SALASALA VISION GROUP - svg.or.tz · Ofisi ya muda ya chama hiki itakuwa Jodari Club, Kiwanja Na...

18
SALASALA VISION GROUP KATIBA August, 2012 Volunteered to Edit & Formatted by: THRILLTON CONSULTING www.thrillton.co.tz

Transcript of SALASALA VISION GROUP - svg.or.tz · Ofisi ya muda ya chama hiki itakuwa Jodari Club, Kiwanja Na...

SALASALA VISION GROUP

KATIBA

August, 2012

Volunteered to Edit & Formatted by: THRILLTON CONSULTING

www.thrillton.co.tz

2 | P a g e S V G

UELEKEZO

UTANGULIZI ......................................................................................................................................................... 3

1.0 JINA NA OFISI YA CHAMA ......................................................................................................................... 4

1.1 JINA LA CHAMA ....................................................................................................................................... 4

1.2 OFISI YA CHAMA ...................................................................................................................................... 4

2.0 KANUNI .......................................................................................................................................................... 4

3.0 LENGO NA MADHUMUNI YA CHAMA ..................................................................................................... 4

4.0 SIFA ZA MWANACHAMA ............................................................................................................................ 4

5.0 KUOMBA UANACHAMA NA HAKI ZA WANACHAMA ........................................................................... 5

5.1 KUOMBA UANACHAMA ......................................................................................................................... 5

5.2 HAKI NA WAJIBU WA WANACHAMA.................................................................................................... 5

6.0 UKOMO, KUJITOA NA TARATIBU ZA KUONDOLEWA KATIKA CHAMA ................................................ 6

6.1 UKOMO WA UANACHAMA ................................................................................................................... 6

6.2 KUJITOA KATIKA CHAMA ........................................................................................................................ 6

6.3 KUONDOLEWA KATIKA CHAMA ............................................................................................................ 6

6.4 TARATIBU ZA KUONDOLEWA KATIKA CHAMA ..................................................................................... 7

7.0 MUUNDO WA CHAMA, ADA, NA MICHANGO ...................................................................................... 8

7.1 MUUNDO WA CHAMA ............................................................................................................................ 8

7.2 ADA NA MICHANGO .............................................................................................................................. 8

7.3 MAPATO NA MATUMIZI YA CHAMA ...................................................................................................... 8

7.3 KUMBUKUMBU ZA MAPATO NA MATUMIZI YA CHAMA ...................................................................... 9

7.4 UKAGUZI WA MAHESABU ........................................................................................................................ 9

7.5 MIFUKO YA KUSAIDIANA NA KULETA MAENDELEO ............................................................................. 9

7.6 KUWEKEZA KATIKA VITEGA UCHUMI ..................................................................................................... 9

8.0 MUUNDO WA UONGOZI NA MAAMUZI YA CHAMA ........................................................................... 10

8.1MUUNDO WA UONGOZI ....................................................................................................................... 10

8.2 MAAMUZI YA CHAMA ........................................................................................................................... 10

9.0 HAKI NA MAJUKUMU YA VIONGOZI ...................................................................................................... 11

9.1 HAKI YA KIONGOZI ................................................................................................................................ 11

9.2 MAJUKUMU ............................................................................................................................................. 11

10.0 WAJIBU WA VIONGOZI ........................................................................................................................... 12

11.0 VIKAO VYA CHAMA NA IDADI YA WANACHAMA ............................................................................ 13

11.1 VIKAO VYA CHAMA ............................................................................................................................ 13

11.2 IDADI YA WANACHAMA .................................................................................................................... 13

12.0. MUDA WA UONGOZI ............................................................................................................................. 14

12.1 MUDA WA UONGOZI .......................................................................................................................... 14

12.2. SABABU ZIFUATAZO NDIYO KIKOMO CHA UONGOZI ................................................................... 14

13. KANUNI ZA CHAMA................................................................................................................................... 15

3 | P a g e S V G

UTANGULIZI

Wanachama waanzilishi wa SALASALA VISION GROUP

tumekubaliana kwa pamoja kuanzisha chama hiki ambacho

kitaunganisha jitihada za wana chama katika kuleta

maendeleo ya kijamii, kiuchumi, na kiutamaduni.

