Kuwa Shujaa Parents' guide 2

8
02 OF 03 INFO YA MAPERO

description

Kuwa Shujaa parents' guide is a HIV education awareness tool developed for all parents.

Transcript of Kuwa Shujaa Parents' guide 2

Page 1: Kuwa Shujaa Parents' guide 2

02 OF 03

INFO YA MAPERO

Page 2: Kuwa Shujaa Parents' guide 2

This publication has been made possible with the generous support of the American people through USAID/Kenya, under the APHIA II Operations Research Project, a cooperative agreement (No. 623-A-00-09-00001-00) between the Kenya Mission and the Population Council.

HEBU TUONGEE

JUU YA HIV!

STIGMA (kubaguliwa) ni shida kubwa sana katika shule. stigma inamaanisha kumbagua mtu kwa sababu ya tabia zao au hali yao – Kwa mfano, labda ana virusi vya HIV. Watoto wengi walio na virusi hivi wanabaguliwa shuleni. Sio haki kumbagua mtu au kumsengenya kwa sababu ana virusi vya HIV. Kitabu hiki cha Kuwa Shujaa kinatarajia kubadilisha tabia kama hii, na tunawahisi nyinyi, kama wazazi na wanaowatunza watoto hawa, mtusaidie.

Tumempa mtoto wako kitabu hiki cha ‘Kuwa Shujaa’ ili aweze

kujifunza kuhusu HIV na Ukimwi; na pia, kuhakikisha kwamba

atajifunza njia za kujikinga.

Page 3: Kuwa Shujaa Parents' guide 2

Ndani ya mwelekezo kuna maswali ambayo utaweza kumuuliza mtoto wako kuhusu HIV. Haya maswali yatakusaidia kuzungumza na mtoto wako kuhusu HIV. Kando ya hayo, maswali haya yatamsaidia mtoto wako kuangalia swala la HIV katika mwangaza mpya..

Tunahitaji usaidizi kuhakikisha kwamba shule iwe na mazingira mema kwa wanafunzi wasio na virusi vya HIV, na pia wale walio na virusi vya HIV. Waweza kutusaidia kwa kusoma mwelekezo huu na kuzungumzia ‘KUWA SHUJAA’ na watoto wako.

Lengo la ‘KUWA SHUJAA’ ni kuhakikisha

kuwa katika shule zote watu

hawatengwi au kubaguliwa kwa sababu

ya hali yao ya HIV. Kutimiza lengo hili,

mtoto wako anatakikana:ajue ukweli kuhusu HIV / UKIMWI

aelewe kuwa ujuzi kuhusu HIV na

Ukimwi utamsaidia kujikinga

aelewe umuhimu wa kujua hali yake ya

HIV ili aweze kujitolea kupimwa

awe na ukarimu na utu akiwa

anahusiana na wanafunzi walio na

virusi vya HIV.awe kiongozi mwema baadaye.

3

Page 4: Kuwa Shujaa Parents' guide 2

Kwa hii hadithi, marafiki wa Manywele wamekataa kucheza mpira naye wanapogundua kwamba ana virusi vya HIV. Watu wasipokua na ujuzi wa kutosha juu ya HIV, huwa wanawadhulumu walio ambukizwa. Tabia hii ndio inaitwa ‘stigma’.

muulize mtoto wako: “MARAFIKI WA MANYWELE WANAWEZA KUAMBUKIZWA VIRUSI VYA HIV KWA KUCHEZA NAYE?”“JE WEWE UNGEJIHISI VIPI KAMA UNGECHOKOZWA NA MARAFIKI WAKO KWA SABABU UNA VIRUSI VYA HIV?”

Msichana huyu hataki kuketi karibu na Manywele kwa sababu Manywele ana virusi vya HIV.

muulize mtoto wako: “kwa nini MSICHANA HUYU ANAOGOPA kukaa karibu na manywele?”“WEWE UNGEFURAHIA KUKETI KARIBU NA MTU AMBAYE AMEAMBUKIZWA VIRUsI VYA HIV?”

Msikize mtoto wako. [Kumbuka ulipokuwa umri wao. Wasaidie na uwape fursa ya kukueleza hisia zao.] Kama mzazi, utamsaidia mtoto wako vipi kuwapenda na kuwaheshimu wanafunzi ambao wameambukizwa virusi vya HIV?

Mtu hawezi kuambukizwa na virusi

vya HIV kwa kumkumbatia

aliyeambukizwa, kumshika mkono

wake, kuwa darasa moja naye au

kumtembelea nyumbani. HIV

inaenea tu, ukiwa na kidonda

kilicho wazi kinachogusa damu ya

mtu aliye na virusi vya HIV; au

kupitia uhusiano wa kimapenzi

bila kutumia kinga na kuhakikisha

wewe na mwenzako mmepimwa.

ukweli:

T W

4

Page 5: Kuwa Shujaa Parents' guide 2

Lengo la kuwauliza wanafunzi kuigiza hadithi hizi ambazo wamesoma, ni

kuwasaidia kuwaelewa walio na virusi vya HIV. Tunafanya hivi kwa

kuwafanya wapitie yale walioambukizwa wanapitia. Wakielewa hisia za

wanobaguliwa, yawezekana hawatadhulumu wengine.

muulize mtoto wako: ALIKUA NANI KATIKA HUU MCHEZO?ALIJIFUNZA NINI KUTOKANA NA HUU MCHEZO? JE, MCHEZO HUU ULIBADILISHA MAONI YAKE KUHUSU HIV?

