MAMBO 7

19

Click here to load reader

Transcript of MAMBO 7

Page 1: MAMBO 7

MAMBO 7 YATAYOIANGAMIZA

ZANZIBAR KATIKA

KATIBA INAYOPENDEKEZWA

MAMBO 7 YATAYOIANGAMIZA ZANZIBAR

KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA OTHMAN MASOUD othman

MAMLAKA YA RAIS UKUU WA KATIBA

SERIKALI MBILIMAMLAKA YA

BUNGE

UHALALI WA RAIS WA MUUNGANO

MAMBO YA MUUNGANO KURA YA MAONI KUBADILI MFUMO

1

Page 2: MAMBO 7

14th June, 1890,

To Marquis Salisbury,

We have heard from our true friend, your Consul-General Colonel Euan-Smith, all that your Lordship proposes to do for our good. And we know, indeed, that

the English Government is always desirous of doing good to us, and we are very grateful to your Lordship in our heart, and we accept everything proposed. And

now, in shaa Allah, our interest will be safely in the care of the English.

This is from your friend

ALI BIN SAID

1. UTANGULIZI SABABU YA WARAKA- WAJIBU WA KIKATIBA KIF. 23(4)

MFANO WA MAMBO AMBAYO ZANZIBAR IMEKUA IKIYALALAMIKIA SIKU ZOTE na kuondolewa kwake kulihitaji mabadiliko makubwa ya kikatiba:

o Suala la Benki Kuu; tokea kuundwa kwake, madai ya Zanzibar ya hisa, kuundwa kwa PBZ, kutungwa kwa Sheria ya Financial Administration Act, 1997 suala hilo hadi leo halijapatiwa ufumbuzi;

o Suala la kuundwa kwa TRA, kutozingatiwa maoni ya Zanzibar;o Suala la kodi ya mapato na uwezo wa Zanzibar kusarifu

uchumi; OFFSHORE COMPANIES BILL, OFFSHORE BANKS

o Suala la Mgawano wa Fedha na Kuchangia Muungano; Tume ya Pamoja ya Fedha;

o Suala la Uvuvi wa Bahari Kuu, la EEZ na usimamizi wa rasilimali;

o Suala la Jumuiya ya Afrika Masharikio Suala la simu na kuanzishwa Zantel Zanzibar na vikwazo

Zanzibar ilivyopambana navyo;

MAMBO 7 YATAYOIANGAMIZA ZANZIBAR

KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA OTHMAN MASOUD othman

2

Page 3: MAMBO 7

o Suala la uwezo wa Serikali ya Zanzibar na mkataba wa utafiti wa baharini na Taasisi ya Utafiti wa baharini China;

2. MAMBO 7 YATAYOIANGAMIZA ZANZIBAR

a. Mamlaka ya Rais wa Muungano kuigawa Zanzibar katika Mikoa, Wilaya na sehemu nyengine [IBARA YA 2(2)]

[inasomeka na ibara ya 83- tofautisha na ibara ya 175 ambapo Rais atalazimika kufata

ushauri katika uteuzi wa Jaji Mkuu kutoka katika Orodha ya majina matatu yaliyopendekezwa na Tume ya Utumishi ya Mahkama. Rais hawezi kuingiza jina lake lazima ateue kutoka miongoni mwa majina matatu;

tofautisha na ibara 181(4) na (5) kuhusiana na suala la kuondolewa Jaji. Rais lazima afuate ushauri wa Tume iliyoundwa kumchunguza Jaji]

HISTORIA FUPI ya mamlaka ya Rais wa Muungano. Katiba ya 1979 iliweka kifungu hicho kwa sababu ya mfumo wa Chama kushika hatamu. Katibu wa Mkoa wa Chama alikua pia ndiye Mkuu wa Mkoa. Hivyo Rais wa Zanzibar hakua na mamlaka peke yake kuunda Mkoa kwani akiunda Mkoa wa kiserikali anaunda Mkoa wa kichama. Hata hivyo, mfumo huo ulipoondolewa Katiba ya Zanzibar ya 1979 ilifanyiwa marekebisho kupitia Sheria namba 9 ya 1982 ambayo ilirejesha mamlaka ya kuigawa Zanzibar katika Mikoa, Wilaya na Sehemu mikononi mwa Rais wa Zanzibar.

