AGANO JIPYA - n-e-v.info · PDF fileMpangilio Wa Masomo Ya Biblia 651 Misingi Wa Biblia 654....

download AGANO JIPYA - n-e-v.info · PDF fileMpangilio Wa Masomo Ya Biblia 651 Misingi Wa Biblia 654. MATHAYO MTAKATIFU 1 Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.

If you can't read please download the document

Transcript of AGANO JIPYA - n-e-v.info · PDF fileMpangilio Wa Masomo Ya Biblia 651 Misingi Wa Biblia 654....

  • AGANO JIPYA

    Ufafanuzi ulifanywa na Duncan Heaster

  • AGANO JIPYA Ufafanuzi ulifanywa na Duncan Heaster

    (Swahili New Testament with commentary by Duncan Heaster)ISBN: 978-1-906951-55-9Commentary and Bible Basics Duncan Heaster

    The Christadelphian Advancement TrustP.O. Box 3034 South Croydon

    Surrey CR2 0ZAENGLAND

    Registered Charity no. 1080393

    This book is not for sale. It is funded by voluntary donations to The Christadelphian Advancement Trust. If you would like to support the work of distributing free Bibles and Biblical literature worldwide, please direct donations and legacies to the above address or contact us online: www.carelinks.net, email: [email protected]

    KITABU CHA MISINGI WA BIBLIA. Kama umefurahia kitabu hiki na ungependa kuendeleza masomo yako, kuna kitabu kingine kiitwacho MISINGI WA BIBLIA kinachoweza kupatikana kutoka kwa anwani hii:Christadelphian Advancement Trust, P.O. Box 3034, SOUTH CROYDON, SURREY CR2 OZA ENGLANDWavuti: www.carelinks.net Barua pepe: [email protected]

  • YALIYOMO

    Mathayo Mtakatifu 5Marko Mtakatifu 83Luka Mtakatifu 133Yohana Mtakatifu 232Matendo Ya Mitume 306Waraka Wa Paulo Mtume Kwa Warumi 387Waraka Wa Kwanza Wa Paulo Mtume Kwa Wakorintho 421Waraka Wa Pili Wa Paulo Mtume Kwa Wakorintho 454Waraka Wa Paulo Mtume Kwa Wagalatia 475Waraka Wa Paulo Mtume Kwa Waefeso 487Waraka Wa Paulo Mtume Kwa Wafilipi 498Waraka Wa Paulo Mtume Kwa Wakolosai 506Waraka Wa Kwanza Wa Paulo Mtume Kwa Wathesolonike 514Waraka Wa Pili Wa Paulo Mtume Kwa Wathesolonike 521Waraka Wa Kwanza Wa Paulo Mtume Kwa Timotheo 525Waraka Wa Pili Wa Paulo Mtume Kwa Timotheo 534Waraka Paulo Mtume Kwa Tito 541Waraka Wa Paulo Mtume Kwa Filemoni 545Waraka Kwa Waebrania 547Waraka Wa Yakobo 572Waraka Wa Kwanza Wa Petro 581Waraka Wa Pili Wa Petro 590Waraka Wa Kwanza Wa Yohana 596Waraka Wa Pili Wa Yohana 605Waraka Wa Tatu Wa Yohana 607Waraka Wa Yuda 609Ufunuo Wa Yohana 612Mpangilio Wa Masomo Ya Biblia 651Misingi Wa Biblia 654

  • MATHAYO MTAKATIFU

    1Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu. 2 Ibrahimu alimzaa Isaka;

    Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake;. 3 Yuda akamzaa Peresi na Zera

    ambao mama yao alikuwa Tama-ri. Peresi akamzaa Esroni, Esroni akamzaa Aramu, 4 Aramu akamzaa Aminadabu,

    Aminadabu akamzaa Nashoni, Nashoni akamzaa Salmoni, 5 Salmoni akamzaa Boazi na

    mama yake Salmoni alikuwa Ra-habu. Boazi akamzaa Obedi, am-baye mama yake alikuwa Ruthi. Obedi akamzaa Yese, 6 Yese akamzaa Daudi ambaye

    alikuwa mfalme. Daudi akamzaa Solomoni ambaye mama yake ni yule aliyekuwa mke wa Uria.7 Solomoni akamzaa Reho-

    bo amu, Rehoboamu akamzaa Abiya, Abiya akamzaa Asa, 8 Asa akamzaa Yehoshafati,

    Yehoshafati akamzaa Yoramua, Yoramu akamzaa Uzia, 9 Uzia akamzaa Yothamu,

    Yothamu akamzaa Ahazi, Ahazi akamzaa Hezekia, 10 Hezekia akamzaa Manase,

    Manase akamzaa Amoni, Amoni akamzaa Yosia, 11 wakati wa uhamisho wa Ba-

    beli, Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake. 12 Na baada ya uhamisho wa