Ili kutekeleza madhumuni haya, itabuniwa mipango na

mikakati ya utekelezaji na pale panapohitajika fedha,

itabuniwa miradi mbalimbali ya kuchangia mapato ili kuleta

maendeleo ndani ya chama chetu cha SALASALA VISION

GROUP.

Chama hiki hakitajihusisha kwa namna yoyote ile na mambo ya kisiasa na wala

hakitakumbatia sera na itikadi za kidini wala ukabila. Chama kitaendeshwa kwa mujibu

wa sheria za nchi, katiba ya chama, na kanuni zake.

4 | P a g e S V G

1.0 JINA NA OFISI YA CHAMA

1.1 JINA LA CHAMA

Jina la chama hiki litakuwa SALASALA VISION GROUP (SVG)

1.2 OFISI YA CHAMA

Ofisi ya muda ya chama hiki itakuwa Jodari Club, Kiwanja Na 485 Kitalu ‘E’ Mtaa wa

Kilimahewa kata ya Wazo.

2.0 KANUNI

Kanuni za chama hiki hazitapingana na katiba, endapo ikitokea kupingana katiba ndiyo itatoa

mwongozo.

3.0 LENGO NA MADHUMUNI YA CHAMA

Lengo na madhumuni ya Chama cha “Salasala Vision Group” kimsingi ni kuleta maendeleo

katika maswala ya kijamii, kiuchumi, na kiutamaduni.

4.0 SIFA ZA MWANACHAMA

I. Awe raia wa Tanzania,

II. Awe mwenye umri usiopungua miaka kumi na nane (18),

III. Awe mtu mwenye akili timamu,

IV. Awe mtu anayekubaliana na madhumuni ya chama hiki.

5 | P a g e S V G

5.0 KUOMBA UANACHAMA NA HAKI ZA WANACHAMA

5.1 KUOMBA UANACHAMA

Muombaji wa uanachama atajaza fomu ya maombi na kudhaminiwa na wanachama wawili.

Maombi yatapokelewa na katibu na kuratibiwa na sekretariati ambayo itafanya tathmini na

kuandika mapendekezo ya kukubaliwa au kukataliwa na kisha kuyawasilisha kwenye mkutano

wa kawaida wa chama kutokana na ratiba itakavyopangwa. Mkutano wa kawaida ndio

utaamua juu ya maombi ya uanachama.

5.2 HAKI NA WAJIBU WA WANACHAMA

5.2.1 HAKI ZA MWANACHAMA

I. Haki ya kutoa mapendekezo yao yanayohusu uendeshaji wa chama,

II. Haki ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa viongozi,

III. Haki ya kujitetea na kujibu shutuma katika maamuzi ya kuondolewa katika chama au uongozi,

IV. Haki ya kujiondoa katika chama kwa kuzingatia taratibu za chama kama zilivyoainishwa katika

Katiba hii,

V. Haki ya kupiga kura ya kuwaondoa viongozi wa chama kama hawataridhika na utendaji wa

kazi yao,

VI. Haki ya kuona na kuhakikisha kumbukumbu za chama,

VII. Haki ya kujadili mwenendo wa wanachama au kujadili mwanachama mpya,

VIII. Haki ya kupendekeza idadi ya wanachama.

5.2.2 WAJIBU WA MWANACHAMA

I. Kutekeleza maagizo na makubalino yatakayofikiwa katika vikao mbalimbali vyachama,

II. Kutoa taarifa sahihi katika matatizo mbalimbali wanayoyapata,

III. Kulipa ada na michango mingine inayoamriwa na wanachama,

IV. Kuhamasisha wanachama katika kutakeleza majukumu mbalimbali ya chama,

V. Kutoa rambirambi/michango wakati wa misiba/starehe licha ya kwamba chama kinawajibika

kutoa fungu kwa muhusika,

VI. Kuhudhuria mikutano/vikao vya chama,

VII. Kutoa mawazo ya kuendeleza chama,

VIII. Kushiriki katika shughuli zote za chama.

6 | P a g e S V G

6.0 UKOMO, KUJITOA NA TARATIBU ZA KUONDOLEWA KATIKA CHAMA

6.1 UKOMO WA UANACHAMA

Mwisho wa uananachama utakuwa ni:

I. Mwanachama kufariki,

II. Endapo mwanachama atapatwa na ugonjwa wa akili,

III. Mwanachama akijiuzulu kwa hiari,

IV. Mwanachama kushindwa kulipa ada na michango mingine kwa miezi 3 mfululizo bila

maelezo ya kuridhisha,

NOTE: Akitaka kurudia uanachama, itabidi aombe upya.

