AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009...

28
UTOKEZO (AL-BADAA) Kimeandikwa na: Sayyid Abdul-Karim al-Bahbahani Kimetarjumiwa na: Abdul-Karim J. Nkusui AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page A

Transcript of AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009...

Page 1: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

UTOKEZO(AL-BADAA)

Kimeandikwa na:Sayyid Abdul-Karim al-Bahbahani

Kimetarjumiwa na:Abdul-Karim J. Nkusui

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page A

Page 2: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

©Haki ya kunakili imehifadhiwa na:AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 978 - 9987 - 512 - 26 - 3

Kimeandikwa na:Sayyid Abdul-Karim al-Bahbahani

Kimetarjumiwa na:Abdul-Karim J. Nkusui

Kimepangwa katika Kompyuta na:Hajat Pili Rajab

Toleo la kwanza: Julai, 2009Nakala: 1000

Kimetolewa na kuchapishwa na:Alitrah Foundation

S.L.P. 19701 Dar es Salaam, TanzaniaSimu: +255 22 2110640

Simu/Nukushi: +255 22 2127555Barua Pepe: [email protected]

Tovuti: www.alitrah.orgKatika mtandao: www.alitrah.info

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page B

Page 3: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page C

Page 4: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

YALIYOMO

1. Al – badau katika Qur’an tukufu............................................................2

2. Kauli za Maulama wa Shia ithna ashariyah juu ya Al-badau.................7

3. Nafasi ya itikadi na malezi yenye kujenga ya Al-badau......................10

4. Maswali juu ya itikadi ya Al-badau.......................................................13

5. Hitimisho...............................................................................................15

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page D

Page 5: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

NENO LA MCHAPISHAJIKitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjumi ya kitabu cha Kiarabukiitwacho, al-Badaa’. Sisi tumekiita, Utokezo.

Kitabu hiki ni matokeo ya kazi ya kielimu iliyofanywa na mwanachuoniwa Kiislamu, Sayyid Abdul-Karim al-Bahbahani.

Kumekuwepo na kutokuafikiana katika miji yetu ya Kiislamu, hususanmiongoni mwa wanavyuoni kuhusu usahihi wa itikadi ya Badaa’ - yaaniutokezo wa jambo fulani kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Baadhi wanase-ma kwamba itikadi hii ni sahihi na wengine wanasema si sahihi. Baadhi yawanavyuoni wamekwenda mbali zaidi hadi kufikia kuwaita Waislamuwenzao wanaoitakidi juu ya Utokezo (Badaa’) kuwa ni washirikina aumakafiri.

Lakini je, Badaa’ haina asili katika dini? Ukweli ni kwamba ina asili kati-ka dini kama utakavyoona katika kitabu hiki.

Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleomakubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale naupotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili zawatu. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imea-mua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuniyake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji waKiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii.

Tunamshukuru ndugu yetu, Abdul-Karim J. Nkusui kwa kukubali jukumuhili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wotewalioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwakwake. Mchapishaji:Al-Itrah FoundationS. L. P. 19701Dar-es-Salaam, Tanzania.

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page E

Page 6: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

NENO LA JUMUIYA

Hakika mirathi ya AHLUL-BAYT ambayo imehifadhiwa na kambi yao nawafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha kambi iliyokusanya aina mbal-imbali za taaluma za kiislamu.

Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kutokakwenye chemchemu hiyo, na kuupa umma wa kiislamu wanachuoniwakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa Ahlul-Bayt.

Wanachuoni waliyokusanya vidodosa na maswali mbalimbali ya madhe-hebu na mitazamo tofauti ya kifikra kuanzia ndani ya desturi ya kiislamuhadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzi makini juuya maswali hayo ndani ya karne zote.

Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt imefanya hima kutetea tukufu zaujumbe wa Uislamu na ukweli wake ambao umechafuliwa na makundi,madhehebu na wanaharakati mbalimbali wenye chuki na uislamu.

Jumuiya imefuata nyayo za Ahlul-Bayt na za wafuasi wa kambi yao njemaambayo imefanya hima kujibu madai yenye kuendelea na daima ikajaribukubaki ndani ya msitari wa mapambano kwa kiwango kinachohitajikandani ya kila zama.

Hakika uzoefu ambao umehifadhiwa ndani ya vitabu vya wanachuoni wakambi ya Ahlul-Bayt katika dhamira hii ni vya aina ya pekee, kwa sababuuna nguzo ya kielimu inayotegemea akili na hoja, huku ukijiepusha namatamanio na uzalendo uliokatazwa.

Unazungumza na wasomi na wanaharakati wenye fani maalumumazungumzo ambayo yanaituliza akili na yanapokewa na maumbile sala-

F

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page F

Page 7: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

ma.Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapawatafuta ukweli hatua mpya ya uzoefu wa thamani katika ulingo wamazungumzo na maswali na kujibu hoja za utata zilizotolewa zama zilizo-pita au zinazotolewa leo kwa njia ya Tovuti, na hasa kwa kupewa nguvu nabaadhi ya nchi zenye chuki dhidi ya uislamu na waislamu.

Jumuiya imejiepusha na udadisi uliokatazwa na ni yenye kuhangaikiakuzidadisi akili zenye kufikiria na nafsi zenye kutafuta haki ili ziwezekufikia kwenye haki ambayo inatolewa na kambi ya Ahlul-Bayt ulimwen-gu mzima, ndani ya zama ambazo akili inaerevuka na nafsi na roho zina-boreka kwa kasi ya pekee.