    Babeli, Yekonia alimzaa Sheal-tieli, Shealtieli akamzaa Zeru-babeli, 13 Zerubabeli akamzaa Abiudi,

    Abiudi akamzaa Eliakimu, Elia-kimu akamzaa Azori, 14 Azori akamzaa Zadoki, Za-

    doki akamzaa Akimu, Akimu akamzaa Eliudi, 15 Eliudi akamzaa Eliezari,

    Eliezari akamzaa Matani, Mata-ni akamzaa Yakobo, 16 Yakobo akamzaa Yosefu am-

    baye alikuwa mumewe Maria, mama yake Yesu, aitwaye Kri-sto. 17 Hivyo, kulikuwapo na jumla

    ya vizazi kumi na vinne tangu Ibrahimu mpaka Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi hadi wakati wa uhamisho wa Babeli

    1:1 Rekodi za injili ni ishara kama Mathayo alivyo anza maelezo yake (Haba-ri Njema) kwa kuonyesha Yesu alikuwa mzaliwa wa Ibrahimu na Daudi. Hii ni muhimu kwa kuwa injili ilikuwa katika ahadi zao.

  • 6 MATHAYO 1:172:1

    na vizazi kumi na vinne tangu wakati wa uhamisho wa Babeli hadi Kristo. 18 Basi Kuzaliwa kwake Yesu

    Kristo kulikuwa hivi: Maria mama yake alikuwa ameposwa na Yosefu, lakini kabla hawaja-kutana kimwili, Maria alione-kana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 19 Kwa kuwa Yosefu, mwa-

    naume aliyekuwa amemposa alikuwa mtu mwadilifu, hakuta-ka kumwaibisha Maria hadha-rani, aliazimu kumwacha kwa siri. 20 Lakini mara alipoazimu

    kufanya jambo hili, malaika wa Bwana akamtokea katika ndo-to na kusema., Yosefu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, kwa ma-ana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 21 Naye atamzaa mwana, nawe

    utamwita jina lake Yesu, kwa maana yeye ndiye atakayewa-

    okoa watu wake kutoka katika dhambi zao. 22 Haya yote yametukia ili

    kutimiza lile Bwana alilokuwa amenena kupitia nabii, akisema: 23 Tazama, bikira atachukua

    mimba, naye atamzaa mwana, nao watamwita jina lake Imanu-eli, maana yake, Mungu pa-moja nasi. 24 Yosefu alipoamka kuto-

    ka usingizini, akafanya kama vile alivyoagizwa na malaika wa Bwana, akamchukua Maria kuwa mke wake 25 Lakini hawakukutana kim-

    wili mpaka Maria alipojifun-gua mwanawe kifungua mimba akamwita jina lake Yesu.

    2Baada ya Yesu kuzaliwa kati-ka mji wa Bethlehemu huko Uyahudi, wakati wa utawala wa mfalme Herode, wataala-mu wa mambo ya nyota kuto-ka Mashariki walifika Yerusa- lemu

    1:19 Yusufu anaeleza wengine kuhusu hali yake na kumfanya kuwa mfano kwa umma ama kumweka katika sheria ya wivu ya kitabu cha Hesabu 5 lakini kamili kwa kuwa Yusufu alikuwa mnofu hakufanya hayo. Alikuwa makini kwake jinsi inavyotupasa kuwa kwa wengine waliojikuta katika hali zaidi ya kuelewa kwetu.1:20 Kuzaliwa. Yesu alianza kwa Maria. Hakuna hapo kitambo. Alizaliwa kwake (1:16)1:21 Yesu inamaanisha mwokozi Kristo inamaanisha Aliyetakasa.

  • MATHAYO 2:22:13 72 wakiuliza, Yuko wapi huyo

    aliyezaliwa mfalme wa Wayahu-di? Kwa maana tumeona nyota yake ikitokea mashariki, nasi tu-mekuja kumwabudu. 3 Mfalme Herode aliposikia

    jambo hili aliingiwa na hofu sana pamoja na watu wote wa Yerusalemu. 4 Herode akawaita pamoja ma-

    kuhani wakuu na waandishi wa watu, akawauliza ni mahali gani ambapo Kristo angezaliwa. 5 Nao wakamwambia, Katika

    Uyahudi, kwa maana hivyo ndi-vyo ilivyoandikwa na nabii: 6 Nawe, Bethlehemu, katika

    nchi ya Yuda wewe si mdogo miongoni mwa watawala wa Yuda, kwa maana kutoka kwako atakuja mtawala atakayekuwa mchungaji wa watu wangu Isra-eli. 7 Ndipo Herode akawaita wale

    wataalamu wa nyota kwa siri na kutaka kujua kutoka kwao uha-kika kamili wa wakati ile nyota ilipoonekana.

