha kufariki katika kipindi fulani. Hii inatokana
na sababu kwamba, watu walio hai hufanya vitu mbalimbali kuonesha kuwakumbuka
wahenga hao na kuwaomba katika shida zao. Wahenga hao pia huwatokea walio hai
kwa njia ya ndoto au maono na kujibu maombi yao. Mtaalamu huyu anatuambia
kuwa mtu akifariki roho yake inaendelea kuwepo karibu na walio hai na
13
kuwatembelea mara kwa mara. Andiko hili limemsaidia mtafiti katika kuelewa
dhana ya roho kama kipengele kimojawapo cha falsafa ya Kiafrika. Licha ya
manufaa hayo, andiko hilo halijabainisha mambo ambayo kupitia kwayo falsafa ya
Kiafrika inajipambanua katika vitendawili vya Kiswahili. Pengo hilo ndilo
limeshughulikiwa na mtafiti kwa kubainisha vijenzi vya falsafa ya Kiafrika katika
muktadha wa kitamaduni.
Jengo na Wenzake, (1982) katika andiko lao wanashadidia uwepo wa falsafa ya
Kiafrika katika jamii za Kiafrika. Fikra za wataalamu hawa zinatia hamasa katika
kujitambua na kulinda heshima ya Waafrika kwa kuwa Waafrika ni binadamu wenye
utashi kama walivyo wengine. Wanaeleza kuwa uchambuzi wa falsafa yoyote lazima
utokane na mfumo wa jamii uliopo wakati falsafa hiyo inatokea. Madai haya ni
muhimu kwa kuwa ili kubaini falsafa ya jamii ni vema kuchunguza msingi ulioijenga
falsafa hiyo hasa kwa kuzingatia ethnofilosofia ya jamii husika. Fikra hizi
zimemsaidia mtafiti katika kuthibitisha kuwa kila jamii ina falsafa yake kutokana na
uzoefu wanaoupata wanajamii kwa kuishi katika mazingira yao kwa muda mrefu.
Hata hivyo, andiko hili limeacha pengo la kutafiti kwa kuwa, halikufafanua namna
falsafa ya Kiafrika inavyojitokeza katika fasihi simulizi. Pengo hilo
limeshughulikiwa katika utafiti huu kwa kujadili namna falsafa ya Kiafrika
inavyojitokeza katika vitendawili vya Kiswahili.
Pia, Menkiti (1984) anakubaliana na mawazo ya John Mbiti katika andiko lake
linalohusisha dhana ya mtu na jumuia. Katika andiko hilo, anafafanua kuhusu mila
na desturi za Waafrika. Anaeleza kuwa, Waafrika wanaamini kifo sio Mwisho wa
uhai bali ni mwanzo wa maisha mengine. Haya yanathibitika pale anaposema:
Following John Mbiti, we can call the inhabitants of the ancestralcommunity by the name of the living dead. For the ancenstral deadare not dead in the world of spirits nor are they dead in the memory ofthe living men and women who continue to remember them, and whoincessantly ask their help through various acts of libation andsacrificial offering. (uk.174)
14
Kwa kufuatia mawazo ya John Mbiti, tunaweza kuwaita wakazi wajumuiya ya wahenga kwa jina la wafu wanaoishi. Wahenga haohawajafa katika ulimwengu wa kiroho. Kadhalika, hawajafa katikakumbukumbu za waliohai, wake kwa waume ambao wanaendeleakuwakumbuka na huendelea kuomba msaada wao kupitia matendombalimbali ya matambiko na kutoa sadaka. (Tafsiri ya mtafiti)
Katika andiko hili, Menkiti amefafanua juu ya imani za Waafrika katika kifo ambapo
anaona kuwa mtu akifa anaendelea kuishi katika ulimwengu mwingine wa kiroho.
Hii ina maana kuwa mwili ndio unaotengana na roho lakini roho inaendelea kuwepo
na kuwatembelea waliohai. Fikra hizi zinashabihiana kwa kiasi kikubwa na Stumph
na Fierser (2008) ambao wanaona kuwa roho ya binadamu ni muunganiko wa mwili
na roho. Baada ya mwili na roho kutengana kutokana na kifo, roho husambazwa kwa
binadamu wengine mmoja baada ya mwingine na kuwa roho hizi haziteketei kwa
kuwa hurudi kuungana na roho za dunia. Maelezo haya yamemsaidia mtafiti katika
kubaini kuwa kifo na uhai ni kipengele kimojawapo cha falsafa ya Kiafrika kwa
kuwa, kinajaribu kujibu maswali ya msingi ya kifalsafa. Maswali hayo pengine
yasingeweza kujibiwa kwa taaluma nyingine. Andiko la mtaalamu huyu limeacha
pengo la kutafiti kwani andiko hilo halikufafanua kwa kina kuhusiana na namna
falsafa hiyo inavyojitokeza katika vitendawili vya Kiswahili. Utafiti huu umeziba
pengo hilo kwa kujadili namna falsafa ya Kiafrika inavyojitokeza katika vitendawili
vya Kiswahili.
2.3.2 Mapitio ya Maandiko Kuhusu Falsafa ya Kiafrika na Fasihi
Wapo watafiti mbalimbali waliofanya tafiti zao kuhusu usawiri wa falsafa ya
Kiafrika katika fasihi yaani fasihi simulizi na fasihi andishi. Mawazo ya wataalamu
hawa kuhusu falsafa ya Kiafrika ni kama ifuatavyo;
Hussein (1976) katika kitabu chake cha Kinjekitile, ameonesha kuhusu falsafa ya
Kiafrika inayohusu imani za “uchawi” na “ushirikina”. Dhana hii imejitokeza katika
harakati za kupambana na kupinga ukoloni nchini Tanzania. Kinjekitile anatumia
uchawi kwa kukaa ndani ya maji kutwa nzima jambo ambalo kwa hali ya kawaida
haliwezekani, na anapoibuka anatoka na dawa ya maji. Dawa hiyo inaaminika kuwa
kinga kwa wapiganaji na imani kuwa risasi ikipigwa itageuka maji na haitamdhuru
mtu yeyeote aliyekunywa dawa hiyo. Jambo hili linaonesha nguvu asilia alizonazo
Kinjekitile. Nguvu hizo zinazomwezesha kutenda mambo yasiyo ya kawaida ambayo
15
mtu mwingine hawezi kutenda, ndizo zinabainisha falsafa ya Kiafrika katika masuala
ya imani. Kazi hii ni miongoni mwa kazi nyingi za fasihi zinazotambulisha imani za
Kiafrika na hivyo kubainisha falsafa yao. Andiko hili limemsaidia mtafiti kutambua
kuwa, suala la “uchawi” na “ushirikina” ni mojawapo ya amali ya kifalsafa ya
Waafrika ambayo pia mtafiti amelijadili kuonesha namna linavyojitokeza katika
vitendawili vya Kiswahili. Pengo lililoachwa katika andiko hilo ni kuwa, mtaalamu
huyu amefafanua kuhusu kipengele kimoja cha falsafa ya Kiafrika na kuacha
vipengele vingine vikiwa bado havijafafanuliwa kwa kina. Pengo hilo limezibwa na
mtafiti katika utafiti huu kwa kujadili kuhusu vipengele vingine vya falsafa ya
Kiafrika kama umoja na ushirikiano, uzazi na ulezi na uduara na kuona namna
vinavyojitokeza katika vitendawili vya Kiswahili.
Gyekye (1987) ameongelea kuhusu dhana ya mizimu ambayo ni kipengele
kimojawapo cha falsafa ya Waafrika. Katika kazi yake, Gyekye amechambua kuhusu
dhana ya kuwepo na sababu za kuwepo kwa jamii ya Waakani. Katika uchambuzi
wake amebainisha kuwa, Waakani wanatofautisha kati ya mizimu na roho. Kwake
mizimu ni dhana inayorejelea kitu kisichojulikana. Aidha, anaongeza kuwa, mizimu
ni mtu anayemithilishwa kuwa na uhusianao kati ya “mwili” na “roho” kwa kutenda
matendo ya mtu aliyehai. Kwake anaona visawe hivi viwili yaani; mizimu na roho
wakati fulani huingiliana katika matumizi na sifa zake. Utafiti wake umemsaidia
mtafiti kuelewa vema dhana ya imani katika mizimu ambayo pia mtafiti katika utafiti
huu, ameibainisha namna inavyojitokeza katika vitendawili vya Kiswahili. Pengo
lililobainika katika utafiti wake ni kuwa, utafiti huo haujafafanua kuhusu namna
suala la imani katika mizimu linavyojitokeza katika vitendawili vya Kiswahili.
Utafiti huu umeziba pengo hilo kwa kujadili namna falsafa hii ya imani katika
mizimu inavyojitokeza katika vitendawili vya Kiswahili.
Katamba (2011) amechunguza kuhusu suala la utoaji majina kwa watoto kama
kipengele kimojawapo cha falsafa ya Kiafrika. Katika tasnifu yake iliyolenga
kuchunguza utamaduni wa kutoa majina wa jamii ya Wanyakyusa. Amebainisha juu
ya asili na chimbuko la majina ya jamii ya Wanyakyusa, kuchunguza juu ya
visababishi vya utoaji wa majina hayo na maana mbalimbali za majina katika jamii
hiyo. Katika utafiti huo alibaini kuwa, kuna sababu mbalimbali zinazosababisha
majina kutolewa. Sababu hizo ni kama vile matatizo ya kifamilia na sababu za
16
kihistoria zinazoambatana na matukio yaliyotokea wakati mtoto anazaliwa. Hata
hivyo, kila jina linalotolewa huwa na maana na hakuna jina ambalo hutolewa
kiholela bila kuwa na maana. Andiko hili ni muhimu kwani linabainisha mila na
desturi za Watanzania katika muktadha wa kitamaduni ambazo kwazo maarifa ya
kifalsafa ya Waafrika huibuliwa ndani yake. Hata hivyo, utafiti huo umeacha pengo
la kutafiti katika kufafanua athari ya utamaduni huo kwa jamii kama inavyosawiriwa
katika vitendawili vya Kiswahili. Pengo hilo limezibwa na utafiti huu kwa
kutathmini athari ya falsafa ya Waafrika kwa jamii kama inavyojitokeza katika
vitendawili vya Kiswahili.
Simchimba (2012) amefanya utafiti wake uliojikita katika kuchunguza falsafa ya
Kiafrika katika methali za Kiswahili. Anasema methali ni kipengele muhimu cha
lugha kinachogusa kwa kiasi kikubwa maisha ya watu. Kupitia methali za Kiswahili
aliweza kuthibitisha kuwepo kwa falsafa ya Kiafrika. Katika utafiti huo anataja
baadhi ya vipendele vya falsafa ya Kiafrika vinavyojitokeza katika methali hizo
kuwa ni falsafa ya umoja, ukweli na maana, hekima na busara, masuala ya ndoa,
falsafa ya uzazi na sanaa jadi. Utafiti huo una mchango mkubwa katika utafiti wetu
kwani umeonesha kupitia methali namna Waafrika wanavyofikiri na kutenda mambo
mbalimbali katika jamii na hivyo kutambulisha falsafa yao. Hata hivyo, vitendawili
kama kipera kimojawapo cha fasihi simulizi hakikushughulikiwa katika utafiti huo,
na hivyo kutoa mwanya kwa mtafiti kuchunguza namna vitendawili vya Kiswahili
vinavyoweza kusawiri falsafa ya Waafrika.
Duwe (2016) amefanya utafiti wake juu ya mdhihiriko wa falsafa ya Uduara katika
sanaa za maonyesho za jamii ya Wangoni. Katika utafiti huo, alibainisha miktadha
mbalimbali ambayo kwayo falsafa ya uduara inadhihirika katika jamii ya Wangoni.
Anafafanua baadhi ya miktadha hiyo kuwa ni katika mkao wa kula, katika miktadha
ya ngoma zao, katika shughuli za mazishi (misiba) na katika sherehe zao za kikabila.
Pia anaeleza kuwa baadhi ya vitu vyao wanavyovitumia kama vile vigoda na nyungo
ni za umbo la duara. Andiko hili linadhihirisha kuwa Waafrika wana falsafa ya
uduara. Andiko hili lilimwezesha mtafiti kuongeza maarifa kwa kubaini kuwa, dhana
ya uduara ni kipengele muhimu katika uibuaji wa maarifa ya falsafa ya Waafrika.
Hata hivyo, licha ya umuhimu huo, andiko hilo halijaonesha chochote kuhusu namna
vitendawili vya Kiswahili vinavyoweza kutumika kudhihirisha falsafa ya uduara kwa
17
kuwa halikuwa lengo lake la utafiti. Utafiti huu umeziba pengo hilo kwa kuonesha
namna falsafa ya Kiafrika ikiwemo uduara inavyodhihirika katika vitendawili vya
Kiswahili.
Naye Makame, (2016) amefafanua dhana ya Usihiri kama inavyojitokeza katika
riwaya za Kiswahili. Katika utafiti wake amechunguza miktadha ambayo usihiri
huelekezwa katika riwaya teule, sababu zinazochangia kutokea kwa falsafa ya usihiri
katika riwaya na kutathmini athari za matumizi ya falsafa ya usihiri kwa jamii na
wasomaji wa riwaya. Utafiti wake ulibaini kuwa sababu zichangiazo kutokea kwa
falsafa ya usihiri katika riwaya ni shughuli za kisiasa, shughuli za kiutamaduni,
shughuli za kiuchumi na sababu za kitajriba au mazoea. Aidha, amefafanua athari
chanya za falsafa ya usihiri kama kuimarisha mapenzi, ufahari na ulinzi na athari
hasi ni kusababisha kuleta ugomvi ndani ya jamii na kujenga maadili mabaya. Utafiti
wake umemsaidia mtafiti katika kubaini kuwa, usihiri ni kipengele kimojawapo
kinachodhihirisha falsafa ya Waafrika. Kwa kuwa utafiti huo umeshughulikia
kipengele kimoja cha falsafa ya Waafrika, umeacha pengo kwa upande wa vipengele
vingine vya falsafa ya Kiafrika kama vinavyojitokeza katika vitendawili vya
Kiswahili. Pia, kipengele hicho kimejadiliwa kwa kuonesha namna kinavyojitokeza
katika riwaya za Kiswahili. Hivyo, hakijajadiliwa kwa upande wa vitendawili ili
kuona namna dhana ya usihiri inavyojitokeza katika vitendawili vya Kiswahili.
Pengo hilo limezibwa na utafiti huu kwa kujadili namna vipengele mbalimbali vya
falsafa ya Kiafrika vinavyojitokeza katika vitendawili vya Kiswahili.
Faustine (2017) alifanya utafiti wake kuhusu falsafa ya Waafrika na ujenzi wa
mtindo wa uhalisiaajabu katika riwaya ya Kiswahili. Katika utafiti huo alibainisha
namna falsafa ya Waafrika inavyosawiriwa katika riwaya teule za Kiswahili za
kihalisiajabu. Pia alijadili namna falsafa ya Waafrika inavyojitokeza kama kijenzi
cha mtindo wa uhalisiajabu katika riwaya teule za Kiswahili za kihasiajabu.
Akifafanua kuhusu falsafa ya Waafrika anasema kuwa Waafrika wanaamini katika
nguvu-hai ambazo zimepangwa kidarajia kwa maana kuwa Mwenyezi Mungu ndiye
mmiliki mkuu wa nguvu-hai wakifuatia wahenga, mababu, wazazi na kadhalika. Hii
ina maana kuwa wahenga wana nguvu kubwa kuliko mababu na mababu wana
nguvu kuliko wazazi na hivyo hivyo mpaka katika ngazi ya chini. Katika hili
anasema kuwa;
18
Kwa Waafrika, mfumo wa kidarajia ndio unaoweka msingi wamaadili ambao umekitwa katika nguvu-hai. Kwa maana hiyo,kuwatii wahenga na mababu ni chanzo cha baraka kubwa aunguvu-hai kubwa kuliko wazazi. Kinyume chake, ni kuitafuta laanainayotokana na upungufu wa nguvu hiyo. Falsafa mbalimbalizinazoijenga falsafa jumuifu ya Waafrika kama vile uzazi na ulezi,uchawi, maisha baada ya kifo, busara na hekima, umoja naushirikiano na dhana ya uduara zinajengwa katika msingi wafalsafa kuu ya kuwapo kwa nguvu-hai.
Maelezo ya mtaalamu huyu yanathibitisha kuwa, Waafrika wana falsafa yao ambayo
imekitwa katika nguvu-hai. Waafrika wanaamini kuwa, mtu akiumwa nguvu hai
zake zinapungua kwa hiyo atakufa na mchawi ndiye anayeweza kupunguza nguvu-
uhai za mtu. Vile vile, wenye uwezo wa kuongeza nguvu-hai wanaoelezwa na
Faustine kuwa ni Mungu – mizimu – wahenga – mababu – wazazi. Andiko la
mtaalamu huyu limemsaidia mtafiti kuelewa falsafa ya Kiafrika katika mawanda
mapana ya kazi za fasihi za kihalisiajabu. Hata hivyo, utafiti wake ulijikita katika
kufafanua namna falsafa ya Kiafrika inavyojitokeza kama kijenzi cha mtindo wa
uhalisiajabu katika riwaya teule za kihalisiajabu. Kwa kuwa, andiko hili halijatoa
ufafanuzi kuhusu namna falsafa hiyo inavyosawiriwa katika vitendawili vya
Kiswahili na wala kubainisha athari za falsafa hiyo kwa jamii kwa sababu suala hilo
halikuwa lengo la mtaalamu huyu. Hali hii ndiyo imemfanya mtafiti kuamua
kulishughulikia ilio kuziba pengo hilo kwa kujadili namna falsafa ya Waafrika
inavyojitokeza katika vitendawili vya Kiswahili pamoja na athari za falsafa hiyo kwa
jamii.
Mlelwa, (2017) alifanya utafiti wake kuhusu falsafa ya Kiafrika katika vitabu teule
vya fasihi ya Kiswahili: Ngoma ya Ng’wanamalundi na Dunia Uwanja wa Fujo.
Katika utafiti wake amebainisha vipengele vya falsafa ya Kiafrika vinavyojitokeza
katika kazi teule pamoja na kulinganisha na kulinganua namna waandishi wa kazi
hizo walivyotumia vipengele vya falsafa ya Kiafrika katika kusuka simulizi na
kuumba wahusika wao. Baadhi ya vipengele hivyo ni kama vile uchawi na ulozi,
uhai na kifo, hekima na busara, umoja na ushirikiano, uzuri, wakati, maadili, uganga
na uongozi. Utafiti wake umekuwa na umuhimu mkubwa katika utafiti huu kwani
umepanua mawanda ya uelewa wetu kuhusu vipengele vinavyodhihirisha falsafa ya
Kiafrika. Andiko hilo halijafafanua athari ya falsafa ya Kiafrika kwa jamii kama
inavyosawiriwa katika vitendawili vya Kiswahili kwa kuwa lilikuwa nje ya malengo
19
yake. Hivyo, pengo hilo limezibwa na utafiti huu kwa kutathmini athari ya falsafa ya
Kiafrika kwa jamii kama inavyosawiriwa katika vitendawili vya Kiswahili.
Kaponda (2018) amefanya uchunguzi kuhusu Ontolojia ya Kiafrika katika mbolezi
za Wanyasa. Amebainisha aina za mbolezi zinazopatikana katika jamii ya Wanyasa
na vipengele vya ontolojia ya Kiafrika katika mbolezi za Wanyasa. Pia, ametoa
tathmini juu ya umuhimu wa ontolojia ya Kiafrika kwa jamii na Waafrika kwa
ujumla. Baadhi ya vipengele vya ontolojia ya Waafrika vilivyodhihirika kupitia
mbolezi za Wanyasa ni ardhi, Mungu, kifo, roho, utu, na wahenga au mizimu.
Anaendelea kueleza kuwa, katika jamii ya Wanyasa fasihi ambayo yamkini ni zao la
jamii imetumika ili kufikisha mawazo ya kifalsafa ambayo ni matokeo ya uzoefu wa
wanajamii katika mazingira yao. Katika utafiti wake ametathmini nafasi ya ontolojia
ya Kiafrika kwa jamii. Baadhi ya faida zinazoelezwa na mtafiti ni kama vile
kudumisha umoja na mshikamano, kujadili masuala muhimu ya jamii, kurithisha
amali za jamii na kulinda maadili. Utafiti wake umekuwa na umuhimu mkubwa
kwani umetusaidia kujua kuwa, fasihi ya jamii ndiyo hutumika kufikisha mawazo ya
kifalsafa ya jamii husika. Hata hivyo, andiko hilo halikugusia chochote kuhusu
falsafa ya Kiafrika katika vitendawili vya Kiswahili kwa sababu suala hilo halikuwa
lengo lake la utafiti wake. Hivyo, ili kuziba pengo hilo, mtafiti ameona ni vema
utafiti huu kujengewa hoja kuhusu usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika semi
hususani vitendawili vya Kiswahili.
2.3.3 Mapitio ya Maandiko kuhusu Vitendawili vya Kiswahili
Mng’aruti (2008) anafasili vitendawili kuwa ni maneno yanayoficha maana ya kitu
ili kisijulikane kwa urahisi. Maneno ya kawaida, vitu au hali mbalimbali za kawaida
huelezwa kimafumbo au kisanaa ili wafumbuzi wayafumbue. Fasili hii ni pana sana
kwani inajumuisha vitu vyote ambavyo hutolewa kwa njia ya mafumbo kuingia
katika kundi la vitendawili ambavyo kiuhalisia sio vitendawili. Vijitanzu kama nahau,
mafumbo na methali pia hutumia mafumbo lakini sio vitendawili. Pamoja na
mapungufu ya fasili hii bado inatupa mwanga juu ya sifa muhimu ya vitendawili ya
hali ya ufiche ambayo hueleza jambo kwa hali za kawaida zilizozoeleka kisanaa au
kimafumbo. Aidha, anaona kuwa vitendawili vina umuhimu mkubwa kama ilivyo
kwa methali. Kwa hiyo, andiko hili limekuwa na umuhimu katika utafiti wetu kwani
limepanua wigo wa ufahamu wetu kuhusu umuhimu wa vitendawili kwa jamii. Licha
20
ya kuwa na umuhimu huo, andiko hili halijaeleza kama vitendawili vinaweza
kutumika kudhihirisha amali za kifalsafa za jamii ya Waafrika. Ili kuziba pengo hilo,
mtafiti ameona ni vema utafiti huu kujengewa hoja juu ya usawiri wa falsafa ya
Kiafrika katika vitendawili vya Kiswahili.
Amana, (2013) anaeleza kuhusu dhana ya vitendawili kuwa ni swali la kisitiari
ambapo sehemu moja ya ulinganishi uliopo inadokezwa tu ilhali ya pili inabakia ya
kukisiwa. Kama sanaa, vitendawili hutegemea uwezo alionao mtu kutambua,
kuhusisha na kulinganisha vitu vya aina tofauti katika mazingira yake. Hii ni sanaa
inayotendwa na inayosimama kivyake tofauti na sanaa tegemezi au elekezi kama
methali. Vitendawili hulenga maisha ya jamii na shughuli wafanyazo. Vitendawili
vingi hushughulikia mambo tofauti yanayomhusu binadamu kama kifo, uhai, chakula,
maisha na mazingira. Pia akielezea kuhusu asili ya vitendawili anasema vitendawili
vinatokana na mahitaji ya kisanaa, mahitaji ya matumizi, mahitaji ya kueleza
mazingira na maendeleo na misemo ya kimtaa. Anataja sifa za vitendawili na
muundo wake.
Katika andiko lake Amana, (2013), amefafanua pia kuwa vitendawili vina umuhimu
mkubwa kwa jamii. Kwa kutaja baadhi ya faida hizo ni kama vile, husaidia kuhifadhi
historia na utamaduni wa jamii, huwa msingi wa kuyachambua maisha ya jamii,
kuonesha hisia za wanajamii kuhusu mtu au kitu fulani, kuelimisha kuhusu
mazingira, imani, amali, mavazi na historia. Pia, vitendawili huchochea kufikiria kwa
wanajamii kwa njia ya kupevusha kukabiliana na maisha yao na kudhihaki au
kukejeli sifa na tabia zisizofaa. Andiko hili limekuwa na umuhimu mkubwa katika
utafiti wetu kwani limevielezea vitendawili katika mawanda mapana ya kimaudhui
na hivyo kumpatia mtafiti nafasi ya kuvielewa vitendawili kwa upana. Pengo
lililoachwa katika utafiti huo ni kuwa, utafiti wake haujatambulisha vitendawili kama
amali ya kifalsafa ya Kiafrika. Kutoshughulikiwa kwa kipengele hicho katika andiko
hili ndio kumemfanya mtafiti kutaka kujua zaidi vitendawili kama amali za
kitamaduni vinavyoweza kusawiri falsafa ya Kiafrika. Hivyo, utafiti huu
unachunguza usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika vitendawili vya Kiswahili.
Gwaravanda na Masaka (2008) wananukuliwa na Badru (2015) katika utafiti wao wa
vitendawili vya jamii ya Washona wa Zimbabwe. Wanashadidia umuhimu wa
21
vitendawili kwa kueleza kuwa vitendawili ndicho kiini cha mfumo wa elimu ya jamii
hiyo. Utafiti wao unaonesha kuwa dhima kubwa ya vitendawili ni kuelimisha na sio
kuburudisha tu kama ilivyoelezwa na watu walio wengi. Vitendawili vinafundisha
vijana masuala yanayohusu mila, desturi, uzoefu wao, miiko na tamaduni katika
mazingira yao. Utafiti huu unaosisitiza umuhimu wa vitendawili umetupa hamasa ya
kutaka kuchunguza zaidi katika utanzu huu ambao kwa baadhi ya watafiti haupewi
kipaumbele ili kubaini uchomozi wa falsafa ya Kiafrika katika vitendawili vya
Kiswahili. Pengo lililojitokeza katika andiko hilo ni kuwa, andiko hilo limefafanua
dhima ya vitendawili kwa jumla bila kutathmini athari ya falsafa ya Kiafrika kwa
jamii kama inavyosawiriwa katika vitendawili vya Kiswahili. Utafiti huu umeziba
pengo hilo kwa kutathmini athari ya falsafa ya Kiafrika kwa jamii kama
inavyosawiriwa katika vitendawili vya Kiswahili.
Naye Badru (2015) amefanya utafiti wake kuhusiana na taswira na ubainishaji wa
mabadiliko ya kiujumi katika vitendawili vya Kiswahili. Katika utafiti wake
amefafanua dhima za vitendawili nakukanusha madai ya baadhi ya wataalmu
wanaoona kuwa vitendawili ni sanaa ya watoto na haina umuhimu wowote kwa jamii
zaidi ya kuburudisha watoto. Amefafanua dhima za vitendawili kiuchumi, kijamii na
kiutamaduni. Utafiti huu ni muhimu kwani umesaidia katika kutoa mwongozo mzuri
katika kufafanua ujumi wa Kiafrika katika vitendawili. Hata hivyo, andiko hilo
halikuzungumzia chochote kuhusu namna vitendawili vya Kiswahili vinavyoweza
kutumika kuhakiki falsafa ya Kiafrika. Pia, halijatathmini athari ya falsafa ya
Kiafrika kwa jamii kama inavyosawiriwa katika vitendawili vya Kiswahili. Ili kuziba
pengo hilo, utafiti huu unakwenda zaidi ya hapo kwa kuchunguza vipengele vya
falsafa ya Kiafrika vinavyojitokeza katika vitendawili vya Kiswahili na kutathmini
athari ya falsafa hiyo kwa jamii.
Mtaalamu mwingine ambaye amefanya uchunguzi wa vitendawili ni Damka (2015).
Yeye alichunguza dhima ya vitendawili vya jamii ya Wanyisanzu wa Iramba Singida.
Katika andiko hilo alitafiti kuhusu chanzo cha mabadiliko ya dhima za vitendawili
vya jamii ya Wanyisanzu na vipengele vya fani vinavyosababishwa na mabadiliko ya
utegaji vitendawili. Anaeleza kuwa vitendawili vilikuwa na dhima kubwa kabla ya
uhuru wa Tanganyika na hata sasa katika jamii yetu. Miongoni mwa dhima
zinazotajwa ni kama kuelimisha jamii kuhusu mambo ya kiuchumi, kiutamaduni na
22
kijamii, kuhifadhi na kuendeleza mila na desturi za jamii inayohusika, kufundishia
msamiati mpya shuleni na kutangaza biashara za watu ili bidhaa zao ziweze
kununuliwa kwa wingi. Andiko hili limekuwa na umuhimu katika utafiti wetu kwani
limetuongoza katika kubaini umuhimu wa vitendawili katika jamii. Hata hivyo,
andiko hili limeacha pengo lililotakiwa kuzibwa na utafiti huu kwani halijafafanua
namna vitendawili vya Kiswahili vinavyoweza kusawiri falsafa ya Kiafrika. Utafiti
huu umeziba pengo hilo kwa kujadili namna falsafa ya Kiafrika inavyojitokeza
katika vitendawili vya Kiswahili.