Ni lazima tugusie kuwa mfululizo huu wa tafiti hizi umeandaliwa naKamati maalum toka jopo la wanachuoni watukufu, hivyo tunatoa shuku-rani njema kwa hawa wote na kwa wasomi na wahakiki kwa kila mmojamiongoni mwao kupitia sehemu ya tafiti hizi na kutoa mchango wao wathamani kuhusu tafiti hizi.

Tunategemea na kutaraji kuwa tutakuwa tumetoa kile tunachokiweza kati-ka juhudi za kutekeleza baadhi ya wajibu tulio nao mbele ya ujumbe waMtukufu Mola wetu Mlezi ambaye alimtuma Mtume Wake na uongofu nadini ya haki ili aidhihirishe juu kuliko dini zote. Na Mwenyezi Munguanatosha kuwa shahidi.

JUMUIYA YA KIMATAIFA YA AHLUL-BAYTKITENGO CHA UTAMADUNI

G

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page G

Page 8: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

H

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page H

Page 9: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page 1

Page 10: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

2

Utokezo (al-Badaa)

AL-BADAU KATIKAQUR’AN TUKUFU

Maudhui ya Badau yanazingatiwa kuwa ni kati ya masuala ya falsafa yakitauhidi ambayo yamechochea utafiti wenye wigo mpana baina ya maula-maa wa elimu ya falsafa, hiyo ni kutokana na yanayopatikana humo mion-goni mwa mas’ala ya kina na ya muhimu.

Al-Badau katika lugha: Ina maana ya kudhihiri baada ya kufichikana, nainatumika katika mijadala ya kawaida katika nyanja za kubadilishana rai,fikra, maoni, malengo na makusudio. Hivyo husemwa: “Rai yake ilikuwahivi kisha akabadili.”

Ni dhahiri kwamba Al-Badau kwa maana hii ni kutotambua jambo mwan-zo kisha ukalitambua baadaye na yote mawili hayapatikani kwa MwenyeziMungu (s.w.t.) kwa sababu elimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni yadhati ambapo haijatanguliwa na ujahili. Lakini tukichunguza Al-Badaukatika maana yake ya kilugha tunaikuta inaundwa na vitu viwili:Ujahili wa mwanzo na elimu mpya.

Kubadilika kwa rai, nia na malengo kufuatana na elimu mpya aliyoipata.

Kisha tunaulizana ni kipi kati ya hivi viwili kinapingana na tawhidi? Chakwanza au cha pili au vyote viwili?

Je, kuna uwezekano wa kutenganisha baina yake kiasi kwamba tunasal-imika na aina ya kubadili na kugeuza ambapo hakutokani na ujahiliuliotangulia wala elimu inayokuja baadaye?

Ama kuhusiana na suala la kwanza: Kwa wepesi tunaona kwamba jambola kwanza linapingana na tawhidi na hakuna Mwislamu anaekubali kuna-

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page 2

Page 11: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

3

Utokezo (al-Badaa)

sibisha ujahili kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na wala hatuhitaji kuletaaya wala riwaya juu ya hilo.

Ama suala la pili: Ikiwa mabadiliko yanalazimiana na dhati ya kuwepoujahili wa awali na kupatikana kwa elimu baadaye basi hali hii inapinganana tawhidi pia. Kama ambavyo ujahili unapingana na tawhidi vivyo hivyounapingana na kila mabadiliko na mageuzi yanayosababishwa na hilo. Naikiwa mabadiliko yana sababu nyingine katika hali hii hayapingani natawhidi.

Kubadili rai na mtazamo – mfano - ni kati ya mambo ya lazima ya dhatikwa ajili ya kudhihiri elimu na kuondoka kwa ujahili, hivyo basi hai-wezekani kunasibisha ujahili kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Vivyohivyo haiwezekani kunasibisha mabadiliko ya rai na mtazamo kwaMwenyezi Mungu Mtukufu. Bali dhana ya rai na mtazamo peke yake hai-wezekani kunasibishwa kwa Mwenyezi Mungu tukiachilia mbali mabadi-liko na mageuzi kwa sababu dhana hii inategemea maana ya kupata nakujifunza elimu, na elimu ya Mwenyezi Mungu haipatikani kwa njia yakujifunza hadi isemwe kuwa huu ni mtazamo wa Mwenyezi Mungu na raiyake bali ni elimu ya dhati na inasimama juu ya dhati yake.

Baada ya jawabu la maswali mawili kuwa wazi tunajaribu kutazamaQur’anTukufu ili tuangalie je, kunapatikana aya inayonasibisha mabadi-liko au mageuzi katika jambo miongoni mwa mambo au nyanja kati yanyanja?Kuna ambao wanafanya haraka kusema Qur’an inakataa kuwepo mabadi-liko au mageuzi kwa Mwenyezi Mungu na hiyo ni kutokana na kauli yake(s.w.t.): “Lakini hutopata mabadiliko katika kawaida ya MwenyeziMungu”1 na kauli yake (s.w.t.): “Na wala hutopata mabadiliko katikakawaida ya Mwenyezi Mungu.”2

1 Suratu Fatir: 432 Suratul Ahzab: 62

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page 3

Page 12: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

4

Utokezo (al-Badaa)

Ila jawabu hili halitoshelezi kwa sababu uhalisia wa Qur’ani ni jambolinalotokana na Qur’ani yote na kinachopatikana katika upande mmoja tuhakiwakilishi isipokuwa nusu ya Qur’ani kwa sababu kinatokana naupande mmoja tu wa Qur’ani Tukufu.