Athari zake: Maswalio Rais wa Muungano katika kuigawa Zanzibar katika

Mikoa, Wilaya na Sehemu atafuata Sheria ipi, ya Zanzibar au ya Muungano itayotungwa kwa mujibu wa ibara ya 2(3) ya Katiba inayopendekezwa?

o Rais wa Muungano anao uwezo chini ya ibara hiyo ya KATIBA INAYOPENDEKEZWA kuunganisha Mikoa mitano na kuufanya 1;

MAMBO 7 YATAYOIANGAMIZA ZANZIBAR

KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA OTHMAN MASOUD othman

3

Page 4: MAMBO 7

o Rais wa Muungano anao uwezo wa kuigawa Zanzibar katika Wilaya, na kwa mamlaka hayo anao uwezo wa kuufanya Mkoa kuwa Wilaya?

o Rais wa Muungano anao uwezo wa kuigawa Zanzibar katika Shehia? na jee anao uwezo wa kuifanya Wilaya kuwa Shehia?

o Kuna kifungu chochote katika Katiba inayopendekezwa kinachomlazimisha Rais wa Muungano kuzingatia Sheria za Zanzibar za Tawala za Mikoa? Kuzingatia ushauri wa Rais wa Zanzibar au kuzingatia maslahi ya Zanzibar katika kuigawa Zanzibar katika Mikoa na sehemu;[ angalia katiba ya Marekani inazuia States kuunganishwa kuwa State moja au kugawanywa kuwa State zaidi ya moja]

o Kuna kifungu chochote kinachomzuia Rais wa Muungano asiifanye Zanzibar kuwa Mkoa mmoja, Wilaya moja au Shehia moja?

o Zanzibar ina haki gani na kwa utaratibu gani wa kikatiba kupinga mgao wa Mikoa, Wilaya na sehemu ataofanywa na Rais wa Muungano inapokua haikuridhika

[Jee kwa Rais wa Muungano kupewa Mamlaka ya kuigawa Zanzibar katika Mikoa, Wilaya na Sehemu Zanzibar haitaangamia?]

b. Ukuu wa Katiba ibara ya 9 zingatia ibara ya 166 [2]“[9(1) Katiba hii ni sheria kuu katika Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Katiba hii..”Katiba inayopendekezwa ibara ya 1(3) inaeleza kuwa Hati ya Muungano ndio msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano. Ibara ya 74(3) inaeleza kuwepo mambo ya Muungano na yasiyo ya Muungano. Ibara ya 75 inaeleza kuwa Serikali ya Muungano itakuwa na mamlaka ya kusimamia mambo ya Muungano tu kwa Jamhuri ya Muungano na mambo yasiyo ya Muungano ya Tanzania Bara na Serikali ya

MAMBO 7 YATAYOIANGAMIZA ZANZIBAR

KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA OTHMAN MASOUD othman

4

Page 5: MAMBO 7

Zanzibar itakua na uwezo wa kusimamia mambo yasiyo ya Muungano kwa Zanzibar. Ibara ya 133 inaeleza mamlaka ya Bunge kutunga Sheria. Ibara ya 166 inaeleza mamlaka ya Baraza la Wawakilishi kutunga Sheria kwa mambo yote yasiyo ya Muungano kwa Zanzibar.Katiba inayopendekezwa itasimamia mambo ya Muungano na yasiyo ya Muungano kwa Tanzania Bara na Katiba ya Zanzibar itasimamia mambo yasiyo ya Muungano kwa Zanzibar.Ni dhahiri kuwa Katiba ya Muungano itatumika Zanzibar kwa mambo ya Muungano kwa mambo yasiyo ya Muungano Katiba ya Zanzibar ndiyo itayotumika

Athari: Maswali Katiba ya Zanzibar nayo ni Sheria sawa na Sheria nyengine

kwa madhumuni ya ibara ya 9(2) ya Katiba inayopendekezwa; [Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Katiba inayopendekezwa aliwahi kujibu swali hili kwa kusema kuwa Katiba ya Zanzibar nayo ni sheria sawa na sheria nyengine. Katiba ya Zanzibar haiwezi kuwa Sheria sawa na Sheria nyengine kwa vile haikutungwa na Mamlaka ya kutunga Sheria bali imetungwa na Wananchi kupitia constituent assembly]

Jee Katiba inayopendekezwa ikipita kifungu cha 2A cha Katiba ya Zanzibar kitahitaji kurekebishwa au kitabatilika wenyewe kwa kufuata masharti ya ibara ya 9(2)

Ibara ya 9(4) inaeleza kuwa sheria, mila na desturi lazima zifuate Katiba hiyo [inayopendekezwa]. Jee sheria ni pamoja na Sheria za kiislamu na jee matumizi ya sheria za kiislamu ni suala la Muungano?