Vilevile, Mshana (2015) amefanya utafiti wake ambapo amechunguza usawiri
chanya wa mwanamke katika vitendawili vya jamii ya Wanyiha. Katika utafiti huo,
alitathmini usawiri chanya wa mwanamke katika vitendawili vya jamii ya Wanyiha
na kuchunguza ujumbe unaopatikana katika vitendawili. Utafiti wake ulibaini kuwa
mwanamke anasawiriwa kama mama na mlezi wa watoto katika jamii. Akitolea
mfano wa kitendawili cha “mama anatembea na kibyongo” ambacho jibu lake ni
“konokono”, mtafiti alieleza kuwa, kitendawili hiki kinamsawiri mwanamke na
mtoto wake tangu akiwa tumboni, kuzaliwa kwake akiwa katika hali ya uchanga
anamlea mwanae hadi anapokufa na hata akifa uhusiano wa mama na mwana
huendelea kwenye ndoto, dua na mizimu. Vitendawili vinamsawiri mwanamke kama
kiumbe mvumilivu na mchapakazi katika jamii. Andiko hili limemsaidia mtafiti
kupanua uelewa wake kuhusu dhima kubwa ya vitendawili katika jamii. Hata hivyo,
utafiti huo haujagusia chochote kuhusu usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika
vitendawili vya Kiswahili. Hivyo, ili kuziba pengo hilo, utafiti huu umechunguza
usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika vitendawili vya Kiswahili.
2.4 Mapengo Yanayojitokeza
Wakati wa kupitia maandiko mbalimbali ya watafiti na wahakiki wa kazi za fasihi,
falsafa ya Waafrika na vitendawili vya Kiswahili, tumebaini mapengo yafuatayo;
Mosi, watafiti hawa hawajabainisha na kueleza kwa kina vijenzi vya falsafa ya
Kiafrika katika muktadha wa kitamaduni. Pili, tafiti nyingi hazijashughulikia suala la
falsafa ya Kiafrika kama inavyosawiriwa katika vitendawili vya Kiswahili. Tatu, kazi
hizo hazijachunguza kwa kina kuhusu athari ya falsafa ya Kiafrika kama
inavyojitokeza katika vitendawili vya Kiswahili. Hivyo, utafiti huu umeshughulikia
23
mapengo hayo yaliyoachwa na watafiti waliotangulia kwa kupitia malengo mahsusi
matatu yaliyotuongoza katika utafiti huu.
2.5 Muhtasari wa Sura ya Pili
Sura hii imefafanua kuhusu kiunzi cha nadharia iliyotumika katika kufafanua na
kuchanganua data za utafiti na maandiko mbalimbali ambayo mtafiti aliyapitia. Kwa
ujumla mapitio hayo yamebeba mawazo na mitazamo mbalimbali ya wataalamu na
wanazuoni kuhusu falsafa ya Kiafrika kwa ujumla wake, falsafa ya Kiafrika katika
fasihi na mitazamo mbalimbali kuhusu vitendawili vya Kiswahili. Hivyo, sura
inayofuata inafafanua kuhusiana na methodolojia iliyotumika katika mchakato
mzima wa kukusanya na kuchambua data za utafiti huu.
24
SURA YA TATU
METHODOLOJIA YA UTAFITI
3.1 Utangulizi
Sura hii imefafanua kuhusu methodolojia iliyotumika katika kufanikisha utafiti huu.
Vipengele vilivyoshughulikiwa katika sehemu hii ni usanifu wa utafiti, mkabala wa
utafiti, eneo la utafiti, walengwa na sampuli ya utafiti, mbinu za ukusanyaji na
uchanganuzi wa data. Vipengele vingine ni vifaa mbalimbali vilivyotumika katika
kukusanya data, itikeli za utafiti, uhalali na uthabiti wa data. Aidha, mtafiti ameeleza
baadhi ya changamoto mbalimbali alizokutana nazo wakati wa kukusanya data na
namna alivyozitatua.
3.2 Usanifu wa Utafiti
Utafiti huu ulitumia usanifu wa fenomenolojia katika kukusanya data na
kuchanganua data za utafiti huu. Kwa mujibu wa Kothari (2004) usanifu wa utafiti ni
uamuzi kuhusu nini, wapi, lini, kwa kiwango gani na namna gani utafiti utafanyika.
Hii ina maana kuwa usanifu wa utafiti ni mpangilio maalumu wa kanuni za
kukusanya data na uchanganuzi wake ili kufikia uyakinifu wa malengo ya utafiti kwa
kuzingatia muda, mahali pa utafiti na hali ya uchumi iliyopo katika kuikamilisha
mada ya utafiti. Utafiti huu ulijikita katika ufafanuzi wa taarifa zilizokusanywa na
kuchambuliwa kwa njia ya maelezo yaliyoakisi mtazamo wa wahojiwa kulingana na
walivyoielewa falsafa ya Kiafrika. Hivyo, ilichukuana na usanifu wa
kifenomenolojia kwa sababu data zilikusanywa kwa kujigeza katika uelewa,
mitazamo, na tajiriba za watafitiwa kuhusiana na falsafa yao. Fenomenolojia
hujihusisha na maisha ya binadamu na namna ya kuufahamu ulimwengu kulingana
na uzoefu wa maisha ya watu hao kuhusiana na jambo fulani. Hivyo, usanifu huu
ulifaa sana katika utafiti huu kwani ulihusiana na maisha halisi ya watu katika
mitazamo yao, na hivyo, kusaidia kumwongoza mtafiti kuchunguza mawazo na
tajiriba za watafitiwa kuhusu falsafa ya Kiafrika katika vitendawili vya Kiswahili.
3.3 Mkabala wa Utafiti
Utafiti huu ulitumia mkabala wa kitaamuli katika ukusanyaji, uchanganuzi wa data
pamoja na kutoa matokeo ya utafiti. Ponera (2016) anaeleza kuwa utaamuli ni aina
mojawapo ya mikabala ya kufanyia utafiti, ambao hutumia zaidi tafakuri katika
kuhusisha taarifa mbalimbali za kitafiti. Pia huhusisha ufafanuzi wa jambo kwa
25
kuzingatia misingi ya nadharia husika, pamoja na ithibati bayana zipatikanazo
maskanini au uwandani. Kwa hiyo, mkabala huu umekuwa na manufaa katika utafiti
huu kwa sababu, data zinazohusiana na falsafa ya Kiafrika katika vitendawili vya
Kiswahili zilizopatikana uwandani na maktabani zimechanganuliwa na kufafanuliwa
kwa njia ya maelezo. Data hizo zimesadifu usanifu wa utafiti huu kwa sababu
zilikusanywa na kuchambuliwa kwa njia ya maelezo yaliyoakisi mitazamo ya
watafitiwa kulingana na walivyoielewa falsafa yao.
3.4 Eneo la Utafiti
Utafiti huu ulifanyika uwandani na maktabani. Maeneo yaliyohusishwa ni Mikoa ya
Dodoma na Kagera. Katika mkoa wa Dodoma, sehemu zilizotumika ni wilaya ya
Dodoma mjini. Eneo hili lilichaguliwa kwa sababu ya uwepo wa maktaba za Chuo
Kikuu cha Dodoma na maktaba ya Mkoa wa Dodoma. Maktaba hizo zilitumika
kudurusu nyaraka mbalimbali zinazohusiana na mada huzika. Mkoa wa Kagera,
utafiti ulifanyika wilaya ya Bukoba ambapo mtafiti aliweza kuwapata walengwa wa
utafiti wake walioshiriki kutoa data za uwandani. Nao ni wanafunzi wa shule za
msingi na sekondari wa Bukoba pamoja na wanajamii wa wilaya ya Bukoba. Eneo
hili lilichaguliwa kutokana na sababu kuwa mazingira na wenyeji wa eneo hilo ni
miongoni mwa jamii za Kiafrika wanaotumia lugha ya Kiswahili ambao mtafiti
aliwakusudia. Pia, sehemu hii hakuna mwingiliano mkubwa wa makabila na, ni
mojawapo ya watu ambao hawajaacha mila na desturi zao kwa kiasi kikubwa. Hivyo,
ilikuwa rahisi kwa mtafiti kupata taarifa sahihi kutoka kwa watafitiwa. Taarifa hizo
zilihusiana na vijenzi vya falsafa ya Kiafrika katika muktadha wa kitamaduni, falsafa
ya Kiafrika katika vitendawili vya Kiswahili na athari za falsafa hiyo kwa jamii kama
inavyosawiriwa katika vitendawili vya Kiswahili.
3.5 Walengwa wa Utafiti
Kwa mujibu wa Kombo na Tromp (2006), walengwa wa utafiti ni kundi la watu, vitu
au elementi ambazo mtafiti amekusudia kuvitumia katika utafiti wake. Kipengele
hiki cha walengwa wa utafiti kimehusisha makundi mawili ambayo ni jamii tafitiwa
na sampuli iliyoshughulikiwa.
26
3.5.1 Jamii Tafitiwa
Faustine (2012) anaeleza kuwa jamii tafitiwa ni jumla ya vitu vyote ambavyo mtafiti
anaweza kuvitumia kwa ajili ya kupata data za utafiti wake. Vitu hivyo huweza kuwa
kundi la watu, eneo fulani la kijiografia au maandiko yanayohusiana na mada husika.
Katika utafiti huu, jamii tafitiwa ilijumuisha:
a) Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za wilaya ya Bukoba. Kundi hili
liliteuliwa kwa sababu mtafiti alikusudia kupata vitendawili vingi
iwezekanavyo kwani ni katika kiwango hiki cha elimu ambapo wanafunzi
hujifunza vitendawili kwa kiasi kikubwa.
b) Wanajamii wa wilaya ya Bukoba mkoani Kagera. Kundi hili liliteuliwa
kutokana na sababu kuwa, mada ya utafiti inamtaka mtafiti kutumia watu
wenye ujuzi au uzoefu wa moja kwa moja juu ya falsafa yao huku akihusisha
na uhalisi wa maisha yao. Wanajamii hawa wametumiwa kama kiwakilishi
tu cha jamii za Kiafrika wanaotumia lugha ya Kiswahili. Hata hivyo, mtafiti
angeweza kuwatumia wanajamii kutoka katika jamii nyingine tofauti na hii,
lakini, kutokana na rasilimali alizokuwa nazo hasa muda na fedha
zilisababisha kuteua walengwa hao kama kiwakilishi cha jamii nyingine za
Kiafrika. Kundi hili limesaidia kupata data kuhusu vijenzi vya falsafa ya
Kiafrika katika muktadha wa kitamaduni na kufafanua athari za falsafa hiyo
kwa jamii kama inavyojitokeza katika vitendawili vya Kiswahili.
c) Matini mbalimbali za kifasihi zilizohusu semi hasa vitendawili na maandiko
yanayohusu falsafa ya Kiafrika. Matini hayo yamesaidia kupatikana kwa
data zinazohusu vitendawili vya Kiswahili na falsafa ya Kiafrika kwa jumla.
3.5.2 Sampuli na Usampulishaji Wake
Ponera (2019) anasema usampulishaji ni kitendo cha kuteua sehemu ya wango ili
itumiwe na mtafiti katika kuchunguza na kupata majibu ya tatizo lake la utafiti.
Usampulishaji ni kitendo cha mtafiti kuteua sehemu ya watu, dhana au vitu ambavyo
vimechaguliwa kutoka katika kundi au jamii fulani ili kuwakilisha kutoa taarifa
zitakazokuwa kiwakilishi cha jamii nzima. Utafiti huu umetumia usampulishaji
lengwa katika kupata sampuli ya watafitiwa. Katika mbinu hii mtafiti hulenga kundi
fulani la watu, vitu au dhana zinazoaminika kuwa na uhakika juu ya utafiti husika
(Kombo na Tromp 2006).
27
Utafiti huu umetumia usampulishaji lengwa wa aina mbili; tajwa na wa kutumia
fursa. Mosi, mtafiti ametumia usampulishaji lengwa wa kutegemea fursa katika
kuwapata wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambao kimsingi walipatikana
kutegemeana na fursa ya muda huo. Hawa walisaidia kupatikana kwa vitendawili
vya Kiswahili wanavyovitumia katika mazingira yao na namna vitendawili hivyo
vinasawiri falsafa ya Kiafrika. Pili, utafiti huu ulitumia usampulishaji lengwa wa
kupokezana au tajwa katika kuwapata wanajamii. Hawa walieleza kuhusu vijenzi vya
falsafa ya Kiafrika na kufafanua athari ya falsafa hiyo kwa jamii kama
inavyosawiriwa katika vitendawili vya Kiswahili. Aidha, matini mbalimbali
zilizotumika pia zimetumia usampulishaji lengwa kwani zimechaguliwa kwa
kuzingatia maarifa yanayopatikana kuhusiana na mada ya utafiti. Hivyo,
usampulishaji huu umerahisisha kupata taarifa za kina kuhusu falsafa ya Kiafrika
inavyosawiriwa katika vitendawili vya Kiswahili, vijenzi vya falsafa ya Kiafrika
kama vinavyojitokeza katika vitendawili vya Kiswahili na athari ya falsafa ya
Kiafrika kwa jamii.
3.5.2.1 Sampuli ya Utafiti
Kwa mujibu wa Gay (1987) sampuli ni sehemu ndogo ya kundi lengwa
iliyochaguliwa kushiriki katika kutoa data za utafiti. Utafiti huu ni wa kitaamuli
ambao huhusisha maelezo katika kutafsiri data. Idadi ya watafitiwa katika tarakimu
haina athari yoyote ya kitafiti bali imewekwa kama mwongozo wa kupata ramani ya
makadirio ya bajeti na muda wa utafiti. Sampuli iliyolengwa katika kutoa taarifa za
utafiti huu ilijumuisha; wanafunzi ishirini (20) kutoka shule za msingi za Wilaya ya
Bukoba. Hawa walishiriki katika kutoa taarifa zinazohusiana na vitendawili vya
Kiswahili. Pia, wanafunzi kumi (10) kutoka shule za sekondari za wilaya ya Bukoba.
Kundi hili lilishiriki katika kutoa taarifa zinazohusiana na vitendawili na kueleza
namna vitendawili vinavyosawiri masuala ya mila, desturi, uzoefu na kaida za jamii
ambavyo kwa jumla vinaunda falsafa ya Kiafrika. Pia wanajamii ishirini na watano
(25) wa wilaya ya Bukoba mkoani Kagera. Hawa walishiriki katika kutoa taarifa
zilizohusiana na vijenzi vya falsafa ya Kiafrika katika muktadha wa kitamaduni,
falsafa ya Kiafrika katika vitendawili na athari ya falsafa hiyo kwa jamii. Matini
nane (8) za falsafa na vitendawili vya Kiswahili zenye maudhui yanayohusiana na
mada yetu. Matini hizi zilisaidia katika kupatikana kwa maudhui yanayohusu
28
vitendawili vya Kiswahili na falsafa ya Kiafrika kwa jumla. Mtafiti alitumia idadi
hiyo ya watafitiwa kutokana na aina ya utafiti wa kitaamuli ambao unaeleza kuwa
idadi ya watafitiwa wanaweza kuwa kuanzia watatu hadi thelathini kutegemeana na
miktadha mingine inayozungukia utafiti wenyewe (Ponera, 2019).
3.6 Ukusanyaji wa Data
Sehemu hii inaelezea njia na zana zilizotumika katika ukusanyaji wa data. Pia,
sehemu hii imefafanua jinsi mchakato wa ukusanyaji data ulivyofanyika.
3.6.1 Njia na Zana za Ukusanyaji wa Data
Njia zilizotumika katika ukusanyaji wa data za utafiti huu ni tatu, nazo ni mahojiano,
mjadala wa vikundi lengwa na udurusu wa nyaraka. Mtafiti ametumia njia za
kukusanyia data zaidi ya moja ili kuongeza kiwango cha uthabiti wa data za utafiti.
Kama anavyoeleza Ponera (2019) kuwa, kutumia mseto wa njia za kukusanyia data
huongeza uwezekano wa kuwa na kiwango kikubwa cha uthabiti. Hii ni kwa sababu
huondoa uwezekano wa kuwapo kwa hitilafu za kiutafiti zinazoweza kuletwa na
watafitiwa au mtafiti. Zana zilizotumika katika ukusanyaji wa taarifa ni simu, shajara,
kalamu. Zana nyingine ni mwongozo wa mahojiano, mwongozo wa mjadala wa
vikundi na mwongozo wa udurusu. Zana hizo zimeakisi vema njia zilizotumika
katika kukusanya taarifa. Ufafanuzi kuhusu njia za ukusanyaji data zilizotumika ni
kama ifuatavyo;
3.6.1.1 Mahojiano
Kothari (2009) anaeleza kuwa mahojiano ni majibizano ya ana kwa ana au ya simu
yanayofanywa na watu wawili au zaidi kwa lengo la kukusanya taarifa au maoni
kuhusu suala fulani la kiutafiti. Mtafiti ametumia mahojiano ya ana kwa ana na
wanajamii wa wilaya ya Bukoba katika kupata vijenzi vya falsafa ya Kiafrika katika
muktadha wa kitamaduni na kueleza athari za falsafa hiyo kwa jamii. Sababu ya
kutumia njia hii ni kuwa, katika mahojiano mtafitiwa anakuwa yuko huru kutoa data
zenye usahihi. Pia, ni njia rahisi inayompa fursa ya kuuliza maswali pale
panapohitajika na hivyo kupata data za kina. Mtafiti alitumia mwongozo wa
mahojiano uliohusu vitendawili vya Kiswahili na falsafa ya Kiafrika ili kupata data
zilizohitajika.
29
3.6.1.2 Mjadala wa Vikundi Lengwa
Hii ni njia ya kukusanya taarifa inayohusisha mazungumzo baina ya mtafiti na
watafitiwa wakiwa katika vikundi juu ya mambo anayotaka kuyapata (Ponera 2019).
Mtafiti ametumia mjadala wa vikundi lengwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na
sekondari ili kupata vitendawili vya Kiswahili vinavyotumika katika jamii. Hivi
vimemsaidia mtafiti kubaini namna falsafa ya Kiafrika inavyojitokeza kutoka katika
vitendawili hivyo. Mtafiti aliamua kutumia njia hii kwa kuwa watafitiwa wake ni
watoto hivyo yawezekana wasiwe huru zaidi kutoa ushirikiano wao wakiwa mmoja
kuliko wakiwa katika kundi.
3.6.1.3 Udurusu wa Nyaraka
Kothari (2004) anaeleza kuwa udurusu wa nyaraka ni njia ya kukusanya data kutoka
katika vitabu, makala na matini za kielektroniki kwa lengo la kuzifanyia uchambuzi.
Anaendelea kueleza kwamba data zinazokusanywa kutoka vyanzo hivyo huitwa data
fuatizi. Mtafiti ameitumia mbinu hii kwa kusoma vitabu, makala na tovuti
mbalimbali zilizohusiana na utafiti huu. Hizi zilimsaidia kupata data zilizohusiana na
vijenzi vya falsafa ya Kiafrika, vitendawili vya Kiswahili na namna vitendawili
hivyo vinavyosawiri falsafa ya Kiafrika.
3.6.2 Mchakato wa Ukusanyaji Data na Udhibiti wake
Ili kupata data zilizohitajika kutoka kwa watafitiwa, mtafiti alianza kukusanya taarifa
zake kutoka kwa wanafunzi. Katika mjadala wa vikundi, mtafiti aliwagawa
watafitiwa wake katika idadi ya wanafunzi watano watano kwa wanafunzi wa shule
za sekondari na watoto kumi kumi kwa wanafunzi wa shule za msingi. Katika
makundi hayo mtafiti aliwafafanulia maswali yanayotakiwa kujibiwa na watafitiwa
katika mjadala na kuwaacha waeleze maoni yao. Mtafiti aliandika katika shajara
yake maoni ya watafitiwa hao. Kwa upande wa wanafunzi wa sekondari, aliwagawia
karatasi walizotumia kuorodhesha vitendawili vya Kiswahili na kisha kujadili kwa
pamoja kuhusu amali za kijamii zinazojitokeza katika vitendawili hivyo. Muda
uliotumika katika mijadala ni dakika themanini (80). Mbinu nyingine iliyotumika ni
mahojiano. Mtafiti aliwahoji watafitiwa wake maswali yaliyohusiana na lengo husika
na kisha kunukuu maelezo ya mahojiano hayo katika shajara yake. Muda uliotumika
kwa kila mhojiwa ni kuanzia dakika arobaini na tano hadi dakika sitini. Mbinu ya
mwisho ilikuwa ni udurusu wa nyaraka. Mtafiti alikusanya nyaraka zinazohusiana na
30
mada ya utafiti kutoka katika vitabu, majarida, makala na tovuti mtandaoni. Mtafiti
alichambua kwa kina maudhui ya nyaraka hizo huku akihusisha na malengo ya
utafiti wake na hivyo kurahisisha upatikaji wa taarifa kutoka katika vyanzo hivyo.
Kwa jumla mchakato huo umesaidia kupatikana data za kutosha kuhusiana na
usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika vitendawili vya Kiswahili.
3.7 Uchanganuzi wa Data
Ponera (2019) anafafanua kuwa, kuchanganua data ni mchakato wa kuzishughulikia
taarifa za utafiti zilizokusanywa ili kupata maana au mantiki pamoja na kupata
taarifa ua data chache zinazohitajika. Utafiti huu umefanywa kwa kutumia mkabala
wa kitaamuli, yaani mkabala usio wa kitakwimu. Enon (1998) anaeleza kuwa utafiti
wa kitaamuli ni utafiti ambao data zake huelezwa na kufafanuliwa kwa njia ya
maelezo. Mtafiti alichagua mkabala huu kwa sababu mada ya utafiti ni ya kifasihi
inayohitaji ufafanuzi wa mawazo na mtazamo juu ya dhana husika.
Katika uchanganuzi wa data za utafiti huu, mtafiti ametumia mbinu ya usimbishaji
wa maudhui. Ponera (2019) anaeleza kuwa hii ni mbinu inayofaa sana kwenye data
zenye uchangamani mkubwa wa dhana. Anamnukuu Masele (2016) anayefafanua
kuwa, mbinu hii hufafanua ujuzi, tajiriba, maana na uhalisi wa watafitiwa. Utafiti
huu ulihusisha ufafanuzi kuhusu ujuzi na mitazamo ya watafitiwa kuhusiana na
falsafa yao hivyo, imesaidia kuchanganua tabia, uzoefu na tajiriba za jamii kuhusu
maisha yao pamoja na mifumo yao ya maisha ili kubaini falsafa yao. Mtafiti alianza
kwa kuzichambua na kuzipanga data kulingana na muoano wa data hizo kimaudhui.
Hii ilifanyika kwa kuziweka data pamoja ili zilingane na malengo ya utafiti pamoja
na kuangalia uhusiano wa data alizozikusanya. Kwa hiyo, data zilizokusanywa kwa
njia ya mahojiano na mijadala ya vikundi lengwa zilichanganuliwa kwa kuwianisha
na njia ya udurusu wa nyaraka. Kwa kuongozwa na nadharia ya Kisosholojia, data
hizo zilifafanuliwa na kuwasilishwa kama matokeo ya utafiti.
3.8 Itikeli za Utafiti
Katika kuendesha mchakato wa utafiti huu, mtafiti alizingatia taratibu zote muhimu
za kimaadili wakati wote wa utafiti kuanzia hatua ya ukusanyaji data, uchanganuzi
wa data za utafiti na uandishi wa ripoti ya utafiti. Taratibu zilizozingatiwa ni pamoja
na:
31
a) Kupata kibali kutoka katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Mtafiti alichukua
barua ya utambulisho kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma iliyomtambulisha
katika maeneo husika aliyoenda kukusanya data za utafiti. Pia, aliwasilisha
barua au kibali hicho katika maeneo husika ya utafiti wake ambayo ni mkoa
wa Kagera na Dodoma.
b) Vilevile mtafiti aliwaomba ridhaa watafitiwa ili kuwafanyia utafiti. Aidha,
aliwafafanulia watafitiwa malengo na umuhimu wa utafiti huu. Watafitiwa
walihiari kuhojiwa na mtafiti alinukuu maelezo yao katika shajara yake.
c) Mtafiti aliwaeleza watafitiwa haki zao za msingi kama kuwa huru kuuliza
maswali pindi wanapoona kuna jambo halijaeleweka vema. Pia aliwaeleza
kuwa taarifa zilizotolewa zitakuwa ni siri na zitatumika kwa shughuli ya
utafiti tu. Hivyo, mtafiti alitunza siri za taarifa za watafitiwa wake ambao
baadhi hawakutaka kupigwa picha na kujulikana kwa watu wengine kama
wao walishiriki kutoa taarifa hizo.
d) Kihaiba, mtafiti alionekana katika mwonekano unaokidhi tamaduni za jamii
husika. Katika hii, mtafiti alivaa mavazi ya heshima yaliyoendana na maadili
na itikeli za jamii ya watafitiwa sambamba na kufuata mila na desturi za
mazingira yao.
3.9 Uhalali na Uthabiti wa Matokeo ya Utafiti
Kothari (2009) anaeleza kuwa, uhalali wa utafiti ni hali ya utafiti kuwa na uwezo wa
kupima mambo yaliyotakiwa kupimwa au kutafitiwa. Pia, kwa upande wa uthabiti
anaeleza kuwa ni hali ya utafiti kuweza kutoa matokeo yanayofanana au kuwiana
ikiwa utafiti utafanyika wakati mwingine, mahali pengine au na mtu mwingine.
Hivyo, mtafiti alizingatia uwazi wa malengo ya utafiti ili yaweze kueleweka kwa
urahisi kwa watafitiwa wake. Pia, mtafiti aliwafafanulia watafitiwa wake kuwa
taarifa watakazozitoa zitakuwa ni siri na zitatumika kwa malengo ya utafiti tu. Hii
ilisaidia watafitiwa kutoa taarifa sahihi kwa uhuru zaidi bila kuhofia. Vilevile, mtafiti
alitumia lugha nyepesi isiyoleta mkanganyiko pamoja na kueleza bayana mipaka ya
utafiti huu.
3.10 Changamoto Zilizojitokeza Wakati wa Utafiti na Utatuzi wake
Changamoto mbalimbali zilijitokeza wakati wa kuendesha zoezi la utafiti huu hasa
katika wakati wa kukusanya data. Baadhi ya changamoto hizo ziliweza kupatiwa
32
ufumbuzi na mtafiti na hatimaye kufanikisha zoezi hili. Changamoto hizo ni kama
vile:
Watafitiwa kusitasita kutoa ushirikiano wao moja kwa moja katika mahojiano na
baadhi yao kukataa kutoa taarifa. Changamoto hii ilitokana na mitazamo hasi ya
baadhi ya watafitiwa kwa sababu jamii haina uelewa wa kina kuhusu umuhimu wa
utafiti unaofanywa katika maeneo yao na kuogopa kwamba huenda kuna mambo
mengine tofauti yanafanywa na mtafiti. Hii ilitokana na ugeni wa mtafiti katika
mazingira yao. Changamoto hii ilitatuliwa baada ya mtafiti kuwafafanulia malengo
ya utafiti na kuwaeleza kuwa taarifa watakazozitoa zitabaki kuwa siri kati ya
mtafitiwa na mtafiti na zitatumika kwa malengo ya utafiti tu
Gharama za kuendesha shughuli za utafiti kuwa juu kuliko makadirio ya bajeti ya
utafiti. Hii ilitokana na ukweli kwamba, gharama hizo zilimhusu mtafiti mwenyewe
kwa kuwa hakuwa na udhamini wowote. Hivyo, kuna wakati ilimuwia vigumu
kusafiri kwenda kukusanya data kwa wakati hivyo alilazimika kusubiri mpaka hali
ya uchumi iwe sawa ndipo asafiri na hivyo ikasababisha kutokukusanya data kwa
wakati aliokusudia.
Kucheleweshwa kwa mchakato wa utoaji vibali vya kukusanya data kutoka katika
taasisi husika. Kuna wakati ambapo mtafiti alicheleweshwa kutokana na sababu za
kimfumo kutokuwa sawa hivyo kusubirishwa mpaka pale mfumo uliporekebishwa.
Tukio hilo lilichukua takribani majuma matatu ambayo hakuwa na budi kusubiria ili
kukamilisha taratibu za kupatiwa kibali cha kukusanya data.
3.11 Muhtasari wa Sura ya Tatu
Sura hii imefafanua kuhusu methodolojia ya utafiti na mchakato mzima uliofanywa
na mtafiti wakati wa kukusanya data. Sura imeelezea usanifu wa utafiti, mkabala wa
utafiti, eneo la utafiti, walengwa wa utafiti na ukusanyaji wa data. Aidha, njia na
zana za ukusanyaji wa data pamoja na mchakato wa ukusanyaji data zimefafanuliwa.
Vipengele vingine vilivyofafanuliwa ni uchanganuzi wa data, itikeli za utafiti, uhalali
na uthabiti wa matokeo ya utafiti. Pia, mtafiti amebainisha changamoto alizokutana
nazo wakati wa ukusanyaji wa data na namna zilivyotatuliwa. Sura inayofuata
inafafanua kuhusu mjadala wa matokeo ya utafiti.