Kuna upande mwingine umenasibisha mabadiliko na mageuzi kwaMwenyezi Mungu Mtukufu mfano kauli yake (s.w.t.): “Mwenyezi Munguhufuta ayatakayo na huimarisha (anayoyataka) na asili ya hukumuiko kwake.”3 Na kauli yake (s.w.t.): “Hakika Mwenyezi Munguhabadilishi yaliyoko kwa watu hadi wabadilishe yaliyoko katika nafsizao.” 4

Aya ya kwanza inaonyesha kwamba Mwenyezi Mungu anafuta nakuthibitisha na katika hilo kunaashiria mabadiliko na mageuzi.

Ama Aya ya pili imeweka wazi kwamba Mwenyezi Mungu anabadilishahali za watu pindi wanapobadilisha yaliyopo katika nafsi zao. Hivyo haliya kidini na kisiasa ya watu ni makadirio ya kiungu yanakubali mabadilikopindi watu wanapoamua kubadilisha hali zao za kinafsi na kiutamadunikutoka katika shirki kwenda kwenye imani, na kutoka kwenye upotovukwenda kwenye uongofu. Hivyo kuna makadirio ya aina mbili, makadirioya kiungu katika hali ya watu katika utii na makadirio ya kiungu katika halizao katika maasi. Wanapochagua utiifu anawapitishia makadirio ya mwan-zo, na wanapochagua uasi anawapitishia makadirio ya pili. Na aina hii Ayana riwaya zimeonyesha kuathiri baadhi ya vitendo katika riziki, vifo nabalaa.

Na haya hayakatai yeyote kati ya Waislamu bali ikhitilafu inatokea katikauelewa wa badau ilipochukuliwa kwa maana yake ya kilugha inayopin-gana na tawhidi, na ikhitilafu inaisha inapogundulika kuwa makusudio

3 Suratu Raad: 394 Suratu Raad: 11

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page 4

Page 13: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

5

Utokezo (al-Badaa)

yake ni maana ya kiistilahi isiyolazimu kunasibisha ujahili kwa MwenyeziMungu (s.w.t.). Hakika makusudio ya badau kwa Ahlul–Bait (a.s.) nikwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anamkadiria mja wake kulingana nahali fulani kisha Mwenyezi Mungu anabadilisha makadirio yake kutokanana hali mpya inayodhihiri kwa mja kutokana na amali fulani anayoifanya,pamoja na kutambua Kwake tangu awali mambo yote mawili na hali zotembili. Na lau wangefahamu maana hii wangetambua kuwa ni kati yamambo ambayo Waislamu wanaafikiana juu yake na ikhitilafu ipo katikamatamshi tu.

Amesema kweli Allammah as-Sayid Abdul-Husein Sharaf Diyn alipose-ma: “Ikhitilafu katika mas’ala haya baina yetu na Ahlus-Sunna ni yamatamshi tu.”

Kisha amesema: “Aking’ang’ania asiyekuwa sisi tutamtaka arejee katikahukumu yake, hivyo abadilishe tamko la badau kama anavyotaka lakiniamuogope Mwenyezi Mungu kwa ndugu yake muumini.”5

Na kabla yake alishaandika Sheikh Al-Mufiyd: “Ama kutamka tamko labadau, hakika nimelifahamu kupitia yaliyopokewa baina ya mja naMwenyezi Mungu Mtukufu na lau kusingepokewa ambayo najua usahihiwake basi nisingekubali kutamka. Kama ambavyo lau nisingepokea kwam-ba Mwenyezi Mungu anakasirika na anaridhika, anapenda na kuchukiabasi nisingesema hayo. Ninasema kwa maana ambayo haipingwi na akilina hakuna ikhitilafu baina yangu na Waislamu wote katika mlango huu,bali amekhalifu aliyewapinga katika tamko bila ya kupinga maana yake, nanimeshaeleza sababu yangu ya kusema hayo kwa kifupi, na huu ndio msi-mamo wa Mashia wote na kila aliyewakhalifu katika madhehebu anapinganiliyoyaeleza kwa jina tu bila ya kupinga maana yake na wala hayaridhii.”6

5 Ajiwibatul-Masa’ail Jarullah Uk: 796 Awaailul Maqalaat Uk: 92 - 93

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page 5

Page 14: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

6

Utokezo (al-Badaa)

Na kabla yake amesema Imamu Swadiq (a.s.) katika tafsiri ya kauli yake(s.w.t.): “Mwenyezi Mungu anafuta ayatakayo na huimarisha anay-otaka na asili ya hukmu iko kwake.” Kila jambo analolitaka basi likokatika elimu yake kabla ya kulifanya, hakuna kitu kinachodhihiri ila kil-ishakuwa katika elimu yake. “Hakika Mwenyezi Mungu hakidhihiri kitukwake ambako kunatokana na kutotambua.”7

Na amesema (a.s.): “Mwenye kudai kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufulinadhihiri kwake jambo asilolijua basi jitengeni naye.”8

Kisha nguvu ya hoja za Shia katika mas’ala ya badau ni mambo matatu:Kauli yake (s.w.t.): “Mwenyezi Mungu anafuta ayatakayo na kuimar-isha ayatakayo na asili ya hukumu iko kwake.”9 Na kauli yake (s.w.t.):“Humuomba Yeye kila kilichomo mbinguni na ardhini kila siku Yeyeyumo katika mambo.”10

Kufanana mas’ala ya kufuta (nasikh) katika sharia, na badau ni nasikhkatika maumbile, na nasikh ni badau ya kisharia, kama ambavyo waislamuwamethibitisha nasikh katika sharia kama vile kubadili kibla tokaMasjidul-Aqsaa kuelekea Al-Ka’aba tukufu na hakukhalifu yeyote kati yaohilo, na hajazingatia yeyote kuwa hilo linakhalifu elimu ya milele yaMwenyezi Mungu (s.w.t.) wala hailazimu kuthibiti ujahili wa mwanzo,vivyo hivyo katika badau na kubadilika katika hukumu za maumbile bilaya kulazimu ujahili wa mwanzo wala haikhalifu elimu ya MwenyeziMungu ya milele, kama yeyote atapinga badau basi upinzani wake piautapinga nasikh na atakayoyataja katika mas’ala ya nasikh basi tunawezakuyajibu pia katika mlango wa badau bila ya tofauti yeyote baina yamambo hayo mawili.