Mila na desturi za Zanzibar ambayo ndiyo sehemu ya utamaduni wa Zanzibar zinafungwa na ibara ya 9(4)? Kama ni hivyo mila na desturi za Zanzibar zitaendelea kuwa salama iwapo zitapingana na Katiba inayopendekezwa? (kwa mujibu wa utaratibu mamlaka ya kutoa tafsiri sahihi ya Katiba yamo mikononi mwa Mahkama na sio executive wala viongozi);

MAMBO 7 YATAYOIANGAMIZA ZANZIBAR

KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA OTHMAN MASOUD othman

5

Page 6: MAMBO 7

Kama Katiba inayopendekezwa ndiyo kuu kwa mambo yote kutakuwa na haja ya kuwa na Katiba ya Zanzibar na kama itakuwepo itakuwa na nguvu ya kikatiba au sheria sawa na sheria nyengine?

c. Mfumo wa Serikali Mbili [ibara ya 73]

Ibara ya 73 imeweka bayana mfumo huo. Ibara ya 75 imeweka bayana zaidi kuwa Serikali ya Muungano itasimamia mambo yote ya Muungano kwa Jamhuri ya Muungano yote na mambo yasiyo ya Muungano kwa Tanzania Bara.

Ibara ya 112 inaeleza kuwa mamlaka ya kuamua juu ya sera zote ni ya Serikali ya Muungano.

Ibara ya 114 inayohusu muundo wa Baraza la Mawaziri, ukiachia Rais wa Zanzibar hailazimishi kuwe na Waziri kutoka Zanzibar katika Baraza hilo.

Katika uteuzi wa Waziri Mkuu chin ya ibara ya 110 haulazimishi kushauriana na Rais wa Zanzibar.

Katika uteuzi wa Mawaziri chini ya ibara ya 115 Rais wa Muungano anashauriana na Makamu wa Kwanza na Waziri Mkuu lakini Rais wa Zanzibar ambaye ni Makamu wa Pili hahusiki katika uteuzi.

Hakuna ibara inayoweka utaratibu wa namna ya kuihusisha, kuishauri au kuishirikisha Zanzibar katika kufanya maamuzi yoyote yanayohusu masuala ya Muungano;

Hakuna mfumo maalum wa kuunda Wizara za Muungano; Hakuna bajeti wala mapato yaliyoainishwa kwa mambo yasiyo

ya Muungano wala hakuna mfumo wa matumizi unaopaswa kutenganisha baina ya mapato na matumizi ya Muungano na mambo yasiyo ya Muungano;

Hakuna mfumo wa kikatiba unaoipa haki Zanzibar kupinga maamuzi ya kisera yatayofanywa na Serikali ya Muungano ambayo ni kinyume na maslahi ya Zanzibar;

MAMBO 7 YATAYOIANGAMIZA ZANZIBAR

KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA OTHMAN MASOUD othman

6

Page 7: MAMBO 7

Hakuna mfumo wa kikatiba unaoibana Serikali ya Muungano kufanya maamuzi yoyote yale kwa faida ya upande mmoja hata bila kuishirikisha Zanzibar na bila ya ridhaa ya Zanzibar;

Matokeo ya jumla ya mapungufu hayo ni kuwa Serikali ya Muungano iliyoundwa bila ya kuishirikisha Zanzibar inao uwezo wa kufanya maamuzi ya kisera na ya kiutawala bila ya ridhaa ya Zanzibar. Serikali ya Muungano inaweza kutumia rasilimali za Muungano kwa faida ya upande mmoja bila ridhaa wala kuishirikisha Zanzibar. Kwa ufupi Serikali ya Muungano ina mamlaka ya kufanya lolote inalopenda.