33
SURA YA NNE
UWASILISHAJI NA MJADALAWAMATOKEO YA UTAFITI
4.1 Utangulizi
Sura hii inajadili matokeo ya utafiti uliolenga kuchunguza falsafa ya Kiafrika katika
semi: mifano kutoka vitendawili vya Kiswahili. Sura imewasilisha data za uwandani
na maktabani pamoja na kufanya mjadala wa matokeo ya utafiti. Uwasilishaji wa
matokeo hayo umegawanywa katika sehemu tatu kulingana na malengo ya utafiti.
Sehemu ya kwanza, inabainisha vijenzi vya falsafa ya Kiafrika katika muktadha wa
kitamaduni. Sehemu ya pili, inajadili namna falsafa ya Kiafrika inavyojitokeza katika
vitendawili vya Kiswahili na sehemu ya tatu ni tathmini ya athari ya falsafa ya
Kiafrika kwa jamii kama inavyosawiriwa katika vitendawili vya Kiswahili.
4.2 Vijenzi vya Falsafa ya Kiafrika katika Muktadha wa Kitamaduni
Sehemu hii inaonesha mjadala kuhusu vijenzi vinavyoijenga falsafa ya Kiafrika
katika muktadha wa kitamaduni. Kupitia mahojiano na watafitiwa, mijadala ya
vikundi lengwa na udurusu wa nyaraka, matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa,
falsafa ya Kiafrika hujengwa katika misingi ya kitamaduni. Utafiti ulibainisha kwa
kina baadhi ya mambo wanayoyafanya katika maisha yao ya kila siku ambayo
yanabeba au kuwakilisha utamaduni wao. Mambo hayo ndiyo huijenga falsafa ya
Kiafrika. Nayo ni:
4.2.1 Suala la Umoja na Ushirikiano
Umoja ni dhana inayorejelea hali ya kuunganika na kuwa wamoja katika jamii
(Mlelwa, 2017). Utafiti umebaini kuwa, Waafrika wanaishi kwa umoja na
ushirikiano katika taabu na raha. Faustine (2017) anaeleza kuwa suala la umoja na
ushikamano ni jambo linalotazamwa kwa namna ya pekee na Waafrika. Hii ni kwa
kuwa kwao, umoja ndio msingi wa kuimarisha na kudumisha mahusiano ya jamii
kuanzia katika familia, ukoo hadi jamii nzima. Anamnukuu Wiredu (1980)
anayeeleza kuwa, kwa jamii ya Waafrika, suala la umoja linaanzia katika ngazi za
familia, ukoo na hatimaye jamii nzima. Hivyo, wanaamini kuwa, hakuna jambo
linaweza kufanyika vizuri pasipo kushirikiana na wengine ndio maana wanafanya
kazi zao kwa umoja.
34
Kupitia mahojiano uwandani, utafiti umebaini kuwa, Waafrika wanaishi kwa
kushirikiana katika kufanya kazi pamoja, kula pamoja na kushirikiana katika kutatua
shida mbalimbali zinazowakumba wanajamii. Kwa mfano, Wanajamii wa wilaya ya
Bukoba ambao ni kiwakilishi cha jamii za Kiafrika huishi kwa kushirikiana katika
shughuli mbalimbali za kijamii. Watafitiwa walieleza baadhi ya mambo ambayo
huibua suala la umoja na ushirikiano kama vile sherehe mbalimbali zinazotokea
katika jamii na shughuli za kitanzia. Hili lilibainishwa na Bw. Rwiza1 anaposema:
Waswahili wana kawaida ya kushirikiana kwa hali na mali. Ikitokeatatizo lolote, jamii huchukulia tatizo hilo kama ni letu sote. Watuhupenda kufanya kazi kwa umoja na hivyo kunaonesha kuwa jamiiinatambua suala la umoja na ushirikiano kuwa ni nguzo ya kuletamaendeleo katika jamii. Kwa mfano watu wanashirikiana katikashughuli za kilimo, ufugaji, uvuvi na hata kusomesha watoto. Hii nikutokana na sababu kuwa ushirikiano unaanza katika ngazi ya familiahadi katika ukoo.
Maelezo katika nukuu hii yanaonesha kuwa wanajamii hufanya kazi kwa umoja,
jambo ambalo linaijenga falsafa ya Kiafrika ya umoja na ushirikiano. Hivyo jamii
inatambua kwamba, bila kuwa na umoja haiwezi kufikia kiwango kikubwa cha
maendeleo yanayotakiwa au kutimiza malengo waliyojiwekea kwa urahisi.
Aidha, mtafitiwa mwingine aliongeza kuwa, suala la kushirikiana katika shida na
raha kuwa si la hiari. Hii inaonesha dhahiri kuwa, kwa Waafrika mtu akipatwa na
msiba watu wote kama sehemu ya jamii hiyo ni lazima kuhudhuria msibani. Mawazo
haya yamefafanuliwa na Johansen2 anayesema:
Kama mwanakijiji ni lazima uende kwenye msiba haijalishi ni nduguau jirani. Watu wote, wake kwa waume, hutakiwa kuwa katika eneo lamsiba na kusaidiana kufanya kazi mbalimbali, kula na kulala hapokwa siku tatu. Mtu wa jamii yao akifiwa ndugu, jamaa, marafiki, nahata majirani huacha shughuli zao na kukusanyika sehemu ya tukiokwa lengo la kuwafariji wafiwa.
1 Bw. Boniface Rwiza ni Mstaafu katika Utumishi wa Umma, Mwalimu wa dini na mtumishi wakiroho wa Parokia ya Bikira Maria Mama Mwenye Heri Jimbo Kuu Katoliki la Bukoba. Mahojiano namtafiti yaliyofanyika tarehe 4.3.2020 kijiji cha Nyamkazi kata ya Kashai.2 Elvis Johansen ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Kashai iliyopomanispaa ya Bukoba kata ya Kashai. Majadiliano na mtafiti yalifanyika tarehe 25.2.2020 shuleni hapo.
35
Nukuu hiyo inathibitisha kuwa, katika misiba ndipo jamii ya Waswahili huonyesha
ushirikiano wa hali ya juu. Dhana hii imejengeka kutokana na kaida za maisha yao
ya kila siku zilizozoeleka katika kutatua matatizo yanayowakumba katika jamii yao.
Kupitia maelezo hayo, utafiti ulibaini kuwa, kwa kufanya hivyo, wanajenga na
kuhamasisha umoja na mshikamano katika jamii. Maelezo haya yanatupa picha halisi
ya namna Waafrika wanavyoishi kwa kushirikiana na kila jambo linalompata mtu
linachukuliwa kama ni jambo lao wote hivyo wanashirikiana katika kulitatua.
Hoja hii inatiwa nguvu na nadharia ya Kisosholojia kupitia msingi wake unaosema
kazi ya fasihi kama taswira ya kijiografia, kimazingira na kiutamaduni ambamo kazi
hiyo imechimbuka kutoka katika jamii husika. Kwa kuwa nadharia ya Kisosholojia
inasisitiza kuhusu kuchunguza matendo ya jamii na kila tendo linalofanyika katika
jamii za Waafrika linakuwa na maana halisi. Kwa hiyo, mambo mbalimbali
yanayotokea katika jamii yanachagiza suala la umoja na ushirikiano na hivyo kuibua
falsafa ya umoja na ushirikiano.
4.2.2 Suala la Maadili katika Jamii
Maadili ni mwenendo mwema, onyo au mafundisho yatolewayo kwa njia ya hadithi
au shairi na yenye nia ya kufundisha mafundisho mazuri (TUKI, 2004). Ni ukweli
usiopingika kuwa jamii yoyote isiyo kuwa na maadili mema ni mfu. Hii inatokana na
ukweli kwamba binadamu ni kiumbe ambaye huhitaji uhuru sana. Hivyo, iwapo
ataachwa afanye mambo kulingana na anavyotaka basi kuna uwezekano mkubwa wa
jamii kutoishi kwa amani. Ili kuwe na namna bora ya kuishi ndani ya jamii, sheria
mbalimbali hutungwa ambazo jamii husika hulazimika kuzifuata. Sheria hizo ndizo
zinaifanya jamii kuishi katika misingi ya maadili. Kaponda (2018) anaeleza kuwa ili
mwanadamu atambulike kuwa na utu sharti atende mambo yanayolingana na misingi
ya kimaadili ya jamii inayomhusu. Iwapo mwanajamii atatenda tofauti na misingi ya
jamii yake, moja kwa moja jamii itamtenga na kumbagua kwa kuwa hafanani na utu.
Matendo hayo ni kama vile; kutokushirikiana na wanajamii wengine katika masuala
muhimu ya kijamii, wizi, chuki, ukatili na mengine yanayofanana na haya.
Naye Chuachua (2016) anathibitisha kuwa, maadili na itikeli ni sehemu ya falsafa ya
Kibantu. Anaeleza kuwa wabantu wana uelewa wa kutosha kuhusu maadili na itikeli.
Maarifa yao kuhusu maadili na itikeli yanajiegemeza zaidi kwenye ontolojia yao.
36
Mtazamo wao ni kuwa hata kama maadili na itikeli vinasababishwa na kuongozwa
na kani uhai, unadhihirisha kuwa Mbantu anaona kuwa, maisha yake si mali yake
peke yake. Hii ni kutokana na kuwa, kuwapo kwake kunawezekana kwa kuwa
wengine wapo. Kwa hiyo, maisha yake yapo chini ya mamlaka ya Mungu, ambaye ni
chanzo cha kani-uhai. Na uhusianao wake na Mungu unadumishwa na wahenga na
wazee.
Aidha, kupitia mahojiano na watafitiwa, utafiti umebaini kwamba, suala la maadili
linaenda sambamba na utii, adabu na uvumilivu. Mtu asipokuwa na utii hawezi kuwa
na maadili mema. Watoto hufundishwa kutii wakubwa na hivyo kuwafanya wakue
katika maadili yanayofaa. Haya yamebainika pale Bi. Theresa3 anaposema:
Kila jamii inaishi kwa kuzingatia maadili ya jamii. Watoto hufunzwakutii na kuwaheshimu wakubwa wao. Suala la utii linawajengeawatoto kuwa na adabu mbele za wakubwa wao na hivyo inawajengeaunyenyekevu na kutokuwa na kiburi. Kwa namna hiyo, watoto haohukua katika misingi ya maadili mema yanayofaa katika jamii.
Maelezo ya mtafitiwa katika nukuu hapo juu yanathibitisha kuwa, wanajamii
hufanya mambo mbalimbali yanayohusu maadili ambayo kupitia hayo falsafa ya
maadili huibuliwa katika jamii. Mambo hayo ndiyo yanayoijenga falsafa ya maadili
katika jamii. Baadhi ya mambo hayo ni kama vile kuheshimu wakubwa, kutokuwa
na kiburi, kuvumilia katika mambo mbalimbali na kuwa na adabu mbele za wakubwa.
Aidha, watafitiwa walieleza kuwa, chanzo kikubwa cha mmomonyoko wa maadili
katika jamii ni kupata malezi duni, kuiga tabia na desturi zisizofaa, elimu duni na
mikumbo ya marafiki wabaya wasio na tabia nzuri.
Pia, hoja hii inatiwa nguvu na nadharia ya Kisosholojia inayojihusisha na uchunguzi
wa jamii mahsusi na kukieleza kile kinachopatikana katika jamii husika. Hii ni
kutokana na msingi kuwa, fasihi ni taswira ya kimazingira na kiutamaduni
inayochipuzwa kutoka katika jamii husika. Hivyo, Utafiti huu umebaini kuwa,
mambo mbalimbali yanayofanywa katika jamii kama vile kuheshimu wakubwa,
kuwa na adabu na utii na kuwa na uvumilivu ni baadhi ya vitu vinavyojenga suala la
3 Bi. Theresa ni mwanajamii, mzazi na mlezi wa watoto anayeishi wilaya ya Bukoba kata ya Bakoba,mtaa wa Buyekera. Mahojiano yalifanyika tarehe 5.3.2020
37
maadili katika jamii. Kutokuwa na vitu hivyo basi maaadili hayatakuwepo. Kwa
kufanya hivyo kunaibua falsafa ya umuhimu wa maadili kwa jamii za Kiafrika.
4.2.3 Suala la Uhai na Kifo
Kifo ni kipimo cha fursa ya kuwapo au kutokuwapo duniani (Chuachua, 2016).
Maneno haya yanamaanisha kuwa, kifo huondoa urazini na kumfanya mtu
kutokuonekana katika uso wa dunia baada ya kukata kwa pumzi ambayo huashiria
uhai wa mtu. Masuala yanayohusu uhai na kifo yameweza kubainika kupitia
matokeo ya utafiti huu. Mtafiti amebaini kwamba, maisha ya mwanadamu yapo
katika mambo mawili yaani uhai na kifo na suala la kifo linaogopwa na kila mtu
katika jamii. Suala hili linaibua imani kuwa mwanadamu huzaliwa, huishi na kisha
hufariki.
Kimsingi hakuna kiumbe hai ambacho huishi milele bila kufa. Temples (1959)
anaeleza kuwa, fikra za Waafrika zimetawaliwa na vitu viwili ambavyo ni uhai na
kifo. Kwa mawazo yake, Waafrika wanaamini kuwa mtu akiumwa nguvu za uhai
zinapungua hivyo anaamini atakufa. Naye Faustine (2017) anabainisha kuwa, suala
la uhai na kifo ni mambo yanayowashughulisha sana Waafrika. Wafrika wanaamini
kuwa kifo kipo na ni matokeo ya laana inayotokana na kupungua kwa nguvu-hai.
Wakati mwingine kifo kinahusishwa na imani za kichawi. Kupitia mjadala wa
vikundi lengwa na mahojiano, mtafiti amebaini kwamba, baadhi ya mambo
yanayojenga falsafa ya Kiafrika kuhusu kifo yanajitokeza katika mambo mbalimbali.
Mambo hayo ni kama vile kuwa na hofu juu ya kuumwa au kufa. Hili limebainika
katika mahojiano na Bw. Kigoye4 anapoeleza kuwa:
Kama ingekuwa inawezekana kwamba mtu anakiona kifo kablahakijamfika na kukimbia basi watu wangekuwa wanakimbia kifokisiwafikie. Hii ni kwa sababu kila mtu anapenda aendelee kuishi. Piamtu akiwa anaumwa anakuwa na huzuni na kukosa furaha kwasababu anaogopa asije akafa. Watu wanaokufa hatujui huwawanaenda wapi. Kwa hiyo, mtu akiumwa anaogopa itakuwaje kamaakifa, familia yake ataiacha vipi na hata mali alizozichuma ataziachapia.
4 Bw. Mwesigwa Kigoye ni mwanajamii na mtaalamu wa masuala ya mila za wahaya wilayaniBukoba. Mahojiano na mtafiti yaliyofanyika tarehe 4.3.2020 mtaa wa Hamgembe Nyangoye.
38
Mtafitiwa alipoulizwa na mtafiti kuwa, yawezekana watu wanaogopaa kufa kwa
kuhofia wanaowaacha au mali zao, mtafitiwa alionekana kutokuwa na uhakika sana
na jambo hilo. Maelezo yake yalithibitisha kuwa hofu yao juu ya kifo ni kwa sababu
wanapenda kuishi maisha marefu wakiwa na wapendwa wao. Hivyo, suala hili
linaijenga falsafa ya Kiafrika kuwa kuna kufa na kifo hakiepukiki kwa kila mtu.
Ni dhahiri kwamba, masuala yanayohusu kifo yanawashughulisha wanajamii wote.
Hata hivyo, kifo kinapotokea katika jamii taratibu fulani hufuatwa ikiwa ni pamoja
na suala la kuzika. Suala la mazishi ikiwa ni shughuli za kitanzia pia linaijenga
falsafa ya Waafrika ya uduara. Hii inatokana na sababu kuwa, watu wanapokuwa
katika msiba taratibu za mazishi hufanywa katika sura ya duara. Haya yalibainika
kupitia majadiliano pale Marwa5 alipoeleza kuwa:
Jamii ya watu wa Bukoba wanapofikwa na msiba hufanya taratibu zakuaga mwili wa marehemu kabla ya kuzika. Shughuli hiyo hufanywawakati jeneza la mwili wa marehemu likiwa limewekwa katikati nawatu wote hujipanga katika mzunguko unaotengeneza duarakulizunguka jeneza hilo na wengine kuendelea kupita kuaga mwilihuo.
Maelezo katika nukuu hiyo yanaonesha namna usimamaji wa kulizunguka jeneza
wakati wa kuzika unajenga falsafa ya uduara kama mojawapo ya falsafa ya Kiafrika.
Utafiti ulibaini kuwa, taratibu za kuaga zikikamilika suala la kuzika hufuatia ambalo
pia hufanyika katika sura ya duara kwa kulizunguka kaburi wakati shughuli za
kuzika zikiendelea. Kwa jumla, ushahidi uliopatikana katika mahojiano na
majadiliano ya vikundi umedhihirisha kwamba, suala la kifo linaogopwa sana na
wanajamii kwa kuamini kuwa kifo hakiepukiki kwa kila mtu. Hivyo, suala la uhai na
kifo linaibua imani kuhusu kifo na falsafa ya uduara.
4.2.4 Dhana ya Uduara
Uduara ni hali ya kitu au mambo kuwa au kufanyika katika sura ya duara au
mviringo (Duwe, 2016). Utafiti umebaini kuwa, dhana ya uduara kwa Waafrika ni
mojawapo ya msingi wa kuyaendesha maisha yao na kuutafakari ulimwengu. Maisha
ya Waafrika yametawaliwa na dhana ya uduara. Duwe (2016) anafafanua kuwa,
uduara ni moja ya mambo yanayodhihirisha kuwapo kwa falsafa ya Kiafrika kwa
5 Alexander Marwa ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kashai iliyopomanispaa ya Bukoba kata ya Kashai. Majadiliano na mtafiti yalifanyika tarehe 25.2.2020 shuleni hapo.
39
sababu katika maisha yao huthamini na kupenda vitu vilivyo katika sura ya duara.
Uduara ulianza sambamba na fasihi simulizi ya jamii ya Waafrika kwa sababu
katika maisha yao walishirikiana katika masuala mbalimbali kwa suara ya duara.
Aidha, Faustine (2017) anabainisha miktadha miwili ambayo kwayo dhana ya uduara
inajitokeza. Muktadha wa kwanza ni ule unaoiangalia dhana ya uduara kama namna
ya kutafsiri maarifa yanayopatikana ndani ya jamii na kuujengea maana ulimwengu
wao. Muktadha wa pili ni ule unaoitazama dhana ya uduara kama dhana ya kiujumi.
Akimnukuu Mbiti (2010) anaeleza kuwa:
Dhana ya uduara imekuwa ikitumika kama alama ya kuwakokusikokuwa na mwisho ambako kunaashiria mwendelezo wa jambo,kitu au maisha. Kwa Waafrika, mtazamo kuhusu dhana ya uduaraumekuwa ukijidhihirisha katika mambo mbalimbali kama vile namnawanavyoutazama wakati, ufanyaji wa matambiko, kazi zao za kisanaana utengenezaji wa vitu vya nyumbani.
Maelezo katika nukuu hiyo yanabainisha kuwa, kwa Waafrika dhana ya uduara
inajitokeza katika mambo mbalimbali. Hivyo, inathibitisha kuwa Waafrika
wanafanya vitu mbalimbali kwa uduara na kwa kufanya hivyo kunaibua falsafa ya
uduara. Aidha, katika muktadha wa kiujumi, uduara unatazamwa kama kigezo cha
kupima uzuri au ubaya wa kitu. Kuhusu hili, Faustine (k.h.j) anafafanua kuwa,
Waafrika wanaamini kuwa uzuri wa kitu umo katika hali ya uduara. Ndiyo maana,
kwa kiasi kikubwa, mazingira yao yametawaliwa na vitu vyenye asili ya uduara.
Kwa hiyo, katika duara ndimo unamopatikana uzuri.
Vilevile, kupitia mahojiano uwandani, watafitiwa walifafanua kuhusu vijenzi vya
falsafa ya Kiafrika ya uduara katika jamii kwa jumla. Imebainika kupitia mahojiano
hayo kuwa, watu wa wilaya ya Bukoba ambao ni kiwakilishi cha jamii za Kiafrika,
hufanya mambo mbalimbali kwa uduara. Mambo hayo ndiyo yanayoijenga falsafa ya
uduara. Mambo hayo ni pamoja na vitu wanavyovitengeneza kwa ajili ya matumizi
ya nyumbani kama vile vigoda, nyungo, mapambo yao ya ndani na samani. Aidha,
uduara unajitokeza katika mkao wa kula kwani wanapokula, huwa wamekaa kwa
40
kutengeneza mduara kuzunguka chakula ambacho huwa kimewekwa katikati yao.
Madai haya yanaelezwa na Bi. Kokwenda6 anayesema kuwa:
Mkao wa kula wa watu wa jamii ya Wahaya ni ule unaotengenezaumbo la duara. Iwe ni nyumbani au katika misiba watu wa jamii yaWahaya hupenda kula huku wakiwa wamekizunguka chakulaambacho hupakuliwa kwenye sinia au sahani kubwa kulingana nawatu watakaoshiriki katika kundi hilo. Chakula kikishapakuliwamboga huwekwa juu ya chakula katikati na hapo watu hukaakuzunguka chakula na kila mtu humega upande wake. Suala hililina maana kubwa kwa sababu lilianza zamani mpaka sasa badolinaendelezwa. Wazee wetu walilianzisha ili kuwafunza watotokuwa na umoja na kuacha tabia ya ubinafsi.”
Aidha, mtafitiwa mwingine ameshadadia hoja hii kwa kusema kwamba, mambo
mengi wanayoyafanya yanafanyika katika umbo la duara. Haya yamethibitika katika
majadiliano na watafitiwa pale Emilian7 anaposema:
Suala la uduara kwetu sisi ni la msingi sana. Katika jamii yetu hatatunapocheza ngoma zetu mara zote wachezaji hutengeneza duarakuwazunguka wale wanaopiga ngoma ambao wanakuwa katikati.Hapo ndipo ngoma hukolea na huchezwa huku wakizunguka. Pia,hata wakati wa mazishi, watu hulizunguka kaburi ili kuwa naushirikiano katika kuzika.
Kutokana na maelezo katika nukuu hizo ni ithibati kuwa, masuala haya yanayohusu
mkao wa kula, uchezaji ngoma na hata mazishi, hufanyika katika sura ya duara na
kuijenga falsafa ya uduara. Aidha, mawazo yanayofanana na haya yameelezwa na
Temples (1957) anayesema kuwa, maisha ya Waafrika yametawaliwa na dhana ya
uzuri unaopatikana katika sura ya duara. Falsafa ya uduara pia, inadhihirika kupitia
vitu mbalimbali wanavyovitumia katika shughuli zao za kila siku. Vitu kama vile
vigoda, viti, meza, ungo na sinia vina maumbo ya duara. Kwa hiyo, kitendo cha
kukaa pamoja na kushirikiana kula katika sahani moja kwa kukizunguka chakula
kilichowekwa katikati kunaijenga falsafa ya uduara
6 Bi. Olivia Kokwenda ni mwanajamii na mwalimu wa dini anayefundisha watoto katika Kigango chaBuyekera Jimbo kuu Katoliki la Bukoba. Mahojiano na mtafiti yalifanyika tarehe 3.3.2020 mtaa waBuyekera kata ya Bakoba.7 Frank Emilian ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Kashai iliyopo manispaaya Bukoba kata ya Kashai. Majadiliano na mtafiti yalifanyika tarehe 25.2.2020 shuleni hapo.
41
4.2.5 Suala la Imani katika Mungu na Mizimu
Tafsiri ya Ki-biblia ya imani inapatikana katika Waebrania11.1. Mtume Paulo
anasema , “imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo
yasiyoonekana.” Kwa hiyo, imani ni jambo ambalo haliwezi kuthibitika kisayansi.
Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwa, Waafrika wanaamini katika nguvu
zinazotokana na Mungu na mizimu. Mbiti (1969) anabainisha kuwa, Waafrika
walikuwa na wanayo dini ambayo wameirithi kutoka katika vizazi vilivyotangulia.
Chuachua (2016) anafafanua mawazo ya Idowu (1966) ambaye anamtaja Lang
akibainisha dhana ya umosi katika imani ya Waafrika kwa kusema, “African
Traditional Religion is a monotheistic religion in which God is believed to be
Eternal” (uk 92). Hapa ana maana kwamba, dini ya kiasili ya Mwafrika inaamini
katika umosi ambapo Mungu anaaminika kuwa ni wa milele. Mawazo haya
yanaonesha kuwa, Waafrika wanaamini kuna nguvu yenye uwezo mkubwa kuliko
nguvu zote; na kwamba nguvu hiyo ni moja na ambayo husababisha kuwapo kwa
kila kitu. Chuachua (2016) anafafanua kuwa nguvu hiyo ni Mungu ambaye ni
ukamilisho wa ubinadamu; na kuwapo kwa mtu kunawezeshwa na Mungu ambaye ni
muumba wa roho na ulimwengu. Mungu ndiye anayetawala huombwa na
kukumbukwa na wanadamu katika shida na raha. Pia, Temples (1959) anatueleza
kuwa:
The Bantu speak of God himself as “the stong one,” he who possessesforce in himself. He is also the source of the source of every creature.(uk. 22)
Wabantu wanamwongelea Mungu kama “mwenye nguvu,” yeyeanayemiliki kani ndani yake. Pia Mungu ni chanzo cha kani kwa kilakiumbe (Tafsiri ya mtafiti).
Maelezo ya mtaalamu huyu yanathibitisha kuwa, Mungu ndiye mwenye nguvu
kuliko kitu kingine na ni chanzo cha kani kwa viumbe wengine. Maelezo haya
yanatupatia dhana kuwa Mungu ndiye mkuu kuliko viumbe wengine.
Kupitia mahojiano uwandani, utafiti umebaini kuwa, watu wengi wa jamii ya
Waafrika ni waabudu au wacha Mungu. Hii ni kutokana na sababu kuwa wanaamini
yupo Mungu au Allah mmoja tu mwenye nguvu na awezaye kutatua matatizo
mbalimbali yanayowakumba wanadamu. Haya yalithibitika kutokana na uwepo wa
42
madhehebu mbalimbali katika jamii ya watu waishio wilaya ya Bukoba. Watafitiwa
walieleza kuwa, katika jamii hiyo siku za ibada watu hukusanyika katika makanisa
yao na misikitini kwa lengo la kuabudu Mungu. Kwa hiyo, imani ya Waafrika
imejengwa katika misingi miwili ambayo ni Mungu au Allah na mizimu. Katika
kuthibitisha hili, Bi. Abdallah8 anaeleza kuwa:
Jamii ya watu waishio Bukoba ina mchanganyiko wa dini namadhehebu mbalimbali. Wote wanamwamini na kumwabudu Mungummoja lakini tofauti ni za kimatazamo. Kuna wanaosali Jumamosi(wasabato) na makanisa mengi ya Jumapili. Mifano kuna makanisa yaKKKT, Roman Catholic, Anglican, Pentekoste (PAG), TanzaniaAssembles of God (TAG), Kanisa la Wokovu, na makanisa yamaombezi. Kwa upande wa Waislamu pia si haba kutokana na wingiwa misikiti katika kila kata na vijiji. Kama ilivyo kwa waamini wakidini wapatapo matatizo huenda mbele za Mungu au Allah nakumuomba ili aweze kuwatatulia matatizo yao hivyo hivyo pia kwaupande wa waamini wa miungu nao wapatapo matatizo huenda kwawaganga wa kienyeji kuomba mizimu ya mababu na mabibi zao.
Maelezo katika nukuu hapo juu yanathibitisha kuwa, Waafrika wanaamini Mungu na
mizimu. Wapo wanaoamini kuwa, tatizo likitokea katika jamii na likashindikana
kupatiwa majibu basi hupelekwa kwa wataalamu ambako huko hutatuliwa kwa
nguvu za mizimu ya mababu na mabibi zao. Kwa hiyo, kitendo cha kwenda kuabudu
katika makanisa na misikitini pamoja na kwenda kwa waganga wa kienyeji katika
vilingeni kunaijenga falsafa ya Kiafrika ya imani katika Mungu na mizimu. Hii ni
kwa kuamini kuwa, watu hao ndio wenye uwezo wa kutatua matatizo mbalimbali
yanayotokea katika jamii.
Kwa kuhitimisha hoja hii, tunaweza kusema kuwa, ni dhahiri kuwa watu wa jamii za
Waafrika imani yao imekitwa katika masuala ya Mungu na mizimu. Hii inajenga
falsafa ya imani katika Mungu au mizimu na kuwa Mungu ndiye mwenye uweza
wote. Mambo haya kwa jumla yanaijenga falsafa ya Kiafrika katika muktadha wa
kiutamaduni. Hii inatokanna na nadharia ya Kisosholojia inayoona kuwa, kazi ya
fasihi kama taswira ya kijiografia, kiutamaduni na kimazingira ambayo imechimbuka
8 Bi Farida Abdallah ni mwanajamii na mwalimu mstaafu wa Shule ya Qudus Nursery and PrimarySchool iliyopo manispaa ya Bukoba. Mahojiano na mtafiti yaliyofanyika tarehe 4.3.2020 mtaa waNational housing- Kashai.