7.Bihrul Anuwari Juz: 4 uk: 121 Hadith Na.: 638 " " " " : 30 9.Suratu Rad: 3910. Suratu Rahman: 29

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page 6

Page 15: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

7

Utokezo (al-Badaa)

Mushkeli katika badau ni kukariri mushkeli waliotoa mayahudi juunasikh katika sharia, ambapo wao wanaona ubatili wa hilo nakutowezekana kunasibisha nasikh kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu,kama ambavyo wamejibu maulamaa wa Kiislamu kwa mushkeli huuna kuthibitisha kwao uwezekano wa nasikh katika sharia bila kulazimuupungufu wowote katika uungu wake mtukufu inawezekana kutumiwakatika nasikh katika ulimwengu wa kimaumbile na mamlaka.

Kitendo huathtiri katika maisha ya mwanadamu, na huu ni ukweli waQur’ani uliothibiti kwa kuongezea yaliyopo katika Sunna za Nabii(s.a.w.w.) kwa kutilia mkazo, nayo ni kwamba amali za mwanadamuimani, shiriki, utii, maasi wema kwa wazazi wawili na kuwaasi kwao,kuwasaidia mafakiri, kutoa, kuunga udugu na kuukata n.k kunaathiri kati-ka riziki, baraka, kurefusha umri na furaha. Na mambo haya Qur’ani imey-ataja mara nyingi na Sunna zinaunga mkono mara nyingi na Qur’aniimeyafupisha kwa kusema: “Hakika Mwenyezi Mungu habadilishiyaliyopo kwa watu hadi wabadilishe yaliyopo katika nafsi zao.”

Na ambaye anapinga badau lazima atambue kwamba upinzani wakeunapelekea kupinga mfano wa ukweli huu ulio wazi, na ikiwa anauaminibasi atambue ya kuwa haya anayoyaamini ndio ambayo Shia wanayoyaitaal-Badau.

KAULI ZA MAULAMAA WA SHIAKATIKA BADAU

Hii ndio maana ya badau ambayo maulamaa wa Shia waliotangulia nawaliokuja baadae wametilia mkazo. Sheikh Mufiyd anasema: “Kauli yaShia katika al-badau njia yake ni ya kusikiwa na wala sio ya kutafakari, namakusudio yake sio kubadili rai na kutambua jambo lililokuwalimefichikana kwake, vitendo vya Mwenyezi Mungu vyote viko dhahirikwa viumbe vyake kabla hata ya kuvimba, navyo vinatambulikana Kwake

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page 7

Page 16: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

8

Utokezo (al-Badaa)

na bado vingali vinatambulika.”11

Sheikh Tusi amesema: “Al-Badau katika lugha ni kudhihiri, hivyohusemwa umedhihri kwetu uzio wa mji na imetudhihirikia rai …” Ama likinasibishwa tamko hili kwa Mwenyezi Mungu humo kuna ambayohayafai kunasibishwa Kwake; Ama ambayo yanafaa ni ambayo yanakusu-dia nasikh (kufuta) na kunasibisha hayo Kwake kuna wigo mpana, katikaupande huu yanachukuliwa yote yaliyopokelewa kutoka kwa wakwelimiongoni mwa habari zenye maana ya kunasibisha badau kwa MwenyeziMungu bila ya kunasibisha yasiyofaa kwake miongoni mwa kutambuabaada ya kutotambua, na wajihi wa kuyasema hayo ni kwamba ikiwayanayoonyesha nasikh inayodhihiri kwa mkalafu ambayo hayakuwadhahiri kwao na kupata kwao elimu baada ya kutokuwa nayo, hayo huitwa“Al–badau.”12

Na amesema As-Sayyid Abdallah Shubar: “Al-Badau ina maana nyingi,baadhi yake zinajuzu na zingine hazijuzu nayo ni - kwa fatiha na madda-aghlab hutumika katika lugha kwa maana ya kudhihiri kitu baada yakufichikana na kupata elimu kwayo baada ya kutojua.

Na umma umeafikiana kukanusha hayo kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ilayale ambayo hayachupi mpaka Kwake, na mwenye kunasibisha hayo kwaShia basi ameshawazulia uongo na Shia wako mbali nao.”13

As-Sayyid Abdul-Husein Sharaf Diyn amesema: “Na matokeo wanayose-ma Shia hapa ni kwamba Mwenyezi Mungu anapunguza riziki nakuongeza humo, vivyo hivyo katika vifo, afya maradhi furaha, matatizo,mitihani, balaa, imani ukafiri n.k. kama ilivyosema kauli Yake tukufu:“Mwenyezi Mungu hufuta atakayo na kuimarisha ayatakayo na asili

11 Taswihihul-Itiqaadatil Imamiyah Uk; 66 chapa ya Darul Mufiyd12 Maswabihu Durar Juz: 1 Uk: 3313 Udstul–Usul Juz: 2 Uk: 29

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page 8

Page 17: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

9

Utokezo (al-Badaa)

ya hukumu iko kwake.”14 Na huu ndio mtazamo wa Umar bin Khattabna Ibnu Mas’ud, Abi Wail na Qatadah. Na amepokea Jabir kutoka kwaMtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na wengi wa Salaf wanaomba nakunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu awajaalie wawe wema na wala wasi-we waovu, na yamepokewa hayo kwa tawaatur kutoka kwa Maimamuwetu katika dua zao zilizopokelewa, na imepokewa katika Sunna kwambasadaka kwa namna yake, wema kwa wazazi wawili, kufanya wema, hayayanabadili uovu kuwa wema na yanaongeza umri.