6.2 KUJITOA KATIKA CHAMA

6.2.1 Mwanachama anayo haki ya kujiondoa katika chama kama hataridhika na

mwenendo wa chama hiki kwa misingi itakayokubalika na Katiba hii. Mwanachama

atakayejitoa atarudishiwa asilimia hamsini (50%) ya kiingilio chake iwapo hajanufaika na

uwanachama mpaka kipindi anachoamua kujiondoa.

6.2.2 Kama Mwanachama atafariki Mume/Mke atasomewa masharti ya chama na

kama atakubaliana nayo ataendelea kutoa michango ya kila mwezi. Kama hatakuwa

amejitoa rasmi katika umoja huu na atakuwa na haki ya kujitoa kama ilivyo ainishwa katika

kipengele cha 6.1 cha Katiba hii.

6.3 KUONDOLEWA KATIKA CHAMA

Mwananchama anaweza kuondolewa katika chama kama tu ataonekana anakwenda kinyume na

utaratibu wa chama katika mambo yafuatayo:

I. Kushindwa kulipa ada ya uanachama ya kila mwezi kwa miezi mitatu mfululizo bila sababu za

msingi zitakazokubalika na wanachama.

II. Kama atajihusisha na udanganyifu katika kumbukumbu zake kwa lengo la kujinufaisha na

fedha za chama.

III. Mwanachama ataondolewa na theluthi mbili ya wanachama.

IV. Kama mwanachama hatahudhuria mikutano 3 mfululizo bila sababu ya msingi.

V. Endapo mwanachama atashindwa kulipa mkopo ndani ya miezi 4 bila sababu ya msingi.

7 | P a g e S V G

6.4 TARATIBU ZA KUONDOLEWA KATIKA CHAMA

i. Kwa mwanachama atakayeshindwa kuendana na taratibu za chama, kama iliyoainishwa

katika kipengele cha 6.3. (I-V) cha Katiba hii, atajadiliwa na Sekretarieti ya chama na

anayo haki ya kujitetea mbele ya Secretarieti hiyo kabla ya mapendekezo ya Sekretarieti hii

kufikishwa mbele ya kikao cha wanachama wote kwa maamuzi ya mwisho.

ii. Mwanachama atakayeondolewa kutokana na kifungu cha 6.3. (i) - (v) hapo, Juu

atapoteza haki zake zote ikiwa ni pamoja na kutorejeshewa kiasi chochote cha fedha.

8 | P a g e S V G

7.0 MUUNDO WA CHAMA, ADA, NA MICHANGO

7.1 MUUNDO WA CHAMA

Muundo wa chama umegawanyika katika sehemu kuu tatu:-

7.1.1 uongozi wa chama unaoundwa na Mwenyekiti, Katibu na Mtunza Hazina. Pia

kutakuwepo Naibu Mwenyekiti, Naibu Katibu na Naibu Mtunza Hazina.

7.1.2 Sekretarieti ya chama itakayoundwa na viongozi walioainishwa hapo juu

pamoja na wajumbe watakaochaguliwa na mkutano wanachama

wote kwa jinsi ambavyo wataona inafaa.

7.1.3 Wanachama wote.

7.2 ADA NA MICHANGO

7.1 Kila mwanachama atawajibika kulipa kingilio, ada na michango yote kadri ya kanuni na

katiba hii na/au kama itakavyopangwa na mkutano wa wanachama wote.

7.2 Akaunti ya Benki

7.2.1 Chama kitafungua akaunti ya chama kadri ya mapendekezo ya wanachama.

7.2.2 Mkutano wa wanachama utaamua kufungua akaunti ya benki kwa kuzingatia

mapendekezo ya sekretariati au wanachama.

7.2.3 Kutoa hela benki lazima ziwepo saini tatu kati ya watu wanne wenye mamlaka

(Mandate). Mwenyekiti na katibu ni lazima wae mojawapo ya wenye mamlaka. Na

sahihi ya mmojawapo ni lazima.