Chini ya mfumo wa Serikali mbili unaojengwa na Katiba inayopendekezwa Zanzibar haimo katika Muungano bali ni sawa na iliomo katika mahusiano ya kimahamiya (Protectorate). Zanzibar ina mfano mzuri wa kujifunza athari za uhuru wake chini ya mfumo wa kimahamiya. Mwaka 1890, tarehe 14 June, Zanzibar iliingia katika mkataba wa kimahamiya na Serikali ya Uingereza. Chini ya kifungu cha 1 cha Mkataba huo uliotiwa saini na Sultan Ali bin Said kwa niaba ya Zanzibar na Colonel Euan-Smith kwa niaba ya Serikali ya Uingereza, Zanzibar ilikubali kuwa chini ya uhami (protectorate) ya Uingereza bila ya masharti yoyote kuanzia siku ambayo Uingereza itaamua. Chini ya kifungu cha II cha Mkataba, Zanzibar ilikubali kuwa masuala yote ya nchi za nje yatashughulikiwa na Uingereza kwa taratibu zitazoekwa na nchi hiyo. Chini ya kifungu cha IV cha mkataba wa uhamiya Sultan alihakikishiwa kubaki katika kiti chake cha ufalme yeye na warithi wake na chini ya kifungu cha V alihakikishiwa uhuru wa kuchagua warithi wa kiti cha ufalme lakini lazima apate idhini ya Serikali ya Uingereza.

Kikubwa ambacho Waingereza waliitaka Zanzibar ni umuhimu wake. Lord Salisbury aliwahakikishia Wabunge wa Bunge la Juu (House of Lords) wakati wa mapatano ya Heligoland kwa maneno yafuatayo:”as for the Island of Zanzibar, there is no spot in all those waters of more value to a maritime and commercial nation”.

MAMBO 7 YATAYOIANGAMIZA ZANZIBAR

KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA OTHMAN MASOUD othman

7

Page 8: MAMBO 7

Chini ya mkataba huo Zanzibar iliendeshwa chini ya Wizara ya Mambo ya Nje lakini hatimaye ilihamishiwa chini ya Ofisi ya Makoloni na hata ilipodai uhuru haikuwa suala la kuvunja tu mkataba wa umahamiya bali ilifanyika sawa na makoloni mengine.

Mfano mwengine mzuri ni namna Ukanda wa Mwambao wa Kenya ambao chini ya Makubaliano ya 1890 ulikuwa miliki ya Zanzibar na kukodishwa Serikali ya Uingereza mwaka 1895 ikauendesha kama sehemu yake ya Kenya hadi kufikia kuufanya sehemu ya Mahamiya ya Kenya mwaka 1920 kupitia Annexation Order ya 1920. Hatimaye mwaka 1960, Uingereza kupitia ripoti ya Robertson iliamua kuwa ukanda huo hauwezi kurejeshwa Zanzibar kwa vile miaka yote ulikuwa ukiendeshwa kama sehemu ya Kenya.

Ni wazi kuwa mfumo wa Serikali mbili unachukua mamlaka kutoka kwa mmoja wa Washirika wa Muungano na kuyakabidhi kwa Mshirika wa pili ambaye ana haki ya kuyatumia kadri anavyopenda.

Athari kubwa ya pili ni kuwa baada ya muda mrefu Muungano unanza kupoteza maana na mshirika aliyepewa mamlaka kuhisi kwamba ni mtawala wa mshirika mwengine. Hisia za mtawala na mtawaliwa zinaweza kufikia hatua ya mmoja wa washirika kudai uhuru badala ya kudai haki yake ambayo mmoja wa washirika amekuwa akiitumia vibaya.

Mfumo wa Serikali mbili hasa kwa nchi ambazo zilikua dola kamili si rahisi kufanya kazi kwa utulivu. Ni kwa sababu hiyo ndio mana mpaka leo Muungano wa Uingereza na Scotland unaendelea kuhojiwa pamoja kwamba ulianza tokea 1603 na ukafanywa rasmi kwa mkataba wa Muungano mwaka 1707.

d. Uhalali wa Rais wa Muungano kwa upande wa Zanzibar [ibara ya 89(6)]