43
kutoka katika jami husika. Kwa hiyo, inaweka mkazo wa fasihi kuendana na
miktadha ya jamii husika kijiografia na kiutamaduni.
4.2.6 Suala la Uchawi na Ushirikina
Chuachua (2016: 248) anaufasili uchawi kuwa, ni dhana ya kimetafizikia9 na wakati
mwingine kiontolojia10 kwa kuwa inafungamana na kuwapo kwa mtu. Nguvu za
kichawi ni kani zinazoweza kuleta athari kutoka kwa mchawi hadi kwa
aliyekusudiwa akiwa umbali wowote ule. Masuala yanayohusu uchawi yamekuwa
yakijitokeza katika kila jamii kwa Waafrika. Mtazamo kuhusu kuwapo kwa uchawi
katika jamii za Kiafrika umekuwa ukijidhihirisha katika maisha yao ya kila siku
kupitia tanzu mbalimbali za fasihi. Faustine (2017) anaeleza kuwa, Waafrika
wanaamini mchawi huweza kusabaisha kifo cha mtu katika hali ya kimiujiza pasipo
yeye kugundulika ni kwa namna gani amefanya jambo hilo. Jambo baya linapotokea
kama vile kifo, kushuka kwa mtu kiuchumi, na hali mbaya ya kimaisha mara nyingi
ni vigumu kwa wanajamii kuamini kuwa limetokana na sababu mbalimbali kama vile
za kimazingira, bali hulihusisha na imani za kichawi. Akimnukuu Mbiti (2010)
anasema:
It is believed too, that a witch can cause harm by looking ata a personor speaking to him words intended to inflict harm on him. All theseare the ways in which evil magic and witchcraft are believed tofunction. In some cases it is even held that powerful magic can make aperson change into ana animal or bird which then goes to attack thevictim (uk 167).
Inasadikika pia kwamba mchawi ana uwezo wa kumdhuru mtu kwakumwangalia au kumnenea maneno yatakayomdhuru. Hizi ndizo njiaambazo uchawi unaaminika kufanya kazi. Katika mazingira mengine,inasadikiwa pia kwamba, nguvu za kimiujiza zinaweza kumbadilishamtu akawa mnyama au ndege ambaye huenda kumdhuru mtumwingine (tafsiri ya mtafiti).
Maelezo yaliyo katika nukuu hapo juu yanathibitisha uwepo wa uchawi katika jamii
za Kiafrika na athari za uchawi kama vile kusababisha vifo na kuwadhuru watu
9Metafizikia ni tawi la falsafa linalotumika kutafakari kuhusu mambo na matukio ya kiulimwengu ilikuyabainisha na kuyatofautisha yale halisi na yasiyokuwa halisi (Chuachua, 2016)10 Ontolojia ni taaluma ya falsafa inayoshughulikia asili ya kuwapo au kuishi. Pia hushughulikiakategoria za kuwapo pamoja na mahusiano yake (Chuachua, 2016)
44
wengine. Aidha, mawazo yanayofanana na haya yanaelezwa na Manala (2004)
anayesema:
In the African’s world of thought, when ill-health, misfortune,accident or death occuers, traditional Africans will immeadiatelyprobe witch crafts as the likely cause (uk. 1501).
Katika mtazamo wa Waafrika, ikitokea vitu kama magonjwa, bahatimbaya, ajali au kifo, Waafrika kwa haraka watamwona mchawi kuwandiye aliyesababisha (Tafsiri ya mtafiti).
Aidha, kupitia mahojiano na watafitiwa, utafiti huu umebaini kuwa, jamii ya watu wa
Bukoba inaamini kuwa uchawi upo na wachawi wapo ingawa ni kwa kiasi kidogo.
Hii ni kutokana na sababu kuwa baada ya kuingia kwa dini mbalimbali watu wengi
waliacha shughuli za kichawi na kuanza kumwabudu Mungu. Pia, ilielezwa kuwa
wachawi kwa sasa hawaogopwi na hawana nguvu ya kudhuru watu kama ilivyokuwa
zamani. Akieleza kuhusu suala hili Bw. Jonas11 anasema:
Katika masuala ya dini watu wameitikia sana ndio maana imetusaidiakatika kufanya njama za kuwahujumu wachawi. Uchawi katika jamiiyetu upo lakini umefifishwa sana na dini kutokana na sababu kuwawatu wengi wanasali sana wachawi wamekuwa hawana nguvu zakudhuru watu kama ilivyokuwa zamani.
Kupitia nukuu hiyo, tunapata ushahidi kuwa, suala la uchawi katika jamii za
Waafrika bado lipo japo kwa sasa wachawi wamepungua kwa kiasi kikubwa. Hata
hivyo, suala la uchawi linashabihiana na suala la uganga ambapo baadhi ya
wanajamii wanaamini kuwa mchawi ni mtu anayeloga na mtu aliyelogwa anatibiwa
na mganga (Samwel, 2015). Naye Chuachua (2016) anafafanua zaidi kuwa, mganga
ndiye anayeweza kutibu uchawi. Uganga na uchawi ni mambo yanayokwenda
pamoja. Mchawi kazi yake ni kuharibu na akiharibu hawezi kutengeneza. Mganga ni
mjuzi zaidi ya mchawi. Mganga anaweza kuutoa uchawi. Aidha, data za uwandani
kupitia mahojiano zinathibitisha jambo hili pale Bi. Kayanga12 anaposema:
11 Bw. Philbert Jonas ni mwanajamii na mtumishi wa kiroho katika Taasisi ya Adolph KolpingSocieties of Tanzania Jimbo Kuu la Katoliki Bukoba. Mahojiano na mtafiti yalifanyika tarehe2.3.2020 mtaa wa Kamizilente- Rwamishenye.12 Bi. Salma Kayanga ni mama wa familia na Afisa Afya ofisi ya Kata Kibeta. Mahojiano na mtafitiyalifanyika tarehe 5.3.2020 ofisini kwake.
45
Kila familia inapitia changamoto mbalimbali ambazo zinawezakushindwa kupatiwa majibu. Kwa mfano mtu akiumwa muda mrefuna ikashindikana kupona kwa tiba za kitabibu watu hufikiria kuwahuenda mtu huyo amelogwa na hivyo hutafutwa mganga wa kienyeji(mtaalamu) ili aweze kumtibia. (Tafsiri ya msisitizo kwenye mabanoni ya mtafiti).
Maelezo yaliyo katika nukuu hiyo yanathibitisha namna ambavyo Waafrika
wanaamini katika masuala yanayohusu uchawi. Pia mtu aliyelogwa na mchawi
anaweza kupona kwa kupatiwa tiba na mganga wa kienyeji.
Aidha, tunaishadadia hoja hii kwa kutumia nadharia ya Kisosholojia kupitia msingi
wake unaosema kazi ya fasihi kama taswira ya kijiografia, kimazingira na
kiutamaduni ambamo kazi hiyo imechimbuka kutoka katika jamii husika. Msingi huu
unahusiana moja kwa moja na lengo letu kwani kipengele hiki kimejikita katika
kubainisha vijenzi vya falsafa ya Kiafrika katika muktadha wa utamaduni wa jamii
za Kiafrika ambavyo vimetokana na fasihi ya Waafrika. Katika kuhitimisha
kipengele hiki kwa jumla tunaweza kusema kuwa, mambo yanayohusu uchawi kama
vile kubadilisha maumbo ya mtu kuwa mnyama au ndege na kuloga ndiyo
yanaijenga falsafa ya Kiafrika ya “uchawi na ushirikina”.
4.2.7 Dhana ya Ndoa na Uzazi
Dhana ya uzazi kwa Mwafrika kama inavyoelezwa na Faustine (2017) imekitwa
katika mambo makuu manne. Jambo la kwanza Waafrika wanautazama uzazi kama
njia ya kuwapo kwa mtu. Pili, uzazi unatazamwa kama njia pekee ya kuviunganisha
vizazi vilivyopo na visivyokuwapo. Tatu, uzazi hutazamwa kama kigezo muhimu
kinachoashiria uimara wa ndoa. Nne, uzazi unatazamwa kama nyenzo ya ujenzi wa
ukoo wenye nguvu, heshima na thamani. Kitendo cha mke au mume kuwa na watoto
kinatazamwa kama njia pekee ya kuukuza na kuuendeleza ukoo. Mlelwa (2017)
anabainisha mawazo kuwa, ndoa ni jambo la msingi sana na ni jambo la heshima
kwa Waafrika. Hii ni kutokana na sababu kuwa wanaamini kuwa kupitia ndoa
familia inaweza kujengwa na hivyo kupanua ukoo. Jambo hili linabainika pale
anaposema:
Ufahari wa Waafrika unatokana na kuoa au kuolewa. Mtu anapokuwahajaoa au kuolewa anaonekana kuwa ana upungufu fulani katika
46
maumbile yake. Lakini ufahari huo huongezeka pale mtu anapozaawatoto.
Maelezo yanayotolewa na mtaalamu huyu yanabainisha wazi kuwa, kwa Waafrika
suala la ndoa na uzazi linapewa heshima na ni jambo la ufahari. Pia, suala la ndoa
linaenda sambamba na kuzaa kwa mwanamke ambapo mwanamke anayeolewa na
asizae haonekani kuwa na thamani sawa na yule anayezaa. Mawazo haya
yanashabihiana na yale ya Faustine (2017) anayeeleza kuwa, furaha ya ndoa
inakamilishwa na uwezo wa wanandoa hao kupata watoto. Wanandoa wasiobahatika
kupata watoto hawathaminiwi katika jamii na mara nyingi ndoa zao hazidumu.
Mimba ni kiashiria cha uimara wa ndoa. Akimnukuu mbiti (2011) anasema kuwa:
In some African societies, marriage is not fully recognized until thewife has given birth. First pregnant becomes, therefore, the final sealof marriage, the sign of complete intergration of the woman into herhusband’s family and kinship circle (uk 110).
Katika baadhi ya jamii za Waafrika, ndoa haitambuliki kikamilifumpaka pale mke anapopata mtoto. Ujauzito wa kwanza, kwa hiyo,ndiyo kihalalisho cha mwisho cha ndoa, ishara ya kuingizwakikamilifu kwa mwanamke katika familia ya mumewe na jamii yaukoo wake (Tafsiri ya mtafiti).
Maelezo ya mtaalamu huyo yanadhihirisha kuhusu umuhimu wa watoto katika
familia za Waafrika. Aidha, kupitia data za uwandani, utafiti ulibaini kuwa, ndoa ni
kipengele muhimu katika kujenga familia na hivyo hujenga falsafa ya umuhimu wa
uzazi na ulezi ambayo inajidhihirisha kupitia suala la ndoa na mahusiano. Jambo hilo
lilithibitika pale Bi. Mnyambo13 anaposema kuwa:
Kwa upande wa binti anapoolewa hutolewa posa na kulipiwa mahari.Kisha hufanyiwa sherehe ya kuagwa mjubulo14 (kapu la mama) nahatimaye sherehe ya harusi. Sherehe za mjubulo huandaliwa nawanawake na huhusisha wanawake katika kumfunda binti anayeolewanamna ya kwenda kuishi na mume na kukabiliana na changamoto zandoa. Pindi mwanamke huyo anapoenda ukweni anatarajiwa kumzalia
13 Bi. Schola Mnyambo ni mwanajamii, mama wa familia na mjasiriamali mdogo wa wilaya yaBukoba. Mahojiano kati yake na mtafiti yalifanyika tarehe 6.3.2020 mtaa wa Kamagera- Kibeta.
14 Mjubulo ni sherehe za kumuaga binti anapoolewa. Maelezo yaliyotolewa katika mahojiano namtafitiwa 6.3.2020.
47
mwanamme watoto. Mwanamke anayezaa hupendwa sana na wakwezake ukilinganisha na yule asiyezaa. Katika jamii mwanamkealiyeolewa na asizae hudharauliwa na hata kusemwa na ndugu wamwanaume kuwa hajailetea faida familia yao kwa sababu hajazaa(Tafsiri katika mabano ni ya mtafiti).
Maelezo katika nukuu hiyo hapo juu yanathibitisha namna ilivyo muhimu kwa
Waafrika kuhusun kuzaa watoto kama kiashiria cha ukamilifu wa ndoa za Waafrika.
Kwa kuzingatia msingi ya nadharia ya Kisosholojia unaosisitiza kuwa fasihi ni kama
taswira ya kijiografia, kiutamaduni na kimazingira ambayo imechimbuka kutoka
katika jamii husika ina maana kuwa fasihi ina akisi kile kinachotendeka katika jamii
katika nyanja mbalimbali. Hivyo, matokeo ua utafiti huu yamebainisha kuwa,
masuala yahusuyo ndoa na mahusiano yamekuwa yakipewa kipaumbele na umuhimu
mkubwa kwa jamii za Kiafrika na ndio maana tukio lenyewe la harusi na mijubulo
hufanywa kwa shamra shamra nyingi. Kwa Waafrika ni suala la heshima kwa mtoto
kuoa au kuolewa kwa hivyo masuala hayo hupewa uzito kwa kiasi fulani.
Kwa hiyo, masuala yahusuyo ndoa kama kijenzi cha falsafa ya Kiafrika ya uzazi na
ulezi huonekana kuwa na umuhimu kwa Waafrika. Jambo hili linatokana na sababu
kuwa, kwa Waafrika ndoa ni suala la muhimu na sehemu ya kumtoa mtu katika utoto
kuingia utu uzima. Hii inathibitika katika jamii ambapo mtu asiyeolewa au kuoa
haheshimiwi katika sawa na mtu aliyeoa au kuolewa. Na pia mtu asiye na uwezo wa
kupata watoto haheshimiwi kama yule anayezaa. Hivyo kupitia maelezo hayo
tunaweza kusema kuwa, ndoa na familia kwa Waafrika ni mojawapo ya jambo
linaloijenga falsafa ya Waafrika kuhusu umuhimu wa uzazi na ulezi.
4.3 Falsafa ya Kiafrika katika Vitendawili vya Kiswahili
Ni dhahiri kuwa falsafa ya Kiafrika imekuwa ikisawiriwa katika tanzu mbalimbali za
fasihi simulizi ya Kiafrika. Kama nadharia ya Kisosholojia inavyosisitiza kuwa,
fasihi haiwezi kujitenga na jamii ambayo kwayo imechipuzwa. Hivyo, mambo
mbalimbali yanayojitokeza katika jamii husawiriwa ndani yake. Hii ina maana kuwa,
fasihi inasawiri matendo ya jamii na kuonesha uhalisia wake kwa jamii. Utafiti huu
umebaini falsafa mbalimbali zinazojitokeza katika vitendawili vya Kiswahili.
Sehemu hii inajadili kwa kina namna falsafa ya Kiafrika inavyojitokeza katika
vitendawili vya Kiswahili. Miongoni mwa falsafa zinazosawiriwa katika vitendawili
vya Kiswahili ni kama zifuatazo:
48
4.3.1 Falsafa ya Umoja na Ushirikiano
Suala la umoja na ushirikiano ni miongoni mwa mambo yanayozingatiwa katika
jamii za Waafrika. Utafiti huu umebaini kuwa, Waafrika wanaamini kuwa umoja na
ushirikiano ni nguzo katika kufanikisha shughuli mbalimbali. Wanaamini kuwa
hakuna jambo linaweza kufanyika vizuri pasipo kushirikiana na wengine. Mitazamo
yao imekitwa katika imani kuwa, ushirikiano unajenga undugu na katika umoja
hakuna ubinafsi. Kwa hiyo, ushirikiano ndiyo nguzo ya kuimarisha mahusiano
kuanzia katika ngazi ya kifamilia hadi kwa jamii nzima kwa jumla. Kwa mfano suala
la umoja na mshikamano linadhihirika pia kupitia vitendawili mbalimbali vya
Kiswahili. Katika mjadala wa vikundi lengwa, Godifrey15 alitega kitendawili
ambacho kinasawiri suala la umoja na mshikamano. Nacho kinasema:
a) Kitendawili: Huyu kambeba huyu na huyu kambeba huyu, huyu kambeba
huyu na huyu kambeba huyu.
Jibu: Ardhi imebeba maji, maji yamebeba meli na meli imebeba watu.
(Chanzo: Uwandani katika mjadala wa vikundi).
Katika kitendawili hiki tumebaini uwepo wa falsafa ya Kiafrika ya umoja na
mshikamano. Falsafa hii inasisitiza suala la umoja na kutegemeana. Kupitia
kitendawili hiki jamii inapata funzo la namna umoja na mshikamano unavyoweza
kufanikisha mambo mbalimbali. Ushirikiano huo utarahisisha kazi hivyo kufikia
mafanikio yaliyokusudiwa kwa muda mfupi. Katika falsafa iliyotumika katika
kitendawili hiki tunaona mnyororo wa utendaji kazi kwa kushirikiana toka upande
mmoja kwenda upande mwingine. Mawazo haya yanabainishwa na baadhi ya
watafitiwa waliotoa mitazamo yao kuhusu umuhimu wa umoja na mshikamano kama
inavyojitokeza katika kitendawili hapo juu. Kwa mfano Bw. Kazaula16 akifafanua
kuhusu kitendawili hiki anasema:
Kutokana na hali ya umaskini tulionao, umoja unaonekana kamanguzo ya kutatua matatizo mbalimbali yanayowakumba wanajamii.Watu wanalazimika kushirikiana katika matatizo mbalimbali ili
15 Belina Godfrey ni mwanafunzi wa shule ya msingi Katerero iliyopo halmashauri ya wilaya yaBukoba kata ya Kyeitema. Majadiliano kati ya mtafiti na watafitiwa yalifanyika tarehe 26.2.2020shuleni hapo.16 Bw. Abel Kazaula ni Afisa Utamaduni wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba. Mahojiano na mtafitiyalifanyika tarehe 2.3.2020 katika ofisi za Halmashauri zilizopo Bukoba vijijini kata ya Kemondo.
49
kufanya wepesi wa kutatua matatizo hayo. Wenyeji wa wilaya yaBukoba ni wakulima, wavuvi na wafugaji. Hivyo katika kufanyashughuli hizo za maendeleo hufanya kwa pamoja na kwa umoja.Ndiyo maana kitendawili hicho kimebeba dhana ya kubebana kwamaana ya kusaidiana. Kwa kufanya hivyo inarahisisha kumaliza kazikubwa kwa muda mfupi.
Maelezo katika nukuu hapo juu yanathibitisha kuwa, suala la umoja na ushirikiano
kama linavyojitokeza katika kitendawili hicho, ni nyenzo katika kutatua matatizo
mbalimbali. Aidha, inasaidia katika kufanikisha jambo ambalo yawezekana
lisingewezekana pasipo ushirikiano. Hii inadhihirisha kuwa mtazamo wa Waafrika
kuhusu ushirikiano umejikita katika imani kuwa jamii inaposhirikiana huondoa
madhaifu ya upande mwingine hivyo kufikia mafanikio kwa haraka. Kitendawili
kingine kinachosawiri falsafa ya umoja na ushirikiano kinasema:
b) Kitendawili: Hufanya kazi daima wakiwa watatu.
Jibu: Mafiga.
(Chanzo: Salla, 2014).
Kitendawili hapo juu kinadhihirisha falsafa ya Kiafrika juu ya umoja na ushirikiano
ndani ya jamii. Akifafanua kuhusu kitendawili hiki, Bw. Rwiza17 (k.h.j) katika
mahojiano alieleza kuwa, “Waafrika wanaamini kuwa mtu hawezi kukamilika akiwa
peke yake bali ukamilifu wake unategemea uwepo wa watu wengine ndio maana
kitendawili hiki kinasema hufanya kazi wakiwa watatu”. Ufafanuzi wa mtaalamu
huyu unatubainishia kuwa, mitazamo ya Waafrika kuhusu falsafa hii imekitwa katika
imani kuwa, ushirikiano ndiyo chachu ya kuyafikia maendeleo yanayotakiwa katika
jamii kwa haraka. Pia, mtafitiwa mwingine akisisitiza kuhusu umuhimu wa
ushirikiano kama unavyojitokeza katika kitendawili hapo juu, Bw. Katabazi18 katika
mahojiano anasema:
Kazi yoyote ndani ya jamii kama kilimo, sherehe na zinginezikifanywa kwa ushirikiano mafanikio yake ni makubwa. Hivyo,falsafa ya umoja na ushirikiano ndani ya jamii hufuatwa kwa kiasikikubwa ili kurahisisha utendaji kazi. Hii ndiyo sababu mfano wakitendawili hicho kinaonesha watu hao hufanya kazi wakiwa watatu.
17 Amekwishatajwa hapo awali.18 Bw. Jualikali Katabazi ni mwanajamii wa wilaya ya Bukoba anayeishi mtaa wa Buyekera kata yaBakoba. Mahojiano na mtafiti yalifanyika tarehe 3.3.2020 nyumbani kwake.
50
Ufafanuzi wa hoja hii katika nukuu hapo juu unaonesha kuwa, jamii za Kiafrika
huishi kwa kushirikiana katika mambo mbalimbali na katika shughuli za uzalishaji
mali. Falsafa ya umoja na ushirikiano inaendelea kujitokeza katika kitendawili
kifuatacho:
c) Kitendawili: Kaa huku tukae kule tulenge mawe pangoni.
Jibu: Kula matonge ya ugali.
(Chanzo: Badru, 2015).
Utafiti huu umebaini kuwa, kitendawili hiki kinasawiri suala la umoja katika kufanya
jambo. Dhana ya umoja inayobebwa katika kitendawili hiki inaonesha uwepo wa
watu wawili au zaidi wanaotoa ushirikiano katika kufanya jambo fulani na hivyo,
kuibua falsafa ya umoja na ushirikiano. Bi. Kokwenda19 anashadadia jambo hili
kama linavyojitokeza katika kitendawili hiki kwa kusema kuwa, “mkao wa kula wa
watu waishio Bukoba ni ule unaotengeneza duara. Hii ni kwa sababu watu
wanapokula huwa wamekaa katika uduara kuzunguka chakula kinachowekwa
katikati”. Katika uduara huo ndipo wanaweza kufahamishana na kujadiliana kuhusu
mambo mbalimbali yanayotokea na kuyapatia ufumbuzi. Mtazamo huu unatokana na
imani za Waafrika katika ushirikiano kuwa ndiyo msingi wa mafanikio katika jamii.
Hivyo, wanashirikiana katika kufanya mambo mbalimbali kwa pamoja na kula kwa
pamoja. Aidha, falsafa ya umoja na ushirikiano inajidhihirisha kupitia kitendawili
kingine kinachosema:
d) Kitendawili: Adui tumemzingira lakini hatumuwezi.
Jibu: Kuota moto.
(Chanzo: Salla, 2014).
Licha ya kitendawili hiki kuonesha kuwa hawamuwezi adui huyo bado kinasawiri
suala la umoja ambao unaonekana kuwa ni nguzo katika kukabiliana na adui.
Ilibainika kuwa, maana ya kitendawili hiki inaonesha ushirikiano wa watu hao katika
kumzingira adui huyo kwani Waafrika husaidiana katika shida na raha. Hii ni kwa
sababu watu wanapoota moto huwa wameuzunguka moto katikati na kutengeneza
duara. Uduara ndio kitovu cha umoja wao. Kwa Waafrika, suala la kushirikiana
linatazamwa kama nguzo ya kuwawezesha kukabiliana na matatizo mbalimbali
wanayokumbana nayo. Mtu mmoja pekee hawezi kutatua matatizo yake, bali
19 Amekwishatajwa hapo awali.
51
anategemea uwepo wa watu wengine. Ndiyo maana kitendawili hiki kinasawiri
namna watu hao walivyomzingira adui yao. Kwa namna hii tunaona mtazamo wa
Waafrika kuhusu falsafa hii umejikita katika imani kuwa, mtu mmoja hawezi
kukamilika katika kupambana na tatizo linalompata bali kwa kushirikiana na
wengine ndipo wanaweza kufanikiwa. Pia, falsafa ya umoja imedhihirika katika
kitendawili kinachosema:
e) Kitendawili: Nina bibi watatu, akiondoka mmoja wawili hawafanyi kazi.
Jibu: Mafiga.
(Chanzo: Salla, 2014).
Vilevile, utafiti umebaini kwamba, kitendawili hapo juu kinaibua suala la umoja na
ushirikiano. Maana ya kitendawili hiki imebeba dhana ya ushirikiano. Hii inatokana
na sababu kuwa katika jamii ambazo hutumia mafiga kupika, ni dhahiri kuwa,
huwezi kufanikisha zoezi la kupika kama figa moja litaondolewa. Hii inaonesha
kuwa, bibi hawa watatu wanafanya kazi kwa pamoja na umoja na kila mmoja ana
nafasi kwa mwingine. Mmoja akitoka wawili wanaobaki hawawezi kufanya kazi
mpaka mwingine huyu wa tatu arudi. Akifafanua kuhusu falsafa hii kama
inavyojitokeza katika kitendawili hapo juu, Rhenus20 katika mjadala anadhihirisha
mawazo haya anaposema:
Katika maisha ya kila siku ya Waafrika wana kawaida ya kushirikianakatika masuala mbalimbali. Waafrika wanaamini kuwa kila mtu ananafasi yake kwa mwingine, hivyo, huishi kwa kutegemeana katikamambo mbalimbali. Jambo hili linadhihirika katika tanzu mbalimbaliambazo zinasawiri mawazo na utendaji wa Waafrika. Ni katika tanzuhizo kama vile vitendawili ambapo Waafrika huonya, hukosoa nahuifunza jamii yao.
Maelezo katika nukuu hapo juu yanathibitisha suala la kutegemeana kwa Waafrika
katika kufanya kazi mbalimbali. Hivyo, kufanya kazi kwa umoja kunasaidia kuleta
mafanikio kwa sababu umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
20Amina Rhenus ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Kashai iliyopo manispaaya Bukoba kata ya Kashai. Majadiliano kati ya mtafiti na watafitiwa yalifanyika tarehe 25.2. 2020shuleni hapo.
52
Kwa hiyo, kitendawili hiki kinasawiri falsafa inayosisitiza umuhimu wa ushirikiano
miongoni mwa wanajamii kwa kufanya mambo kwa kutegemeana. Jambo hili
linadhihirika katika maisha ya kila siku ya Waafrika kwani wanaamini kuwa kila mtu
ana nafasi yake kwa mwingine, hivyo, huishi kwa kutegemeana katika mambo
mbalimbali.
Hoja hii inashadidiwa na Faustine (2019) anayesema kuwa suala la umoja na
ushirikiano kwa Waafrika ndio msingi wa kuimarisha na kudumisha mahusiano ya
jamii kuanzia katika familia, ukoo hadi jamii nzima. Anasema:
Mahusiano mazuri katika jamii za Waafrika yamesababisha kuwapokwa umoja unaotazamwa kama kitambulisho kwa mgeni yeyote ajayeAfrika. Umoja na ushirikiano hufungamanishwa na sababu za kuwapokwa mtu katika ukamilifu wa utu wake. Utu ambao umekitwa katikaimani ya kuwapo kwa nguvu hai inayopatikana kutokana na namnamtu anavyoishi kwa kutii na kuzingatia mitazamo na maadili ya jamiiyake. Hivyo, kwa Waafrika, ukamilifu wa mtu unatokana na auhutegemea uwepo wa watu wengine.
Kupitia mawazo yaliyo katika nukuu hiyo, tunaweza kusema kuwa, kwa Waafrika
mtu tajiri ni yule mwenye watu wengi kwa sababu kupitia watu hao kunamfanya
yeye kuwa mtu aliyekamilika. Mawazo hayo yanadhihirisha kuwa, Waafrika
wanaishi kwa umoja na ushirikiano kwa kiasi kikubwa.
Kwa namna hii tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa, suala la umoja na
mshikamano ni vyema likazingatiwa katika jamii kwani jamii inayoungana katika
kufanya jambo lolote katika misingi ya usawa hupiga hatua za kimaendeleo haraka
kuliko jamii isiyoungana. Umoja na mshikamano unaweza kufanywa kwenye
shughuli za kilimo, sherehe, viwandani, kwenye biashara na hata kwenye siasa.
Hivyo, itasaidia kufanikisha mambo mbalimbali kwa haraka.
4.3.2 Falsafa ya Umuhimu wa Maadili Katika Jamii
Maadili ni mwenendo unaokubalika ambao jamii imejiwekea kama msingi wa
kuongoza jamii katika utaratibu unaofaa. Kila mtu, jamii au taifa kwa jumla huishi
kulingana na maadili ya jamii hiyo. Nadharia ya Kisosholojia inasisitiza fasihi
kumulika matendo ya jamii na kuyaweka bayana. Matokeo ya utafiti huu yamebaini
kuwa, Waafrika ni miongoni mwa watu wanaoheshimu mila na desturi zao na huishi
53
kwa kufuata miiko ya jamii yao. Watafitiwa walieleza kuwa, miiko hiyo ikikiukwa
huweza kuleta athari au maafa kwa jamii. Baadhi ya mila hizo ni kama vile
kuheshimu wakubwa, kutoshiriki mahusiano ya kimapenzi na ndugu wa damu na
wizi. Waafrika wanaamini kuwa, suala la maadili ni msingi katika kuyaendesha
maisha yao; hivyo maadili hayo yanajengwa kuanzia katika ngazi ya kifamilia, ukoo
na hata jamii nzima. Aidha, mfumo wa maadili ya Waafrika unajengwa kidarajia
kuanzia kwa mkubwa mpaka mdogo (Faustine, 2017). Wanaamini kuwa, maadili
mema ni msingi wa kujenga amani, utu na adabu katika jamii. Falsafa ya Kiafrika
kuhusu umuhimu wa maadili inathibitika kupitia mifano ya vitendawili vya
Kiswahili. Vitendawili hivyo ni kama vifuatavyo:
a) Kitendawili: Miti yote nitakwea, mtarawanda utanishinda.