7.3 MAPATO NA MATUMIZI YA CHAMA

MAPATO

Mapato ya chama yatatokana na michango ya wanachama kama vile kiingilio pamoja

na michango ya kila mwezi. Pia mapato ya kikundi yaweza kutokana na miradi ambayo

chama utakuwa umeamua kuwekeza.

MATUMIZI

Matumizi makubwa ya mfuko huu yatahusu maswala ya kijamii, kiuchumi, na utamaduni

kama ilivyoainishwa katika Katiba hii.

9 | P a g e S V G

7.3 KUMBUKUMBU ZA MAPATO NA MATUMIZI YA CHAMA

I. Ni jukumu la mtunza hazina kutunza kumbukumbu sahihi za mapato na matumizi,

ya chama , pamoja na kuziwasilisha katika vikao mbalimbali vya chama,

II. Kuidhinisha matumizi ya kawaida yahusuyo chama,

III. Kutunza muhuri wa chama.

7.4 UKAGUZI WA MAHESABU

Wanachama watapendekeza mkaguzi wa mahesabu ya chama na ripoti

itawasilishwa kwenye Mkutano mkuu wa wanachama wote.

NOTE:

MUHURI

Muhuri wa chama utatunzwa na mweka hazina wa chama au vinginevyo

itakavyoamriwa na wanachama. Muhuri utatumika kwenye nyaraka iwapo tu ni

mbele ya wanachama angalau wawili ambao watatia saini zao kwenye nyaraka

hizo.

7.5 MIFUKO YA KUSAIDIANA NA KULETA MAENDELEO

Itaundwa mifuko ya kusaidiana na kuleta maendeleo itakayowezesha

wanachama kukopeshwa kwa riba nafuu na kurejesha mkopo na riba ndani ya

kipindi kitakachoamUliwa na halmashauri au wanachama.

7.6 KUWEKEZA KATIKA VITEGA UCHUMI

Chama kinaweza kuwekeza fedha zake katika Kitega Uchumi kwa mslahi ya

wanachama wote. ( kama vile kuanzisha Saccos)

10 | P a g e S V G

8.0 MUUNDO WA UONGOZI NA MAAMUZI YA CHAMA

8.1MUUNDO WA UONGOZI

Chama kitaongozwa na wafuatao:-

I. Mwenyekiti

II. Makamu Mwenyekiti

III. Katibu

IV. Katibu msaidizi

V. Mweka hazina

8.1.1Viongozi watakaochaguliwa na Kikao cha wanachama wote kwa njia ya kura. Mwenyekiti,

Katibu, Mtunza hazina, Naibu Mwenyekiti, Naibu Katibu, Naibu mweka hazina na wajumbe

watakaochaguliwa na mkutano mkuu wa mwaka.

8.1.2Viongozi hao watakuwa katika madaraka kwa kipindi cha mwaka Mmoja.

8.1.3Katika vikao vya uchaguzi wa viongozi, asilimia 66 au theluthi mbili ya wanachama wote

wanayo haki ya kuchagua viongozi wa chama.

8.1.4 Uchaguzi utakuwa wa kupiga kura za siri.

8.2 MAAMUZI YA CHAMA

Maamuzi ya chama yatafanywa kwa kunyoosha mkono au kura za siri kutegemea na suala

linalotakiwa kutolewa uamuzi.