MAMBO 7 YATAYOIANGAMIZA ZANZIBAR

KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA OTHMAN MASOUD othman

8

Page 9: MAMBO 7

Ibara ya 89, Rais wa Jamhuri ya Muungano anaweza kuwa mgombea wa Chama au mgombea binafsi. Chini ya ibara ya 89(6), mgombea urais atatangazwa ameshinda iwapo atapata zaidi ya asilimia hamsini ya kura zilizopigwa.Mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ni makubwa ikiwemo yale ya kuigawa Zanzibar katika Mikoa, Wilaya na sehemu.Masuala muhimu:

Kama Zanzibar ni mshirika sawa katika Muungano kwa nini isiwe na sauti hata kidogo katika kumchagua mtu wanayemkabidhi mamlaka ya utaifa wao;

Iwapo kama Rais wa Muungano na chama chake hawakupata kura hata moja Zanzibar, uhalali wake wa kutekeleza mamlaka makubwa ya kiutawala kwa watu ambao hawakukuchagua unatokana na nini.

Iwapo Zanzibar ambayo ni mshirika katika Muungano haikubaliani na usimamizi wa Rais katika masuala yao yaliopo chini ya Muungano wana haki gani ya kikatiba au ya kisheria ya kumdhibiti Rais huyo ikiwemo tabia ya Rais huyo kuonyesha dhahiri kuikandamiza Zanzibar;

Hicho ni kielelezo tosha kuwa Zanzibar haimo katika Muungano kama mshirika bali kama mahamiya.

e. Mamlaka ya BUNGE [ ib. 134]

Ibara ya 134 ndio inayokamilisha maangamizi ya Zanzibar. Ibara hiyo katika maneno ya pembeni (marginal note) inaeleza kuwa inahusu utaratibu wa kubadili Katiba lakini inahusu utaratibu wa kutunga Sheria zote ndani ya Bunge ikiwemo Sheria za kurekebisha Katiba. Ibara inaeleza utaratibu wa namna 3;

Kwanza ni chini ya 134(1)(a)- aya hii inahusu utaratibu wa kupitisha Miswada ya inayohusu ama:

o Sheria ya mambo yasiyo ya Muungano; au

MAMBO 7 YATAYOIANGAMIZA ZANZIBAR

KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA OTHMAN MASOUD othman

9

Page 10: MAMBO 7

o Sheria ya Mambo ya Muungano yaliomo katika Nyongeza ya Kwanza; au

o Sheria ya kubadili Katiba Utaratibu utaotumika ni kwa kupitishwa Mswada huo ikiwa utaungwa mkono na Wabunge walio wengi;

Pili ni ibara ya 134(1)(b)- aya hii inahusu utaratibu wa kupitisha sheria inayohusu ama:

o Kubadili masharti ya Katiba [ni dhahiri kuwa sharti hili limejirudia kwani ni sawa na sharti la ibara ya 134(1)(a) iliyoelezwa hapo juu];

o Kubadili masharti ya jambo lililotajwa katika Nyongeza ya Pili ya Katiba [ni mambo mawili 2- kubadili masharti ya Katiba ya Muungano yanayohusu Mambo ya Muungano na kuongeza au kupunguza jambo la Muungano]

Utaratibu ni utaotumika ni kupitishwa iwapo Mswada huo utaungwa mkono na theluthi mbili ya wabunge wa kila upande.

Tatu ni ibara ya 134(1)(c)-ibara hii inahusu utaratibu wa kupitisha sheria kwa mambo yaliyotajwa katika Nyongeza ya Tatu ambayo ni mambo matatu. Kwanza ni Muundo wa Jamhuri ya Muungano, pili, Kuwepo au kutokuwepo Jamhuri ya Muungano na tatu ni kubadili masharti ya ibara ya 134. Utaratibu utaotumika ni wa kura ya maoni itayoungwa mkono na nusu ya wananchi wa kila upande.

Ibara hii ya Katiba inayopendekezwa kwanza imerejea masharti ya ibara ya sasa ya 98 ya Katiba ya Muungano ambayo imekuwa ikipingwa na Zanzibar katika nyaraka, ripoti na maandiko yote. Imekuwa ikipingwa kwa sababu kadhaa lakini muhimu ni kama zifuatazo:

Inainyima Zanzibar kama mshirika katika Muungano kauli katika kuamua sheria za mambo ya Muungano. Sheria ambazo kwanza zimependekezwa na Baraza la Mawaziri ambalo

MAMBO 7 YATAYOIANGAMIZA ZANZIBAR

KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA OTHMAN MASOUD othman

10

Page 11: MAMBO 7

Zanzibar haina ushiriki. Lakini sheria hizo ndio zinazoamua haki za kila upande katika Muungano;

Inawafanya Wabunge wa Zanzibar wasiwe na kazi yoyote katika Bunge la Muungano;

Inakamilisha dhana ya kuwa Zanzibar si mshirika katika Muungano bali imo kama mahamiya.