Jibu: Ndugu wa damu kutoweza kuoana.
(Chanzo: Badru, 2015).
Kitendawili kinaonesha mtu mwenye uwezo wa kupanda miti yote isipokuwa mti wa
mtarawanda. Swali linaloibuka akilini ni kwanini ashindwe kupanda mti huo wakati
mingine yote anaweza kupanda? Je huo ni mti wa namna gani? Hivyo jibu
lililotolewa kwa kitendawili hiki ni ndugu wa damu ambao hawawezi kuoana. Maana
ya kitendawili hiki ni kuwa, mtu huyo anaweza kuoa au kuolewa na watu wengine
lakini si ndugu wa damu. Mtafiti alipouliza sababu ya kuwakataza ndugu wa damu
wasioane kama inavyobainika katika kitendawili hicho, mtafitiwa (hakutaka jina lake
lijulikane)21 alieleza kuwa:
Kukiuka miiko ya jamii kunasababisha matatizo mbalimbali. Jamiiinatambua kuwa, kama ndugu wa damu wataoana basi huendawakapata laana ambayo hupatilizwa na mizimu ya ukoo husika nawahenga. Laana hizo zinaambatana na kuzaa viumbe visivyoeleweka.Zamani ilikuwa watu wakifanya hivyo wanazaa vilema au viumbe waajabu. Wakati mwingine maovu yakizidi mizimu inaweza kukasirikana kusababisha mvua isinyeshe kwa muda mrefu hadi wazeewatakapoenda kuomba msamaha kwa mizimu au kutubu kwa Mungu.Kwa kufanya hivyo, jamii inaziishi mila na desturi zao na kulindamaadili ya jamii. Na ndiyo maana kitendawili hicho kinasisitiza kuwampandaji (kaka) hawezi kukwea mti huo (dada) kwa sababu yakutunza maadili ya jamii.
21 Ni mwanajamii anayeishi wilaya ya Bukoba kata ya Bakoba. Mahojiano na mtafiti yalifanyikatarehe 2.3.2020 nyumbani kwake.
54
Maelezo yaliyo katika nukuu hapo juu yanathibitisha kuwa, suala la kulinda maadili
ya jamii ni msingi wa kuyaendesha maisha ya Mwafrika. Iwapo maadili yakakiukwa
basi huenda madhara makubwa yakatokea. Kwa hiyo, suala hili linaiendeleza falsafa
hii ya maadili. Falsafa ya maadili inaendelea kujitokeza katika kitendawili
kinachosema:
b) Kitendawili: Nyumbani kwetu kuna papai lililoiva, lakini siwezi kulichuma.
Jibu: Mwali.
(Chanzo: Badru, 2015).
Kitendawili hiki kinaonesha taswira ya papai ambalo tayari limeiva lakini
anayezungumza anasema kuwa hawezi kulichuma. Akieleza kuhusu kitendawili hiki,
Dismas22 katika mjadala anafafanua kuwa:
Taswira ya papai linalotajwa hapa inamaanisha binti au mwaliambaye tayari amefikia umri wa kuolewa lakini msemaji (kaka)anasema hawezi kulichuma (kumuoa au kuwa na uhusiano naye wakimapenzi). Kwa hiyo, kitendawili hiki kinaibua suala la umuhimu wakuzingatia maadili ya jamii za Waafrika yanayowakataza ndugu wadamu kuoana.
Nukuu hiyo inaonesha kuwa, falsafa hii ya maadili inayojitokeza katika kitendawili
hapo juu ndiyo inayomzuia kaka kumuoa dada yake na hivyo kutenda kinyume na
katazo hilo ni kuvunja taratibu za jamii yenyewe. Hii ni kutokana na sababu kuwa,
Waafrika wanaamini kwamba kama ndugu wa damu wataachwa waoane basi kuna
madhara yanayoweza kutokea katika familia, ukoo au jamii kwa jumla. Pia, kupitia
mjadala, Josbert23 alitega kitendawili kingine chenye maudhui sawa na haya. Nacho
kinasema:
c) Kitendawili: Nina kitu kizuri sana nyumbani kwetu lakini siwezi
kukichukua.
Jibu: Dada.
(Chanzo: Uwandani katika mjadala wa vikundi lengwa).
22 Azas Dismas ni mwanafunzi wa wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Kashai iliyopomanispaa ya Bukoba kata ya Kashai. Majadiliano kati ya mtafiti na watafitiwa yalifanyika tarehe 25.2.2020 shuleni hapo.23 Jasintha Josbert ni mwanafunzi wa shule ya msingi Katerero iliyopo Halmashauri ya Wilaya yaBukoba kata ya Kyeitema. Majadiliano na mtafiti yalifanyika tarehe 26.2.2020 shuleni hapo.
55
Kitendawili hiki pia kinaibua maswali ya kujiuliza kuwa, kwanini mzungumzaji
anasema ana kitu kizuri nyumbani kwao na asikichukue? Ni kitu gani kinamzuia
asikichukue? Katika kujiuliza maswali hayo tunapata jawabu kuwa kitu kizuri hicho
ni dada yake ambaye ni mzuri sana lakini kwa kuwa yeye ni ndugu hawezi
kumchukua au kumuoa. Mawazo haya yanabainishwa na Bw. Rwekaza24 katika
mahojiano anayefafanua kuhusu kitendawili hiki kwa kusema:
Kwa kufanya hivyo siku zote watoto wa Kiafrika wamekuwa wakiishikwa kuheshimu maadili hayo kuwa, dada au kaka hata awe mzurikiasi gani haupaswi kumfikiria katika masuala ya kimapenzi ni katazokatika jamii. Hii ni kwa sababu za kimaadili ya Kiafrika zinazokatazandugu wa damu kuoana. Kwa kuwa, jamii inatambua kuwa inatakiwakuishi katika maadili yanayofaa ndiyo maana kitendawili hikikinadhihirisha mawazo kuwa ndugu wa damu hawawezi kushirikikatika mahusiano ya kimapenzi.
Maelezo katika nukuu hapo juu yanaonesha wazi kuhusu maadili ya Waafrika.
Umuhimu wa maadili mema yanayosisitizwa na falsafa hii ni pamoja na kuifanya
jamii kuwa sehemu ya amani hivyo kusaidia utendaji wa kazi katika hali nzuri.
Hivyo, kupitia mifano ya vitendawili hivyo kama vilivyofafanuliwa na watafitiwa
hao tumebaini kuwa, jamii wa Waafrika ina maadili yake na mfumo wake wa kutolea
na kujifunza mambo mbalimbali. Waafrika hujifunza maadili kutokana na maisha
yao ya kila siku, hivyo mtu huishi akijifunza.
4.3.3 Falsafa ya Uhai na Kifo
Waafrika wanaamini kuwa kifo kipo kwa kila mwanadamu. Utafiti umebaini kuwa,
Waafrika wanaamini kuwa, wakati mwingine kifo kikitokea basi kuna mtu
anayesababisha kifo ambaye ni mchawi. Temples (1959) anaeleza kuwa, fikra za
Mwafrika zimetawaliwa na vitu viwili ambavyo ni uhai na kifo. Waafrika huamini
kuwa mtu akiumwa nguvu uhai zinapungua hivyo anaamini atakufa. Imani katika
uhai na kifo ni vitu vinavyowashughulisha sana Waafrika. Data za uwandani
zinathibitisha hoja hii kwani watafitiwa walieleza kuwa, kila mwanadamu atakufa
ingawa sio kila kifo kinachotokea ni mpango wa Mungu. Hii ina maana kuwa, vifo
24Hasimu Rwekaza ni mwanajamii katika wilaya ya Bukoba kata ya Hamugembe mtaa wa Nyangoye.Mahojiano kati yake na mtafiti yalifanyika tarehe 4.3.2020 nyumbani kwake.
56
vingine vinasababishwa na wachawi. Mawazo haya yanathibitishwa na Bi.
Abdallah25 anayesema:
Hatukatai kuwa ni kweli binadamu lazima afe lakini sio kila kifo nimpango wa Mungu. Mungu hakumuumba mwanadamu iliamwangamize lakini kuna watu wachache wasiopenda maendeleo yawatu wengine ndio hutumia nafasi za nguvu zao kuwaangamizawenzao kwa faida yao binafsi au kufanya visasi.
Maelezo katika nukuu hapo juu ni ithibati tosha kuwa, Waafrika wana imani
mbalimbali katika masuala ya kifo. Aidha, falsafa ya kifo imebainika kupitia
vitendawili vya Kiswahili vinavyotumika katika jamii za Kiafrika. Utafiti huu
umebaini kuwa, Waafrika wanaamini mtu akiumwa basi atakufa. Tunapoongelea
kuhusu mitazamo ya Waafrika kuhusu uhai na kifo, tunapata ushahidi kutoka katika
vitendawili vifuatavyo:
a) Kitendawili: Ini la ng’ombe huliwa hata na walioko mbali.
Jibu: Kifo.
(Chanzo: Badru, 2015).
Watafitiwa walifafanua kuwa, Waafrika wanayo falsafa yao inayohusu masuala ya
uhai na kifo. Akifafanua kuhusu suala la kifo kama linavyojitokeza katika
kitendawili hiki Bi. Katunzi26 katika mahojiano alieleza kuwa, “kifo humtokea mtu
yeyote katika dunia na hakuna ambaye anaweza kukikimbia kifo ili aishi miaka yote
hapa duniani. Walioko mbali hukumbwa na kifo na hata walioko karibu nao
hukumbwa na kifo”. Maelezo hayo yanaonesha dhahiri kuwa kifo kwa mwanadamu
hakiepukiki. Kwa upande mwingine mfano wa kitendawili chetu unaibua dhana ya
ushirikiano wa Waafrika katika suala la kifo kwamba linawashughulisha hata
walioko mbali. Hii ni kwa sababu wanaamini kuwa, hili ni suala zito la kijamii hivyo,
linatakiwa kupewa uzito fulani kwa kuzingatia kuwa, kila mtu ataweza kukumbana
nalo wakati wowote. Aidha, Badru (2015) anaunga mkono mawazo haya
anapofafanua kuwa, taarifa kuhusu msiba huwashughulisha sana Waafrika bila kujali
25 Bi Farida Abdallah ni mwanajamii na mwalimu mstaafu wa Shule ya msingi ya Qudus iliyopomanispaa ya Bukoba. Mahojiano na mtafiti yaliyofanyika tarehe 4.3.2020 mtaa wa National housing-Kashai.26 Bi. Marina Katunzi ni mwanajamii wa wilaya ya Bukoba na mtumishi katika taasisi ya WolrdVision tawi la Bukoba. Mahojiano na mtafiti yalifanyika tarehe 3.3.2020 ofisini kwake.
57
umbali ambao kifo hicho kimetokea. Taarifa za kifo hata kama kimetokea mbali
zinaweza kusambaa na kuwafikia hata walioko mbali. Falsafa hii inatukumbusha
kuwa, hakuna mtu atakayekwepa kifo haijalishi umbali atakaokuwa, kifo kitamfuata
popote alipo. Falsafa ya Waafrika ya uhai na kifo inaendelea kujidhihirisha katika
kitendawili kifuatacho:
b) Kitendawili: Akitokea watu wote hunung’unika na kuwa na huzuni.
Jibu: Ugonjwa au kifo.
(Chanzo: Salla, 2014).
Kitendawili hiki kinaonesha namna ambavyo taarifa za ugonjwa au msiba huwa ni za
masikitiko na huzuni pale vinapotokea katika jamii. Kwa hiyo, kifo kinapotokea
watu huomboleza na kuwa na majonzi. Bw. Kigoye27 (k.h.j) katika mahojiano
alifafanua kuwa, “kitendawili hiki kinaibua suala la hofu kuhusu kifo kwa Waafrika.
Kwa kuwa, wanaogopa kufa, wanakuwa na huzuni pindi mtu akiumwa kwa sababu
wanaamini atakufa”. Hata hivyo, utafiti umebaini kuwa, wanajamii katika jamii ya
Waafrika, huamini mtu akifa hawezi kurudi tena na kuishi kama mtu mwenye nafsi
hai ndiyo maana watu wanaogopa kufa au kuumwa. Kitendawili kinachoshadadia
mawazo haya kilitegwa na Gidius28 katika mjadala. Nacho kinasema:
c) Kitendawili: Kitanda changu cha dhahabu nikilalia siamki tena.
Jibu: Jeneza.
(Chanzo: Uwandani kupitia mjadala wa vikundi lengwa).
Anaendelea kufafanua kuwa, dhana ya kitanda hapa imechukuliwa kama jeneza
ambalo msemaji anakiri kuwa akilalia hataamka tena. Utafiti umebaini kuwa, maana
inayotolewa katika kitendawili hiki inahusisha suala la kifo ambapo mtu aliyefariki
akishalazwa kwenye jeneza hataweza kuamka tena. Suala hili linaibua falsafa ya
Waafrika katika kifo na uhai kwani ni ukweli kwamba mtu akifa hawezi kurudi kuwa
nafsi hai. Katika uhalisia hakuna mwanadamu ambaye atakufa na kurudi tena duniani
27 Amekwishatajwa.28 Nicera Gidius ni mwanfunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Kashai iliyopo manispaaya Bukoba kata ya Kashai. Majadiliano kati ya mtafiti na watafitiwa yalifanyika tarehe 25.2.2020shuleni hapo.
58
na kuishi kama mwanadamu wa kawaida. Aidha, kitendawili chenye maudhui sawa
na haya ni kile kinachosema:
d) Kitendawili: Nikipanda gari la baba sirudi kamwe.
Jibu: Jeneza.
(Chanzo: Salla, 2014).
Kitendawili hiki kinafanana na kilichotegwa awali hapo juu. Gari inayoelezwa hapa
ni jeneza na dhana ya kutorudi inahusishwa na dhana ya kifo, ambapo mtu akifa
hawezi kurudi tena. Vitendawili hivi vinafafanua kuwa, mtu akifa hawezi kurudi tena
na kuweza kuishi kama binadamu wa kawaida mwenye nafsi hai. Kupitia vitendawili
hivi ambavyo ni fasihi ya Waafrika, vinaonesha kuhusu falsafa ya Waafrika katika
suala la uhai na kifo.
Vilevile, imani na mitazamo ya Waafrika kuhusu kifo imebainishwa na Kaponda
(2018) anayesema kuwa, kwa Waafrika, kifo husababishwa na mchawi, roho za wafu,
laana na kifo cha asili. Kimsingi mtu hufa taratibu mpaka watu wanaomkumbuka
waishe. Waafrika wana hofu na kifo. Katika msiba watu huweza kulia na hata
kuzimia pale wanapoondokewa na mtu ambaye walikuwa wanampenda na alikuwa
na umuhimu kwao. Hii ni kutokana na imani kuwa mtu huyo hawataweza kumwona
tena. Hivyo, tunaweza kuhitimisha hoja hii kwa kusema kuwa, vitendawili hivyo
pamoja na maelezo mbalimbali tuliyoeleza hapo juu yanathibitisha kwamba, masuala
yahusuyo uhai na kifo ni mojawapo ya falsafa ya Kiafrika na kuwa Waafrika wana
hofu na kifo.
4.3.4 Falsafa ya Uduara
Uduara ni mojawapo ya falsafa inayojitokeza katika jamii za Waafrika. Kwa
Waafrika, mtazamo kuhusu uduara ni namna ya kuufasli ulimwengu wao. Matokeo
ya utafiti huu yamebainisha kuwa, Waafrika wanaamini kuwa vitu vizuri ni vile
vilivyo katika umbo la duara. Falsafa ya uduara inajitokeza katika jamii nyingi za
Waafrika kutokana na vitu wanavyotumia au mambo wanayoyafanya kuwa na umbo
la duara. Aidha, kupitia data za uwandani, utafiti umebaini kwamba, jamii za
Kiafrika hufanya mambo mbalimbali kama michezo ya watoto, mikao ya kula,
shughuli za kijamii kama misibani na katika sherehe hufanywa kwa uduara.
59
Katika utafiti huu, falsafa ya uduara imeweza kuthibitika kupitia vitendawili vya
Kiswahili vinavyotumika katika jamii za Kiafrika. Ipo mifano mingi ya vitendawili
inayodhihirisha falsafa ya uduara kwa Waafrika. Vitendawili hivi vipo katika namna
mbili. Mosi, vinaonesha dhana ya uduara katika vitu na pili, vinaibua uduara katika
utendekaji wa jambo. Kwa kuanza na mifano ya vitendawili vinavyoonyesha
utendekaji wa jambo katika uduara ni kama vifuatavyo:
a) Kitendawili: Amekaa kimya na watoto wamemzunguka pande zote.
Jibu: Mgomba katikati na machipukizi yake pembeni yake.
(Chanzo: Salla, 2014).
Katika kukichunguza kitendawili tajwa hapo juu tumebaini uwepo wa falsafa ya
uduara. Maana inayopatikana katika kitendawili hiki inaibua falsafa ya uduara kwa
kuwa, Waafrika wanaamini kuwa, kukaa kwa uduara kunasaidia kujenga
mshikamano kuanzia katika familia, ukoo mpaka katika jamii nzima. Akifafanua
kuhusu kitendawili hiki, mtafitiwa (hakutaka jina litajwe)29 katika mahojiano
anasema:
Uduara unajitokeza katika mambo mengi. Karibia kila jambolinalofanyika hufanywa kwa uduara. Kwa mfano kwenye shughuli zakitanzia, sherehe mbalimbali za kijamii zote matukio yake hufanyikakwa uduara. Hii inasaidia hata kufahamiana kwa watu kwa kuwamnakuwa mnaonana. Hapa inakuwa ni rahisi kutambua naniameshiriki na ambaye hajashiriki katika shughuli hiyo ya kijamii. Kwhiyo utakuta wanapokula, wanapocheza au hata wanapozika huwawanakuwa katika mzunguko unaotengeneza duara. Hiindio maanakitendawili kinaonesha kuna kitu kilichopo katikati na wenginewamekizunguka pande zote kutengeneza duara.
Maelezo yaliyo katika nukuu hapo juu ni ithibati kuwa, kitendawili hicho kimesawiri
vema falsafa ya uduara kwani mambo mengi yanayofanywa katika jamii za Waafrika
hufanywa kwa suara ya duara. Hivyo, inadhihirisha imani kuwa uzuri wa kitu au
mambo katika jamii unatokana na umviringo au uduara. Pia, kupitia mjadala wa
vikundi lengwa, Clophas30 alitega kitendawili kinachosawiri falsafa ya uduara.
Kitendawili hicho kinasema:
29 Ni mwanajamii anayeishi katika wilaya ya Bukoba kata ya Kibeta. Mahojiano na mtafiti yalifanyikatarehe 5.2.2020 nyumbani kwake.30 Eneliko Clophas ni mwanafunzi wa shule ya msingi Katerero iliyopo Halmashauri ya Wilaya yaBukoba kata ya Kyeitema. Majadiliano na mtafiti yalifanyika tarehe 26.2.2020 shuleni hapo.
60
b) Kitendawili: Askari wamekaa pembeni na mfalme yupo katikati.
Jibu: Watu wakiota moto huku wakiwa wameuzunguka.
(Chanzo: Uwandani katika mjadala wa vikundi lengwa).
Falsafa ya Kiafrika katika kitendawili hiki imejikita katika masuala ya uduara.
Akiendelea kufafanua kuhusu kitendawili hiki mtafitiwa huyo alisema, “Waafrika
huamini katika uduara ndiyo maana, kwao mambo mazuri ni yale yaliyoko kwenye
umbo la duara”. Wanaamini kuwa vitu vizuri ni vile vilivyoko kwenye umbo la
duara. Kwa hiyo, kupitia falsafa hii hujikuta wakifanya mambo yao wakiwa kwa
uduara. Kwa kufanya hivyo kunawawezesha watu hao kujadiliana kuhusu mambo
mbalimbali ya kimaendeleo jambo ambalo litasababisha kufanikiwa katika
maendeleo yanayofanywa na jamii. Akishadadia kuhusu falsafa ya uduara kama
inavyojitokeza katika kitendawili hicho, Muganyizi31 katika mahojiano uwandani
anasema:
Falsafa ya uduara inasisitizwa ndani ya jamii huku wakifundishwakupitia njia mbalimbali umuhimu wa kuthamini vitu vilivyokokwenye umbo la duara. Kwa mfano masuala ya tambiko hufanywakwa uduara na hata baadhi ya nyumba za kuishi hujengwa kwa umbola uduara. Kwa hiyo, kitendawili hiki kinaibua falsafa ya uduaraambao unajitokeza kutokana na kitendo cha kuuzunguka moto uliopokatikati.
Kupitia maelezo katika nukuu hiyo, mtafiti amebaini kuwa, uduara ni mhimili
mkubwa wa ushirikiano wa Waafrika. Ipo mifano mingi ya vitu au mambo
yanayofanywa kwa uduara katika jamii Waafrika. Wao huamini katikati
panapozungukwa na kitu huwa ndiyo chanzo cha nguvu zao, ndiyo maana katika
kitendawili hapo juu tunaona moto upo katikati. Aidha, Mussa32 katika mjadala
alitega kitendawili kinachoonesha falsafa ya uduara katika kitu. Nacho kinasema:
c) Kitendawili: Nina nyumba yangu ya mviringo.
Jibu: Yai.
(Chanzo: Uwandani katika mjadala wa vikundi lengwa).
31 Binamungu Muganyizi ni mwanajamii wa wilaya ya Bukoba anayeishi kata ya Kibeta mtaa waKankwila. Mahojiano na mtafiti yalifanyika tarehe 2.3.2020 nyumbani kwake.32 Akramu Mussa ni mwanafunzi wa shule ya msingi Katerero iliyopo Halmashauri ya Wilaya yaBukoba kata ya Kyeitema. Majadiliano na mtafiti yalifanyika tarehe 26.2.2020 shuleni hapo.
61
Utafiti umebaini kuwa, kitendawili hiki kinachomoza falsafa ya uduara ambapo
msemaji anaeleza kuwa, “nyumba yake ni ya mviringo”. Akiendelea kufafanua
kuhusu kitendawili hiki, mtafitiwa huyo anasema, “suala la nyumba kuwa ya
mviringo linaibua dhana ya uzuri wa nyumba hiyo katika uduara. Kwa hiyo, uzuri
katika kitu umedhihirika kupitia kitendawili hiki na hivyo, kuibua falsafa ya
Waafrika kupenda vitu vilivyo katika umbo la duara kwani wanaamini vitu hivyo ni
vizuri kuliko vile ambavyo siyo vya duara.” Maelezo hayo yandhihirisha kuwa, ni
jambo la kawaida kusikia watu katika jamii ya Kiafrika wakisifia vitu vya duara.
Vitu kama vile nyumba zao za misonge huwa ni za duara, mitungi, vyombo vyao vya
kupikia na hata vifaa vya kukamulia maziwa. Pia kitendawili kingine kinasema:
d) Kitendawili: Fupi fupi la mviringo limeleta utamu.
Jibu: Ngoma.
(Chanzo: Salla, 2014).
Dhana ya uzuri katika kitu imejibainisha katika kitendawili hiki ambapo kichocheo
chake cha msingi ni “fupi fupi la mviringo kuleta utamu”. Kupitia mfano huu
tumeweza kutambua kuwa, kumbe utamu unatokana na umviringo wa kitu hicho na
hapo dhana ya uzuri katika duara inaibuliwa. Aidha, hapa inaonesha ni kwa namna
gani Waafrika huona vitu vya duara kuwa na thamani kubwa, ndiyo maana katika
jamii inasisitizwa kuthamini vitu vyenye umbo la duara. Kwa mfano visima vyao na
hata mabwawa ambayo huyachimba kwa lengo la kunyweshea mifugo huwa ya
duara. Mawazo yaliyo katika kitendawili hicho yanafanana na Mlelwa, (2017)
anayesema:
Utamaduni wa Waafrika unaonesha wazi kuwa wanaamini kituchochote kikifanyika katika hali ya duara kinakuwa kizuri. Hii ni kwasababu kunakuwa na umoja katika kutenda. Pia kitu kikiwa katikaumbo la duara kinakuwa ni kizuri. Kwa hiyo, umbo la duara ni kigezocha uzuri kwa Waafrika.
Maelezo katika nukuu hiyo hapo juu ni ithibati kuwa, mtazamo wa Waafrika kuhusu
uzuri au kitu kizuri ni kile kilicho katika umbo la duara. Kwa maana hiyo baadhi ya
vitu wanavyovitumia Waafrika ni vya umbo la duara. Pia, utendekaji wa mambo
katika uduara kunahamasisha umoja na mshikamano katika jamii.
62
Hoja hii inatiwa nguvu na nadharia ya Kisosholojia kupitia msingi wake unaosema
fasihi haiwezi kujitenga na jamii ambayo kwayo imechipuzwa. Hii ina maana kuwa
fasihi inaakisi kile kinachotendeka na kukitoa kwa jamii. Vitendawili hivi vinaakisi
maisha halisi ya jamii na hivyo kutupatia picha halisi ya Waafrika wanavyoishi
katika mazingira yao. Hata hivyo, utafiti huu umebaini kuwa, falsafa ya uduara
inaenda sambamba na masuala ya umoja na ushirikiano kwa maana kuwa mambo
mengi yanayofanywa na Waafrika, hufanywa kwa kushirikiana na hivyo kujenga
falsafa ya uduara. Kwa hiyo, uduara wa Waafrika una maana kubwa katika jamii
kwani husaidia kuleta umoja na mshikamano katika jamii na hivyo, kurahisisha
kufikiwa kwa mafanikio makubwa katika mambo mbalimbali.
4.3.5 Falsafa ya Imani katika Mungu na Mizimu
Hii ni mojawapo ya falsafa ya Kiafrika inayosawiriwa katika fasihi simulizi
mathalani katika vitendawili vya Kiswahili. Utafiti huu umebaini kuwa, Waafrika
wanaamini katika nguvu na uweza wa Mwenyezi Mungu kwa kuwa, Mungu ndiye
muweza wa yote na ndiye suluhisho la matatizo ya mwanadamu. Katika utafiti huu,
falsafa ya imani katika Mungu na mizimu imeweza kudhihirika kupitia mifano ya
baadhi ya vitendawili wanavyovitumia katika jamii zao kusawiri suala hili. Mifano
ya vitendawili hivyo ni kama:
a) Kitendawili: Ana nguvu na uwezo kutushinda sote.
Jibu: Mungu.
(Chanzo: Salla, 2014).
Falsafa ya imani katika Mungu inajidhihirisha katika kitendawili hapo juu kwani
jamii huamini kuwa, ipo nguvu isiyoonekana ambayo ndiyo hutumika kuongoza
maisha ya mwanadamu. Akifafanua kuhusu kitendawili hiki, Bw. Kigoye (k.h.j)
katika mahojiano anasema:
Kwa asili Muhaya anajua kuwa, Mungu yupo ndio maana Munguamepewa majina mengi kudhihirisha uwezo na nguvu zake. Baadhiya majina hayo ni kama Ruanga33, Katonda34 na Nyarubamba35.Majina hayo yana maana tofautitofauti kudhihirisha uwezo na
33 Ruanga ni jina la Mungu wa Kihaya linalomaanisha kuwa na uwezo wa kutoa maamuzi sahihi naanachokitolea maamuzi kinakuwa mwafaka.34 Katonda ni jina la Mungu lenye maana kuwa yeye ni asili ya kila kitu kilichopo duniani (muumbaji).35Nyarubamba ni Mungu ana uwezo wa kila kitu hasa kwa upande wa kutoa riziki kwa watu.
63
nguvu alizo nazo Mungu. Hata kabla ya kuja kwa wamisionari,watu wa jamii ya Wahaya tulikuwa tunatambua kuwa Mungundiye muweza wa yote katika kufanya mambo mbalimbali. Hatahivyo suala la kuamini wahenga na mababu lipo sambamba.Kwenye familia hapawezi kukosa changamoto ambazo zitashindwakupatiwa majibu. Kwa hiyo, tunaamini kuwa mababu au wazazi niwatu wa hekima hata wakifa hawatuzuii sisi kuendeleakuwaheshimu na kuwaomba katika shida mbalimbali. Kama mtuhuyo aliyefariki alikuwa maarufu kama vile Mfalme au Mtemi,ataendelea kupelekewa maombi kwa kufuata taratibu fulani zakimila. Taratibu hizo ni kama vile, kumgawia kahawa na pombekwa muda wa siku tatu na hapo maombi yakishakamilika siku yatatu pombe hurudishwa nyumbani na kunywewa.
Maelezo ya mtafitiwa huyo yanadhihirisha kuwa, kwa Waafrika Mungu ndiye
mtawala, asili ya kila kitu duniani na mwenye uwezo wa kutoa riziki kwa watu.