Na imesihi kwa Ibnu Abbas kwamba yeye amesema: “Tahadhari hainu-faishi kitu katika Qadar lakini Mwenyezi Mungu anafuta kwa dua anay-otaka miongoni mwa Qadar.” Hii ndio badau ambayo wanaisema Shia,inajuzu kuinasibisha badau kwake kwa uhusiano wa kufanana. Ikhitilafukatika hili baina yetu na Ahlus-Sunna ni ya matamshi tu, na anayosemaShia katika badau kwa maana tuliyoitaja wanaisema Waislamu wote.15

Sheikh Agha Bazarak at-Twaharaniy anasema: “Al-Badau maana yakekatika lugha ni kudhihiri rai ambayo haikuwepo na kusahihisha kitu kili-chojulikana baada ya kutojulikana, lakini haifai kunasibishwa kwaMwenyezi Mungu Mtukufu kwa kulazimu kudhihiri rai juu ya kitu amba-cho hakikuwepo kwa kutokijua Kwake awali au kushindwa Kwake naMwenyezi Mungu (s.w.t.) ametakasika na hayo.

Al-Badau wanayoisema Shia ni kwa maana ambayo lazima kila mwislamuanaitakidi mkabala na wayahudi wanaosema kwamba Mwenyezi Munguamemaliza kazi hivyo hakidhihiri kitu chochote kwake: “Mkono waMwenyezi Mungu umefumba” au mwenye kufuata kauli za wayahudiwenye kudai kwamba Mwenyezi Mungu ameumba vyote vilivyopo maramoja hivyo hakuna kitu ila alichokiumba awali au alikuwa anaitakidimfumo wa ulimwengu kwa kusema kwamba Mwenyezi Mungu ameumba

14 Suratu Raad: 3915 Ajuwibatu Masaail Jarullah Uk: 101 -103

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page 9

Page 18: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

10

Utokezo (al-Badaa)

mfumo wa ulimwengu nao uko nje umevuliwa katika mamlaka yake, mifu-mo mingine ndio inaoiendesha, ambapo lazima kila mwislamu akanushekauli hizi na aitakidi kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu “ kila sikuyuko katika mambo”16

NAFASI YA ITIKADI NA MALEZI YENYE KUJENGA KATIKA BADAU

Imedhihiri katika yaliyotangulia kwamba al- badau ina maana ya Qur’aniimeenea baina ya waislamu wote na kwamba Shia hawatofautiani na wais-lamu wengine isipokuwa katika jina ambalo kwalo linafahamika kosa lakunasibisha ujahili kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na imebainika kutosi-hi kunasibisha huku, na kilicho muhimu kwetu sasa ni kueleza upandemwingine wa utafiti, nao ni umuhimu wa fikra ya badau kuhusu itikadi yamwanadamu mwislamu, kwani fikra zinapimwa kwa misingi yake ya kie-limu na hoja zake za kimantiki na kwa malengo yake na matunda yake kwaupande mwingine.

Na katika maudhui ya badau inaweza kusemwa kwa njia ya kuuliza: Ikiwamakadirio ya awali hayatakuwa na kazi bali yatamalizikia kwa kufutwa,nini faida ya kutoa taarifa juu yake? Na nini matunda yanayopatikana kwakuitakidi al-Badau wakati huo?

Jawabu: Hakika kuitakidi al-Badau kunarejea kwenye umuhimu mkubwasana katika pande mbili: Upande wa itikadi na upande wa malezi.

Ama upande wa kiitikadi yanatutosha maneno ya Allammah al-Majlisiyambapo ameandika anasema: “Hakika wamevuka mpaka katika al-Badaukwa kuwajibu Wayahudi ambao wanasema: “Hakika Mwenyezi Munguamemaliza kazi na utawala.” Na baadhi ya Mu’tazila wanasema: “Hakika

16 Suratu Rahman: 29

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page 10

Page 19: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

11

Utokezo (al-Badaa)

Mwenyezi Mungu ameumba viumbe mara moja kama ilivyo hivi sasamiongoni mwa madini, mimea, wanyama, wanadamu, na wala kuumbwaAdamu hakujatangulia kuumbwa watoto wake, na kutangulia ni katikakudhihiri kwake sio katika kuumbwa kwake na kuwepo kwake, baliwamechukua makala haya kwa watu wa falsafa wenye kusema kuhusianana mfumo wenye kuendesha ulimwengu, na wenye kusema kwamba mam-laka ya Mwenyezi Mungu hayakuathiri isipokuwa katika uumbaji wa awalitu, hivyo wao wanamuengua Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika mamlakaYake na wananasibisha uendeshaji kwenye mfumo wa ulimwengu na walasio kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.” 17

Kwa maana kwamba mkazo wa Maimamu (a.s.) juu ya al-Badau umekujaili kubatilisha kila fikra zinazofanya uwezo wa Mwenyezi Mungu namatakwa Yake (s.w.t.) kuwa na kiwango maalum, na kuthibitisha kuwa niuhakika wa jumla kwa pande zote hata katika upande wa Qadar ambayoanaikadiria Mwenyezi Mungu Mtukufu mwenyewe katika ulimwengu wamaumbile, uumbaji, uendeshaji na malezi. Na kwamba makadirio yaMwenyezi Mungu (s.w.t.) katika makadirio hayo, hayamfanyi kuwa nimwenye kupokonywa hiari Yake na matakwa Yake kutokana na hayo.