11 | P a g e S V G

9.0 HAKI NA MAJUKUMU YA VIONGOZI

9.1 HAKI YA KIONGOZI

I. Haki ya kujitoa katika uongozi iwapo ataona hayuko katika nafasi ya kutekeleza majukumu ya

chama,

II. Haki ya kusikiliza na kujadili matatizo ya mwanachama anayetaka kuondolewa katika chama

kabla ya kufikisha mapendekezo katika kikao chawanachama wote,

III. Haki ya kuchaguliwa kuwa kiongozi mara baada ya muda wake wa uongozi kumalizika,

IV. Hawana haki ya kuwa na kura ya veto katika maamuzi ya chama katika vikao vya

wanachama wote,

V. Haki ya kujadili wanachama wapya.

9.2 MAJUKUMU

I. Kukiongoza chama kwa mujibu wa Katiba hii na si kwa matakwa yao binafsi,

II. Kuhamasisha wananachama katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya chama,

III. Kutayarisha na kuwasilisha taarifa za mapato na matumizi ya chama katika kila kikao cha

wanachama,

IV. Kuhakikisha na kuidhinisha mafao/mikopo kwa wanachama kulingana na taratibu za chama,

2/3 ya wajumbe wa sekretarieti wanaweza kuidhinisha,

V. Kuandaa vikao vyote vya sekretarieti na vya wanachama,

VI. Mhazini atakuwa na jukumu la kutunza na kushughulikia masuala yote yahusuyo fedha.

12 | P a g e S V G

10.0 WAJIBU WA VIONGOZI

WAJIBU WA MWENYEKITI

I. Kuongoza vikao vyote vya chama,

II. Kuitisha vikao vya dharura,

III. Ndiyo msemaji mkuu chama,

IV. Kutoa maamuzi ya dharura akisaidiwa na Secretariati.

WAJIBU WA MAKAMU MWENYEKITI

I. Atakaimu majukumu ya Mwenyekiti asipokuwepo,

II. Atapewa majukumu na mwenyekiti kama atakavyoona inafaa.

WAJIBU WA KATIBU

I. Kuratibu shughuli zote za umoja,

II. Kuandaa na kuitisha vikao vyote vye Sekretarieti na wanachama wote. Kwa kushirikiana na

mwenyekiti,

III. Mtendaji mkuu wa chama muandishi na mtunzaji wa kumbukumbu za mikutano na vikao vya

IV. Chama,

V. Kuitisha mikutano na vikao vya halmashauri vinavyo tambulika kikatiba akishirikiana na

mwenyekiti,

VI. Kusambaza taarifa kwa wana chama,

VII. Kusoma muhtasari wa mkutano/kikao kilichopita,

VIII. Kuhakikisha akidi kabla ya mkutano/kikao,

IX. Kuandaa sehemu ya kufanyia mkutano au kikao.

WAJIBU WA KATIBU MSAIDIZI

Atakuwa anamsaidia katibu kwa kipindi ambacho katibu hatakuwepo au kwa maombi ya

katibu mwenyewe.

WAJIBU WA MWEKA HAZINA

I. Mtunza hazina mkuu wa chama,

II. Kutoa taarifa ya fedha za wanachama katika mikutano/vikao au kwa njia ya mtandao

wa chama,

III. Kuweka kumbukumbu za mapato na matumizi ya chama,

IV. Kusimamia akaunti za chama katika benki,

V. Kukumbusha michango,

VI. Mkusanyaji mkuu wa fedha za chama,

VII. Mshauri mkuu wa masuala ya fedha kwenye chama.

13 | P a g e S V G

11.0 VIKAO VYA CHAMA NA IDADI YA WANACHAMA

11.1 VIKAO VYA CHAMA

I. Mkutano mkuu wa mwaka,

II. Mkutano wa kawaida wa wanachama wote,

III. Mkutano wa dharura wa wanachama wote,

IV. Mkutano wa Sekretariati ya chama,

11.1 (a) Mkutano mkuu wa mwaka

Hiki ndicho chombo chenye mamlaka ya juu katika chama na kina majukumu yafuatayo:-

I. Marekebisho ya katiba na kanuni,

II. Kupitisha bajeti,

III. Kuchagua viongozi,

IV. Kujadili taarifa ya mwenyekiti , mapato , matumizi, na madeni,

V. Kuhakikisha haki na maslahi ya mwanachama yanalindwa,

VI. Kuteua wadhamini.

(b) Mkutano wa wanachama

Mkutano wa wanachama hutafanyika kila mwisho wa mwezi:

I. Kupokea, kujadili na kupitisha au kukataa mapendekezo ya Sekretariati,

II. Kurekebisha na kujadili kanuni,

III. Kupitia na kujadili agenda za chama,

IV. Kujadili taarifa za mapato, matumizi na madeni ya chama,

V. Kupokea na kupendekeza marekebisho ya katiba na kanuni,

VI. Kushughulukia nidhamu katika chama,

(c) Mkutano wa Secretariati

I. Kupitia maombi ya uanachama mpya na kupeleka kwenye chombo cha maamuzi,

II. Kujadili taarifa ya fedha,

III. Kushughulikia nidhamu katika chama,

IV. Kushughulikia marekebisho ya katiba na kanuni na kupeleka kwenye chombo cha

maamuzi.