Licha ya imani kuwa Mungu ndiye muweza bado Waafrika wanaamini katika wafu
yaani wahenga na mizimu ambayo huendelea kuwasikia wakiomba katika shida
mbalimbali. Edisson36 katika mjadala anashadadia kitendawili hiki kwa kusema
kuwa:
Mungu hashindwi na jambo lolote; akiamua jambo lolote limtokeemwanadamu huwa linatokea. Jamii ya Waafrika wanaamini kuwa,kuna viumbe vyenye nguvu na uwezo mkubwa wa kutenda mamboambayo binadamu wa kawaida hawezi kufanya. Viumbe hao ni kamavile Mungu, mizimu, wahenga na mababu. Ndio maana jibu lakitendawili chetu linaonesha ni Mungu tu ndiye mwenye uwezo huo.
Maelezo haya yanathibitisha kuwa, Waafrika wanaamini katika nguvu na uwezo wa
Mungu katika kutenda mambo yasiyowezekana kufanyika kwa hali ya kawaida.
Aidha, kitendawili kingine kinasema:
b) Kitendawili: Anatuona lakini sisi hatumuoni.
Jibu: Mungu.
(Chanzo: Badru, 2015).
Katika kuichunguza falsafa ya imani katika Mungu, utafiti huu umebaini kuwa,
Waafrika wanaamini kuhusu uwepo wa nguvu zisizoonekana ambazo ndizo
huongoza maisha yao hivyo, zinapaswa kuheshimiwa na kuaminiwa. Katika
36 Happiness Edisson ni mwanafunzi wa shule ya msingi Katerero iliyopo Halmashauri ya Wilaya yaBukoba. Majadiliano na watafitiwa yalifanyika tarehe 26.2.2020 shuleni hapo
64
kitendawili hiki “anatuona lakini sisi hatumuoni” jibu lake ni “Mungu”, kinasawiri
falsafa ya imani katika Mungu. Katika mjadala, Projestus37 alieleza kuwa, “Waafrika
katika imani wanafahamu kuwa Mungu ana uwezo mkubwa kuliko kiumbe chochote,
ana uwezo wa kutuona wakati wowote na mahali popote tulipo”. Hivyo, kwa
kuamini kuwa Mungu anaona matendo ya kila mwanadamu; inawafanya Waafrika
kuishi kwa kufuata misingi ya utu bora siku zote na kuogopa kutenda mabaya.
Kitendawili kingine chenye maudhui yanayofanana na haya ni kile kilichotegwa na
Selestine38 ambacho pia kinasawiri falsafa ya imani katika Mungu. Kitendawili
kinasema:
c) Kitendawili: Popote niendapo yupo lakini haonekani.
Jibu: Mungu.
(Chanzo: Uwandani katika mjadala wa vikundi lengwa).
Kitendawili hiki kinaonesha masuala ya imani ya Waafrika katika Mungu.
Akifafanua kuhusu kitendawili hiki, Kaigara39 katika mahojiano uwandani anasema:
Waafrika wanaamini kuwa, wapo viumbe wenye nguvu na uwezowanaoaminika kuwepo lakini binadamu wa kawaida hawawezikuwaona isipokuwa kupitia imani tu kuwa yupo. Uwezo wakeunatokana na nguvu za kiuajabu alizonazo ambazo zinamfanya yeyekuwepo popote na asionekane. Waafrika huamini Mungu ana uwezowa kutembea mahai popote na asiweze kuonekana kwa macho yakawaida. Kwa hiyo kitendawili hiki kimesawiri vema falsafa ya imanikatika Mungu na mizimu.
Maelezo katika nukuu hapo juu yanaonesha namna ambavyo Waafrika huamini
katika Mungu na kuwa yeye ndiye muweza wa yote. Falsafa ya imani inawapelekea
Waafrika kuishi katika misingi ya maadili mema yanayompendeza Mungu na
kuyakataa maovu yaliyo kinyume na maagizo ya Mungu. Hii inasababishwa na
imani kuwa Mungu anamuona kila mtu na kila tendo jema au ovu alifanyalo
mwanadamu. Kupitia Mungu au miungu Waafrika hujenga familia na jamii yenye
37 Proscovia Projestus ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari iliyopo manispaaya Bukoba. Majadiliano na mtafiti yalifanyika tarehe 25.2.2020 shuleni hapo.38 Faustine Selestine ni mwanafunzi wa kitato cha nne katika shule ya Sekondari Kashsi iliyopomanispaa ya Bukoba. Majadiliano na mtafiti yalifanyika tarehe 25.2.2020 shuleni hapo.39 Elizabeth Kaigara ni mama na mlezi wa watoto katika kigango cha Mt. Inyasi parokia ya YohanePaulo wa pili kata ya Kibeta- Tanesco. Mahojiano na mtafiti yalifanyika tarehe 4.3.2020 ofisini kwake.
65
misingi bora na imani thabiti katika masuala ya dini. Hivyo, yeyote anayefanya
maovu huadhibiwa na Mungu.
Aidha, hoja hii imetiliwa nguvu na Temples (1959) anayesema kuwa, Mwafrika
anaamini kuna nguvu kubwa kuliko zote ambayo ni Mungu. Hivyo, ameamua
kugawa nguvu hizo katika darajia za nguvu ambazo ni: Mungu- mizimu- wahenga-
wazee- binadamu wa kawaida- wanyama- miti. Kwa hiyo, kupitia maelezo ya
mtaalamu huyu na nukuu hapo juu ni dhahiri kuwa Waafrika wanaamini katika
nguvu za Mungu na mizimu katika kuwawezesha kufanikisha mambo mbalimbali.
Hussein (1976) anakubaliana na hoja hii kwa mtazamo kuwa, Waafrika wanaamini
watu waliokufa wapo karibu na Mungu na wale walio hai humwomba Mungu kupitia
wale waliokufa. Hili linadhihirika kupitia matambiko au kuomba mizimu ya mababu
inayofanywa na Waafrika wengi katika maisha yao ya kila siku. Hivyo, Waafrika
wengi wanaamini kuwa, wahenga wanaweza kuwa na nguvu katika kila kitu
kinachowatokea katika maisha yao. Mambo kama vile kuumwa, vifo, ajali, talaka,
mimba kuharibika, ulemavu na mikosi inaaminiwa kutokea kwa sababu ya wachawi
au hasira za mababu na wahenga. Kwa jumla mawazo haya yanatudhihirishia
mtazamo wao kuhusu imani katika nguvu za Mungu na mizimu.
4.3.6 Falsafa ya Uchawi na Ushirikina
Makame, (2016) anafafanua kuwa ushirikina ni tabia ya mshirikina kufanya matendo
au maneno juu ya uwezo mkubwa wa kiumbe kingine kuleta madhara badala ya ule
wa Mwenyezi Mungu kwa kutumia majini, mizimu, talasimu za kisihiri na hirizi
katika kufanikisha jambo fulani. Ushirikina hujitokeza katika nyanja mbalimbali
ambazo ni; Mosi, kufanya matendo yasiyo ya kawaida ya kuogofya na kushangaza.
Pili, mtendaji wa ushirikina hushiriki na kufuata maelekezo ya viumbe wa ajabu na
kuwasiliana nao katika ufanikishaji wake. Tatu, mshirikina hutawaliwa na lugha za
majini na mashetani pamoja na kuzungumza nao katika sehemu maalumu kama vile
mapango au kilingeni. Utafiti huu umebaini kuwa, jamii nyingi za Kiafrika huamini
katika nguvu za miujiza katika kutenda mambo yasiyo ya kawaida. Nguvu hizo
hujulikana kuwa ni za kichawi au kishirikina. Mtafiti amebaini uwepo wa vitendawili
vya Kiswahili vyenye falsafa ya “uchawi na ushirikina”. Falsafa hii inadhihirika
katika vitendawili vifuatavyo:
66
a) Kitendawili: Mchawi wa manga hulala mchana na kufanya kazi usiku.
Jibu: Mwezi.
(Chanzo: Salla, 2014).
Kupitia kitendawili hiki, utafiti huu umebaini uwepo wa falsafa ya Kiafrika
inayozungumzia masuala ya “uchawi na ushirikina”. Kitendawili kinaonesha namna
ambavyo wachawi hufanya kazi usiku na hii inasawiri suala la imani za Waafrika
kuhusu uchawi na wachawi ambao huaminika kufanya shughuli zao nyakati za usiku.
Akisisitiza kuhusu falsafa hii kama inavyojitokeza katika kitendawili hicho, Bw.
Bwemero40 alieleza kuwa, “mambo hayo hufanyika kupitia nguvu za giza, yaani
“uchawi na ushirikina” na shughuli hizo hufanyika usiku kwa kuwa ni jambo ovu
ambalo halikubaliki katika jamii”. Maelezo hayo yanathibitisha mtazamo wa
Waafrika kuhusu uwepo wa uchawi katika jamii. Aidha, kupitia mahojiano na
watafitiwa ilielezwa kuwa, uchawi na wachawi wapo katika jamii za Kiafrika na
hutumia nguvu zao kuwadhuru watu wengine. Na kwa kutambua hilo ndio maana
watu wengi wameokoka na wanamwabudu Mungu ili kupata ulinzi wa Mungu dhidi
ya wachawi. Mawazo haya yanayothibitisha kuhusu uwepo wa uchawi katika jamii
yanabainishwa katika mahojiano pale Bw. Rwegasira41 anaposema:
Tunaamini kuwa uchawi upo na unafanya kazi katika mazingirahalisi. Jambo hili linathibitika katika jamii zetu kutokana na sababukuwa, hata wakristo wanaomjua Mungu hufanya baadhi ya vituvinavyoashiria kuwa wanaamini katika uwepo wa uchawi. Mambohayo ni kama vile kuomba kabla ya kulala na baada ya kuamka.Kwa mfano katika salamu zao huomba ulinzi wa Mwenyezi Munguna kukemea nguvu za kichawi dhidi yao. Hii inadhihirisha kuwa,wanaamini kuwa wachawi wapo na wanaweza kuja kuwadhuruwakati wakiwa wamelala kama kitendawili hicho kinavyooneshakuwa wachawi wanafanya kazi usiku.
Maelezo katika nukuu hii ni ushahidi kuwa, Waafrika wanaamini kuwa wachawi
wapo na wanaweza kutumia nguvu zao kuwadhuru watu wengine. Mambo hayo ni
kama vile kusababisha vifo, kujibadili au kumbadili mtu mwingine katika maumbo
40 Bw. Deogratius Bwemero ni mwanajamii katika wilaya ya Bukoba anayeishi kata ya Rwamishenyemtaa wa Kamizilente. Mahojiano na mtafiti yalifanyika tarehe 2.3.2020 nyumbani kwake.41 Bw. Audax Rwegasira ni mwanajamii wa wilaya ya Bukoba, mstaafu katika utumishi wa umma naaliwahi kuwa afisa katika Ofisi ya Utamaduni Halmashauri ya Bukoba. Mahojiano na mtafitiyalifanyika mnamo tarehe 6.3.2020 mtaa wa Buyekera kata ya Bakoba.
67
mbalimbali. Pia, falsafa ya “uchawi na ushirikina” imedhihirika katika kitendawili
kisemacho:
b) Kitendawili: Kaa huku nikae kule tumfinye mchawi.
Jibu: Kula ugali kwa mikono.
(Chanzo: Badru, 2015).
Kitendawili hiki kinasawiri mapokeo ya jamii kuhusiana na uchawi. Akifafanua
kuhusu kitendawili hiki, Theobard42 katika mjadala anasema:
Katika jamii za Kiafrika japo uchawi upo, lakini bado haukubalikimiongoni mwa wanajamii na unapingwa vikali. Pindi wanapojuakuwa mtu wa jamii yao ni mchawi huweza kumkemea na kumdhihakiili aachane na uchawi. Hivyo, maana ya kitendawili hiki inaibuadhana ya ushirikiano katika (kumfinya) kumuadhibu mchawi”.
Hivyo, maelezo haya yanayofafanua kitendawili hapo juu yanaonesha kuwa,
Waafrika wanaamini katika masuala yanayohusu “uchawi na ushirikina” na pia
wanawachukia wachawi na shughuli zao za kichawi. Katika kuunga mkono mtazamo
wa hoja hii, Manala (2004) anasema:
Witches are not only feared, but also hated because they make lifeunbearably difficult for individuals, families, communities andsocieties. In the African’s world of thought, when ill-health,misfortune, accident or death occuers, traditional Africans willimmeadiately probe witch crafts as the likely cause (uk. 1501).
Wachawi sio tu kwamba wanaogopwa lakini pia wanachukiwa kwasababu wanayafanya maisha bila shaka kuwa magumu kwa mtubinafsi, familia na hata jamii kwa ujumla. Kwa mtazamo wa Waafrika,ikitokea magonjwa, bahati mbaya, ajali au hata vifo basiwatamtazama moja kwa moja mchawi kwamba ndiye aliyesababisha(Tafsiri ya mtafiti).
Nukuu hiyo inathibitisha kuwa, wachawi hawapendwi katika jamii na hivyo,
wanapingwa kwa sababu uchawi unahusisha matendo maovu. Pia, Faustine (2017)
anaeleza kuwa, Waafrika wanaamini mchawi anaweza kutumia viumbe wengine
katika kutenda matendo mbalimbali kinyume na uhalisi wao au kumbadilisha mtu na
kumfanya aishi katika ulimwengu wa wachawi bila watu wengine kumwona. Huko
42 Adelaida Theobard ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Kashai iliyopomanispaa ya Bukoba. Majadiliano na watafitiwa hao yalifanyika tarehe 25.2.2020 shuleni hapo.
68
hutumikishwa na mchawi huyo kwa kufanyishwa kazi mbalimbali kama ilivyo katika
ulimwengu wa kawaida. Hivyo, tunaweza kuhitimisha hoja hii kwa kusema kuwa,
mtazamo wa Waafrika kuhusu falsafa hii ya uchawi unajipambanua kwa kiasi
kikubwa katika jamii za Kiafrika. Mawazo haya yanafungamanishwa na nadharia ya
Kisosholojia inayosisitiza kuwa fasihi haiwezi kujitenga na jamii ambayo kwayo
imechipuzwa. Hii ni kutokana na sababu kuwa kazi nyingi za fasihi ya Waafrika
zimesawiri kwa wingi falsafa hii kama tulivyoona katika vitendawili tulivyovitumia
katika hoja yetu vimedhihirisha kuwepo kwa falsafa ya “uchawi na ushirikina” katika
jamii ya Waafrika.
4.3.7 Falsafa ya Uzazi na Malezi
Suala la uzazi linaonekana kuwa ni la muhimu sana kwa Waafrika. Matokeo ya
utafiti huu yamebaini kuwa, Waafrika wanaamini kuwa, ukamilifu wa ndoa za
Waafrika unategemea uwezo wa mwanamke kuzaa watoto. Waafrika wanaamini
katika familia pana ambapo kuzaa watoto wengi ni ufahari na kunaifanya familia au
ukoo kupanuka. Aidha, Faustine (2017) anaeleza kuwa, mtu mwenye uzazi
hutazamwa kama mtu mwenye baraka nyingi zinazotokana na kuwapo kwa nguvu-
hai. Waafrika wanautazama uzazi kama njia ya kuwapo kwa mtu na njia pekee ya
kuukuza na kuuendeleza ukoo. Hivyo, mtu mwenye uzazi hupewa heshima kuliko
yule asiye na uwezo wa kuzaa. Hata hivyo, kupitia utafiti huu imebainika kwamba,
Waafrika wanaamini kuwa suala la malezi ya watoto hao ni jukumu la wanawake
kwa kiasi kikubwa. Hoja hii inaungwa mkono na mtafitiwa aliyeeleza kuwa, suala la
uzazi na malezi ya watoto kwa Waafrika linamshughulisha mwanamke wa Kiafrika
kuliko mwanaume. Haya yamethibitika pale Bi. Kayanga43 (k.h.j) anaposema:
Suala la ndoa kwa jamii zetu linaenda sambamba na kuzaa kwamwanamke. Mwanamke anapoolewa na kwenda ukweni anatarajiwakumzalia mwanaume watoto. Mwanamke anayezaa hupendwa sana nawakwe zake ukilinganisha na yule asiyezaa. Siku zote mwanamkealiyeolewa na asizae hudharauliwa na hata kusemwa na ndugu wamwanamme kwa kuwa hajailetea faida familia au ukoo wao.
Maelezo katika nukuu hiyo hapo juu ni ithibati tosha kuwa wanawake wa Kiafrika
ndio wanaobebeshwa mzigo wa malezi ya watoto na pindi mwanamke huyo asipozaa
43 Bi. Salma Kayanga ni mwanajamii, mama wa familia na Afisa afya ofisi ya kata Kibeta.Mahojiano na mtafiti yalifanyika tarehe 5.3.2020 ofisini kwake.
69
basi yeye ndiye hupewa lawama za kutokuzaa. Pia, utafiti umebaini kuwa, falsafa ya
uzazi na ulezi imejitokeza katika vitendawili mbalimbali vya Kiswahili. Theobard44
alitega kitendawili kinachosawiri falsafa ya uzazi. Kitendawili kinasema:
a) Kitendawili: Dada yangu hazai mtoto mmoja mmoja, bali mapacha wengi
wakubwa kwa wadogo.
Jibu: Mapapai.
(Chanzo: Uwandani katika mjadala wa vikundi lengwa).
Katika Kitendawili hiki tunaona uwepo wa falsafa ya Kiafrika ambayo imejikita
kwenye uzazi. Akiendelea kufafanua kuhusu kitendawili hiki, Theobard45 (k.h.j)
katika mjadala anasema:
Hapa tunaiona falsafa ya uzazi ambayo inasisitiza umuhimu wa kuzaawatoto wengi. Kama mti wa mpapai unavyozaa matunda mengindivyo unavyofananishwa na uzazi wa watoto kwa Mwafrika. Hii nikwa sababu, Waafrika wanaamini katika uzazi wa watoto wengi kamaufahari na kwa kufanya hivyo, wanapanua ukoo na kuwa na familiapana.
Maelezo katika nukuu hiyo yanahibitisha kuwa, katika jamii za Kiafrika ni jambo la
kawaida kuzikuta familia zenye watoto zaidi ya kumi. Hata hivyo, suala la malezi
husisitizwa na kuzingatiwa kwa jamii ili kuwaandaa watoto hao kuja kushika
majukumu ya jamii husika.. Familia yenye watoto wengi huwa imara na thabiti
katika nyanja mbalimbali. Pia, Clemens46 anatoa mfano mwingine wa kitendawili
chenye falsafa ya malezi. Kitendawili kinasema:
b) Kitendawili: Mama yangu kila aendako na mtoto wake mgongoni.
Jibu: Konokono.
(Chanzo: Uwandani katika mjadala wa vikundi lengwa).
Utafiti umebaini kuwa, kitendawili hiki kinasawiri suala la uzazi na malezi.
Kitendawili hiki kinamtaja mama na mtoto wake mgongoni. Kinaeleza kuwa, mama
44 Teodata Teobard ni mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Katerero iliyopaHalmashauri ya Wilaya ya Bukoba. Majadiliano na mtafiti yalifanyika tarehe 26.2.2020 shuleni hapo.45 Amekwishatajwa46 Filipo Clemens ni mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Katerero iliyopoHalmashauri ya Wilaya ya Bukoba. Majadiliano kati ya mtafiti na watafitiwa yalifanyikatarehe26.2.2020 shuleni hapo.
70
huyu kila anapokwenda anakuwa na mtoto wake na katu hamwachi. Akisisitiza
kuhusu maudhui ya kitendawili hiki, Mwemezi47 katika mjadala alifafanua kuwa,
“kitendawili hiki kinaibua suala la mahusiano ya mama na mtoto katika mazingira
halisi ya maisha ya jamii. Mahusiano hayo yanadhihirika katika jamii zetu kwani
mama wa Kiafrika ndiye anayeonekana akijali sana kuhusu watoto wake kila wakati
kuliko baba”. Maelezo haya yanathibitisha kuwa, falsafa tunayoipata kwenye
kitendawili hiki ni ya malezi ya watoto katika jamii kwani ni jukumu la mama zaidi
ya baba. Falsafa ya uzazi na ulezi inaendelea kudhihirika katika kitendawili kingine
kinachosema:
c) Kitendawili: Bibi hutembea na mzigo wake, daima hautui chini.
Jibu: Kobe au konokono.
(Chanzo: Badru, 2015).
Japo kitendawili kinamtaja bibi, lakini ni suala la umri kwamba huyu bibi naye
alikuwa mama ambaye amefikia umri mkubwa wa kuitwa bibi. Utafiti umebaini
kuwa, kitendawili hiki kinasawiri suala la malezi ambapo bibi anawakilisha nafasi ya
mama katika malezi. Mara nyingi mama ndiye anayeonekana kulemewa na mzigo
wa malezi ya mtoto wake tangu anapozaliwa anamlea mpaka anapokuwa mtu mzima.
Kwa namna yeyote wazazi wa kike huwa tayari kufa na watoto wao katika mazingira
ya aina yeyote. Kitendawili hiki kinadhihirisha uwepo wa falsafa ya Kiafrika ya
uzazi na malezi. Aidha, kitendawili kingine ni kile kinachosema:
d) Kitendawili: Wakikua mama yao huwatupa nje kwa kishindo.
Jibu: Mbaazi au mnyonyo.
(Chanzo: Badru, 2015).
Katika kukichunguza kitendawili hiki, tumebaini uwepo wa falsafa ya Kiafrika juu
ya uzazi na malezi. Falsafa hii inasisitiza juu ya kuwa na watoto ambao wanapaswa
kupewa malezi bora. Medadi48 katika mjadala anafafanua maudhui ya kitendawili
hiki kwa kusema kuwa:
47 Venezuela Mwemezi ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Kashai iliyopomanispaa ya Bukoba. Majadiliano na watafitiwa hao yalifanyika tarehe 25.2.2020 shuleni hapo.48 Dicksoni Medadi ni mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Katerero iliyopoHalmashauri ya wilaya ya Bukoba. Majadiliano na watafitiwa yalifanyika tarehe 26.2.2020 shulenihapo.
71
Tukikitazama kitendawili hiki, tunabaini wazi uwepo wa falsafa yauzazi na ulezi. Hapa tunaona namna wazazi (mama)wanavyohakikisha malezi ya watoto kuwa yako sawa ndipo huwaachaili wakajitegemee. Hii ina maana kuwa wakiwa wadogo wanakuwakatika uangalizi wa mama mpaka pale watakapokuwa wakubwa nakuweza kujitegemea.
Maelezo katika nukuu hiyo yanaonesha namna kitendawili hiki kinavyosawiri falsafa
ya ulezi wa watoto na kwamba, watoto hao tangu wakiwa wadogo, wanakuwa katika
mikono ya malezi ya mama zao.
Kwa kuhitimisha hoja hii, utafiti umebaini baadhi ya vitendawili vya Kiswahili
vinavyosawiri falsafa ya uzazi na malezi. Falsafa hii inasisitiza umuhimu wa jamii
kuwa na watoto na pia, watoto hao kupewa malezi bora. Aidha, kupitia nadharia ya
Kisosholojia katika msingi wake unaosisitiza kuwa, fasihi haiwezi kujitenga na jamii
ambayo kwayo imechipuzwa; tumeweza kuthibitisha kuwa, falsafa ya Kiafrika
haitoki katika ombwe, bali hutoka katika jamii husika. Hii ni kwa sababu vitendawili
tulivyovitumia katika hoja yetu vimedhihirisha suala la malezi ya watoto katika jamii
za Kiafrika kuwa ni jukumu la mama zaidi kuliko baba. Kwa hiyo, vitendawili hivi
ni mali ya jamii kwani yanayozungumzwa ndani yake yanahusu jamii husika. Hivyo,
tunaweza kuhitimisha hoja zetu kwa kusema kuwa, falsafa mbalimbali zilizojadiliwa
katika sehemu hii zimedhihirika vema katika vitendawili vya Kiswahili.
4.4 Athari za Falsafa ya Kiafrika kwa Jamii Kama Inavyosawiriwa katika
Vitendawili vya Kiswahili
Athari za falsafa ya Kiafrika zimeweza kuthibitika kupitia matendo mbalimbali ya
jamii. Kila jambo linalofanywa na jamii kwa kuzingatia mila na desturi za Waafrika
linaakisi falsafa yao. Kupitia mahojiano, pamoja na vitendawili vilivyochambuliwa
na kusawiri falsafa ya Kiafrika, mtafiti ameweza kutathmini athari zitokanazo na
falsafa ya Kiafrika kwa jamii kama zinavyosawiriwa katika vitendawili vya
Kiswahili. Athari hizo zipo katika namna mbili yaani uzuri na ubaya wake. Mtafiti
ameziita athari chanya kwa upande wa yale mazuri na athari hasi kwa upande wa
ubaya. Ufafanuzi kuhusu athari hizo ni kama ifuatavyo:
72
4.4.1. Athari Chanya za Falsafa ya Kiafrika kwa Jamii
Fasihi ni zao la jamii hivyo, chochote kinachosawiriwa katika kazi za fasihi ni kwa
ajili ya jamii. Inaweza kuwa ni katika kuonya, kuelimisha au kukosoa jamii katika
mambo mbalimbali. Kupitia vitendawili vya Kiswahili, utafiti huu umebaini kuwa,
falsafa ya Kiafrika ina athari kubwa kwa jamii. Miongoni mwa athari hizo ni kama
vile kuhifadhi na kurithisha amali za kitamaduni za jamii husika, kudumisha umoja
na mshikamano miongoni mwa wanajamii, kulinda maadili ya jamii. Maelezo
yaliyoko hapa chini ni ufafanuzi wa athari chanya za falsafa ya Kiafrika kama
inavyosawiriwa katika vitendawili vya Kiswahili.
4.4.1.1 Inasaidia Kudumisha Umoja na Mshikamano
Utafiti huu umebaini kuwa, falsafa ya Kiafrika inayopatikana katika vitendawili vya
Kiswahili inasaidia kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwa wanajamii. Hii
inatokana na sababu kwamba, matukio mbalimbali ya kijamii yanayotokea kama
misiba au sherehe huifanya jamii nzima kuweza kushiriki katika shughuli hizo. Kwa
mfano kifo kama kipengele kimojawapo cha falsafa ya Kiafrika huwakumbusha watu
kukumbuka uhalisia wa jambo lenyewe na hivyo kuwahamasisha kushiriki kwa dhati.
Kwa kuwa wao ni binadamu ni binadamu na wanaamini ipo siku nao watafikwa na
umauti au wapendwa wao watapoteza maisha na hivyo, watahitaji msaada wa watu
wengine. Jambo hili lilithibitishwa na Bw. Jonas49 anaposema:
Masuala haya ni endelevu kwa sababu tangu mababu zetuwamekuwa wakiishi kwa misingi hii. Mta akipata tatizo wanajamiitunasaidiana kulitatua. Akiwepo mtu asiyeshirikiana na wenzakebasi jamii humtenga kwa maana kwamba mtu huyo atakapopatwana tatizo lolote hatapata ushirikiano mzuri kutoka kwa wenzake.Kutokana na adhabu hii humfanya mtu huyo kubadilika na kuishikulingana na taratibu ambazo jamii imejiwekea.
Maelezo katika nukuu hiyo yanathibitisha kuwa, jamii hushinikiza watu kushirikiana
katika kutatua matatizo mbalimbali ya kijamii. Kwa kufanya hivyo, wanadumisha
umoja na mshikamano na kuwafanya wanajamii kushiriki kikamilifu katika shughuli
mbalimbali za kijamii zinazotokea katika jamii yao. Kwa hiyo, suala la umoja na
ushirikiano kwa jamii za Kiafrika huendelea kudumishwa kwa njia hiyo. Hii
49 Bw. Philbert Jonas ni mwanajamii na mtumishi wa kiroho katika Taasisi ya Adolph KolpingSocieties of Tanzania Jimbo Kuu la Katoliki Bukoba. Mahojiano na mtafiti yalifanyika tarehe2.3.2020 mtaa wa Kamizilente- Rwamishenye.
73
inatokana na kaida walizojiwekea ambazo kila mwanajamii huishi kwa misingi ya
taratibu hizo.
Aidha, suala la kudumisha umoja na mshikamano kama linavyodhihirika katika
kitendawili kilichojadiliwa kipengele 4.3.1 uk 49 kinaonesha kuwa suala la umoja na
ushirikiano katika jamii ni nguzo katika kufanikisha kukamilika kwa jambo fulani
kwa muda mfupi. Jambo hili lilibainishwa pale Bi. Tiimanywa50 alipoeleza kuwa,
“Faida ya kufanya kazi kwa kushirikiana ni pamoja na kufikia mafanikio kwa muda
mfupi. Kazi inayofanywa na kundi la watu lililoungana haiwezi kulingana na mtu
mmoja. Hivyo basi, hapa tunasisitizwa kufanya kazi kwa kushirikiana ambapo kwa
kufanya hivyo tunadumisha na kuuendeleza umoja wetu. Kitendawili kingine chenye
falsafa ya Kiafrika kinasema:
50 Atugonza Tiimanywa ni mwanajamii na mfanyabiashara katika wilaya ya Bukoba. Anaishi katikamtaa wa National Housing kata ya Kashai. Mahojiano kati yake na mtafiti yalifanyika tarehe 2.3.2020ofisini kwake.