Mifano ya namna Zanzibar ilivyoathirika na mamlaka haya ya upande mmoja katika kutunga sheria za pamoja ipo mingi sana na ndio miongoni mwa mizizi ya fitna za Muungano.

Mbali ya hayo, ibara hii sasa imekwenda mbali zaidi kwa kuutia kufuli mfumo huu wa ajabu na kandamizi wa Muungano kwa kuulinda kuwa hauwezi kubadilishwa mpaka kwa kura ya maoni. Sijui kama yapo maangamizi makubwa kuliko mtu kujifunga katika dhulma ya wazi kiasi hichi,

f. Mambo ya Muungano

Kwa miaka mingi Zanzibar imekuwa ikilalamika katika mambo ya Muungano kwa sababu zifuatazo:

Wingi wa mambo ya Muungano; Kukosa ufafanuzi wa mambo ya Muungano; Mambo ya Muungano kuikosesha Zanzibar nyenzo za

kiuchumi

Mambo ya Muungano chini ya Katiba inayopendekezwa ni 21. Mambo yote hayana ufanunuzi. Kwa mfano elimu ya juu.

Jambo litaloiangamiza Zanzibar ni katika nyenzo za kiuchumi hasa kodi.

Kodi ya mapato ndiyo nyenzo kuu ya kuendesha uchumi wowote wa kisiwa ambacho hakina rasilimali. Kodi ya mapato ndiyo nyenzo ya kuvutia mitaji na ndio nyenzo kupata mapato hata katika rasilimali za nchi.

MAMBO 7 YATAYOIANGAMIZA ZANZIBAR

KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA OTHMAN MASOUD othman

11

Page 12: MAMBO 7

g. Kura ya Maoni Kubadili Muundo wa Muungano [ibara ya 134(1)(c) na Nyongeza ya Tatu

Katiba inayopendekezwa imejenga misingi ya dhulma na kukosekana usawa na haki za washirika wa Muungano, jambo ambalo linawafanya watu wa upande mmoja wauchukie Muungano. Kwa upande wa pili inawalazimisha dhulma hiyo iendelee mpaka pale anayedhulumu atapokubali kubadili dhulma hiyo.

3. HITIMISHO

Kwa hakika inasikitisha kwamba pamoja na mapungufu haya yote ambayo ni ya dhahiri na ya hatari kwa Zanzibar bado wapo Wazanzibari ambao wana wajibu wa kikatiba kulinda uhuru na mamlaka ya Zanzibar wanaitetea Katiba inayopendekezwa. Katiba ambayo ni hakika itaiangamiza Zanzibar kama itapitishwa kuwa Katiba.

Wengine wanasema Zanzibar imepata manufaa katika Katiba inayopendekezwa kwa vile mafuta yameondolewa na Rais wa Zanzibar amekuwa Makamu wa Rais bila kuangalia ufinyu wa faida hizo kuliko vile Zanzibar inavyoangamizwa na Katiba hiyo. Aliyewahi kuwa Chancellor wa Ujerumani, Chancellor Bismark ambaye alijiuzulu mwaka 1890 wakati akiwa hajakamilisha mapatano ya Heligoland alimwambia aliyemfuatia, Chancellor Caprivi ambaye alikamilisha mapatano hayo kwa njia ambayo haikumridhisha Bismark kwamba ni sawa na aliyeingia mapatano ya kutafuta suruali na badala yake akaishia kupata kifungo. Kwa Zanzibar nadhani tuliingia katika mapatano ya Katiba kutafuta suti tukaishia kupata kifungo cha chawa…unapomsikia mtu anajisifia kwa mafanikio hayo sijui utamueka katika kundi gani.

MAMBO 7 YATAYOIANGAMIZA ZANZIBAR

KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA OTHMAN MASOUD othman

12