Wanafunzi walizungumza juu ya uzuri na ubaya wa kuwa na rafiki ambaye ana virusi vya HIV. Tuliwasihi waangalie sekta ya ‘True or False’ katika kitabu cha kwanza cha Kuwa Shujaa, watambue jinsi ‘ubaya’ unaosemakana umetokana na kudanganywa.

nawe pia angalia ili ujikumbushe njia ambazo watu huambukizwa virusi vya HIV?!

WHAT WOULD YOU DO?

T WOULD YOU DO?

WHAT WOULD YOU DO?

WHAT WOULD YOU DO? WHAT WOULD YOU DO? WHAT WOULD YOU DO? WHA

Katika sekta hii, wanafunzi walitumia ujuzi walioupta katika kitabu cha Kuwa Shujaa 1 kufanya mtihani mdogo. Uliza mtoto wako asome maswali haya nawe uone kama utapita mtihani?

“Zifuatazo ni njia ambazo watu wanaweza kuam-bukizwa na virusi vya HIV...”

Kuwa na uhusiano wa kimapenzi bila ya kutumia kinga na mtu ambaye ameambukizwa.Kutumia visu na sindano pamoja (sana sana wanaotu-mia madawa ya kulevya, na wakati wa kutahiriwa)Kuongezwa damu ilio ambukizwa. (Siku hizi damu hupimwa ili kuona kama ina virusi hivi)Kina mama wanaweza kuambukiza watoto wao wakiwa na mimba, wakiwa wanajifungua na wanaponyonyesha.

5

Page 6: Kuwa Shujaa Parents' guide 2

Jipendo anaachana na mpenzi wake kwa sababu alimwona akiingia kituo cha VCT. Jipendo alidhani mpenzi wake akitembelea kituo cha VCT ni kwa sababu hakuwa mwaminifu. Lakini, mpenzi wake alienda kupata ujuzi juu ya HIV na kupatiwa mawaidha ya jinsi kumtunza Jipendo na yeye binafsi.

Hakuna shida yoyote mtu akitem

belea

VCT. Kutembelea VCT hakumaanishi

kwamba una uhusiano wowote wa

kimapenzi VCT ni pahali ambapo habari

za kiafya zinapatikan

a.

JE, WAJUA KAMA MTOTO WAKO AMEWAHI KUTEMBELEA VCT?

Malkia anamsaidia Jipendo wanafunzi wengine wanapombagua kwa kumtukana na kuamua kwamba ana virusi vya HIV.

muulize mtoto wako:“KWA NINI WANAFUNZI WENGINE wanasema JIPENDO ANA HIV?” “UNADHANI jipendo anajihisi vipi anapobaguliwa?”

muulize mtoto wako: “ULIANDIKA NINI KATIKA BARUA YAKO?”

Watu wal

iombukizwa

virusi vy

a

HIV wana

takikana

wasaidiwe na

wahimizwe ku

la vizur

i, kufany

a

tizi na wa

we wasafi

ili wasip

ate

magonjwa meng

ine. NI v

izuri

pia wahim

izwe wamwone

daktari w

anapoanza

kuhisi

ugonjwa. Waka

ti huu, w

atu

walio na

virusi vy

a HIV

wanastah

ili kuhimizwa

kuwa na

afya na

kinga mwilini.

ukweli:

ukweli:

6

Page 7: Kuwa Shujaa Parents' guide 2

TUSAIDIE KUKOSOA FIKRA HIZI KUHUSU HIV ILI SHULE ZA

KENYA ZIWE HURU!

“Stigma (ubaguzi) unatokana na kutokuwa na ujuzi wa kutosha. Hali

hii hutandaza uoga na uoga, husababisha dhulma. Kuwa Shujaa inanuia kubadilisha tabia hii katika

shule. Utatusaidia?”

1. Mtu akiwa na virusi vya HIV lazima atajua.

Uongo. Watu walioambukizwa na virusi vya HIV dalili haionekani wazi kwa muda mrefu, hata kwa miaka!

2. Wale wanaoambukizwa na virusi vya HIV ni wale tu walioanza uhusiano wa kimapenzi.

Uongo. Watoto wanaweza kuambukizwa na virusi vya HIV wakiwa wanazaliwa au wakinyonyeshwa. Wengine wanaambukizwa wanapoongezwa damu ya kuambukizwa.

3. Nitaambukizwa virusi nikitumia kikombe kimoja au nikiwa kwa darasa moja na mtu aliye na virusi vya HIV.

Uonga: HIV haipitii hewa.Huwezi kupata HIV ukiwa kwa chumba moja na mtu ambaye ana virusi vya HIV.Hatuwezi kuambukizwa kwa kukumbatia wengine au kushika mtu aliye na virusi vya HIV.Hatuwezi kuambukizwa na mtu ambaye ana virusi akikohoa au akipiga chafya, au kunywa kutoka Kwa kikombe kimoja.

“Tafadhali mweleze mtoto wako kwamba sio lazima aogope HIV kwa sababu...”

Tunajua mengi kuhusu HIV na UKIMWI. Hatuna tiba lakini tunajua watu wanavyoambukizwa na kwamba watu wanaweza kuishi kwa muda mrefu kwa kutumia madawa. Tunajua kwamba tunaweza kujikinga na HIV/UKIMWI kwa kuhakikisha kwamba tunaangalia afya yetu.Tunajua jinsi watu wanaambukizwa virusi vya HIV.Tunajua jinsi ya kujikinga.

7

Page 8: Kuwa Shujaa Parents' guide 2

8kuwa shujaa production charles j ouda | bridget deacon | fatima aly jaffer design salim busuru art salim busuru | eric muthoga | noah

mukono | kevin mmbasu stories grace irungu | daniel muli | peter kades published by well told story: www.wts.co.ke