74
a) Kitendawili: Nina wanangu watatu, mmoja akiondoka wawili
hawafanyi kazi.
Jibu: Mafiga.
(Chanzo: Salla, 2014).
Suala la umoja na ushirikiano linalojitokeza katika kitendawili hiki inasababisha
athari katika kudumisha umoja huo ili kuleta maendeleo ya jamii. Kitendawili
kinaonesha kuwa, watoto hawa watatu wanaishi kwa kutegemeana na kila mmoja
ana nafasi katika maisha ya mwingine. Vivyo hivyo, katika jamii ya Waafrika, Bw.
Byabato51 alifafanua kuwa, “kila mtu ana nafasi yake katika maisha ya mtu
mwingine kiasi kwamba akiondoka wanaobaki hawawezi kufanya kazi hiyo kwa
ufanisi”. Hapa tunaona kuwa tunapoungana tunakuwa na uwanja mkubwa wa kufikia
mafanikio ukilinganisha na kutoungana.
Katika kuhitimisha hoja hii tunaweza kusema kuwa, mojawapo ya athari ya falsafa
ya Kiafrika katika jamii ni pamoja na kusisitiza umoja na mshikamano. Jamii
inapaswa kufanya kazi kwa kushirikiana ili kufikia mafanikio haraka na kwa ufanisi
zaidi. Kwa hiyo, ni vizuri kuendeleza falsafa hii kutoka kizazi kimoja kwenda
kingine ili kuifanya jamii ya Waafrika kunufaika nayo. Hivyo basi, katika utafiti
wetu tumeona kuwa falsafa ya Kiafrika inayo athari kubwa katika jamii hasa katika
kudumisha umoja na mshikamano.
4.4.1.2 Inasaidia Kulinda Maadili ya Jamii
Utafiti umebaini athari nyingine za falsafa ya Kiafrika kwa jamii ambayo ni kulinda
na kuikuza jamii katika maadili yanayofaa. Imebainishwa katika utafiti huu kuwa,
kila mtu, jamii au taifa kwa ujumla hutakiwa kuwa na maadili mema na huishi kwa
misingi ya maadili ya jamii. Utafiti umegundua kuwa, vipengele mbalimbali vya
falsafa ya Kiafrika vinavyojitokeza katika vitendawili vya Kiswahili husaidia katika
kulinda maadili ya jamii kwa kuikumbusha jamii kuzingatia kanuni na taratibu
zilizowekwa. Kukumbusha huku ndiko huifanya jamii kuwa na maadili mema pindi
wanapozifuata taratibu hizo. Kwa mfano katika kitendawili kilichojadiliwa kipengele
4.3.2 uk 53 kimejikita katika imani kuwa ndugu wa damu kwa Waafrika hawaoani
51 Amos Byabato ni mwanajamii wa wilaya ya bukoba anayeishi kata ya Hamugembe mtaa waomukishenye. Mahojiano kati yake na mtafiti yalifanyika tarehe 5.3.2020 nyumbani kwake.
75
wala kuwa na uhusiano wa kimapenzi. Hivyo, suala la miiko ambayo inatokana na
uzingatizi wa maadili ya jamii katika suala la ndoa na mahusiano kama
inavyojitokeza katika kitendawili hicho linaifanya jamii kuwa na hofu juu ya
masuala ya mahusiano na ndugu. Kama ilivyofafanuliwa na Bw. Rwekaza52 (k.h.j)
kuwa, “kwa kufanya hivyo siku zote watoto wa Kiafrika wamekuwa wakiishi kwa
kuheshimu maadili hayo kuwa, dada au kaka hata awe mzuri kiasi gani haupaswi
kumfikiria katika masuala ya kimapenzi ni katazo katika jamii ya Kiafrika”. Kwa
hiyo, jamii inaishi kwa kufuata misingi ya maadili hayo na hivyo, kuikuza jamii
katika maadili yanayofaa. Mfano mwingine wa kitendawili ni kile kinachosema:
a) Kitendawili: Nimeuona mti mmoja mzuri lakini kuukata nashindwa.
Jibu : Dada yako.
(Chanzo: Salla, 2014).
Kitendawili hiki kinaeleza kuhusu mti mzuri ambao msemaji ameuona, lakini anakiri
kushindwa kuukata mti huo. Maswali yanayozuka katika hili ni kuwa kwa nini
ashindwe kuukata? Je huo ni mti wa aina gani? Jibu linalotolewa linajibu maswali
tuliyojiuliza kwa sababu huenda kutokana na kuzingatia maadili ya Kiafrika ndio
maana msemaji anasema hawezi kuukata mti huo akimaanisha kuwa hawezi kuwa na
mahusiano ya kimapenzi na ndugu yake huyo. Kwa kuendelea kufuata miiko hii,
ndiyo kunaifanya jamii kulinda maadili yao.
Aidha, kupitia mahojiano na watafitiwa walieleza kuwa, masuala ya kimaadili
huenda sambamba na kushika imani ya dini. Kwa hiyo, watu wakishika dini
hawawezi kufanya matendo maovu. Bw. Rwegasira53 (k.h.j) anathibitisha jambo hili
kwa kusema kuwa,
Katika jamii za Kiafrika watu wengi wameshika imani ya diniijapokuwa wanaonekana kutokuacha mizizi ya dini zao za jadi.Watu wengi wanashiriki ibada za kumwabudu mwenyezi Mungu.Mambo haya ni miongoni mwa nguzo zinazoshikilia falsafa yaKiafrika. Kushiriki katika masuala ya ibada husaidiakuwaunganisha na Mungu wao na kwa kuwa, wanaamini kuwaMungu ndiye mwenye nguvu na mamlaka iliyo kuu, basi
52Hasimu Rwekaza ni mwanajamii katika wilaya ya Bukoba kata ya Hamugembe mtaa wa Nyangoye.Mahojiano kati yake na mtafiti yalifanyika tarehe 4.3.2020 nyumbani kwake.53 Keshatajwa hapo awali. Mahojiano na mtafiti yalifanyika tarehe 6.3.2020.
76
wanadamu wanapaswa kutenda kulingana na matakwa ya Mungu.Wakifanya kinyume wataadhibiwa na Mungu. Hii inasaidia katikakutenda mambo mema ya kimaadili na kuepuka kutenda maovu.
Maelezo katika nukuu hii yanathibitisha kuwa, watu wanaoshika dini kikamilifu
wapo mstari wa mbele katika kutenda matendo mema na maisha yao hujengeka
katika misingi ya kimaadili. Kwa kufanya hivyo, wanalinda maadili ya jamii na
kuikuza jamii katika maadili yanayofaa.
Kwa kuhitimisha hoja hii, tunaweza kusema, falsafa ya Kiafrika ina athari chanya
katika maisha ya jamii. Kulingana na athari hiyo, ndiyo maana falsafa hii imeendelea
kurithishwa kizazi kimoja kwenda kingine. Falsafa ya Kiafrika inasaidia katika
kulinda na kuendeleza maadili mema ndani ya jamii ili kuleta amani. Jamii yeyote
iliyo na amani hutokana na uimara wa maadili yaliyopo ambayo yanaifanya jamii
hiyo kuepukana na vitendo viovu kama wizi, ukabaji, umalaya, na mambo mengine
yanayofanana na hayo. Hivyo basi, tunaweza kusema kuwa ufafanuzi wa hoja hii
hapo juu ni ithibati kuwa, falsafa ya Kiafrika ina athari chanya kwa jamii ya Kiafrika.
4.4.1.3 Inasaidia Kutambulisha Jamii ya Waafrika Ndani na Nje ya Afrika
Maelezo na ufafanuzi kuhusu falsafa ya Waafrika kwa ujumla yameweza
kuwapambanua waafrika katika mawanda mapana ya kiutamaduni. Waafrika
(Wabantu) wamejibainisha kupitia falsafa waliyonayo inayopambanua imani na
mitazamo yao katika vipengele mbalimbali vya falsafa. Utafiti umebaini kuwa,
falsafa ya Kiafrika kama ilivyosawiriwa katika vitendawili vya Kiswahili inasaidia
watu kupata elimu kama mojawapo ya njia ya kufundisha jamii nyingine kuhusu
mawazo na mitazamo ya Waafrika juu ya mambo mbalimbali. Kwa mfano masuala
ya uduara, maadili, “uchawi na ushirikina”, uzazi na ulezi, kifo na maisha baada ya
kifo ni mambo yanayowashughulisha sana Waafrika. Mathalani, kitendawili
kinachosawiri suala la maadili lilichojadiliwa katika kipengele 4.3.2 (uk 54)
kinatambulisha suala la maadili ya Waafrika yanayowakataza kuwa na mahusiano ya
kimapenzi na ndugu wa damu. Aidha, mawazo haya yanashadidiwa na Bw. Katto54
anapoeleza kuwa:
54 Bw. Vedasto Katto ni mwanajamii wa wilaya ya Bukoba anayeishi kata ya Hamugembe mtaa waomukishenye. Mahojiano kati yake na mtafiti yalifanyika tarehe 2.3.2020 nyumbani kwake.
77
Jamii inatambua kuwa ndugu wa damu hawawezi kuoana. Ikifikiasuala la kuoa, kijana anatakiwa kumtafuta mtu wa koo tofauti kabisana akishampata anatakiwa kuwataarifu wazee ili apate ruhusa yaokama anaweza kumwoa huyo mtu au la. Hii inasaidia kulinda maadiliili vijana wasije wakaoa ndugu zao mwisho wa siku ikawa aibu nalaana kwa familia.
Maelezo katika nukuu hiyo yanadhihirisha miiko ya Waafrika katika masuala ya
ndoa na mahusiano na hivyo, yanatambulisha falsafa ya maadili ya Kiafrika kwa
Waafrika wenyewe na kwa jamii nyingine zisizo za Kiafrika. Kwa hiyo falsafa ya
Kiafrika ina athari katika kutambulisha jamii za Kiafrika ndani na nje ya Afrika kwa
ujumla.
4.4.1.4 Inasaidia Kuhifadhi na Kurithisha Amali za Kitamaduni za jamii
Utafiti huu umebaini kuwa, falsafa ya Kiafrika inasaidia katika kutunza na kurithisha
amali za jamii kama vile mila na desturi. Mlacha (1996) anaeleza kuwa, usambazaji
na utunzaji wa mila na desturi unaweza kufanyika kwa njia nyingi na kwa viwango
tofauti. Njia hizo zaweza kuwa kwa mapokezi ya mdomo au kwa maandishi.
Utunzaji na usambazaji huo unaweza kuwa kwenye kiwango cha familia moja, kwa
jamii moja au hata baina ya jamii moja na nyingine. Matokeo ya utafiti huu
yamebaini kuwa, athari hii ya falsafa ya kuhifadhi na kurithisha amali za
kiutamaduni imeweza kuthibitika kutokana na mifano ya vitendawili mbalimbali
iliyojadiliwa katika kipengele 4.3. Aidha, kupitia mahojiano na watafitiwa, suala hili
limethibitika pale Bw. Rwezaula55 anapoeleza kuwa, watoto wa jamii za Kiafrika
wanalelewa katika misingi ya dini ambao humo hufunzwa kutii na kuheshimu wazazi.
Anasema:
Suala la utii linaenda sambamba na heshima kwani kuwezi kutiikama hujamheshimu mtu huyo. Kupitia dini watoto wanafunzwakutii na kuheshimu wazazi wao na watu wanaowazidi umri. Hiiinawajengea unyenyekevu na kutokuwa na kiburi. Vilevile utii kwaupande wa wakubwa unajitokeza katika shughuli mbalimbali zakijamii zinazojitokeza. Imejengeka kasumba kuwa mtu apatapotatizo tunasaidiana kulitatua tatizo hilo na kwa namna hiyo tunatiikulingana na utaratibu tuliojiwekea.
55 Bw. Kamugisha Rwezaula ni mwanajamii wa wilaya ya Bukoba. Aliwahi kuwa mtumishi wa ummakatika Ofisi ya Kata ya Kibeta mtaa wa Magoti; pia ni mzee wa kimila. Mahojiano na mtafitiyalifanyika tarehe 2.3.2020 mtaa wa Kamagera – Kibeta.
78
Maelezo katika nukuu hiyo ni ithibati tosha kuwa, falsafa ya maadili inayo athari
yake inayoonekana kwa jamii za Kiafrika zinazoishi kwa kufuata mila na desturi zao.
Jamii za Kiafrika zinatambua kwamba, vijana hawawezi kutimiza wajibu wao
endapo hawataandaliwa vema. Hivyo basi, katika jamii suala la kurithisha amali za
jamii limekuwa endelevu. Kizazi kilichopo kimerithishwa falsafa ya jamii hiyo na
hutegemewa kuendelea kurithisha amali hizo za kifalsafa kwa vizazi vinavyofuata
kupitia vitendawili vya Kiswahili.
4.4.1.5 Inasaidia wanajamii kushika imani ya dini
Mbali na maadili, suala la imani katika Mungu na mizimu kama kipengele
kimojawapo cha falsafa ya Waafrika kimeelezwa kuwa na athari chanya kwa jamii.
Utafiti huu umebaini kuwa, wanajamii wa wilaya ya Bukoba ambao ni kiwakilishi
cha jamii za Waafrika wameshika imani ya dini ya Kikristo na Kiislamu. Pia, wapo
wanaoamini katika mizimu. Mbali na kushiriki katika ibada kwenye makanisa na
misikiti yao, wamekuwa pia wakiomba mizimu. Hivyo, kupitia imani kuwa yupo
Mungu, na kwa kuwa wanatambua kuwa Mungu ndiye mwenye nguvu na mamlaka
iliyo kuu, basi wanadamu hutenda kulingana na matakwa ya Mungu. Kwa mfano
kitendawili kinachobainisha falsafa ya imani katika Mungu katika kipengele 4.3.4
(uk 62) kinaonesha namna Waafrika wanavyoishi kwa kutambua kuwa Mungu ndiye
mwenye mamlaka iliyo kuu, hivyo inamlazimu mwanadamu kutii na kufuata
mapenzi ya Mungu ambayo yanajengwa katika misingi ya mambo mema
yanayokubalika. Pia, wanatambua kuwa Mungu na wahenga wanaona kila jambo
baya au zuri analofanya mwanadamu kwa hiyo yule anayetenda mabaya ataadhibiwa
na wahenga hao. Hii inasazidia wanajamii wengi kuishi kwa kufuata misingi sahihi
ya jamii na kuogopa kukiuka taratibu za jamii yao kwa hofu ya kupewa adhabu kali
na wahenga. Kupitia imani hizo, inawafanya wanajamii hao washike kikamilifu
imani ya dini na hivyo kutenda mamtendo mema yanayokubalika katika jamii.
4.4.2. Athari Hasi za Falsafa ya Kiafrika kwa Jamii
Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwa, falsafa ya Kiafrika kwa upande
mwingine huweza kusababisha athari hasi kwa jamii. Miongoni mwa athari hasi hizo
ni kuchochea vitendo vya uvunjifu wa amani, kukwamisha maendeleo ya jamii na
kuendeleza ukoloni. Ufuatao ni ufafanuzi wa athari hizo kama zinavyojitokeza katika
vitendawili vya Kiswahili.
79
4.4.2.1. Kuchochea Vitendo vya Uvunjifu wa Amani katika Jamii
Utafiti umebaini kwamba, imani kuhusu masuala yahusuyo “uchawi” na “ushirikina”
huweza kusababisha uvunjifu wa amani kwa baadhi ya jamii za Kiafrika. Kupitia
mahojiano na watafititwa pamoja na vitendawili mbalimbali, utafiti umebaini kuwa,
jambo hili linatokana na sababu kwamba, watu wenye hasira kali wamekuwa
wakijichukulia sheria mkononi kwa kuwaua watu wanaohisiwa kuwa wachawi kama
vikongwe. Pia, mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yanatokana na sababu za
“kishirikina” zinazohusisha watu wanaofanya ramli chonganishi. Kuwepo kwa imani
ya “uchawi” kunachochea maovu kutendeka ndani ya jamii juu ya wahusika wa
“uchawi” na “ushirikina”. Masuala ya uchawi kama yalivyodhihirika katika
kitendawili kilichojadiliwa katika kipengele 4.3.6 (uk 67) yanaonesha kuwa uchawi
na wachawi hawakubaliki na wanapingwa katika jamii. Pindi wanajamii
wanapobaini kuwa mtu fulani ni mchawi huweza kumshambulia na kumdhuru.
Matokeo ya jambo hili huweza kusababisha umwagaji wa damu wa watu wasio na
hatia kwani uchawi hauonekani na hauwezi kuthibitika kisayansi. Iwapo kila mmoja
atajichukulia sheria ya kumdhuru mwanadamu mwenziwe anayemhisi kuwa ni
mchawi huweza kusababisha kupotea kwa amani. Aidha, matokeo ya utafiti huu
kupitia mahojiano yalibainisha kuwa, suala la uchawi halikubaliki na linachangia
katika kuchochea vitendo vya uvunjifu wa amani katika jamii. Haya yanathibitika
pale Bi. Mnyambo56 anaposema:
Imedhihirika katika jamii ya Tanzania baadhi ya mikoa yakitokeamauaji ya wazee na vikongwe waliodhaniwa kuwa wachawi kwasababu mbalimbali. Vilevile, imani kuhusu masuala yanayohusuushirikina yamesababisha kutokea kwa matukio mbalimbaliyanayohusu mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino)kutokana na sababu za kishirikiana na ramli chonganishi zawaganga wa jadi wasiokuwa na maadili. Pia wapo walewanaotafuta utajiri kupitia njia za kishirikina. Kutokana na kutakautajiri wa haraka wengi wao wamejikuta wakiwauwa ndugu zao ilikupata mali. Matokeo ya hili ni kupoteza nguvu kazi ya jamiikutokana na mauaji hayo. Masuala haya yalihusishwa na imani zakishirikina za watu wachache katika kupata utajiri. Pindi inapokujakujulikana kuwa kuna mtu kama huyo anayeua ndugu zake kwaajili ya mali huweza kupewa adhabu na hata kumuua.
56 Bi..Schola Mnyambo ni mwanajamii, mama wa familia na mjasiriamali mdogo wa wilaya yaBukoba. Mahojiano kati yake na mtafiti yalifanyika tarehe 6.3.2020 mtaa wa Kamagera- Kibeta.
80
Maelezo katika nukuu hiyo yanaonesha kuwa, masuala ya uchawi katika jamii
hayakubaliki na hivyo uwepo wa wachawi unasababisha au kuchochea vitendo vya
uvunjifu wa amani na kupelekea mauaji. Kwa namna hiyo, tunaona falsafa hii ya
“uchawi na ushirikina” inasababisha uvunjifu wa amani ndani ya jamii.
4.4.2.2 Kukwamisha Maendeleo ya Jamii
Athari mojawapo inayosababishwa na falsafa ya ““uchawi na ushirikina”” katika
jamii ni kukwamisha maendeleo ya jamii. Utafiti umebaini kwamba, jambo hili
linatokana na hofu ya baadhi ya wanajamii kuhusu masuala yahusuyo uchawi.
Wachawi wengi hawapendi maendeleo ya watu wengine ndio maana suala la
“uchawi” halikubaliki katika jamii. Kwa mfano, kama kitendawili kilivyofafanuliwa
katika kipengele 4.3.6 (uk 68) kinaonesha kuwa uchawi haukubaliki katika jamii za
Kiafrika na hivyo unapingwa vikali. Baadhi ya watu waishio kwenye vijiji ambavyo
watu wake wanashikilia masuala ya “uchawi” huogopa hata kujenga nyumba nzuri
huko vijijini kwa kuhofia kulogwa. Kwa asilimia kubwa, “uchawi” unapotumiwa
vibaya huleta madhara makubwa ndani ya jamii. Madhara hayo ni pamoja na
upotevu wa mali, mauaji, magonjwa, kukosekana kwa amani na mambo mengine
yanayofana na hayo. Pia, hofu kuhusu kifo inaweza kukwamisha maendeleo ya jamii
kwani mtu anaweza kuhofia kufanya vitu vya maendeleo kwa imani kuwa atakufa na
kuziacha mali zote alizozichuma. Falsafa hii siyo nzuri kwa msakabali wa maendeleo
ya jamii kwani, kuufuata mtazamo huu wa kifalsafa kunaweza kurudisha nyuma
maendeleo ya jamii.
Hapa tunajifunza kuwa, falsafa ya Kiafrika kuhusu masuala ya “uchawi na
ushirikina” bado yanafanya kazi katika jamii na hivyo kusababisha athari kwa namna
moja au nyingine. Kutokana na maelezo haya tunaona ni jinsi gani falsafa ya
Kiafrika (““uchawi na ushirikina””) inasababisha madhara kwa jamii na kurudisha
nyuma maendeleo ya jamii. Athari hii pia, inaweza kutokea kutokana na falsafa ya
imani kuhusu kifo kama ilivyofafanuliwa hapo juu.
4.4.2.3 Inasababisha Hofu na Mashaka kwa Wanajamii
Utafiti huu umebaini kuwa, falsafa inayohusu “uchawi na ushirikina” kama
ilivyosawiriwa katika vitendawili vya Kiswahili inaweza kusababisha hofu na
mashaka kwa jamii hasa kwa kuhofia kuwa wachawi wanaweza kutumia nguvu zao
81
na kuja kuwaroga pindi wafanyapo mambo makubwa kuwashinda wao kwa kuwa
wachawi hawapendi maendeleo ya watu wengine. Kwa mfano katika kitendawili
kilichofafanuliwa katika kipengele 4.3.6 uk 67 imedhihrika kuwa wachawi hufanya
shughuli zao za kichawi nyakati za usiku kwa kuwa ni jambo ovu ambalo
halikubaliki ndani ya jamii. Kwa hiyo, wanajamii huwa na hofu kutembea nyakati
hizo au hata wakilala huomba ulinzi wa Mwenyezi Mungu dhidi yao wakiamini
kuwa wachawi wanaweza kuja kuwadhuru wakati wakiwa wamelala. Pia, imani za
kishirikina zinazohusisha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino)
zinasabaisha watu hao kuishi kwa hofu na mashaka katika jamii. Akitolea mfano
katika mahojiano Bi. Mnyambo57 (k.h.j) katika suala hili anasema kuwa, “baadhi ya
wanafamilia wenye mtoto mwenye ulemavu wa ngozi wamekuwa wakiishi kwa
mashaka wakijua kuwa mtoto wao anaweza kukamatwa na watu wanaotumwa
kupeleka viungo vya albino kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya kupata utajiri.”
Hali hii inasababisha watu wengine kukimbia makazi yao na kwenda kuishi mbali
kwa kujificha ili wasionekane. Kwahiyo, kupitia imani hizi za kishirikina huwafanya
wanajamaii kuishi kwa hofu na mashaka kama athari hasi ya falsafa ya Kiafrika.
Kwa jumla mawazo haya yanashadidiwa na nadharia ya Kisosholojia kupitia msingi
wake unaoona kuwa, fasihi haiwezi kujitenga na jamii kwani dhima yake ni
kuyamulika matendo ya jamii na kuyaweka bayana. Hivyo, kupitia vitendawili vya
Kiswahili tumeweza kubaini mawazo, imani na mitazamo mbalimbali ya Waafrika
juu ya mambo mbalimbali. Aidha, mitazamo hiyo ina athari kwa jamii kama utafiti
huu ulivyotathmini hapo juu. Athari za falsafa ya Kiafrika kupitia vitendawili
huzikumba jamii moja kwa moja kwa kuwa falsafa hizo ni amali ya jamii.
4.5 Muhtasari wa Sura ya Nne
Sura hii imejadili kwa kina matokeo ya data zilizokusanywa uwandani na maktabani
kutokana na malengo matatu mahsusi ya utafiti huu. Lengo kuu la utafiti huu
lilikuwa ni kuchunguza usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika semi: mifano kutoka
vitendawili vya Kiswahili. Mjadala wa matokeo ya utafiti huu umejikita katika
malengo matatu mahsusi. Nayo ni; Mosi, kubainisha vijenzi vya falsafa ya Kiafrika
katika muktadha wa kitamaduni. Hapa utafiti umebainisha mambo mbalimbali
57 Bi..Schola Mnyambo ni mwanajamii, mama wa familia na mjasiriamali mdogo wa wilaya yaBukoba. Mahojiano kati yake na mtafiti yalifanyika tarehe 6.3.2020 mtaa wa Kamagera- Kibeta.
82
yanayofanywa na Waafrika ambayo yanaitambulisha falsafa ya Kiafrika katika
muktadha wa kitamaduni. Vijenzi hivyo vimejitokeza katika masuala ya umoja na
ushirikiano, maadili, uhai na kifo, ndoa na uzazi, dhana ya uduara, imani katika
Mungu na mizimu; na “uchawi na ushirikina”. Mambo hayo kwa ujumla yanaijenga
falsafa ya Kiafrika katika muktadha wa kitamaduni.
Pili, tumejadili falsafa ya Kiafrika kama inavyojitokeza katika vitendawili vya
Kiswahili. Hapa, utafiti umejikita katika ufafanuzi wa falsafa yenyewe kwa kuonesha
imani na mitazamo ya Waafrika kuhusiana na falsafa husika huku tukithibitisha kwa
mifano mbalimbali ya vitendawili vya Kiswahili. Miongoni mwa falsafa
zilizojadiliwa ni falsafa kuhusu umoja na ushirikiano, ““uchawi na ushirikina””,
uzazi na ulezi, falsafa ya uduara, falsafa ya kifo na uhai, falsafa kuhusu maadili
katika jamii na falsafa kuhusu imani katika nguvu za Mungu na mizimu.
Aidha, lengo la tatu lilikuwa ni kutathmini athari za falsafa ya Kiafrika kwa jamii
kama zinavyosawiriwa katika vitendawili vya Kiswahili. Athari hizo zimetathminiwa
katika pande mbili yaani athari hasi na athari chanya. Athari chanya ni zile
zinazohusiana na kutunza na kuhifadhi amali za kiutamaduni, kulinda maadili ya
jamii na kudumisha umoja na mshikamano katika jamii, kutambulisha jamii ya
Kiafrika ndani na nje ya Afrika na kushika imani za kidini. Aidha, kwa upande wa
athari hasi ni pamoja na kuchochea vitendo vya uvunjifu wa amani, kukwamisha
maendeleo ya jamii na kusababisha hofu na mashaka kwa jamii. Sura inayofuata
inatoa muhtasari wa tasnifu nzima, mahitimisho pamoja na kutoa mapendekezo ya
nini kifanyike katika tafiti zijazo..
83
SURA YA TANO
MUHTASARI, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO
5.1 Utangulizi
Sura hii imejadili muhtasari wa tasnifu nzima ambapo mtafiti ameigawa katika
sehemu tatu. Sehemu ya kwanza ya sura hii inaeleza muhtasari wa tasnifu nzima,
sehemu ya pili inaonesha hitimisho na mchango wa utafiti huu katika jamii na
sehemu ya tatu inatoa maoni na mapendekezo kwa tafiti zijazo.
5.2 Muhtasari wa Tasnifu
Tasnifu hii imejadili kuhusu Usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika semi: Mifano
kutoka vitendawili vya Kiswahili. Utafiti huu umehusisha vitendawili vya Kiswahili
vinavyosawiri falsafa ya Kiafrika. Ripoti ya utafiti huu imewasilishwa katika sura
tano. Nazo ni utangulizi, mapitio ya maandiko na kiunzi cha nadharia, methodolojia,
uwasilishaji wa data na hitimisho. Utafiti huu umeonesha umuhimu wa vitendawili
kama amali za kifalsafa na hutumika katika kutunza, kuhifadhi na kurithisha amali za
kitamaduni za jamii.
Sura ya kwanza ni ya utangulizi wa tasnifu. Sura hii ya utangulizi imetoa ufafanuzi
wa vipengele muhimu katika utafiti wetu. Vipengele vilivyofafanuliwa katika sura
hii ni pamoja ufafanuzi wa istilahi muhimu zilizotumika katika utafiti, usuli wa tatizo
la utafiti na tamko la utafiti. Vipengele vingine vilivyojadiliwa ni malengo ya utafiti,
maswali ya utafiti, manufaa ya utafiti na mawanda ya utafiti.
Sura ya pili imejadili kuhusu kiunzi cha nadharia na mapitio ya maandiko
mbalimbali yaliyopitiwa na mtafiti ili kubaini pengo la utafiti huu kuhusu falsafa ya
Kiafrika katika vitendawili. Mapitio ya maandiko yamegawanywa katika makundi
matatu. Kundi la kwanza, linahusu falsafa ya Kiafrika kwa jumla, kundi la pili ni
falsafa ya Kiafrika katika fasihi na kundi la tatu ni maandiko kuhusu vitendawili vya
Kiswahili. Pia, mapengo ya utafiti yamebainishwa katika sura hiyo.