(d) Mkutano au kikao cha dharura

Mkutano au kikao cha dharura kitaitishwa kwa kutoa notisi ikibainisha agenda, muda wa

kuanza n.k.

11.2 IDADI YA WANACHAMA

Kwa kuanzia idadi ya wanachama itakuwa……………… (………….) Hata hivyo idadi hii inaweza

kubadilika wakati wowote endapo wanachama wapya watajiunga au iwapo baadhi ya

wanachama watajiondoa au kuondolewa uanachama kwa mujibu wa Katiba hii.

14 | P a g e S V G

12.0. MUDA WA UONGOZI

12.1 MUDA WA UONGOZI

I. Viongozi wote wa chama watashika madaraka hayo kwa muda wa mwaka mmoja kwa

vipindi visivyozidi vitatu,

II. Kiongozi atakayeshindwa kutimiza wajibu wake na akapigiwa kura ya kutokuwa na

imani naye na ikathibitishwa na asilimia hamsini (51%) ya wanachama anaweza

kuondolewa kabla ya muda wake kumalizika,

III. Nafasi ya kiongozi ikiwa wazi itajazwa na mkutano unaofuatia.

12.2. SABABU ZIFUATAZO NDIYO KIKOMO CHA UONGOZI

I. Kifo

II. Kujiuzulu mwenyewe

III. Kuvuliwa uongozi

IV. Matatizo ya akili

15 | P a g e S V G

13. KANUNI ZA CHAMA

Chama kitakuwa na kanuni zifuatazo:-

UTANGULIZI

Katiba na kanuni na maamuzi ya vikao ndiyo miongozo halali ya chama hiki. Ni vyema kila

mwanachama kuzingatia hayo ili kufanikisha malengo ya Chama.

TAFSIRI

Katiba- maana yake ni katiba hii ya Salasala Vision Group

I. Mwanachama ni yule aliyejiunga kwa mujibu wa katiba ya chama na anayetekeleza

katiba, kanuni na miongozo mbalimbali itakayotolewa katika vikao vya Chama.

II. Matatizo- inajumuisha majanga, kufiwa, kufariki na kuugua.

III. Raha – Matukio yaletayo furaha.

13.1 KUJIUNGA NA CHAMA

I.Mwombaji atalazimika kujaza fomu ya maombi kutoka Kwa katibu na kudhaminiwa na

wanachama wawili.

ii. Katibu atatowa taarifa ya maandishi Kwa mwombaji maamuzi ya kikao.

iii. Mwombaji atalipa kiingilio na michango mingine ndani ya siku tisini (90) kuanzia tarehe

aliyopata taarifa ya kukubaliwa kujiunga na chama.

13.2 WAJIBU WA CHAMA KWA WANACHAMA

Chama kitawajibika kuwasaidia wanachama wake wakati wa raha na matatizo.

I. Wakati wa raha, chama hakitatoa pesa isipokuwa wanachama wake watatoa

michango na kushiriki kikamilifu

II. Matukio ya Raha:-

� Sherehe ya Harusi

� Kumuaga bi harusu mtarajiwa (Send off)

� Mahafari.

III. Wakati wa matatizo Chama kitatoa pesa kwa aliyefikwa na na matatizo kutoka katika

mfuko wa dharura. Kiwango kitakachotolewa ni kama kilivyoainishwa katika jedwali la

hapo chini (KIFO)

16 | P a g e S V G

NA MAELEZO CHAMA KITATOA

TSHS

1. Mwanachama 2,000,000/=

2. Mume/mke wa mwanachama 2,000,000/=

3. Mtoto wa mwanachama 2,000,000/=

4. Baba/Mama wa mwanachama 2,000,000/=

IV. Matatizo yanajumuisha:-

� Majanga: Chama kitatoa shilingi laki tano tu (500,000/=)

� Kuumwa: Mwanachama akilazwa hospitali siku saba atapewa shilingi laki tatu tu

(300,000/=)

13.3 MFUKO WA DHARURA

I. Kila mwanachama atachangia shilingi Mia Moja Elfu (Tshs. 100,000/-) katika mfuko wa

dharura wakati wa kujiunga na chama. Fedha hizo ndizo zitakazotumika wakati wa

matatizo.

II. Baada ya pesa kutumika wanachama watachanga tena kurejesha kiasi kilichotumika

ndani ya mwezi mmoja kunzia pesa zilipotolewa.