Kama ambavyo al-Badau imekuja ili kutilia mkazo juu ya hiari yamwanadamu na matakwa yake wakati wa kubainisha uwezo wa kiungu,humo kuna Lauhul-Mahfuudh haikubali mabadiliko, na Lauhu nyingine niya kufuta na kuthibitisha ambayo anayakadiria Mwenyezi Mungu (s.w.t.)tangu mwanzo wa kuumba, hii inakubali mabadiliko kulingana na anayoy-afanya mwanadamu miongoni mwa amali katika dunia. Kana kwambaitikadi ya al-Badau imekuja ili kukamilisha itikadi ya Qadhwaa na Qadarili kuondolewa “Ghuluu” kuchupa mpaka na kufifiliza katika itikadi yaQadhwaa na Qadar, na isichukuliwe kwa maana ambayo itapokonya hiarikwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kwa mwanadamu. Hivyo hakuna budikuikamilisha kwa itikadi ya badau ambayo imekuja kutilia mkazo kwam-

17 Biharul-Anwar Juz: 4, Uk: 129 – 130 chapa ya Tehran

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page 11

Page 20: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

12

Utokezo (al-Badaa)

ba Qadar haifikii kiwango cha kupokonya hiari ya Mwenyezi Mungu walahaipokonyi hiari ya mwandamu.

Na katika upande wa malezi tunaona kwamba itikadi ya al-Badau inaathari ya kimalezi yenye kujenga katika maisha ya wanadamu, naAllammah al-Majlisiy anabainisha athari hii katika kukamilisha maanayake yaliyopita juu ya sababu za kutilia mkazo Maimamu (a.s.) juu ya al-Badau, ambapo kwanza anataja faida ya kuitakidi ambazo tumezitaja naakaongezea kwa kutaja faida ya kimalezi kwa kusema: “Hivyo Maimamu(a.s.) wakakataza hayo na wakathibitisha kwamba (s.w.t.) kila siku yukokatika kazi miongoni mwa kuondoa, kuleta kingine, kumfisha mtu nakumhuisha mwingine, n.k. ili waja wasiache kunyenyekea kwa MwenyeziMungu, kuomba, kutii, kujikurubisha kwake kwa yale yanayofaa katikamambo ya dunia yao na akhera yao, na ili wataraji wanapotoa sadaka kwamafakiri, kuunga udugu, kuwafanyia wema wazazi wawili, kufanya memana ihsani kwa yale waliyoahidiwa katika kuongezewa umri na kuongeze-wa riziki.”

Na katika upande mwingine itikadi ya al-Badau ni kuhamasisha juu yauzuri wake katika itikadi ya toba na masharti ya kukubaliwa mbele yaMwenyezi Mungu, kama ambavyo toba ina athari nzuri katika kumjengamwanadamu, na kwa upande mwingine ni kufunga mianya ya kukatatamaa na kufungua milango ya matumaini na matarajio na kujenga moyowa mageuzi na maandalizi ya mafanikio, vivyo hivyo badau ina athari hiikatika maisha ya mwandamu, bali badau ni dharura kati ya dharura za tobana vigezo vyake ni katika amali, kwani kati ya dharura za toba ni mwenyekutubia kuitakidi kwamba kalamu ya Mwenyezi Mungu bado wino wakehaujakauka katika ubao wa kufuta na kuthibitisha, hivyo MwenyeziMungu anaweza kufuta na kuthibitisha anayotaka, anamneemeshaamtakaye na kumfanya amtakaye kuwa muovu kulingana na anavyojipam-ba mja miongoni mwa tabia njema na amali njema, au kulingana na anavy-ofanya amali mbaya, na wala matakwa ya Mwenyezi Mungu hayaji burebure tu, bila ya kudhibitiwa na hekima. Bali lau mja akitubu na kutekeleza

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page 12

Page 21: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

13

Utokezo (al-Badaa)

ya wajibu na kushikamana na wema anatoka katika kundi la watu waovuna kuingia katika kundi la waja wema, na kinyume chake pia ni sahihi.

Na katika hayo yote tunaweza kufahamu maana ya maneno ya Maimamu(a.s.) kwamba: “Hajaabudiwa Mwenyezi Mungu kwa chochote mfano waanavyoabudiwa kwa badau.”18 Na wala “Hajatukuzwa Mwenyezi Mungumfano wa anavyotukuzwa kwa al-Badau.”19 Na “Mwenyezi Mungu haja-tuma Nabii hadi achukue kwake ahadi ya mambo matatu: Kukubali ibadaya Mwenyezi Mungu, kuivua shirki, na kwamba Mwenyezi Mungu hutan-guliza ayatakayo na huchelewesha ayatakayo.” 20

MASWALI KUHUSU ITIKADI YA BADAU

Hapa tunatoa maswali yanayotaka majibu yenye kutosheleza nayo:1. Hakika kauli ya al-Badau inasababisha Mwenyezi Mungu kufanya upu-

uzi kwani pamoja na kutambua yatakayotokea kwake miongoni mwamabadiliko na kudhihiri, basi kutoa taarifa kwa makadirio ya mwanzoitakuwa ni upuuzi?