Sura ya tatu imefafanua methodolojia iliyotumika katika utafiti huu. Hii ni pamoja na
mbinu na zana mbalimbali zilizotumika. Sura imeeleza kuhusu usanifu wa utafiti,
mkabala wa utafiti, eneo la utafiti, walengwa wa utafiti, mbinu za ukusanyaji wa data,
uchanganuzi wa data, itikeli za utafiti na uhalali na uthabiti wa matokeo ya utafiti.
84
Aidha, changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa ukusanyaji data pamoja na
namna zilivyotatuliwa zimefafanuliwa katika sura hiyo.
Sura ya nne ndiyo imebeba kiini cha utafiti huu. Sura hii inajibu maswali matatu ya
utafiti huu yaliyotokana na malengo mahsusi. Sura hii imeanza kwa kufafanua
kuhusu vijenzi vya falsafa ya Kiafrika katika muktadha wa kitamaduni. Utafiti
umebaini kuwa, Waafrika wanaishi kulingana na mila na desturi za jamii. Baadhi ya
mambo wanayoyafanya katika maisha ya kila siku yanajenga au kubeba falsafa yao
katika muktadha wa utamaduni. Mambo hayo yanajitokeza katika masuala ya umoja
na ushirikiano, suala la maadili katika jamii, dhana ya uhai na kifo, dhana ya uduara,
suala la uchawi, imani katika Mungu na mizimu na suala la ndoa na uzazi. Mambo
hayo ndiyo yanaijenga falsafa ya Kiafrika.
Lengo la pili limefafanua vipengele vya falsafa ya Kiafrika vinavyojitokeza katika
vitendawili vya Kiswahili. Baadhi ya vipengele vilivyojadiliwa ni falsafa kuhusu
umoja na ushirikiano wa Waafrika. Utafiti ulibaini kuwa, Waafrika hufanya mambo
mbalimbali kwa kushirikiana miongoni mwa wanajamii. Mtu akipata tatizo,
wanajamii huchukulia tatizo hilo kama ni la jamii nzima hivyo hushirikiana kulitatua.
Vipengele vingine ni kama vile, falsafa kuhusu umuhimu wa maadili katika jamii,
falsafa ya “uchawi na ushirikina” na falsafa ya uzazi na ulezi. Kikubwa zaidi ni
katika ushirikiano wa Waafrika ambao kwa namna nyingine unasababisha kuwa na
sura ya uduara kwa vitu na mambo mbalimbali ya kijamii wanayoyafanya. Uduara
wa Waafrika umejidhihirisha kupitia vitendawili vya Kiswahili wanavyovitumia
katika mazingira yao. Baadhi ya vitu vinavyotajwa katika vitendawili kama vile
nyumba na ngoma ni vya umbo la duara.
Aidha, lengo la tatu limejadili kuhusu athari za falsafa ya Kiafrika kwa jamii. Falsafa
ya Kiafrika ina athari nyingi kwa jamii kama zilivyofafanuliwa katika utafiti huu.
Mtafiti amefafanua athari za falsafa ya Kiafrika kwa jamii kama vile kutunza na
kuhifadhi amali za kitamaduni za jamii, kulinda maadili yanayofaa, kudumisha
umoja na mshikamano katika jamii, kuitambulisha jamii ya Waafrika na kushika
imani ya dini. Kwa upande mwingine, athari hasi za falsafa ya Kiafrika ni kama
kuchochea vitendo vya uvunjifu wa amani, kukwamisha maendeleo ya kijamii na
kusababisha hofu na mashaka kwa jamii.
85
Sura ya tano ya tasnifu hii imejadili kuhusu muhtasari wa kazi nzima kwa ufupi
ambapo muhtasari huo umefafanua mwelekeo wa sura moja baada ya nyingine
zinazounda tasnifu hii. Aidha, hitimisho lililotolewa limejikita katika kueleza
mchango wa utafiti huu kwa jamii. Mwisho, ni mapendekezo yaliyotolewa juu ya
nini kifanyike katika jamii na kwa wanazuoni kwa jumla katika kutoa mchango wa
kuikuza na kuiendeleza sanaa ya vitendawili.
5.3 Hitimisho
Kutokana na matokeo ya utafiti huu, ni wazi kuwa dhana hasi ya baadhi ya
wataalamu kuhusu umuhimu wa vitendawili imepanuka. Hivyo, jamii itaweza
kuondokana na dhana hii na kutilia maanani umuhimu mkubwa wa vitendawili
katika jamii na uga wa fasihi.
5.3.1 Mchango Mpya wa Utafiti
Utafiti huu umejikita katika kuchunguza falsafa ya Kiafrika katika vitendawili vya
Kiswahili. Tafiti nyingi zilizofanyika katika uga wa fasihi na falsafa kwa ujumla
hazikuhusisha au kutambulisha vitendawili kama amali za kifalsafa za jamii. Utafiti
huu utawafanya wanazuoni kuondokana na ile dhana ya kuwa vitendawili havina
umuhimu mkubwa kwa jamii kama ilivyo misemo na methali hivyo kuchukulia
vitendawili kama sanaa yenye lengo la kuwaburudisha watoto tu. Matokeo ya utafiti
huu yameonesha kuwa vitendawili ni nyenzo muhimu katika jamii kwani hutumika
katika kutunza na kuhifadhi amali za kifalsafa za jamii.
Pia, utafiti huu ni mojawapo ya kazi nyingi zilizowashughulisha sana wanataaluma
katika kutetea falsafa ya Kiafrika na fasihi ya Kiafrika. Maandiko mbalimbali
pamoja na utafiti huu vinathibitisha uwepo wa falsafa ya Kiafrika unaodhihirika
kupitia kazi mbalimbali za fasihi simulizi na fasihi andishi kwa jumla. Hivyo, utafiti
huu utaweza kuondoa ile dhana ya wachache wanaowabeza na kudharau Waafrika
kuwa ni watu wasio na utamaduni wao na hivyo, hawana falsafa yao. Data
zilizochambuliwa na kuwasilishwa katika utafiti huu zimeweza kubainisha vipengele
vya falsafa ya Kiafrika katika vitendawili vya Kiswahili ambavyo ni zao la uzoefu
wa maisha yao katika mazingira yao.
86
5.3.2 Utoshelevu wa Nadharia
Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Kisosholojia. Nadharia hii imetumika katika
uchambuzi wa data hadi kupata matokeo ya utafiti kwa kutumia misingi ya nadharia
hii. Msingi mkubwa wa nadharia hii ni ule unaosisitiza kuhusu uhusiano wa fasihi na
jamii na kuona kuwa, fasihi haiwezi kujitenga na jamii bali ina mfungamano
mkubwa na maisha ya jamii. Kwahiyo, jambo linalosawiriwa katika fasihi limebeba
maisha halisi ya jamii kwa jumla. Kwa maana hiyo, falsafa ya jamii ya Kiafrika
imeweza kusawiriwa vema katika vitendawili vya Kiswahili vinavyotumika katika
jamii za Kiafrika. Pia, kuhusu kazi ya fasihi kama taswira ya kimazingira na
kitamaduni ambamo kazi hiyo imechipuka utafiti umeweza kutusaidia katika kupata
vijenzi vya falsafa ya Kiafrika katika muktadha wa kitamaduni.
5.4 Maoni na Mapendekezo kwa Tafiti Zijazo
Utafiti huu ulihusisha dhana kuu mbili ambazo ni falsafa ya Kiafrika na Vitendawili
vya Kiswahili. Kwa maana hiyo, utafiti huu umekuwa ni sehemu ndogo sana katika
fasihi simulizi ambayo ina tanzu nyingi na vipera vingi ambavyo yamkini ni muhimu
zaidi na vinahitaji utafiti wa kina. Hivyo, utafiti huu, unapendekeza kuwa, wataalamu
waone umuhimu wa vitendawili vya Kiswahili na vile vya lugha za kibantu na hivyo
kutilia maanani katika kutafiti zaidi eneo hili la vitendawili. Utafiti unaweza
kufanywa kwa kuchunguza Ontolojia ya Waafrika katika vitendawili Kiswahili na
vile vya lugha za kibantu. Pia, utafiti unapendekeza kuwa, bado kuna haja ya tafiti
nyingi zaidi kufanyika katika uga wa fasihi simulizi, ili kubaini ni kwa namna gani
tanzu za fasihi simulizi zinaweza kutumika kama darasa la kufunza na kuhifadhi
maarifa ya kifalsafa ya jamii za Waafrika.
Aidha, kwa upande wa falsafa ya Kiafrika, watafiti wa baadae wanaweza
kuchunguza zaidi katika tanzu nyingine za fasihi simulizi kama vile hadithi za
Kiswahili, maigizo, na ushairi wa Kiswahili na hivyo kuisheheneza zaidi fasihi
simulizi ya Kiswahili. Pia, vipengele vya falsafa ya Kiafrika vina mawanda mapana
sana. Ni dhahiri kuwa tafiti nyingine zinaweza kufanywa kwa kuchunguza kipengele
kimojawapo cha falsafa ya Kiafrika namna kinavyojitokeza katika utanzu mwingine
wa fasihi. Kwa mfano, utafiti unaweza kufanywa kwa kuchunguza kipengele cha
uchawi na uganga ambayo ni falsafa ya Waafrika namna kinavyojitokeza katika
ushairi wa Kiswahili.
87
5.5 Muhtasari wa Sura ya Tano
Sura hii inahusu muhtasari, hitimisho na mapendekezo. Vipendele vilivyojadiliwa
katika sura hii ni utangulizi, muhtasari wa tasnifu nzima na hitimisho. Aidha,
mchango mpya wa utafiti umetolewa pamoja na utoshelevu wa nadharia. Mwisho,
sura hii imetoa mapendekezo kwa tafiti zijazo na muhtasari wa sura. Sehemu
inayofuata ni marejeleo ya kazi mbalimbali zilizopitiwa na mtafiti wakati wa
kuandika kazi hii.
88
MAREJELEO
Amana, B. (2013). Vitendawili katika http://educationkenyan.Blogspot.com/2013/11/
vitendawili.html (imepakuliwa tarehe 17/1/2020).
Anaclet, A. O na Wenzake (1979). Utamaduni chombo cha maendeleo. Dar es
Salaam: Wizara ya Utamaduni.
Babbie, E. (1999). The Basics of Social Research. Belmont: Wadisworth Publishing
Company.
Badru, Z. A. (2015). “Taswira na Ubainishaji wa Mabadiliko ya Kiujumi katika
Vitendawili: Mfano wa Vitendawili vya Kiswahili”. Tasnifu ya Shahada ya
Uzamivu ya Sayansi ya Jamii katika Fasihi ya Kiswahili (Haijachapishwa).
Chuo Kikuu cha Dodoma.
Balisidya, M. L. Y. (1973). “Fasihi ya Kiswahili”. Katika Mulika. TUKI: Chuo
Kikuu cha Dar es salaam. Na. 2 uk 12-17.
Burke, K. (1941). The Philosophy of Literary Form: Studies in Symbolic Action.
Baton Rouge, Louisiana: Louisiana State University Press.
Chuachua, R. (2010). “Suala la Itikadi katika Riwaya za Shaaban Robert”. Tasnifu
ya Shahada ya Umahiri katika Fasihi ya Kiswahili (Haijachapishwa). Chuo
Kikuu cha Dodoma.
Chuachua, R. (2016). “Falsafa ya Riwaya za Shaaban Robert na Euphrase Kezilahabi
katika Muktadha wa Epistemolojia ya Kibantu”. Tasnifu ya Shahada ya
Uzamivu (Haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Dodoma.
Damka, A. B. (2015). “Kuchunguza Dhima ya Vitendawili vya Jamii ya Wanyisanzu
wa Iramba, Singida, Tanzania”. Tasnifu ya Shahada ya Uzamili katika Kitivo
cha Fani na Sayansi Jamii (Haijachapishwa). Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Duwe, M. (2016). “Mdhihiriko wa Falsafa ya Uduara katika Sanaa za Maonyesho za
Jamii ya Wangoni”. Tasnifu ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili
(Haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Dodoma.
89
Enon, J. C. (1998). Educational Reseach; Statistics and Measurement. Kampala:
Makerere University.
Faustine, S. (2012). “Matumizi ya Mtindo wa Uhalisiamazingaombwe katika Riwaya
Teule za E. Kezilahabi: Dhima na Athari Zake kwa Hadhira”. Tasnifu ya
Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Jamii katika Fasihi ya Kiswahili
(Haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Dodoma.
Faustine, S. (2017). “Falsafa ya Waafrika na Mtindo wa Uhalisiajabu katika Riwaya
ya Kiswahili”. Tasnifu ya Shahada ya Uzamivu katika Fasihi ya Kiswahili
(Haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Dodoma.
Fautine, S. (2019). “Falsafa ya Waafrika kama Kijenzi cha Mtindo wa Uhalisiajabu
katika Riwaya za Kiswahili.” Katika Ponera, A. S & Badru, Z. A (Wah),
Koja la Taaluma za Insia: Kwa heshima ya Prof. Madumulla. Dar es salaam:
Karljamer Publishers Ltd.
Gay, L. R. (1987). Educational Research: Competence for Analysis and Application.
Ohio: Merril Publishing House.
Gyekye, K. (1987). An Essay on African Philosophical Thoughts. Philadephia:
Combridge University Press.
Hoppenau A. na Wenzake. (2009). “Kubadilisha Tamaduni za Kijerumani na za
Kitanzania”: Katika DTP & TYC (Wah), Mwongozo wa Utamaduni. German:
vol.1. Iliyosomwa tarehe 8/9/2020 katika http://www.beyondintractability.
org/action/essay.jsp?id=26234&nid=1186.
Hountondji, P.J. (2004). “Knowledge as a Development Issue”, katika A Companion
to AfricanPhilosophy. Blackwell Publishing. Ilisomwa Tarehe 12/7/2019
katika http:// philosophy.org/archive/manamba.
Hussein, E. (1976). Kinjekitile. Nairobi: Oxford University Press.
Jengo, E. na Wenzake. (1982). Falsafa ya Sanaa Tanzania. Dar es Salaam: Baraza la
Sanaa la Taifa Tanzania.
90
Kaponda, G. J. (2018). “Ontolojia ya Kiafrika katika Mbolezi za Wanyasa.” Tasnifu
ya Shahada ya Umahiri katika fasihi ya Kiswahili (Haijachapishwa). Chuo
Kikuu cha Dodoma.
Katamba, L. (2011). “Utamaduni wa Kupeana Majina katika Jamii ya Wanyakyusa.”
Tasnifu ya Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili (Haijachapishwa).
Chuo Kikuu cha Dodoma.
Khumalo, J. S. M. (1974). “Zulu Riddles”. Katika African Studies, vol. 33, Na. 4,
Uk 193-226.
Kombo, D. K na Tromp, D, L. (2006). Proposal and Thesis Writing and Introduction.
Nairobi: Pauliness Publications.
Kothari, C. R. (2009). Research Methodology, Methods and Techniques. New Delhi:
New Age Internation Publishing Ltd.
Kothari, C. R. (2004). Research Methodology. Methods and Techniques 2 Edition.
New Delh Wiley.
Mbiti, J. S. (1969). African Religion and Philosophy. London: Morrison and Gibb
Ltd.
________ (1975). Introduction to African Religion. Heinemann: University of
Michigan
Makame, S. F. (2016). “Matumizi ya Falsafa ya Usihiri katika Riwaya Teule za
Euphrase Kezilahabi.” Tasnifu ya Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya
Kiswahili (Haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Dodoma.
91
Manala, J. M. (2004). “Witchcrafts and its Impact on Black African Christians”: A
Lacuna in the Ministry of Hervormde Kerk in Suidelike Africa. University of
South Africa. Katika http://www.researchgate.net/publication/45681425.
Ilisomwa tarehe 28.9.2020.
Menkiti, I. (1984). “Person and Community in African Traditional Thought”. Katika
R. Wright (mhariri). African Philosophy, An Introduction of Lanham. MD:
University Press of America.
Mgunda, J. M (2014). “Dhima ya Visasili katika Kuhifadhi na Kurithisha Amali za
Kitamaduni: Mifano kutoka kwa Wasukuma.” Tasnifu ya Shahada ya
Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili (Haijachapishwa) Chuo Kikuu Cha
Dodoma
Mlacha, S. A. K (1996). “Utamaduni wa Mwafrika katika Riwaya ya Bwana
Myombekere na Bibi Bugonoka.” Katika Kiango, J.G na Masabo, Z. N (Wah)
Mulika 23. TUKI: Dar es salaam.
Mlelwa, A. A (2017). “Falsafa ya Kiafrika katika Vitabu Teule vya Fasihi ya
Kiswahili: Dunia Uwanja wa Fujo na Ngoma ya Ng’wanamalundi”. Tasnifu
ya Shahada ya Umahiri katika Fasihi ya Kiswahili (Haijachapishwa). Chuo
Kikuu cha Dodoma.
Mng’aruti, T. K. (2008). Fasihi Simulizi na Utamaduni: Kitabu cha Walimu na
Wanafunzi (Shule na Vyuo). Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.
Mshana, S. K (2015). “Kuchunguza Usawiri Chanya wa Mwanamke katika
Vitendawili vya Jamii ya Wanyiha”. Tasnifu ya Shahada ya Umahiri katika
Fasihi ya Kiswahili. (Haijachapishwa) Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Mulokozi, M. M (2017). Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili. Dar es salaam:
KAUTTU
Mungah, C. I. (1999). “Dhana ya Maisha katika Novela mbili za Kezilahabi: Nagona
na Mzingile”. Tasnifu ya Shahada ya Umahiri katika Fasihi.
(Haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Nairobi.
92
Narizvi, S. (1982). The Sociology of Literature of Politics. Nairobi: Standard
Textbooks Graphics and Publishing Company.
Ponera, A. S. (2016). “Suala la Matumizi ya Nadharia kama Kiunzi cha Tafiti za
Kitaamuli: Mfano wa Matumizi ya Nadharia ya Ukanivali”. Katika Jounal of
Humanities, vol.3, The University of Dodoma.
Ponera, A. S. (2019). Misingi ya Utafiti wa Kitaamuli na Uandishi wa Tasnifu.
Dodoma: Central Tanganyika Press.
Salla, H. D. (2014). Vitendawili vya Kikwetu. Dar es salaam: African Proper
Education Network
Samwel, M. (2015). Umahiri katika Fasihi ya Kiswahili: Mwongozo kwa
Mwanafunzi na Mwalimu wa Fasihi Simulizi na Andishi. Dar es Salaam:
Meveli Publishers (MVT)
Senkoro, F. E. M. K. (1996). Nadharia ya Fasihi na Fasihi ya Kiswahili ya
Majaribio. Katika Kioo cha Lugha. Na. 2 TUKI. Dar es salaam.
Simchimba, E.A. (2012). “Falsafa ya Kiafrika katika Methali za Kiswahili”. Tasnifu
ya Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili (Haijachapishwa). Chuo
Kikuu cha Dodoma.
Stanley, A. (2018). Katika http://tamadunizetu547216239.wordpress.com.
Imesomwa tarehe24/12/2019.
Stefanova, A. (2003). “Riddles as a Community Psychological Phenomenon: Myths,
Fairy Tales, Personal Literature Art”. In folkrole, vol 35.
Stumph, S. E. & Fierser, J. (2009). Socrates to Sartre and Beyond a History of
Philosophy. New York: Mac Graw- Hill Company.
Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. (2004). Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dar-es-
salaam Tanzania: TUKI.
Taine, H. (1873). The Philosophy of Art. New York: Holt & Williams.
93
Temples, P. (1959). Bantu Philosophy. Paris: Presence Africaine.
TUKI. (2004). Kamusi la Kiswahili Sanifu. Nairobi: Oxford University Press.
Wafula, R. M. na Njogu, K. (2007). Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Jomo
Kenyata Foundation
Wamitila, K.W. (2010). Kanzi ya Fasihi: Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi.
Nairobi: Vide Muwa Publishers.
Wamitila, K. W. (2003). Kichocheo cha Fasihi Simulizi na Andishi. Nairobi: Focus
Books Publication Limited.
Wizara ya Elimu na Utamaduni. (1992). Historia ya Falsafa ya Elimu. Dar es salaam:
National Printing Company.
94
VIAMBATANISHO
Kiambatanisho 1: Miongozo ya Mijadala ya Vikundi na Mahojiano
A. Mwongozo wa Mjadala wa vikundi kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi
1. Tafadhali tutajie jina lako na umri wako.
2. Je, unasoma darasa la ngapi?
3. Je, unafahamu vitendawili ni nini?
4. Taja vitendawili kumi unavyovifahamu
5. Eleza kwa kifupi majawabu ya vitendawili hivyo
6. Je, unadhani vitendawili vina tija kwa jamii? Kama jibu ni ndio eleza kwa
ufupi kwa nini unaona vitendawili vina tija
B. Mwongozo wa Mjadala wa Vikundi kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari
1. Tafadhali ututajie jina lako na kidato unachosoma.
2. Eleza namna unavyoifahamu dhana ya vitendawili katika fasihi ya Kiswahili.
3. Taja vitendawili vya Kiswahili unavyovifahamu na ueleze majibu ya
vitendawili hivyo. Vitendawili vijikite katika mambo yafuatayo
a) Umoja na ushirikiano
b) Maadili ya jamii
c) Kifo
d) Masuala ya uzazi na ulezi
e) Dhana ya uduara
f) “uchawi na ushirikina”
4. Je, kwa mtazamo wako unadhani vitendawili vina umuhimu wowote kwa
jamii? kama jibu ni ndio eleza kwa nini?
5. Vitendawili vinatumika katika kuhifadhi amali za kitamaduni, taja
vitendawili vinavyohusiana na masuala ya kitamaduni unavyovifahamu.
C. Mwongozo wa Mahojiano kwa Wanajamii Kuanzia Miaka Hamsini na Tano
na Kuendelea
Taarifa za Mtafiti
Mtafiti ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wa ngazi ya umahiri katika
fasihi ya Kiswahili (MA KISWAHILI LITERATURE). Utafiti huu unahusu usawiri
wa falsafa ya Kiafrika katika semi: mifano kutoka vitendawili vya Kiswahili.
95
Unaombwa kutoa mchango wako kadri uwezavyo na unahakikishiwa kuwa maelezo
utakayoyatoa yatatumiwa kuleta ufanisi kwa malengo yaliyokusudiwa katika utafiti
huu tu.
SEHEMU A
TAARIFA ZA MTAFITIWA
Jina la mtafitiwa………………….
Jinsia………………………………
Umri………………………………….
Mahali unapoishi………………………
Cheo/ kazi unayofanya…………………
SEHEMU B
Maswali kwa Watafitiwa
1. Vitendawili ni nyenzo muhimu katika kutunza na kurithisha amali za
jamii, kwa maoni yako eleza namna unavyouelewa utanzu huu wa
vitendawili.
2. Kila jamii inaishi kwa kufuata mila na desturi za jamii yao. Je katika
jamii yenu ni mila na desturi zipi zinazozingatiwa sana na wanajamii?
3. Unafahamu nini kuhusu falsafa ya jamii yenu ambayo kwa jumla inaunda
falsafa ya Waafrika?
4. Eleza mambo yanayofanywa na jamii ambayo kupitia mambo hayo
masuala ya mila, desturi, tamaduni na uzoefu wa jamii hujipambanua.
5. Taja na ueleze kwa ufupi vijenzivya falsafa ya Kiafrika katika muktadha
wa utamaduni unavyovifahamu.
6. Je, unadhani falsafa ya Kiafrika inaweza kusawiriwa kupitia vitendawili
vya Kiswahili?
7. Eleza namna falsafa ya Kiafrika inavyojitokeza katika vitendawili vya
Kiswahili
8. Je, unahisi kwamba falsafa ya Kiafrika kama inavyosawiriwa katika
vitendawili vya Kiswahili inaweza kuwa na athari yoyote kwa jamii?
9. Taja athari hizo na ueleze kwa ufupi.
96
D. Mwongozo wa Udurusu wa Matini
Udurusu wa maandiko ulishughulika na usomaji wa maandiko mbalimbali
yanayohusiana na mada ya utafiti. Maandiko yaliyodurusiwa ni yale ya maktabani na
kwenye vyanzo vya kielektroniki. Udurusu wa vyanzo vya kielektroniki ulizingatia
vyanzo vinavyohusisha Taasisi zinazojulikana na kuaminika. Mwongozo wa udurusu
wa maandiko umefafanuliwa katika jedwali lifuatalo:
Vyanzo vya
Maarifa
Vipengele Vinavyodurusiwa Lengo
Vitabu, tasnifu,
makala, tahakiki,
majarida na
vyanzo vya
kieletroniki
Vitabu vya fasihi simulizi, nakala
zinazohusiana na falsafa ya
Kiafrika, tasinifu zinazohusiana na
falsafa ya Kiafrika na tasinifu za
vitendawili vya Kiswhili.
Kupata mawazo/
taarifa mbalimbali
kutoka kwa wataalamu
mbalimbali kuhusiana
na mada ya utafiti
97
Kiambatanisho 2: Orodha ya Watafitiwa
2A Mahojiano
Na Jina Jinsia Umri Mtaa
1 Boniface Rwiza Me 68 Nyamkazi
2 Mwesigwa Kigoye Me 64 Hamgembe
3 Farida Abdallah Ke 60 National Housing
4 Olivia Kokwenda Ke 58 Buyekera
5 Salma Kayanga Ke 56 Kibeta
6 Kamugisha Rwezaula Me 70 Kamagera
7 Philbert Jonas Me 57 Kamizilente
8 Bi. Theresa Ke 67 Buyekera
9 Vedasto Katto Me 56 Omukishenye
10 Scholastica Mnyambo Ke 58 Kamagera
11 Aabel Kazaula Me 58 Uswahilini
12 Audax Rwegasira Me 62 Buyekera
13 Hashim Rwekaza Me 61 Nyangoye
14 Amos Byabato Me 58 Omukishenye
15 Atugonza Tiimanywa Ke 60 National Housing
16 Jualikali Katabazi Me 58 Buyekera
17 Deogratius Bwemero Me 72 Kamizilente
18 Elizabeth Kaigara Ke 64 Kibeta Tanesco
19 Binamungu Muganyizi Me 55 Kankwila
20 Marina Katunzi Ke 63 Nyamkazi
21 Debora Mushegezi Ke 59 Uswahilini
22 Renatus Rugema Me 57 Kamagera
98
2B Majadiliano
Na. Jina Umri Jinsia Shule
1 Alexander Marwa 17 Me Kashai
2 Adelaida Theobard 16 Ke Kashai
3 Frank Emilian 17 Me Kashai
4 Dion Dickson 17 Me Kashai
5 Faustine Selestine 17 Me Kashai
6 Proscovia Projestus 17 Ke Kashai
7 Richard Egidius 16 Me Kashai
8 Dismas Azas 17 Me Kashai
9 Nicera Gosbert 17 Ke Kashai
10 Elvis Johansen 17 Me Kashai
11 Venezuela Mwemezi 17 Ke Kashai
12 Innocensia Abel 13 Me Katerero
13 Akramu Musa 13 Me Katerero
14 Nusura Zuberi 12 Ke Katerero
15 Belina Godfrey 13 Ke Katerero
16 Jasintha Josbert 13 Ke Katerero
17 Abdul Samilati 13 Me Katerero
18 Jacklina Johansen 12 Ke Katerero
19 Lidya Godwin 12 Ke Katerero
20 Happiness Edisson 13 Ke Katerero
21 Gisela Gidison 13 Ke Katerero
22 Aodatha Aodax 13 Ke Katerero
23 Timoni Eneliko 12 Me Katerero
24 Dickson Medadi 13 Me Katerero
25 Levina Gosbert 12 Ke Katerero
99
26 Filipo Clemens 13 Me Katerero
27 Amina Rhenus 13 Ke Katerero
28 Datius Chilizostom 13 Me Katerero
29 Eneliko Clophas 13 Me Katerero
30 Teodata Theodory 13 Ke Katerero
100
Kiambatanisho 3: Barua za Utambulisho wa Kufanya Utafiti
3A: Barua Kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma
101
3B: Barua Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
102
3C: Barua Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bukoba
103
Kiambatanisho 4: Picha Mbalimbali za Utafiti
Picha 1: Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Katerero iliyopo Hlamashauri ya
Wilaya ya Bukoba wakiwa wamenyoosha mikono ili kutoa jibu la
kitendawili kilichotegwa katika mjadala wa vikundi katika uwanja uliopo
nyuma ya madarasa shuleni hapo. (Utafiti, 2020)
104
Picha 2: Mtafiti akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Katerero iliyopo
Halmashauri ya wilaya ya Bukoba baada ya mjadala. (Utafiti, 2020)
105
Picha 3: Mtafiti akiwa na wanafunzi wa shule ya sekondari Kashai iliyopo Bukoba
mjini katika mjadala wa vikundi katika mojawapo ya darasa shuleni hapo.
(Utafiti, 2020)
106
Picha 4: Mtafiti akiwa kwenye mahojiano na Bw. Mwesigwa Kigoye katika kata ya
Hamgembe mtaa wa Nyangoye wilayani Bukoba. (Utafiti, 2020)
107
Picha5: Mtafiti akiandika maelezo yaliyoelezwa na Bw. Boniface Rwiza katika
mahojiano nyumbani kwa mtafitiwa katika kata ya Kashai wilayani Bukoba.
(Utafiti, 2020)