III. Mhusika aliyefikwa na dharura atalipwa mara moja baada ya taarifa kufika kwa

uongozi.

13.4 ADA NA MICHANGO YA CHAMA.

I. Kiingilio ni Tshs 250,000/= tu kwa wanachama waanzilishi.

II. Ada ya mwanachama kila mwezi itakuwa Tshs 20,000/= tu.

III. Watakaojiunga baada ya chama kusajiliwa (wasio wanachama waanzilishi) watalipa

kiingilio Tshs. 300,000/= tu.

IV. Kila mwanachama atachangia Tshs. 100,000/- katika mfuko wa dharura wakati wa

kujiunga. .

V. Michango yoyote itakayopitishwa na sekretarieti atalipwa na wanachama wote.

17 | P a g e S V G

13.5 ADHABU NA FAINI

I. Kushindwa kuhudhuria mkutano/kikao cha halmashauri bila taarifa kwa yeyote faini ni

Tshs 10,000/= tu.

II. Kuchelewa kikao ni Tshs. 5000/- tu.

III. Kuvuruga mkutano/kikao/sherehe au shughuli yoyote ya Chama faini Tshs. 10,000/= tu.

IV. Endapo mwanachama:

� Atakuwa anadaiwa malimbikizo ya ada ya mwezi kwa miezi mitatu

mfululizo bila maelezo yanayokubalika, ataandikiwa barua la kusudio la

kufukuzwa uanachama.

� Akishindwa kurejesha mkopo na riba atafukuzwa uanachama. Deni lake

litalipwa na wadhamini wake wa mkopo.

13.6 VYANZO VYA MAPATO

I. Kiingilio

II. Ada ya kila mwezi

III. Michango ya kuendesha mikutano, sherehe n.k.

IV. Kutunisha mfuko

V. Amana ya dharura

VI. Adhabu, faini, riba,

VII. Misaada na ufadhili

VIII. Miradi ya uwekezaji

13.7 MATUMIZI

I. Kuendesha vikao vya chama, sherehe, misiba, mikopo na uwekezaji.

II. Gharama za uendeshaji wa chama kama zitakavyowasilishwa na Sekretarieti na

kuidhinishwa na mkutano wa wanachama.

13.8 UTUNZAJI WA FEDHA

I. Chama kitafungua akaunti katika benki Kwa ajili ya kutunza fedha za chama

II. Orodha ya watia saini (signatories) ni wanne wakiwemo Mwenyekiti, Mtunza Hazina na

Wajumbe wawili (Mwenyekiti kamati ya fedha na Mwenyekiti wa kamati ya maadili).

18 | P a g e S V G

13.9 UTUNZAJI WA TAARIFA ZA CHAMA

I. Mambo yote yanayozungumzwa katika vikao vya Chama ni siri ya Chama

II. Nyaraka na taarifa zote za chama zitatunzwa na Katibu wa chama

13.10 AGENDA ZA MKUTANO MKUU

I. Ripoti ya Katibu

II. Mabadiliko ya katiba/kanuni kama yapo.

III. Ripoti ya fedha

� Bajeti

� Mapato na matumizi ya mwaka uliopita

� Matarajio ya mwaka ujao

IV. Uchaguzi wa viongozi na wanakamati ya utendaji (Sekretarieti), utafanyika kila mwaka

au utafanyika pale panapotokea pengo katika kamati ya utendaji.

V. Agenda za mkutano wa kawaida, dharura zitatolewa na sekretarieti

13.11 MABADILIKO YA KATIBA

Endapo kutatokea ulazima wa kubadili katiba, mapendekezo yatapelekwa kenye mkutano

mkuu ambao utapitia na kutoa maamuzi,

13.12 MKUTANO NA /AU KIKAO CHA DHARURA

I. Mkutano/Kikao cha dharura kitaitishwa na mwenyekiti katika muda wa mwezi mmoja

baada ya kupata maombi ya wanachama/wajumbe wasiopungua asilimia hamsini na

moja (51%) ya wanachama.

II. Endapo mwenyekiti atashindwa kuitisha mkutano/kikao cha dharura bila ya kutoa

sababu za msingi.

III. Mwenyekiti atakuwa na mamlaka ya kuitisha kikao cha dharura endapo ataona

umuhimu wa kufanya hivyo.