    8 Kisha akawatuma waende Bethlehemu akiwaambia, Nen-deni mkamtafute kwa bidii huyo mtoto. Nanyi mara mumwona-po, mniletee habari ili na mimi niweze kwenda kumwabudu. 9 Baada ya kumsikia mfal-

    me, wale wataalamu wa nyota wakaenda zao, nayo ile nyota waliyoiona mashariki ikawa-tangulia, nao wakaifuata mpaka iliposimama mahali pale alipo-kuwa mtoto. 10 Walipoiona ile nyota waka-

    jawa na furaha kubwa mno. 11 Walipoingia ndani ya ile

    nyumba, wakamwona mtoto pa-moja na Maria mama yake, wa-kamsujudu na kumwabudu yule mtoto Yesu. Ndipo wakafungua hazina zao, wakamtolea zawadi za dhahabu, uvumba na mane-mane. 12 Nao wakiisha kuonywa kati-

    ka ndoto wasirudi kwa Herode, wakarudi kwenda katika nchi yao kwa njia nyingine. 13 Walipokwisha kwenda zao,

    2:5 Kupitia kwa Nabii Manabii waliandika maneno ya Mungu bali sio ma-neno yao. Biblia ni neno la Mungu.2:6 Yesu alitoka Bethlehemu Hakutoka mbinguni kama mtu. Zingatia jinsi Mathayo anavyo onyesha Yesu alitimiza unabii wa agano la kale.2:8 Askari wa mfalme hawakumheshimu kwa kuwa Mungu aliwakataza (:12) Tusiwe tunafanya vile tunavyomwambia na walio na cheo kama ni kinyume na neno la Mungu.

  • 8 MATHAYO 2:132:22

    malaika wa Bwana akamtokea Yosefu katika ndoto akamwam-bia, Ondoka, mchukue mtoto na mama yake mkimbilie Misri. Kaeni huko mpaka nitakapowa-ambia, kwa maana Herode ana-taka kumtafuta huyu mtoto ili amwue. 14 Kisha Yosefu akaondoka,

    akamchukua mtoto na mama wakati wa usiku, nao wakaenda Misri 15 ambako walikaa mpaka He-

    rode alipokufa. Hili lilikuwa, ili litimie lile lililonenwa na Bwana kwa kinywa cha nabii kusema, Kutoka Misri nilimwita mwa-nangu 16 Herode alipongamua kwa-

    m ba wale wataalamu wa nyota wamemshinda kwa akili, alikasi-rika sana, naye akatoa amri ya ku-waua watoto wote wa kiume we-nye umri wa miaka miwili kurudi chini katika mji wa Bethlehemu na sehemu zote za jirani, kufu-atana na ule muda alioambiwa

    na wale wataalamu wa nyota. 17 Ndipo lile lililonenwa na na-

    bii Yeremia lilipotimia. 18 Sauti ilisikika huko Rama,

    kilio cha huzuni na maombolezo makuu, Raheli akilia kwa ajili ya wanawe, akikataa kufarijiwa, kwa sababu hawako tena. 19 Baada ya Herode kufa, mala-

    ika wa Bwana akamtokea Yosefu katika ndoto huko Misri 20 na kusema, Ondoka, mchu-

    kue mtoto na mama mwende, mrudi katika nchi ya Israeli kwa sababu wale waliokuwa wanata-futa uhai wa mtoto wamekufa. 21 Basi Yosefu, akaondoka

    akamchukua mtoto na mama yake wakaenda mpaka nchi ya Israeli. 22 Lakini aliposikia kwamba

    Arkelao alikuwa anatawala huko Uyahudi mahali pa Herode baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye akiisha kuonywa katika ndoto, akaenda zake sehemu za Galilaya,

    2:14 Aliinuka Utiifu wa Yusufu kwa neno la Mungu inasisitizwa kama mfano kwetu 2:202:15 Kutoka Misri Waisraeli walipoitwa nje ya Misri Wana wote wa Mun-gu watoke Misri.2:20-22 Yusufu aliambiwa na Salama kurudi lakini alikuwa na Shauku. Na hivyo Mungu akamwambia aende aishi Galilaya.Kubatizwa katika bahari kubatiza ni kutumbukizwa bali si kunyunyizwa. Kwa hivi ubatizo ulifanyika baharini.

  • MATHAYO 2:233:12 923 akaenda, akaishi katika mji

    ulioitwa Nazareti, hivyo likawa limetimia lile lililonenwa na ma-nabii, Ataitwa Mnazareti.

    3Siku hizo Yohana Mbatizaji alikuja akihubiri katik