Jawabu: Hakika itakuwa ni upuuzi kama tutajaalia kutokuwepo lengo namanufaa yanayotarajiwa kutokana na kutoa taarifa ya makadirio yamwanzo, na haya ni ambayo hatuwezi kuyathibitisha, hivyoinawezekana kuwepo lengo na manufaa yanayorejea kwa mja kwa faidakubwa kutokana na taarifa hiyo.

2. Hakika Nabii au Imamu akitoa taarifa ya kitu kisha ikatokea al-Badaukatika kutokea kwake, ni lazima ategemee katika taarifa yake ya awalikwenye kitu kinachokuwa ni chanzo (rejea) cha taarifa yake na asili yachanzo cha elimu yake, sasa ni kwa jambo gani atategemea Nabii auImamu katika taarifa yake ya awali?

18 Usulul-Kafiy Juz: 1, Uk: 14619 Usulul-Kafiy : Jz. 1, Uk. 146 kitabu Tawhid Babul-Badai20 Usulul-Kafiy : Jz. 1, Uk. 146 kitabu Tawhid Babul-Badai

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page 13

Page 22: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

14

Utokezo (al-Badaa)

Jawabu: Inahitaji kubainisha mfano kama lau mwanadamu akila sumuyenye kuangamiza inayosababisha kifo chake hakika utakapoona tukio hiliunaweza kumpa taarifa ya kutokea kifo chake baada ya masaa, nayo nihabari ya kweli kulingana na hali halisi isiyo na shaka, na kama mautihayakutokea kwa sababu ya kutokea kizuizi kisichotarajiwa kama vilekutokea tabibu wa kumtibu mwenye ujuzi wa hali ya juu, taarifa hiyo haiwiya uongo wala haihesabiwi kuwa ni taarifa isiyo na chanzo, vivyo hivyokatika taarifa ya mbinguni ambayo inatoa taarifa za kutokea baadhi yamambo katika siku zijazo, kwani ni za kweli kulingana na hali yakutokuwepo na kizuizi wala hakuna ubaya katika jambo hili isipokuwakutotambua Nabii au Imamu kupatikana kwa kizuizi hapo baadae. Hivyotuseme kwamba Mwenyezi Mungu amempa Nabii taarifa ya jambo nahakutaka kumpa taarifa ya kutokea kwa kizuizi baadaye kwa maslahiyanayohusiana na waja.

3. Hakika kutokea badau inasababisha Nabii au Imam kutuhumiwa kwauongo.

Jawabu: Hakika kutuhumiwa Nabii au Imamu kwa uongo ni jambo amba-lo dhambi yake inamwangukia mwenye kulifanya, na tuhuma kama itato-ka kwa kafiri basi hii sio ajabu kwake baada ya kukataa kuamini asili yatawhidi, utume na marejeo, na kama itatoka kwa muumini tunajaalia kuwaimani yake itamzuia juu ya hilo, na kama haitamzuia basi hiyo ni dalili yaudhaifu wa imani yake.

Cha muhimu ni kwamba badau sio sababu ya kimantiki ya kumtuhumukwa uongo bali hali nyingi za badau zilikuwa zikiambatana nayanayosadikisha ukweli, kama ilivyo katika kisa cha Ibrahim (a.s.) palealipoamrishwa kumchinja mtoto wake, kwani amri mpya ya fidia ina-maanisha kusadikisha amri ya awali ya kumchinja Ismail (a.s.) na kamahiyo taarifa ya awali haikuwa ya kweli basi amri ya kuchinja kondooisingekuja ni fidia badala yake, hivyo fidia ni kwa maana ya badala.

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page 14

Page 23: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

15

Utokezo (al-Badaa)

HITIMISHOHakika al-Badau kwa maana ya kubadili rai haitokei kwa MwenyeziMungu na wala Shia hawasemi hivyo, bali wanasema kutowezekana hilona ukafiri wa mwenye kusema hivyo, na kwamba inalazimu kujiepusha naanayesema hivyo.21

Ndio, al-Badau inayokubaliwa na ambayo ni wajibu kuitakidi kwayoimeelezwa na Aya za Qur’ani tukufu: “Mwenyezi Mungu anafutaayatakayo na huimarisha anayoyataka na asili ya hukumu ikokwake.”

Na kufuta huku na kuimarisha kunakuwa wazi na kuthibiti katika anayoy-adhihirisha Mwenyezi Mungu miongoni mwa mambo kwa ulimi wa Nabiiwake au Walii wake katika dhahiri kwa masilahi yanayohitajia kudhi-hirishwa, kisha anayafuta na yanakuwa yale yasiyodhihiri mwanzo pamo-ja na kutambua hilo tangu mwanzo kwa elimu yake. Badau inafanana nanasikh (kufuta) hukumu za kisharia zilizotangulia kabla ya NabiiMuhammad (s.a.w.w.) au nasikh ya baadhi ya hukumu ambazo zimekujakatika sharia ya Nabii wetu (s.a.w.w.) kwa hukumu zilizofuata baadaye.22

Hakika ambaye haamini itikadi hii ya badau basi atakuwa amemuwekeaMwenyezi Mungu kikomo katika uwezo Wake na matakwa Yake yasiyo nampaka, kama ilivyoashiria Qur’ani tukufu juu ya hilo katika itikadi yakiyahudi kwa kauli yake: “Wamesema Wayahudi mkono wa MwenyeziMungu umefumba, bali imefumba mikono yao.”23 Na haya ndioambayo yameenea kwa baadhi ya makundi ya Kiislamu yasiyokuwa ShiaIthina Ashariyah.

21 Aqaidul-Imamiyah cha Mudhafar uk: 45 chapa ya pili ya Najaf22 Aqaidul-Imamiyah cha Mudhafar uk: 45 chapa ya pili ya Najaf23 Suratul Maida: 64

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page 15

Page 24: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NAAL-ITRAH FOUNDATION:

1. Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Ishirini na Nne

2. Uharamisho wa Riba3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili5. Hekaya za Bahlul6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)8. Hijab vazi Bora9. Ukweli wa Shia Ithnaashari10. Madhambi Makuu11. Mbingu imenikirimu12. Abdallah Ibn Saba13. Khadijatul Kubra14. Utumwa15. Umakini katika Swala16. Misingi ya Maarifa17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia18. Bilal wa Afrika19. Abudharr20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu21. Salman Farsi22. Ammar Yasir23. Qur'an na Hadithi24. Elimu ya Nafsi25. Yajue Madhehebu ya Shia26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu27. Al-Wahda

16

Utokezo (al-Badaa)

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page 16

Page 25: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

28. Ponyo kutoka katika Qur'an. 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii30. Mashukio ya Akhera31. Al Amali32. Dua Indal Ahlul Bayt33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna.34. Haki za wanawake katika Uislamu35. Mwenyeezi Mungu na sifa zake36. Amateka Na Aba'Khalifa37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s)38. Adhana.39 Upendo katika Ukristo na Uislamu40. Nyuma yaho naje kuyoboka41. Amavu n’amavuko by’ubushiya42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya swala mbili44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya46. Kusujudu juu ya udongo47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s)48. Tarawehe49. Malumbano baina ya Sunni na Shia50. Kupunguza Swala safarini51. Kufungua safarini52. Umaasumu wa Manabii53. Qur’an inatoa changamoto54. as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s)

17

Utokezo (al-Badaa)

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page 17

Page 26: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili63. Kuzuru Makaburi64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu67. Tujifunze Misingi Ya Dini68. Sala ni Nguzo ya Dini69. Mikesha Ya Peshawar70. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu71. Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliy

onyooka72. Shia asema haya, Sunni asema haya, Wewe wasemaje?73. Liqaa-u-llaah74. Muhammad (s) Mtume wa Allah75. Amani na Jihadi Katika Uislamu 76. Uislamu Ulienea Vipi?77. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 78. Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 79. Urejeo (al-Raja’a )80. Shahidi kwa ajili ya Ubinadamu81. Kuanzia ndoa hadi kuwa wazazi 82. Myahudi wa Kimataifa83. Uislamu na dhana84. Mtoto mwema85. Adabu za Sokoni86. Johari za hekima kwa vijana87. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza88. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili89. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu90. Tawasali91. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia92. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu

18

Utokezo (al-Badaa)

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page 18

Page 27: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

93. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi94. Swala ya maiti na kumlilia maiti95. Shiya na Hadithi (kinyarwanda)96. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu97. Hadithi ya Thaqalain98. Fatima al-Zahra99. Tabaruku100. Sunan an-Nabii101. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)100. Idil Ghadiri102. Mahdi katika sunna103. Kusalia Nabii (s.a.w)104. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza105. Ujumbe - Sehemu ya Pili106. Ujumbe - Sehemu ya Tatu107. Ujumbe - Sehemu ya Nne108. Shiya N’abasahaba109. Iduwa ya Kumayili110. Maarifa ya Kiislamu.111. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza112. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili113. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu114. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne115. Ukweli uliopotea sehmu ya Tano

19

Utokezo (al-Badaa)

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page 19

Page 28: AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009 ...ibn-tv.co.tz/wp-content/uploads/2011/03/Utokezo.pdf · ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa

BACK COVER

Maudhui ya Utokezo (Badaa’) yanazingatiwa kuwa ni kati ya masuala yafalsafa ya Kitawhidi ambayo yamechochea utafiti wenye wigo mpanabaina ya maulamaa wa elimu ya falsafa, hiyo ni kutokana na yanay-opatikana humo miongoni mwa masuala ya kina na ya muhimu.

Kumekuwepo na kutokuafikiana katika miji yetu ya Kiislamu, hususanmiongoni mwa wanavyuoni kuhusu usahihi wa itikadi ya Badaa’ - yaaniutokezo wa jambo fulani kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Baadhi wanase-ma kwamba itikadi hii ni sahihi na wengine wanasema si sahihi. Baadhi yawanavyuoni wamekwenda mbali zaidi hadi kufikia kuwaita Waislamuwenzao wanaoitakidi juu ya Utokezo (Badaa’) kuwa ni washirikina aumakafiri .

Lakini je, Badaa’ haina asili katika dini? Ukweli ni kwamba ina asili kati-ka dini kwani uhalisi wake umeelezwa katika Qur’ani Tukufu, kamautakavyoona katika kitabu hiki. Hivyo ungana na mwaandishi wa kitabuhiki, Sayyid Abdul-Karim al-Bahbahani katika utafiti wake huu wa kie-limu.

Kimetolewa na kuchapishwa na:Alitrah FoundationS.L.P. 19701 Dar es Salaam, TanzaniaSimu: +255 22 2110640Simu/Nukushi: +255 22 2127555Barua Pepe: [email protected]: www.alitrah.orgKatika mtandao: www.alitrah.info

20

Utokezo (al-Badaa)

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd 6/29/2009 9:40 AM Page 20